Tuesday 24 February 2015

TAARIFA KWA UMMA : KUHUSU TOZO KWENYE KATIKA MITANADAO YA SIMU ZA MIKONONI

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY

TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU TOZO KWENYE SEKTA YA TEHAMA
Katika wiki ya pili ya Februari 2015, baadhi ya watoa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi walianzisha vifurushi vya mawasiliano na bei na kusabababisha malalamiko kutoka kwa watumiaji na umma kwa ujumla. TCRA, kwa kuzingatia upeo wa shughuli zake, imechambua hali hiyo na inapenda kutoa maelezo na maagizo ambayo yatawezesha kuondoa sintofahamu iliyopo na kujenga mustakabali kwa siku zijazo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, miongoni mwa kazi za TCRA ni kufuatilia utoaji wa huduma katika sekta inazozisimamia kwa kuzingatia kiwango cha upatikanaji wa huduma hizo, ubora na viwango vya huduma, bei ya huduma na kuhimiza ushindani na ufanisi wa kiuchumi. Katika kutelekeza majukumu yake, TCRA inawajibika kupitia na kuchambua, mara kwa mara, utoaji wa huduma katika sekta na kuchukua hatua dhidi ya chochote kinachotokea kwenye soko, kiwe chanya au hasi.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inaongozwa na Sera za Kisekta, Sheria ya Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania ya 2003, Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya 2010, na Kanuni zake za mwaka 2011 zilizotungwa kwa kuzingatia matakwa ya EPOCA. Kifungu 6(1) cha Sheria ya TCRA kinaitaka Mamlala kufuatilia utoaji wa huduma unaofanywa na sekta inazozisimamia ikiwa ni pamoja na upatikanaji, ubora na viwango vya huduma, gharama za huduma hizo na kufanikisha ufumbuzi na utatuaji wa malalamiko na migogoro. Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kuhusu tozo mpya zilizotangazwa na makampuni ya simu za mkononi.  Endelea kusoma taarifa yote hapa
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger