Thursday 18 December 2014

UTEUZI KUTOKA IKULU:WILLY KITIMA ATEULIWA KUWA MSAAIDIZI WA RAIS NYARAKA

...
INNOCENT-THE BLOGGER-BOY



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ateuliwa Msaidizi wa Rais
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Willy Kitima kuwa Msaidizi wa Rais – Nyaraka (Documentation) kuanzia Alhamisi iliyopita, Desemba 11, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kitima alikuwa Mratibu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Biashara nchini yaBusiness Action Against Corruption (BAAC) Tanzania.
Taasisi hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Madola na Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (PCCB) na Taasisi ya Uendelezaji Sekta Binafsi nchini ya PPSF.
Bwana Kitima pia amewahi kuwa Mkrugenzi Mtendaji wa Shirika la Kufutilia Nyendo za Rushwa Kimataifa laTransparency International (TI) nchini. Aidha, ana ujuzi wa shughuli za benki na vyombo vya habari.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

17 Desemba, 2014
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger