Saturday, 23 August 2025

CCM YAVUNJA REKODI:SURA MPYA, SURA ZILIZOREJEA NA WALIOSHUKA



Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Katika kile kinachotajwa kuwa ni mojawapo ya maamuzi muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza rasmi majina ya wanachama wake walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia majimbo mbalimbali na viti maalum.

Taarifa hiyo imetolewa leo, Agosti 23, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa – Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, kufuatia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichofanyika kwa lengo la kupitisha uteuzi wa mwisho.

katika mkoa wa Arusha, jina lililovuta hisia za wengi ni Paul Makonda, aliyeteuliwa kugombea Ubunge wa Arusha Mjini – hatua inayotafsiriwa na wachambuzi kama "comeback" ya kisiasa kwa aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Joshua Nassari, ambaye zamani alikuwa mbunge kupitia upinzani na baadaye kujiunga na CCM, naye amepitishwa kuwania tena Ubunge wa Arumeru Mashariki, hatua inayoonesha msimamo wa chama kuvuta na kuwekeza kwa wanasiasa waliobobea hata kutoka nje ya mfumo wake wa awali.

Majina mengine yaliyopitishwa Arusha ni pamoja na Dkt. Johannes Lukumay – Arumeru Magharibi,Daniel Tlemah – Karatu,Dkt. Steven Kiruswa – Longido,Isack Copriao – Monduli na Yannick Ndoinyo – Ngorongoro.

Kwa Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kuwa eneo lenye mvuto mkubwa kisiasa, na safu ya walioteuliwa mwaka huu inadhihirisha mchanganyiko wa sura zile zile zenye uzoefu wa muda mrefu serikalini na ndani ya chama.

Prof. Kitila Mkumbo, aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Mbunge wa Ubungo, amerudi tena kuwania jimbo hilo.

Aidha, wabunge wakongwe kama Bonnah Kamoli (Segerea), Mussa Zungu (Ilala), na Jerry Silaa (Ukonga) wameendelea kuaminiwa na CCM na kupitishwa tena.

Kwa upande wa vijana, Geofrey Timoth (Kawe) na Kakulu Buchard (Mbagala) ni miongoni mwa sura mpya zilizopitishwa – ishara kuwa CCM inaendelea kujenga kizazi kipya cha wanasiasa.

Majina mengine yote ya Dar es Salaam ni Haran Sanga – Kigamboni,Angellah Kairuki – Kibamba,Prof. Kitila Mkumbo – Ubungo,Mariam Kisangi – Temeke
,Abdallah Chaurembo – Chamazi,Kakulu Buchard – Mbagala,Geofrey Timoth – Kawe,Abbas Gulam “Tarimba” – Kinondoni,Mussa Zungu – Ilala,
Jerry Silaa – Ukonga, Bonnah Kamoli – Segerea na Dougras Masaburi – Kivule

WAONGOZAJI WA KURA ZA MAONI WAKATWA – WAPYA WAIBUKA

Katika hali ya kushangaza baadhi ya waliokuwa vinara wa kura za maoni hawakurejeshwa kwenye uteuzi wa mwisho, hali iliyoacha maswali na mijadala miongoni mwa wanachama.

Waliokosa uteuzi licha ya kuongoza kura za maoni ni pamoja na Ummy Mwalimu – aliyekuwa Mbunge wa Tanga Mjini,Samuel Malecela – mshindi wa kura za maoni Dodoma Mjini

Katika jimbo la Kigoma Mjini, jina lililoibuka ni la Clinton Revocutus maarufu kama Baba Leo, ambaye amepitishwa licha ya kutokuongoza kwenye kura za maoni.

Majimbo mengine yaliyoshuhudia mabadiliko makubwa ni Tarime Mjini – Ester Matiko,Bunda Mjini – Ester Bulaya,Urambo – Magreth Sitta,Vwawa – Exaud Kigahe (Naibu Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara)

WALIOPENYA KWENYE ORODHA YA MABADILIKO

Miongoni mwa waliopenya kwenye uteuzi huo wa mwisho ni
Paul Makonda – Arusha Mjini Nape Nnauye – Mtama,Kangi Lugola – Mwibala,Livingston Lusinde – Mvumi,Isaya Moses – Kongwa (akitwaa nafasi ya Hayati Job Ndugai)


MABADILIKO YA VIONGOZI WA JUU NDANI YA CCM

Katika kikao hicho pia, CCM imetangaza mabadiliko ya kiutendaji ndani ya chama ambapo Dk. Asha-Rose Migiro amepitishwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, akichukua nafasi ya Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye sasa ni mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya chama hicho.

Kenani Kihongosi ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Amos Makalla. Makalla ametoa wito kwa waandishi wa habari kumpa ushirikiano Kihongosi kama walivyompa yeye.

Joshua Milumbe ameteuliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM

Kutokana na hatua hiyo Wachambuzi wa siasa wanasema uteuzi wa mwaka huu ni wa kuvutia, ukijumuisha mabadiliko ya kizazi, uhamasishaji wa sura mpya na uimarishaji wa uongozi wa chama kwa kuteua viongozi wenye maono mapya.

Pia, uteuzi huu umeashiria juhudi za chama kuongeza uwakilishi wa jinsia na maeneo mbalimbali nchini.










Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 23,2025



Magazeti










Share:

Friday, 22 August 2025

WAANDISHI WA HABARI WAHAMASISHWA KUJILINDA WAKITIMIZA MAJUKUMU YAO




NA HAJI NASSOR, PEMBA

WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa kuzingatia ulinzi na usalama wao kwanza ,wanapokuwa katika majukumu yao ya kazi, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa vyama vingi nchini.

Akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari, huko katika ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani Chake chake Pemba, mkufunzi wa mafunzo hayo Mwandishi Maryam Nassor ambaye amejengewa uwezo na Umoja wa vilabu vya waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na yeye kutakiwa kuipeleka elimu hiyo kwa waandishi wengine.


Mkufunzi huyo, amesema kuwa, ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari unaanza na mwandishi mwenyeye , hivyo kuwataka waandishi hao kuwa makini wanapotimiza majukumu yao.


“ Waandishi wa Habari lazima Kujifunza kusoma mazingira kwa haraka (kama vile maandamano au machafuko) ili kubaki salama wakati munatimiza majukumu yenu”


Amesema kuwa, tafiti zinaonesha katika kipindi hichi waandishi wengi huingia matatizoni na wengine kupoteza maisha.


Aidha ameongeza kuwa, ni vyema waandishi wa Habari kutoa taarifa kwa watu wao wa karibu , wanapokwenda kwenye kazi hatarishi, ili kuepuka hatari zinazoweza kujitokeza endapo watapatwa na hatari wakiwa pekee yao.


“ Ulinzi na Usalama wa mwandishi wa Habari huanza na mwandishi mwenyewe hivyo ni lazima kutambua mazingira tunayofanyia kazi na watu tunaofanya nao kazi, ili kujihakikishia Ulinzi na Usalama wakati tunatimiza majukumu yetu”, amesema.

Aidha amewataka waandishi wa Habari Kujua namna ya kushughulikia msongo wa mawazo baada ya kazi (trauma) na kupata muda wa kupumzika.


Mkufunzi huyo, amewaasa Waandishi wa habari kupata elimu ya saikolojia kwa sababu taaluma yao inawahusisha moja kwa moja na mazingira yenye changamoto nyingi za kiakili, kihisia, na kijamii.

Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mafuzo hayo, Fatma Hamad mwandishi wa blog ya Pemba ya leo na Is’haka Mohamed wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha usalama wao sehemu za kazi.

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo Salum Hamad, amesema mafunzo hayo yamemuongezea uwelewa mkubwa wa kujua mipaka yake kama mwandishi katika kutekeleza majukumu yake.

Mafunzo hayo, ya ulinzi na usalama wa kimwili, kimtandao na kisaikolojia yametolewa kwa baadhi ya waandishi wa Habari wa klabu ya waandishi wa Habari ya Pemba (PPC).
Share:

MUME WANGU ALIMWANDIKISHA MPANGO WA KANDO KATIKA BIMA YA AFYA LEO ANANIOMBA RADHI KILA SIKU


Wakazi wa Mbezi Beach, Dar es Salaam walishtuka baada ya mwanamke mmoja kugundua kuwa mume wake alikuwa amemwandikisha mwanamke mwingine kwenye bima ya afya ya kampuni alikofanya kazi akimwita “mke wake wa ndoa.” Tukio hilo lilizua taharuki kwa familia hiyo, huku likizua mjadala mkubwa kwenye makundi ya wanawake mtandaoni.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAAAGOSTI 22,2025


Magazeti


















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger