Saturday, 20 September 2025

JAJI MWAMBEGELE AFANYA UKAGUZI WA VIFAA VYA UCHAGUZI MBEYA



Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele Septemba 19, 2025 ametembelea Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika Majimbo ya Uchaguzi ya Mbeya Mjini na Uyole na kupokea taarifa ya mkoa kutoka kwa wasimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya. Jaji Mwambegele pia alipata fursa ya kutembelea kampeni za wagombea Ubunge wa chama cha CUF na CCM katika majimbo hayo.


Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume,Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.


"Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"






Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya ambapo alisisitiza uadilifu wakati wa utendaji kazi wao.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na Wasimamizi wa Uchaguzi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
Share:

Friday, 19 September 2025

DKT. TULIA : SERIKALI IMEJIPANGA KUBORESHA MIUNDOMBINU NA HUDUMA ZA JAMII KISHAPU

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson akimtambulisha Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe Lucy Thomas Mayenga(kulia) Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela Wilayani KishapuSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela.

Na Suma Salum – Kishapu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, amefanya ziara Wilayani Kishapu, Mkoani Shinyanga ambapo amezungumza na Wananchi kuhusu mipango ya maendeleo iliyomo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uchaguzi ya mwaka 2025/2030.

Katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela, Spika Tulia amewataka Wananchi wa Kishapu kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu ujao, akibainisha kuwa ni njia pekee ya kuchagua viongozi wanaowaamini kuwaletea maendeleo.

"Ndugu zangu wa Kishapu Ilani ya CCM imebainisa mambo mengi mtakayonufaika nayo wakazi wa eneo hili hasa changamoto yenu ya Barabara ya Kolandoto -Mhunze Itatengenezwa Kwa kiwango Cha lami ili kuongeza kipato Kwa Wananchi kutokana na kufanya Kazi bila kikwazo Cha miundombinu" amesema Tulia

Katika hotuba yake, Spika Tulia amewafikishia wananchi salamu kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwashukuru kwa uvumilivu wao na namna wanavyoendelea kuiamini Serikali katika kusimamia maendeleo ya Taifa.

Aidha, amewaahidi wananchi wa Kishapu kuwa Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya, kuimarisha miundombinu ya barabara, kuinua kiwango cha elimu, kupeleka huduma za maji safi na salama, pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme Kwa kila Kitongoji na unaongezeka.

Mhe. Tulia amewatambulisha rasmi kwa Wananchi,Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kishapu kupitia CCM, Mhe. Lucy Thomas Mayenga, pamoja na wagombea udiwani wa Kata zote 29 zinazounda Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Akizungumza baada ya utambulisho huo, Mhe. Lucy Mayenga amekishukuru Chama Chake kwa imani waliyoonyesha kwake kwa kumpa nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM. Ameahidi kuwa endapo Wananchi watampa ridhaa ya kuwa Mbunge wao, atahakikisha analeta maendeleo yenye tija yanayogusa maisha ya kila mmoja.

“Nataka niwahakikishie Wananchi wa Kishapu, nikipewa nafasi ya kuwa mwakilishi wenu, nitashirikiana nanyi bega kwa bega kuhakikisha huduma bora za jamii zinapatikana kwa wakati na miradi ya maendeleo inatekelezwa ipasavyo,” amesema Mayenga.

Vilevile, Mhe. Lucy Mayenga amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, kwa usimamizi mzuri ndani ya Wilaya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bw. Emmanuel Johnson, kwa kusimamia ipasavyo matumizi ya fedha za serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ziara ya Spika Tulia Akson Kishapu imeendelea kuongeza hamasa ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ifikapo Oktoba 29 ambapo wananchi wamehimizwa kushiriki kwa amani na mshikamano.Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe Lucy Thomas Mayenga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa 31 wa Umoja wa Mabaraza ya Kitaifa Duniani (IPU) Mhe.Dr Tulia Ackson na Wananchi wa Wilaya hiyo mnamo Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela.Mgombea Udiwani Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Joel Ndettoson kwatiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa 31 wa Umoja wa Mabaraza ya Kitaifa Duniani (IPU) Mhe.Dr Tulia Ackson na Wananchi wa Wilaya hiyo mnamo Septemba 19,2025 katika Viwanja vya Mabela.
Share:

MWANA FA KUSHUGHULIKIA MAWASILIANO YA SIMU JIMBO LA MUHEZA





Na Mwandishi Wetu, Muheza

MGOMBEA ubunge Jimbo la Muheza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA amesema katika miaka mitano ijayo atahakikisha anaongeza minara ya simu ili Jimbo la Muheza liweze kuwa na mawasiliano katika maeneo ambayo yana changamoto hiyo.


Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kwezitu tarafa ya Amani, MwanaFA alikiri kwamba yapo maeneo katika Jimbo hilo, yana changamoto ya ukosefu wa mawasiliano.



"Katika miaka mitano ijayo tutaimarisha mawasiliano ya simu...Moja ya mambo yanayonisikitisha ni kufika baadhi ya maeneo kwenye Jimbo la Muheza ikawa simu haiwezi kushika mawasiliano, huwezi kupigiwa simu," alisema na kuongeza,

"Tunachotaka kufanya ni kuhakikisha tunaongeza minara ya simu ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi wetu,".



MwanaFA ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2020-2025 Jimbo hilo lilipata minara Saba ambayo kutokana na jiografia ya Jimbo hilo, bado haijakidhi mahitaji ya mawasiliano katika maeneo mengi kutokana na hali hiyo.

Hivyo, alisema anakwenda kuzifanyia kazi kuhakikisha minara ya simu inaongezeka na hali ya mawasiliano inazidi kuimarika katika Jimbo hilo.



"Sitaki kuahidi mambo mengi na nikashindwa kuyatekeleza lakini niwahakikishie jambo moja changamoto zote za kata ya Kwezitu, Jimbo la Muheza kwangu ni kipaumbele...Miaka mitano hii nimejua kona zote za kutatua changamoto zilizopo katika Jimbo letu," alisema.

Aliwaomba wananchi wa Kwezitu kufanya kazi mbili ambazo ni kwenda kupiga kura Oktoba 29 na kuwachagua wagombea wa CCM ili waweze kumalizia kazi ambazo wamezifanya katika miaka mitano iliyopita.



Alisema wananchi wa Kwezitu wanakila sababu za kumchagua Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa ameleta fedha nyingi katika kata hiyo na Jimbo zima la Muheza.

Rais ameleta fedha nyingi katika miradi ya afya, elimu, maji, barabara na miradi mingine hivyo anastahili kupigiwa kura nyingi katika Jimbo letu.

"Nichagueni na Mimi miaka mitano hii nimeisema wilaya hii, hatuwezi kusema matatizo yetu yote tumeyamaliza bali dhamira yetu ni ya dhati kwakuwa kila sekta tumeigusa," alisema na kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Mch. John Mzalia awe diwani wa kata hiyo.



Akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo Mgombea udiwani Mch Mzalia alisema kuwa kata hiyo imepata miradi mingi kuliko wakati wowote ule ikiwemo miradi ya Elimu, afya, barabara na huduma za jamii.

"Tumepata mradi wa Boost ambao shule yetu ya Kwezitu imekuwa nzuri mno hadi watoto wetu wanasoma kwenye shule ya vioo wakati mwingine wanachungulia kwenye madirisha hayo kama watoto wa Kihindi," alisema na kuwaomba wananchi hao wawachague wagombea wa CCM.

Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng'ese amewataka viongozi wa CCM wa ngazi zote za kata hiyo kuhakikisha wanatoka na kwenda kwa wananchi kuomba kura za wagombea wa CCM ili kukifanya chama hicho wagombea wake kupata kura za kishindo.



"Viongozi wa kata, matawi, mashina, mabalozi mtoke kwenda kuomba kura kwa wananchi katika maeneo yenu, haya ni maagizo nawapa mwende kukifanya chama chetu na wagombea wetu waweze kupata kura nyingi," alisema Leng'ese.

Meneja wa kampeni wa mgombea wa Jimbo la Muheza Aziza Mshakang'oto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Muheza (UVCCM), amewataka wananchi wa kata ya Kwezitu wasifanye makosa kwa kuwachagua wagombea wa upinzani kwakuwa hawana jipya.

Alisema CCM imekuja na ilani ambayo kwa wilaya ya Muheza imekuwa na miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo hilo hivyo wasifanye makosa katika uchaguzi huo.

Mwisho
Share:

TBS YAZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amezindua maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kuliagiza shirika hilo kutumia maadhimisho hayo kama fursa ya kutangaza huduma zao.

Uzinduzi huo umefanyika Septemba 18,2025 katika ofisi za TBS zilizopo Ubungo Jijini Dar es Salaam ambapo Dkt. Abdallah amesema shirika hilo linafanya kazi kubwa ya kuhakikisha viwango vya ubora wa bidhaa unafikiwa.

Amesema kaulimbiu ya maadhimisho hayo yanayotarajia kuhitimishwa desemba mwaka huu, yana kaulimbiu ya "Uhamasishaji Ubora na Usalama kwa Maisha Bora" ambayo itasaidia kuendelea kujenga uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa uzingatiwaji wa viwango vya ubora na uimarishwaji wa bidhaa na huduma za viwango.

Amesema katika kipindi cha miaka 50, TBS imepiga hatua kubwa ikiwe kupanua wigo wa utoaji huduma na kuzisogeza kwa wananchi pamoja na kuboresha mifumo ya kielektroniki.

"Katika kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, TBS imejenga heshima kubwa kimataifa kutokana na utekelezaji mahiri wa majukumu yake kwa kupata tuzo mbalimbali ikiwepo ya Mdhibiti Bora Barani Afrika na kupata daraja la juu la Shirika la Afya Duniani (WHO), kuwa wa kwanza SADC kupata Ithibati ya Kimataifa ya uthibitishaji ubora, na ilifanikiwa kupata Ithibati ya kimataifa ya mfumo wa usimamizi wa chakula" amesema Dkt. Abdallah.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt. Ashura Katunzi amesema maadhimisho hayo yatakuwa na mafanikio makubwa ikiwepo viwango vya Marathon na viwango vya business forum, na kilele cha maadhimisho hayo ambayo yatawakutanisha wadau zaidi ya mia tano wa masuala ya ubora wa viwango, viwanda na biashara kutoka ndani na nje ya nchi, uzinduzi wa kitabu cha historia ya TBS na maonesho ya biashara.
Share:

KADOGOSA AANZA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA BARIADI VIJIJINI.. AAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA, MIUNDOMBINU NA UWEZESHAJI VIJANA


Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa kampeni zake za kuwania ubunge wa jimbo hilo.
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa, akizungumza na wananchi wa Ngulyati katika mkutano wa kampeni kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi ili achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Wananchi wakiendelea kufuatilia sera za mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa katika mkutano wake wa kampeni.
Wananchi wakiendelea kufuatilia sera za mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa katika mkutano wake wa kampeni.
Wananchi wa kijiji cha Ngala wakimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa katika mkutano wa kampeni alioufanya kijijini hapo kwa ajili ya kunadi sera zake ili achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Wananchi wa Ngulyati waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kisikiliza sera za mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa.

****
Na Annastazia Paul, Simiyu

Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Masanja Kadogosa, ameanza rasmi kampeni zake kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi wa jimbo hilo, ili waweze kumchagua na kuwa mbunge wa jimbo hilo ambapo ameahidi kuzishughulikia na kuzitatua changamoto zinazowakabili wakulima katika uuzaji wa mazao, miudombinu ya barabara pamoja na uwezeshaji vijana katika jimbo hilo ili kuwasaidia wananchi kuwa na maisha bora, kupitia shughuli zao mbalimbali wanazozifanya.

Kadogosa ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ngala na Ngulyati vilivyopo kata ya Ngulyati jimbo la Bariadi vijijini na kueleza kuwa changamoto hizo zimekuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo na kwamba zitakapotatuliwa zitachochea maendeleo jimboni hapo.

"Suala la mazao, suala la kilimo ndio maisha yetu haya, kwahiyo ndugu zangu nataka mniamini, chama cha mapinduzi hakijakosea kunileta, haya tutayazungumza ya kimfumo tutayabadilisha ili kuhakikisha wakulima wananufaika na uzalishaji wao" ,amesema Kadogosa.

Aidha ameeleza namna ambavyo ilani ya CCM ya mwaka 2025 - 2030 itazishughulikia changamoto za miudombinu ya barabara katika kata ya Ngulyati.

"Tuna barabara yetu ya kutoka Bariadi - Salama inakutana na wenzetu wa Magu, kilomita 76 hiyo barabara ni muhimu sana, kazi yangu ni kufuatilia na kuhakikisha inajengwa pamoja na daraja katika mto Bariadi, na tutaimarisha ile barabara ya kutoka Gambosi kwenda Ikungulyabashashi hadi Dutwa", amesema Kadogosa

Kuhusu uwezeshaji wa vijana Kadogosa ameeleza namna ambavyo ataanzisha program zitakazowasaidia vijana kuimarisha uchumi wao.

"Vijana wanasoma si ndio? Wanamaliza shule hawana ajira, tatizo hili ni la kidunia, lakini lina majibu yake tutakuwa na miradi, pamoja na ile mikopo ambayo inatolewa kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu, lakini tutakuwa vile vile na program kwa vijana wetu ambao wanataka kufanya kazi, tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba vijana wetu wana kitu wanachokifanya vijijini huku huku, mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshasema katika siku 100 za uongozi wake atatoa bilioni 200 nchi nzima kwa ajili ya vijana tu na wajasiriamali, mimi kazi yangu ni kuibua miradi kwa vijana wenzangu" ,amesema Kadogosa.

Kadogosa ataendela na kampeni kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi wa jimbo la Bariadi vijijini ili wamchague na kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger