Wednesday 31 December 2014

BREAKING NEWS:UKWELI KUHUSU KUBADILIKA KWA RATIBA YA MTIHANI KIDATO CHA SITA 2015

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY
                                    
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2015
HAIJABADILIKA
Baadhi ya watu wamekuwa wakitumiana ujumbe kwenye mitandao ya
kijamii wenye kupotosha kwamba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
ametangaza kuwa Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015 utafanyika
kuanzia tarehe 2 hadi 25 Machi 2015 badala ya tarehe 4 hadi 27 Mei
2015. Aidha, ujumbe huo umetoa sababu kuu ya mabadiliko ya ratiba ya
mtihani kuwa inatokana na mwingiliano wa ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa
mwaka 2015 na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwafahamisha watahiniwa wa
Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni
za UONGO na zinalenga kuupotosha umma wa watanzania. Baraza
linapenda kusisitiza kuwa ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2015
HAIJABADILIKA na kwamba Mtihani huo utafanyika kuanzia tarehe 4
hadi 27 Mei 2015 kama ilivyopangwa awali, Baraza la Mitihani linaomba
wadau wazipuuze taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii
kwa kuwa zina lengo la kupotosha umma.
Imetolewa na,
AFISA HABARI NA UHUSIANO
 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger