Gareth Southgate amechaguliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya England kwa kumpa mkataba wa mika minne aliosaini.
Southgate
mwenye umri wa miaka 46 aliacha wadhfa wake kama mkufunzi wa timu ya
England ya vijana wasiozidi miaka 21 mnamo mwezi Septemba baada ya
aliyekuwa meneja wa Uingereza Sam Allardyce kujiuzulu baada ya kuhudumu
kwa siku 67 pekee.
Aliisaidia
Uingereza kushinda mara mbili pamoja na sare mbili kama kaimu mkufunzi
na sasa ametia saini kandarasi ya miaka minne yenye thamani ya pauni
milioni 2 kwa mwaka.
”Nimefurahia sana kushirikiana na wachezaji katika mechi nne na ndhani kuna vipaji vingi”,alisema.
0 comments:
Post a Comment