Sunday 7 December 2014

MPYA: TAMKO KUHUSU UTOAJI WA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STAHAHADA KWA KUTUMIA MITAALA MIPYA ILIYOANDALIWA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY




 

          


TAMKO KUHUSU UTOAJI WA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STAHAHADA KWA KUTUMIA MITAALA MIPYA ILIYOANDALIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE) KWA MWAKA WA MASOMO 2014/15



Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na taasisi zake ambazo ni Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Taasisi ya Elimu (TIE) na Baraza la Mitihani ya Taifa (NACTE) iliandaa Mitaala mipya ya Ualimu wa Shule za Msingi na Sekondari kwa ngazi ya Diploma ya kawaida (NTA level 6) na Diploma ya Juu (NTA level 7). Mitaala hii inakusudia kumwezesha mhitimu kukuza uwezo wake wa kitaaluma na kitaalamu katika masomo ya Elimu ya Msingi na Sekondari na masuala mtambuka ili aweze kudhihirisha uelewa mkubwa kwenye masomo yanayofundishwa katika ngazi hizo za Elimu.



Mitaala iliyoandaliwa ni ya programu za Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Awali - Miaka 3, Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi – Miaka 3 na Stashahada ya Juu ya Elimu ya Sekondari - Miaka 3. Aidha, kwa walimu wenye Cheti (Daraja ‘A’), watasoma

Stashahada ya Elimu ya Msingi kwa muda wa miaka 2 (NTA ngazi ya 5 na 6).



Kwa kuwa Mitaala hii ni mipya na Programu za Mafunzo ni mpya, Baadhi ya vyuo vya Ualimu na Idara za Elimu za baadhi ya Vyuo Vikuu viliteuliwa kutoa mafunzo haya kwa mwaka wa masomo 2014/15. Vyuo vilivyoteuliwa kutoa Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada kwa kutumia Mitaala mipya iliyoandaliwa na NACTE kwa mwaka wa masomo 2014/15 ni vifuatavyo:




1

A: Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Awali
Na                      Chuo

1           Chuo cha Ualimu Bunda

2           Chuo cha Ualimu Butimba

3           Chuo cha Ualimu Dakawa

4           Chuo cha Ualimu Ilonga

5           Chuo cha Ualimu Kabanga

6           Chuo cha Ualimu Katoke

7           Chuo cha Ualimu Kinampanda

8           Chuo cha Ualimu Mandaka

9           Chuo cha Ualimu Mhonda
10        Chuo cha Ualimu Mpwapwa

11        Chuo cha Ualimu Mtwara Kawaida

12        Chuo cha Ualimu Mtwara Ufundi

13        Chuo cha Ualimu Murutunguru

14        Chuo cha Ualimu Nachingwea

15        Chuo cha Ualimu Singachini

16        Chuo cha Ualimu Sumbawanga

17        Chuo cha Ualimu Tandala

18        Chuo cha Ualimu Tarime

19        Chuo cha Ualimu Vikindu

B:   Stashahada ya Juu ya Elimu ya Sekondari
1           Chuo cha Ualimu Kleruu (Sayansi na Hisabati)

2           Chuo cha Ualimu Korogwe (Sayansi na Hisabati)

3           Chuo cha Ualimu Monduli (Sayansi na Hisabati)

4           Chuo cha Ualimu Songea (Lugha)

5           Chuo cha Ualimu Patandi (Elimu Maalum)

6           Chuo cha Ualimu Kasulu (Sayansi ya Jamii)

7           Chuo cha Ualimu Tabora (Sayansi ya Jamii)

8           Chuo cha Ualimu Tukuyu (Sayansi ya Jamii)
C: Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Msingi
1    Chuo cha Ualimu Morogoro
2

2      Chuo cha Ualimu Marangu

3       Chuo cha Ualimu Bustani

4       Chuo cha Ualimu cha Aggrey

5       Idara ya Elimu ya Chuo cha Al Haramain

6       Chuo cha Ualimu Capital

7       Chuo Cha Ualimu Kisanga

8       Idara ya Elimu ya Chuo cha Green Bird

9       Idara ya Elimu ya Chuo cha Hagafilo

10       Idara ya Elimu ya Chuo cha Mount Sinai

11       Idara ya Elimu ya Chuo cha St. Rock

12       Chuo cha Ualimu cha Paradigms

13       Chuo cha Ualimu Singida

14       Idara ya Elimu ya SAUT – Kampasi ya Mwanza
15       Idara ya Elimu ya St. John's University – Kampasi ya St. Marks-DSM

16         Idara ya Elimu ya St. Joseph University – Kampasi ya Arusha

17         Idara ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro
18.    Chuo cha Idara ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dodoma
D: Stashahada ya Kawaida ya Elimu ya Sekondari (Sayansi)
1
Chuo cha Elimu katika Chuo Kikuu cha Dodoma





TANBIHI: Chuo chochote ambacho hakimo katika orodha hii hakiruhusiwi kutoa Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada kwa kutumia Mitaala mipya iliyoandaliwa na NACTE kwa mwaka wa masomo 2014/15. Aidha, utaratibu unaandaliwa kwa ajili ya kuongeza idadi ya vyuo vitakavyotoa mafunzo hayo kwa mwaka wa masomo 2015/16 iwapo vitakidhi vigezo husika.


IMETOLEWA NA:

KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

04/12/2014




3

 
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger