Tuesday, 30 June 2020

CSR Project | TECNO Mobile Tanzania Kutembelea Kituo Cha Watoto Yatima

TECNO MOBILE TANZANIA
P.O.BOX
DAR ES SALAAM, 
TANZANIA
25/06/2020

PRESS RELEASE: Tecno Mobile Tanzania Kutembelea Kituo Cha Watoto Yatima
Mnamo tarehe 27 Juni mwaka huu Tecno Mobile Tanzania kwa kushirikiana na Startimes Tanzania ilitembelea  kituo cha watoto yatima kilichopo Chanika hapa hapa jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa misaada mbalimbali ikiambata na elimu ya masuala ya kiafya ambapo pia watapata vifaa vya kujikinga na virusi vya homa ya mapafu (covid-19) pamoja na ushauri wa ujasiriamali.
 
Tecno Mobile Tanzania imedhamiria kuwasaidia na kuwaelimisha watoto hao juu ya masuala mbalimbali ya kifedha, ujasiriamali na elimu ya afya juu ya kujikinga na homa ya mapafu (covid-19) na kwa kuhakikisha hayo yanakwenda vizuri tulikua na mtaalamu wa saikolojia hapa nchini MC Anthony Luvanda pamoja na shirika lisilo la kiserikali lijulikanalo kama ‘Her Initiative’.
 
Pia sisi kama Tecno Mobile Tanzania tumedhamiria kutoa misaada mbalimbali  kama tulivyoainisha awali lakini hatutoishia kwa watoto pekee kwa sababu tunatambua uwepo wa wafanyakazi wa kituo husika ambao watapata pia vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona unaosababishwa na virusi vya homa ya mapafu (covid-19)
 
Washirika wetu Startimes Tanzania wamedhamiria kuwasaidia watoto hawa kwa kuwapa kingamuzi kipya chenye kifurushi cha mwaka mzima kitakachoonyesha channel zinazotoa mafundisho kwa ajili ya watoto. Shirika tajwa hapo juu lisilo la kiserikali linategemea kuwaacha watoto hawa na elimu ya afya nzuri, kujitambua pamoja na ujasiriamali.
 
Kwa kumalizia tungependa sana kuwashukuru washirika wetu wote waliokubali kushirikiana nasi katika siku hii muhimu sana kwa kampuni yetu inayojali jamii yetu pendwa inayotuzunguka.
 
Asanteni sana
Tecno Mobile Limited
Tanzania.
MWISHO





Share:

Waziri Simbachawene Ashangaa Magari Ya Sekondari Ya Magereza Kusajiliwa Namba Binafsi, Atoa Siku Moja Apewe Taarifa

Na Mwandishi Wetu, Pwani.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Sekondari Bwawani ambayo inamilikiwa na Jeshi la Magereza na kubaini madudu ikiwemo magari ya Jeshi yamesajiliwa kwa namba binafsi.

Waziri Simbachawene alianza ziara yake kwa kutembelea Gereza la Kilimo Ubena na baadaye kuelekea katika shule hiyo ambazo zote zipo jirani ndani ya Kata ya Bwawani Mkoani Pwani.

Akizungumza na uongozi wa shule hiyo, Simbachawene alisema Sekondari hiyo ni mali ya umma lazima mali za shule hizo zisajiliwe kwa namba za Jeshi la Magereza zinazojulikana kwa kifupisho cha MT (Magereza Tanzania).

Alisema haiwezekani magari matatu ikiwemo ya Mkuu wa Shule hiyo imesajiliwa kwa namba binafsi, lori pamoja na gari lingine mali ya shule hiyo, kitendo hicho ni uvunjifu wa taratibu za serikali na anahitaji kupewa taarifa ya maandishi.

“Mkuu wa Gereza Ubena wewe ndio kiongozi hapa, nakuagiza umfikishie ujumbe CGP (Kamishna Jenerali wa Magereza), ifikapo kesho mchana nipate taarifa ya shule hii ikiwemo kwanini magari ya Jeshi yamesajiliwa kwa namba ‘private’ (binafsi), na pia nipate CV za walimu wa shule hii pamoja na watumishi wote,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, “inawezekana shule hii ikawa nikijiwe fulani ambacho watu wanajipatia fedha, mpaka magari wanasajili kwa namba private ili wafanyie nini?, gari la serikali tunajua hata kama itakua inasomba mawe, lakini sio ajabu hiyo gari inafanya kibarua huko mtaani inafanya vibarua vya watu, inabeba matofali, unaitofautisha vipi na magari mengine, siwezi kuhukumu moja kwa moja naomba nipate taarifa ya maandishi kutoka kwa CGP kupitia kwako.”

Waziri Simbachawene kutokana na mapungufu hayo aliyoyaona, alitaka kujua zaidi ufaulu wa wanafunzi wanamaliza masomo yao, pia alitaka kujua mapato na matumizi ya shule hiyo ambayo amesema inamazingira mazuri, eneo zuri lakini uongozi umeshindwa kuiitangaza na haina umaarufu wowote hapa nchini.

Kwa upande wake Makamo Mkuu wa Shule hiyo, Solomon Mwambingu alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1981, na kuhusu ufaulu inafanya vizuri kuanzia kidato cha nne hadi cha sita.

“Shule inafanya vizuri kitaaluma, matokeo ya kidato cha pili kwa mwaka jana 2019 wanafunzi wote walifaulu, pia kidato cha nne walifanya vizuri na matokeo ya kidato cha sita wanafunzi wote walifaulu na hakukua na hakukua na daraja zero wala daraja la nne,” alisema Mwambingu.

Aidha, Waziri Simbachawene kwa upande wa Gereza la Mifugo aliwapongeza kwa kutunza mifugo iliyopo katika gereza hilo, na kuwataka kuwepo na soko la nyama kwa kuchinja ng’ombe ili waweze kuuza na kupata mapato  kupitia ufugaji wa kuvuna.

“Lazima magereza ijitegemee, gereza la mifugo halina hata nyama za kuuza, tunataka uchungaji wenye faida, kuwepo na ‘brandy’ yenu, mnaweza mkachukua mfuko mkaweka nyama na kuandika bwawani meat, na pia kuzalisha maziwa yakutosha, hivyo ndivyo kujitangaza,” alisema Simbachawene.

Pia aliwataka aliagiza kuwa, mifugo mbalimbali ng’ombe zichinjwe na nyama ziweze kutangazwa kwa kuwa na utambulisho maalumu ili kuliletea mapato Jeshi hilo kwa kuwa wana eneo hilo.

Kwa upande wake Msimamizi wa Shamba la Magereza katika Gereza hilo, Charles Masuka alisema shamba hilo lina ekari 12 ambapo wanafuga ngombe, mbuzi, kondoo na bata, hivyo shamba hilo linatoa ngombe wa nyama ambapo wanatoa kwa wahitaji.

“Tunashukuru kiongozi kwa kututembelea, ujuoio wake umetupa hamasa, na shmaba hili ni kubwa lina mifugo 2,335, shmaba hili linategemewa utoaji wa ngomnbe wa nyamba,” Masuka.

Simbachawene alimaliza ziara yake ya siku moja katika Gereza hilo, na aliwataka viongozi wa Gereza hilo wampe ushirikiano Mkuu wa Jeshi hilo, kwa kuwa na mipango mizuri ya kulipeleka mbele Jeshi hilo, na aliwataka waendelee kuchapa kazi zaidi pamoja na kuhakikisha wanajitegemea kwa chakula ili Magereza nchini yaweze kusonga mbele.



Share:

Picha : MUONEKANO WA MAJENGO YA KISASA HOSPITALI YA WILAYA YA SHINYANGA

Muonekano wa sehemu ya Majengo 8 ya Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga iliyopo katika kijiji cha Iselamagazi kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020. 

Majengo yaliyopo ni Jengo la wagonjwa wa nje (OPD), (Maabara (Laboratory), Stoo ya dawa (Pharmacy) , Mionzi (X- Ray), Wazazi (Maternity), Kuhifadhia dawa za chanjo(DVS), Kufulia (Laundry), Kuhifadhia maiti (Mortuary). 

Ujenzi ulianza Januari 4,2019 na umekamilika kwa asilimia 98 ukigharimu jumla ya shilingi bilioni 1.5 na tayari huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje (OPD) zimeanza kutolewa. 

Kwa Mujibu wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko Mboneko uwepo wa hospitali hiyo utasaidia kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua kutokana na kuchelewa kupata huduma,ambapo kwa sasa wananchi wamesogezewa huduma karibu na wataondokana na adha ya kusafiri umbali mrefu. 

“Wananchi walikuwa wanasafiri umbali mrefu kufuata huduma za hospitali katika hospitali ya rufaa ya Shinyanga zaidi ya kilometa 100 kutoka Kata ya mwisho ya Halmashauri ya Shinyanga”,amesema Mboneko. 

“Tunamshukuru Rais wetu mpendwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwakumbuka wananchi wanyonge wa wilaya ya Shinyanga kwa kuboresha huduma za afya ili wananchi wapate huduma karibu na makazi yao ili kuondoa adha ya kusafiri umbali mrefu. Na sisi tumeongezea majengo hayo mawili ya kuhifadhia maiti na jengo la dawa za chanjo kwa chenji iliyobaki, tumetumia pesa vizuri”,amesema Mboneko.
Muonekano wa Jengo la Mionzi katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Mionzi katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa majengo katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Kufulia katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Kufulia katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Kufulia (kulia),mengine ni majengo ya chanjo na stoo ya dawa (kushoto) katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Kufulia katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la maabara  katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la kuhifadhia maiti  katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Maabara katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Wazazi katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Maabara katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa Jengo la Mionzi katika hospitali ya Wilaya ya Shinyanga leo Jumanne Juni 30,2020 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:

KAMPUNI YA VEGRAB ORGANIC FARMING LTD YAZINDUA SOKO LA PILIPILI KICHAA SINGIDA




 Mkurugenzi wa Kampuni ya Vegrab Organic Farming LTD,Gladness Nyange,akizungumzia kilimo cha pilipili kichaa wakati wa uzinduzi wa zao hilo uliofanyika Kitongoji cha Kipunda,Kjiji cha Mtunduru,wilaya ya Ikungi, mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
 Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi,Gurisha Msemo akizungumza kwenye uzinduzi huo.


Mwenyekiti wa Kipunda AMCOS, Omari Nyuda, akizungumza kwenye uzinduzi huo.

 Zao la pilipili baada ya kuvunwa.
 Zao la pilipili baada ya kuvunwa.


 Wakulima wa zao la pilipili wakiwa shambani.
 Mkulima Mohemed Salehe,  akizungumzia kilimo hicho.
Mkulima Mwanaidi Iddi, akizungumzia kilimo hicho.







Na Jumbe Ismailly,  Ikungi

KAMPUNI ya  Vegrab Organic Farming LTD kwa kushirikiana na kampuni inayouza matrekta ya AGRI-COM wamezindua soko la zao la pilipili kichaa litakaloweza kuwaongezea kipato wananchi wa Kitongoji cha Kipunda,Kjiji cha Mtunduru,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo,Gladness Nyange alifafanua kwamba masoko ya zao la pilipili kichaa ni makubwa sana isipokuwa kinachotakiwa ni uzalishaji mkubwa na wenye ubora zaidi.

“Mimi nina imani na zao hili nyie mnaliona hivi lakini ni zao ambalo litatupeleka mbali sana kupitia juhudi ile tuliyoanzanayo tuendelee nayo,kwani masoko ni makubwa sana lakini yanataka uzalishaji mkubwa lakini pia wenye ubora.”alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Kwa mujibu wa Nyange Mkoa wa Singida unaweza kuwa kituo kikubwa sana cha uzalishaji wa zao la pilipili kichaa na siyo kwa Tanzania tu bali hata kwa Afrika Mashariki na kwamba endapo wataweka jitihada wanaweza kuongoza katika Afrika katika uzalishaji wa zao hilo.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa mazingira pamoja na ardhi iliyopo katika Mkoa wa Singida inadhihirisha wazi kabisa kwamba pilipili itakayozalishwa kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Singida itakuwa nzuri kuliko inayotoka sehemu yeyote ile ya Tanzania na hata Afrika Mashariki.

Akizindua mnada wa soko hilo la pilipili kichaa,Afisa ushirika wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi,Gurisha Msemo alisema Kampuni inayonunua zao hilo imesaini mkataba wa miaka mitatu na kwa msimu wa 2019/2020 kampuni hiyo itanunua pilipili kichaa iliyoiva kwa bei ya shilingi 4,500/=kwa kilo moja na shilingi 5,000/= kwa pilipili mbichi kwa kilo moja.

Aidha Msemo alitoa sababu za soko la zao hilo kuzinduliwa katika Kata ya Mtunduru kuwa ni kutokana na idadi kubwa iliyopo ya wakulima wa zao hilo ambapo kati ya wakulima 159 waliolima pilipili kichaa Mkoani Singida,110 ni wakulima kutoka wilaya ya Ikungi.

Akimkaribisha kuzindua soko hilo,Mwenyekiuti wa Kipunda Amcos,Omari Nyuda huku akitumia kauli mbiu isemayo ongeza tija pilipili inalipa,alisisitiza juu ya uzalishaji bora wa zao hilo ili waweze kuendelea kupata fedha nyingi zaidi.

“Zao hili ambalo limekuwa na tija kwetu na kauli mbiu tunasema ongeza tija pilipili inalipa mradi na msimu umeshazinduliwa,kwa hiyo yetu ni mapesa,tupate pesa tuongeze uzalishaji tuongeze zao ubora zaidi tuweze kusonga mbele zaidi.”alifafanua Nyuda ambaye ni mwenyekiti wa Kipunda Amcos.


Share:

LIVE: Rais Magufuli Akirudisha Fomu Ya Kugombea Urais Kupitia CCM

Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, arudisha fomu ya kugombea nafasi ya Urais kupitia chama chake cha (CCM) katika Ofisi ya CCM, White House Dodoma.

==>>Tazama hapo chini


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JULAI 30,2020


 













Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger