MKAZI wa mtaa wa Mageuzi, kata ya Ngokolo, manispaa ya Shinyanga,
Ibrahimu Daniel (42) amemuua mke wake, kwa kushindwa kuhifadhi vizuri
kachumbari na kupika mboga isiyo na kiwango.
Friday, 20 January 2017
RATIBA YA KUHAMIA DODOMA IPO PALEPALE
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amesema ratiba ya kuhamia Dodoma kwa
mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na manaibu iko palepale.
Amesema watakaoshindwa kufanya hivyo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
atatoa mwongozo. Jenista alisema jana kuwa baada ya Februari 28, mwaka
huu kutafanyika tathimini na kuangalia utekelezaji wake umefikia wapi,
na kwamba kwa wale ambao hawatatekeleza agizo hilo, Waziri Mkuu Majaliwa
atatoa mwongozo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Jenista alisema uamuzi ulitolewa na Rais John Magufuli uko palepale.
Alisema hata Waziri Mkuu amekuwa akisisitiza ratiba ya kuhamia Dodoma
kwa awamu ya kwanza Februari mwaka huu ambayo itahusisha mawaziri,
manaibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu wao na baadhi ya watumishi
wa wizara.
"Kazi yetu itakuwa ni kuangalia utekelezaji utakuwa umefikia wapi na
asiyetekeleza Waziri Mkuu atatoa mwongozo,” alisema Jenista.
Pia alisema amekuwa akikagua nyumba ambazo zinafanyiwa ukarabati kwa
ajili ya watumishi watakaohamia Dodoma ikiwemo nyumba za Mamlaka ya
Ustawishaji Makao Makuu (CDA) eneo la Kikuyu, ambapo ukarabati wake
unaendelea vizuri.
Alisema nyumba hizo za ghorofa, zitawezesha baadhi ya watumishi
kupata nyumba za makazi, ambapo pia taasisi nyingine zinaendelea na
ujenzi wa nyumba za watumishi.
Julai mwaka jana, Rais Magufuli alitangaza kuhusu serikali yake
kuhamia Dodoma kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa kwanza wa miaka
mitano, na tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikwisha kuhamia katika
makao makuu hayo ya nchi yaliyotangazwa mwaka 1973.
Akiahirisha Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 mwishoni mwaka jana, Waziri
Mkuu Majaliwa alisema serikali itahamia Dodoma kwa awali, na kueleza
kuwa awamu ya kwanza itakuwa kati ya Septemba 2016 hadi Februari, 2017
ikiwahusisha Waziri Mkuu, mawaziri, makatibu wakuu, manaibu makatibu
wakuu na walau idara mbili za kila wizara.
Alisema awamu ya pili itakuwa Machi 2017 hadi Agosti 2017, ya tatu
Septemba 2017- Feb 2018, ya nne Machi 2018- Agosti 2018, na ya tano
Septemba 2018-Februari 2019; na kwamba awamu hizo zitatumika kwa ajili
ya kuendeleza mchakato wa kuhamisha watumishi hadi wote wawe wamehamia
Dodoma.
WANAFUNZI WANAOSOMEA DIPLOMA KUANZA KUPEWA MIKOPO KUTOKA BODI YA MIKOPO
SERIKALI imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada
katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua
elimu husika.
Thursday, 19 January 2017
PICHA: Rais Magufuli Alivyomuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma Kuwa Kaimu Jaji Mkuu Wa Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Januari 18, 2018. Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Januari 18, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Januari 18, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria
na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Januari 18, 2018.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika
picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama kuu
baada ya kumuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu
wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Januari 18, 2018.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika
picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama baada ya kumuapisha Profesa
Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar
es salaam Jumatano Januari 18, 2018.
JESHI LA SENEGAL KUIVAMIA GAMBIA USIKU WA KUAMKIA LEO ILI KUMNG'OA RAIS YAHYA JAMMEH ALIEOGOMA KUACHIA MADARAKA
Jeshi
la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala
la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha
Jammeh ambayo ni leo ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu
uliofanywa mwezi uliopita.
Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.
Rais
wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz yuko nchini Gambia kwa kile
kilichotajwa kuwa ni juhudi za mwisho za kumshauri bwana Jammeh kuachia
madaraka kwa Rais mteule wa Gambia Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko
nchini Senegal.
Senegali
imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa
nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika
kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.
Chanzo: BBC
Wednesday, 18 January 2017
Tuesday, 17 January 2017
Nogesha Upendo Ya Vodacom Yaja Na Tsh Bilioni 32 Za M-pesa
Wakati
wateja na wananchi mbalimbali wakiendelea kunufaika na promosheni ya
Nogesha Upendo ya Vodacom katika kujishindia mamilioni ya fedha kila
siku pindi wanunuapo vifurushi kwenye simu zao, sasa malipo ya faida ya
kutumia M-Pesa ambayo yameanza wiki hii yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya
kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja na mawakala wa M-Pesa.
Awamu
hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh
Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri
ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya
akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na
yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya
Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio
hilo kampuni hiyo imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu
zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, ni zaidi
ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya
wateja wetu.
“Ugawaji
huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni
muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila
mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo
atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua
vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake.
Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa “zaidi
la faida” Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Kuona
kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea
SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako.
Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa
kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa
uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha
chagua kifurushi unachohitaji.
Promosheni
ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200
washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda
Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi
za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua
kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa
moja.