Tuesday 24 February 2015

JAMAA ANUSURIKA KIFO, BAADA YA WIZI WA FEDHA KWA MITANDAO YA SIMU

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

amaa mmoja ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akinusa kifo baada ya kula kipigo ‘hevi’ wakati akifanya jaribio la wizi wa fedha kiasi cha shilingi laki 450,000 kupitia huduma za fedha kwa mitandao ya simu.

Akiomba kuachiwa baada ya kupewa kichapo kikali.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilijiri wikiendi iliyopita maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo jamaa huyo alidaiwa kuingia kwenye duka moja akijifanya anataka kutoa shilingi laki nne na nusu (450,000/=) jambo lililomfanya wakala kumuonesha namba za kutolea kwa uchangamfu akijua ni mteja wa kawaida.
Dakika chache baadaye wakati wateja wengine wakiendelea kuhudumiwa, jamaa huyo alionesha meseji kuwa ametoa kiasi hicho cha fedha kupitia moja ya mitandao ya simu.
Wakala huyo alipoichukua meseji ya jamaa huyo ili kuhakikisha muamala wake alishangaa kuona meseji hiyo kuwa ni ya mtandao mwingine tofauti na alioutaja huku ikionesha imeandikwa au kutumwa na namba ya kawaida ya simu badala ya namba ya huduma hiyo ya mtandao husika.

Wakizidi kumshushia kichapo.
Wakala huyo, Maulid Vedasto alishangaa na kuamua kumshikilia jamaa huyo akimuitia mwizi ndipo wananchi wenye hasira kali walipofika na kumzingira wakimtaka atoe maelezo ya kutosha ambapo njemba huyo ilikiri kutaka kuiba jambo lililoamsha hasira za watu walioamua kumshushia kipigo hevi nusura afe.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wakala huyo alisema kuwa jamaa huyo alifika mara ya kwanza siku hiyo dukani kwake akitaka kutoa shilingi elfu sabini lakini alighairi na kurudi baada ya muda mfupi akitaka kufanya jaribio hilo la wizi.

Kichapo kikiendelea.
“Nilianza kumtilia shaka mara ya kwanza alipokuja na kujifanya anataka kutoa fedha huku akiwa na wasiwasi na kila mara alipokuwa akiwaona watu wengi ndipo alipokuwa akiniongelesha akijifanya ana haraka ya kutoa fedha, akiona watu wachache anasubiri,” alisema wakala huyo.Baada ya kunaswa jamaa huyo alipekuliwa kwenye simu yake ambapo iligundulika kuwa kweli meseji hiyo haikuwa ya mtandao husika huku akiwa hana salio.
Katika kuhakikisha hilo, wakala huyo aliwapigia simu makao makuu ya mtandao huo na kupata taarifa kuwa hakuna salio la aina hiyo lililohamishwa kutoka kwenye simu ya jamaa huyo.Katika utetezi wake, jamaa huyo aliomba watu wasimuue kwa kuwa ni tamaa za kidunia zilimponza huku akikiri kufanya utapeli huo kwa kushirikiana na wenzake watatu ambapo wamefanikiwa kutapeli mawakala kibao jijini Dar.
“Jamani inatosha mlivyonipiga, naomba msiniue ni shetani tu amenipitia. Kweli nakiri kuwa nimewaibia mawakala wengi sana lakini nimekoma. Nipelekeni polisi msiniue,” alisema jamaa huyo ambaye alikuwa akivuja damu chapachapa kisha kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ kusubiri sheria kuchukua mkondo wake.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger