Monday, 28 July 2025

WAFANYAKAZI WA BARRICK WALIVYOSHIRIKI NBC DODOMA MARATHON 2025

Wafanyakazi wakifurahia baada ya kumaliza mbio za NBC Dodoma Marathon

***
Kwa mara nyingine tena wafanyakazi wa Kampuni ya Barrick nchini wameshiriki katika mbio za riadha za NBC Dodoma Marathon 2025 zilizofanyika mkoani Dodoma kwa lengo la kuchangisha fedha za kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya katika jamii nchini, ambapo wamemudu kukimbia mbio za masafa mbalimbali.

Kampuni ya Barrick nchini imekuwa na program za mazoezi kwa ajili ya kuhakikisha wafanyakazi wake wanakuwa na nguvu na afya bora.

Kila mwaka kampuni imekuwa ikiwezesha wafanyakazi wake kushiriki riadha mbalimbali na michezo ndani na nje ya nchi ikiwemo mbio za kilomita 42 za Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon zinayofanyika kila mwaka.

Migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu pia imewekeza kujenga miundombinu ya michezo na mazoezi ili kuwawezesha wafanyakazi wake kushiriki michezo na mazoezi katika mazingira rafiki kwa ajili ya kujenga afya zao.

Lengo kuu la mbio hizi zilizowashirikisha maelfu ya wakimbiaji kwa mujibu wa waandaaji Benki ya NBC lilikuwa ni kukusanya fedha ili kusaidia mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi , kutoa ufadhili wa elimu kwa wakunga ili kusaidia watoto wenye changamoto ya ugonjwa wa usonji na kampeni dhidi ya Saratani ya kizazi na jumla ya shilingi milioni 700 zilipatikana.
Picha mbalimbali za wafanyakazi wakifurahia baada ya kumaliza mbio za NBC Dodoma Marathon
Share:

Sunday, 27 July 2025

UCHAGUZI MKUU 2025: WANAWAKE WAMEJITOKEZA, VYAMA VIWATEUE


Wadau wa masuala ya wanawake na uongozi wamevitaka vyama vya siasa nchini kuhakikisha vinawateua wanawake waliokidhi vigezo kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, hususan kwenye nafasi za uwakilishi, ubunge na udiwani zinazoshindaniwa majimboni.

Wakizungumza katika taarifa yao kwa vyombo vya habari, wadau hao wameeleza kuwa kwa muda mrefu wanawake wamekuwa wakipewa nafasi za viti maalum pekee, hatua inayowanyima nafasi ya kushindana moja kwa moja na wanaume na kuonesha uwezo wao katika siasa za ushindani.

Katika kipindi hiki cha mchakato wa chaguzi za ndani ya vyama kuelekea uchaguzi mkuu, wanawake wengi wamejitokeza kuchukua fomu, licha ya kuwa idadi yao bado ni ndogo kulinganisha na wanaume.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu Zanzibar, wanachama 1,640 wamechukua na kurejesha fomu za kugombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, ambapo kati yao wanawake ni 406, sawa na asilimia 24.7.

Chama cha ACT Wazalendo kwa upande wake kimeripoti kuwa kati ya wanachama 435 waliotangaza nia ya kugombea nafasi hizo visiwani humo, wanawake ni 40 pekee, sawa na asilimia 9.2.

Vyama hivyo vinasubiri vikao vya Kamati Kuu na Kamati Maalum kupitisha rasmi majina ya wagombea, mchakato unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa Julai hadi Agosti 2025.

Wadau wametoa pongezi kwa wanawake hao kwa ujasiri wa kujitokeza lakini wakasisitiza kuwa hatua hiyo haitoshi iwapo hawatapewa nafasi halisi ya kugombea majimboni.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Zanzibar ilifanikiwa kupata wanawake wanane pekee (sawa na asilimia 16) katika Baraza la Wawakilishi na wabunge wanne (asilimia 8), kupitia siasa za ushindani.

“Tunaomba wajumbe wa vikao vya uteuzi kwenye vyama mbalimbali kuwapigia kura wanawake wakati wa mchakato wa kuwapata wagombea wa mwisho. Huu ni wakati wa kufanya mabadiliko halisi ya kisiasa na kijamii kwa kuzingatia usawa wa kijinsia,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Wadau wamesisitiza kuwa uwepo wa wanawake kwenye nafasi za juu za uongozi ni chachu ya maendeleo ya taifa, kwani tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa wanawake ni viongozi waadilifu, wanaoweka mbele maslahi ya familia na jamii, na ni wasikivu na wenye kujitoa.

Wakirejea Mkataba wa Kimataifa wa Kuondoa Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, wadau hao wamekumbusha wajibu wa Tanzania kama nchi mwanachama kuhakikisha inachukua hatua za kuongeza ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi.

Taarifa hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa taasisi kadhaa za wanawake zikiwemo Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania – Zanzibar (TAMWA ZNZ), kwa kushirikiana na Ubalozi wa Norway.

Wamewatia moyo wanawake waliotia nia wasikate tamaa bali waendelee kuwa imara na waaminifu kwa dhamira ya uongozi kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.











Share:

MRADI WA SEQUIP WAJENGA SHULE 6 MPYA IRAMBA-DC MWENDA



Na Mwandishi wetu, Singida

Serikali kupitia mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) imetumia Bilioni 6.361 kujenga shule mpya sita za sekondari, shule sita zimefanyiwa ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, Ujenzi wa vyoo na nyumba za walimu katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Akitoa taarifa ya miradi ya elimu iliyojengwa katika Wilaya ya Iramba, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Suleiman Mwenda amesema kuwa ujenzi wa shule hizo utaimarisha sekta ya elimu ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Amezitaja shule hizo zilizojengwa wilayani hapo kuwa ni pamoja na Ujenzi wa shule ya sekondari -MALUGA uliogharimu shilingi Milioni 470, Ujenzi wa shule ya sekondari NDULUNGU uliogharimu shilingi milioni 470, Ujenzi wa shule ya sekondari -Mtoa darajani uliogharimu shilingi milioni 544.225.


Miradi mingine mipya ni pamoja na Ujenzi wa shule ya sekondari -Makunda uliogharimu shilingi milioni 544.225, Ujenzi wa shule ya sekondari-KIZEGA uliogharimu shilingi milioni 544.225, na Ujenzi wa shule ya sekondari Amali-Kitukutu uliogharimu shilingi Bilioni 1.6.

Pia ujenzi wa vyoo matundu 9 shule ya sekondari MTOA kwa gharama ya shilingi milioni 15.3 na Ujenzi wa vyoo matundu 9 katika shule ya sekondari SHELUI kwa gharama ya shilingi milioni 15.3

Katika hatua nyingine Dc Mwenda ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Dkt samia Suluhu Hassan kwa kusimamia kwa weledi Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya sekondari MALUGA kwa gharama ya shilingi Milioni 110, Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya sekondari NDULUNGU kwa gharama ya shilingi milioni 110, na Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya sekondari IRAMBA kwa gharama ya shilingi Milioni 95.


Kuhusu ujenzi wa upanuzi wa miundombinu ya kidato cha 5 na 6, Mhe Mwenda amesema kuwa jumla ya shule sita zimepata miundombinu hiyo ikiwemo shule ya sekondari LULUMBA iliyopata kiasi cha shilingi milioni 352.8.

Nyingine ni Shule ya sekondari TUMAINI shilingi milioni 252.4, Shule ya sekondari NDAGO shilingi milioni 362.4, Shule ya sekondari KINAMBEU shilingi milioni 362.4, Shule ya sekondari KIZAGA shilingi 316.4 na shule ya sekondari SHELUI shilingi milioni 212.








Share:

KONGAMANO LA WANAWAKE WA KIISLAMU LATOA TUMAINI KWA WATOTO YATIMA NA WAJANE SONGEA

Kongamano la wanawake wa Kiislamu wakiwa katika kituo cha watoto yatima cha Luhila kwa Mangoma Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiburudika kwa pamoja 

Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma 

Kongamano maalum la wanawake wa Kiislamu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar limefanyika katika kituo cha watoto yatima cha Luhila kwa Mangoma, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, likiwa na lengo la kusaidia watoto yatima, wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wajane. 

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa taasisi mbalimbali na kikundi cha Umoja wa Wanyonge kinachosaidia jamii kwa moyo wa kujitolea.Akizungumza katika kongamano hilo, Bi Aziza Issa, mwanzilishi wa kituo cha watoto yatima cha Luhila, amesema kuwa kituo hicho kinahudumia watoto 59 na kwa sasa kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa nyumba ya mwalimu na fensi kwa usalama. 

Ameeleza kuwa jumla ya shilingi milioni 56 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo wa nyumba ya mwalimu pamoja na  fensi amewaomba wadau kujitokeza kuchangia chochote walichonacho. 

Kwa yeyote atakayeguswa, anaweza kuwasiliana naye moja kwa moja kupitia namba 0784 856 649.Bi Zena Mtamba kutoka wilaya ya Masasi, ambaye ni amirathi wa kanda ya kusini na muhamasishaji wa kulea watoto yatima na wasiojiweza.

 Amekabidhi mchango wa shilingi milioni 1 na laki moja kwa kituo hicho na kusisitiza kuwa malezi ya watoto si jukumu la serikali pekee bali kila mwanajamii anapaswa kushiriki. 

Aidha, ametangaza kuwa kongamano lijalo litafanyika wilayani Masasi mwezi Oktoba au Novemba.

Kwa upande wake, Bi Lulu Ramadhani, mjane mwenye watoto wanne, ameeleza kwa hisia namna kituo hicho kilivyomsaidia baada ya mume wake kufariki dunia akiwa mjamzito wa miezi saba. 

Amemshukuru Bi Aziza kwa moyo wake wa huruma na kujitolea, akisema kuwa kupitia msaada wa kituo hicho, yeye na mke mwenzie wameweza kulea watoto wao kwa heshima na utu pamoja na kupatiwa mahitaji muhimu.

Kongamano hili limekuwa jukwaa muhimu la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba watoto yatima na wajane, huku likiwaunganisha wanawake wa dini tofauti kwa lengo la kusaidia jamii. 

Wanawake hao wametoa wito kwa viongozi wa serikali, vyama vya siasa na wananchi kwa ujumla kujitokeza kusaidia kundi hilo lenye uhitaji mkubwa, ili kuepusha watoto kuingia katika mazingira ya hatari na ukatili wa kijinsia.Mjane aliesaidiwa na kituo cha Luhila kwa Mangoma Bi Lulu Ramadhani pichani akiwa na mwanae ambaye aliachwa na mumewe akiwa na ujauzito wa miezi saba pindi mume wake anafariki dunia



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 27,2025

Magazetini leo
 






Share:

Saturday, 26 July 2025

KATIBU MKUU MKOMI AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA UJENZI WA MAKAZI YA WATUMISHI KIJIJI CHA KIJIWENI

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (wakwanza kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (aliyevaa miwani) akisisitiza jambo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijiweni, Bw. Hassan Kalembo (wapili kutoka kulia) na Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo, Bw. Samson Bihole mara baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (kushoto) akitoka kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kijiweni, Bw. Hassan Kalembo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi (watano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi kutoka katika ofisi yake na Viongozi na Watendaji wa Shule ya msingi Kijiweni mara baada ya Katibu Mkuu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa makazi ya watumishi wa umma katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi
Mwonekano wa jengo la mradi wa makazi ya watumishi wa umma lililopo katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.


Na. Veronica Mwafisi-Lindi


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa makazi ya Watumishi wa Umma unaojengwa katika Kijiji cha Kijiweni, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ili kuwasaidia watumishi hao kuwa karibu na ofisi wanazofanyia kazi kwa lengo la kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo leo, Katibu Mkuu Mkomi amesema ujenzi wa makazi ya watumishi hao utawasaidia kuepeukana na changamoto ya makazi ambayo imekuwa ikiwakabili na kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Amesema Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiwajali sana watumishi wa umma katika kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo utekelezaji wa mradi wa makazi ya watumishi.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kuujenga utumishi wa umma pamoja na kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa watumishi wa umma ili wawe na tija katika utoaji wa huduma kwa maendeleo ya taifa,” Katibu Mkuu Mkomi ameongeza.

Bw. Mkomi amesema mradi wa ujenzi wa makazi hayo ya watumishi upo katika hatua ya majaribio katika Manispaa ya Lindi, mkoa wa Lindi ambapo pia unatekelezwa katika Mikoa ya Dodoma, Singida na Ruvuma.

Katibu Mkuu Mkomi katika ziara hiyo aliambatana na baadhi ya Wakurugenzi wa ofisi yake ambapo kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini, Bw. Patrick Allute amesema Watumishi Housing Investments ndiyo kandarasi inayojenga makazi katika mradi huo.


Bw. Allute ameongeza kuwa, mradi huo unafuatiliwa na kusimamiwa kikamilifu ili uweze kukamilika kwa wakati.
Share:

AGNESS SULEIMAN 'AGGY BABY' AANDIKA HISTORIA MPYA: ASHINDA TUZO MBILI KWENYE AFRICA ARTS ENTERTAINMENT AWARDS 2025


Mrembo maarufu, mwenye vipaji lukuki na msanii mwenye ushawishi mkubwa katika jamii, Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby, ameweka historia mpya katika tasnia ya burudani na maendeleo ya jamii baada ya kutangazwa Mshindi wa tuzo mbili kubwa kwenye Africa Arts Entertainment Awards (EAEA) 2025.

Tuzo hizo zilitolewa rasmi tarehe 25 Julai 2025 katika hoteli ya kifahari ya Protea Hotel Courtyard, jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Aggy Baby ameshinda katika vipengele viwili vinavyothibitisha mchango wake mkubwa ndani na nje ya sanaa:

Best Inspirational Youth Icon / Motivator
Fastest Rising Foundation of Excellence (kupitia taasisi yake ya kijamii – Tupaze Sauti Foundation)

Ushindi huu si wa kawaida. Ni uthibitisho wa jitihada zake si tu kwenye muziki na burudani, bali pia kwenye kuhamasisha maendeleo ya vijana wa Kitanzania kupitia elimu, maadili na miradi ya kijamii.

Mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla wanahimizwa kuendelea kumuunga mkono msanii huyu wa kipekee, ambaye kwa sasa ni nembo ya ubunifu, kipaji na uzalendo wa kweli.

Aggy Baby si msanii tu – ni kielelezo cha matumaini, uthubutu na mabadiliko chanya kwa kizazi kipya.

🔗 Fuata kurasa rasmi za tuzo hizi kwa taarifa zaidi:
@eaea_tanzania na @eaea_awards_inc

#AggyBabyFahariYaTanzania 🇹🇿
#EAEATanzania2025
#TalantaZaKikwetu
#EAEACountryLevelAwards2025

Share:

BANDARI KAVU YA KWALA KUZINDULIWA RASMI JULAI 31

Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa

Na Sheila Ahmadi – Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua rasmi Bandari Kavu ya Kwala, mkoani Pwani, tarehe 31 Julai 2025.

Uzinduzi huo utahusisha pia upokeaji wa mabehewa ya mizigo, pamoja na safari za treni za mizigo ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Hii ni hatua muhimu katika kuboresha usafirishaji wa mizigo nchini na kuongeza ufanisi wa shughuli za bandari.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amesema kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari, inaendelea kuboresha miundombinu kwa wakati ili kuchochea ukuaji wa uchumi na biashara nchini, hasa katika maeneo ya Dar es Salaam na Pwani.


 “Bandari Kavu ya Kwala itasaidia kupunguza msongamano mkubwa wa magari katika barabara ya Mandela, sambamba na kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo ya jirani,” amesema Prof. Mbarawa.


Ameongeza kuwa serikali inatarajia pia ongezeko la viwanda katika eneo hilo, hali itakayoongeza mapato ya serikali kwa kiwango kikubwa.


Aidha, Prof. Mbarawa amefafanua kuwa serikali haijaitelekeza reli ya zamani ya MGR, ambapo katika hafla hiyo ya uzinduzi, Rais Dkt. Samia atapokea mabehewa mapya 50 kati ya 100 yaliyonunuliwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC). Vilevile, mabehewa 20 ya MGR yamefanyiwa ukarabati na Wakala wa Uwezeshaji wa Ushoroba wa Kati.


Kwa mujibu wa Waziri huyo, usafirishaji wa mizigo kati ya Dar es Salaam na Dodoma ulianza rasmi Juni 27, 2025 ambapo makontena 10 yenye jumla ya tani 700 za bidhaa mchanganyiko kutoka Kampuni ya Azania yalisafirishwa. 

Julai 9, makontena 20 yenye tani 1,400 za saruji kutoka Kampuni ya Dangote nayo yalisafirishwa. TRC inatarajia kuongeza treni yenye mabehewa 30 ili kubeba mizigo ya tani 210,000 hadi kufikia uwezo wa juu uliosanifiwa.

Bandari hiyo ya Kwala inatarajiwa kuhudumia makasha 823 kwa siku, sawa na makasha 300,395 kwa mwaka, ambayo ni asilimia 30 ya makasha yote yanayohudumiwa kwa sasa na Bandari ya Dar es Salaam. Pia, bandari hiyo itakuwa kituo muhimu cha kusafirisha shehena ya makasha kwenda nchi jirani.

“Tunatoa wito kwa wadau wote wa usafirishaji, wafanyabiashara na wawekezaji kuchangamkia fursa ya gharama nafuu na usafiri wa uhakika kupitia Bandari Kavu ya Kwala,” amesema Prof. Mbarawa.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger