Wednesday, 13 March 2019

MAMA AJIFUNGUA WATOTO WATANO KWA MKUPUO

...
Mama aitwaye Evelyn Namukhula mwenye umri wa miaka 28  amejifungua salama watoto watano katika Hospitali Kuu ya Kakamega nchini Kenya

Evelyn Namukhula  amejifungua kupitia njia ya upasuaji, ambapo madaktari wamethibitisha hali ya afya ya watoto wake ni nzuri. 

Amejifungua wasichana watatu na wavulana wawili. 

Kabla ya kujifungua, Namukhula alikuwa na watoto wanne anaoishi nao na baba yao Herbert Nabwire katika kijiji cha Sisokhe, eneo bunge la Navakholo.

 "Namshukuru Mungu kwa mujiza huu. Hata hivyo, nawaomba wahisani kujitokeza kwa kuwa sitakuwa na uwezo wa kuwalea pekee yangu," alisema. 

Share:

Related Posts:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © 2025 MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger