Monday, 21 July 2025

INEC YATOA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA UCHAGUZI MKUU MIKOA YA SHINYANGA NA SIMIYU... "KAZINGATIENI USAWA KWA VYAMA VYOTE VYA SIASA"

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele amefungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu huku akiwataka kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na Maelekezo mbalimbali ya Tume.

Mafunzo hayo ya siku tatu yamefunguliwa loe Julai 21, 2025 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, yakihusisha Waratibu wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi kutoka Halmashauri mbalimbali, kama sehemu ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Jaji Mwambegele amesisitiza umuhimu wa watendaji hao kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu na weledi ili kuhakikisha uchaguzi unaofanyika ni wa haki, huru na unaozingatia misingi ya sheria na demokrasia.
"Mafunzo haya ni sehemu muhimu ya maandalizi ya uchaguzi. Hatuwezi kuwa na uchaguzi wenye kuaminika endapo wasimamizi wake hawajafundwa ipasavyo. Nawaomba mzingatie mafunzo haya kwa umakini, mkiwa na dhamira ya kulinda imani ya wananchi kwa Tume," ameeleza Jaji Mwambegele.

Ameongeza kuwa nafasi ya msimamizi wa uchaguzi ni ya msingi katika mchakato mzima wa uchaguzi, kwani ndiye anayehakikisha taratibu zote zinafuatwa, kuanzia ugawaji wa vifaa, uendeshaji wa shughuli za siku ya kupiga kura, hadi usimamizi wa zoezi la kuhesabu na kutangaza matokeo.

Amewataka watendaji wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutoa taarifa mapema kwa vyama vya siasa kuhusu utaratibu wa kuwaapisha mawakala.

“Wakati wa kuapisha mawakala, toeni taarifa mapema kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya Tume na kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala,” amesema Jaji Mwambegele.

Mwenyekiti huyo wa INEC pia amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanazingatia usawa kwa vyama vyote vya siasa na kuhakikisha mazingira ya uchaguzi ni salama, shirikishi na yenye amani kwa kila mshiriki, ikiwemo wanawake, vijana na makundi maalum.
Washiriki wa mafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.

Aidha amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha vifaa vya uchaguzi wanavyopokea kutoka Tume, wanavihakiki, kuvikagua na kuhakikisha vinasambazwa kwenye vituo vyote na kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi vinavyohitajika mapema.

Amewataka kuhakikisha kuwa siku ya uchaguzi wanaweka utaratibu utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 kamili asubuhi na kufanya mawasiliano na Tume pale ambapo ushauri utahitajika kuhusiana na masuala ya uchaguzi.

Tume imeyagawa mafunzo hayo kwenye awamu mbili ambapo awamu hii ya pili inahusisha mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Mwanza, Mara, Dar es Salaam, Pwani, Rukwa, Katavi, Manyara, Arusha, Songwe na Mbeya.

Awamu ya kwanza ilifanyika tarehe 15 hadi 17 na ilihusisha watendaji kutoka mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Mjini Magharibi, Geita, Kagera, Mtwara, Lindi, Tabora, Kigoma, Tanga, Kilimanjaro, Ruvuma, Iringa na Njombe.

Mafunzo hayo yanajumuisha mafunzo ya sheria ya uchaguzi, maadili ya uchaguzi, matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi, pamoja na namna bora ya kushughulikia changamoto au malalamiko yatakayojitokeza katika vituo vya kupigia kura.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea na mafunzo ya aina hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2025 unafanyika kwa mafanikio makubwa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21, 2025. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo kutoka majimbo yote ya Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa watendaji wa Uchaguzi mkuu 2025 kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu leo Julai 21,2025
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo pia alitoa mada.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ambapo pia alitoa mada.
Hakimu mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Goodselda Kalumuna akitoa maelezo kabla ya kuwaapisha washiriki hao wa mafunzo kwa watendaji wa Uchagzi Mkuu ambapo aliwaongoza kula kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao ya Uchaguzi.
Washiriki wa mafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wamafunzo kutoka Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri.
Washiriki wa mafunzo hayo ambayo yanawajumuisha waratibu wa uchaguzi, wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo kutoka majimbo yote ya Mikoa ya Shinyanga na Simiyu.






Share:

🟢HAWA NDIYO WASHINDI UCHAGUZI WA MADIWANI VITI MAALUM CCM TARAFA MANISPAA YA SHINYANGA

Msimamizi wa Uchaguzi, Katibu wa Vijana CCM Mkoa wa Shinyanga,Salama A. Mhampi akitangaza matokeo

Na Mwamvita Issa - Shinyanga

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini kimeendesha uchaguzi wa ndani wa madiwani wa viti maalum kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, katika Tarafa mbalimbali, ambapo wanachama walijitokeza kwa wingi kushiriki mchakato huo muhimu uliofanyika Julai 20, 2025.


🔸 TARAFA YA MJINI

Jumla ya wagombea: 18
Kura zilizopigwa: 763
Kura halali: 751
Kura zilizoharibika: 12
Idadi ya viti vinavyogombewa: 5

Washindi waliopatikana ni:
🔹 Moshi Husein Kanji – Kura 536
🔹 Ester Festo Makune – Kura 445
🔹 Veronica E. Masawe – Kura 431
🔹 Mwanakhamis Kazoba – Kura 355
🔹 Eunice Z. Manumbu – Kura 272


🔸 TARAFA YA OLD SHINYANGA

Jumla ya wagombea: 3
Kura zilizopigwa: 554
Kura halali: 553
Kura zilizoharibika: 1
Idadi ya mshindi: 1

Mshindi aliyepatikana:
🔹 Mwanaidi Abdul Sued – Kura 539


🔸 TARAFA YA IBADAKULI (ZUHURA)

Jumla ya wagombea: 3
Kura zilizopigwa: 759
Kura halali: 758
Kura zilizoharibika: 1
Idadi ya mshindi: 1

Mshindi aliyepatikana:
🔹 Zuhura Waziri Mwambashi – Kura 695


Mchakato mzima wa uchaguzi ulifanyika kwa amani na uwazi, ambapo wanachama walionyesha mshikamano na utayari wa kuendelea kujenga chama chao kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Ushindi wa wagombea hawa ni ushahidi wa imani kubwa waliyonayo wanachama kwao, huku wakiahidi kuendeleza sera na mwelekeo wa CCM katika kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu.


🖊️ Imeandaliwa na – Mwamvita Issa

Share:

Sunday, 20 July 2025

MUME WANGU ALIKUA ANARUDI SAA 6 USIKU BILA MAJIBU



Kuna wakati nilijiuliza, “Hivi mimi ni mke au mpangaji tu wa nyumba hii?” Ndoa yangu ilikuwa imegeuka uwanja wa maumivu ya kimya. Mume wangu, ambaye zamani alikua rafiki yangu wa karibu, ghafla alianza kurudi nyumbani usiku wa manane. Saa tano, saa sita, saa saba… Bila ujumbe, bila simu, bila hata maelezo. Nikimuuliza, alikua na majibu makali kama vile: “Kwani wewe ni saa ya polisi?”

Awali nilidhani ni kazi. Baadaye nikaanza kuhisi kuna mwanamke mwingine. Nilianza kumfuatilia kwa macho, nikaanza kuhisi vitu ambavyo sikutaka kuvihisi kama mke. Kulikuwa na harufu za manukato ambazo si zangu, majina yasiyo ya kawaida kwenye simu yake, na tabia ya kuoga kabla hata ya kuniambia “hi.” Nilianza kupoteza amani. Soma zaidi
Share:

KAMPUNI YA CRCEG INATEKELEZA KWA UBORA NA KASI UJENZI UWANJA WA AFCON ARUSHA - SERIKALI

Na Prosper Makene, Arusha

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma ameipongeza Kampuni ya CRCEG ya kutoka nchini China ambayo inajenga uwanja wa mpira wa miguu jijini Arusha utakaotumika kwa michuano ya AFCON 2027 kwa kuweza kujenga uwanja huo kwa kasi na viwango vya hali ya juu.

Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa halfa ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa zege na kuanza rasimi kufunga paa la uwanja huo, Naibu Waziri amesema kuwa ni mara ya kwanza nchini kuona mkandarasi anamaliza kazi aliyopewa kabla ya muda kwani amemaliza awamu ya kwanza siku 20 kabla ya  muda uliopangwa kwenye mkataba.

Mwinjuma alimaalufu kama Mwana Fa amesema: "Mkataba huu wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo jijini Arusha, ulitiwa saini tarehe 19, mwezi wa 3, mwaka jana (2024), lakini natambua kazi rasmi zilianza tarehe 25, mwezi wa 7, mwaka huo huo, baada ya utaratibu wa kukabidhiana site pamoja na shughuli zingine za awali kukamilika. Mkandarasi amepewa jukumu la kufanya usanifu, kujenga, na kufanya manunuzi muhimu yatakayokamilisha usanifu wa mradi huu kwa kuzingatia vigezo elekezi." 

Aliongezea, "Hivyo, tangu mradi kuanza, mkandarasi ulijielekeza kuanza kazi zako katika maeneo hayo mara moja kwa kushirikiana na Mshauri Elekezi wa Wizara, Dar Al-Handasah, ili kutekeleza majukumu yako ya kikimkataba. Kwa kumbukumbu nilizonazo, kazi hii kwa upande wa ujenzi katika saite, hususan umwagaji wa zege, ulianza kutekelezwa tarehe 25, mwezi wa 11, mwaka 2024. .Leo hii, tarehe 19, mwezi wa 7, mwaka 2025, ikiwa ni siku 236 baadaye, shughuli kubwa ya kumwaga zege takribani mita za ujazo elfu 50 inakamilika. Hii inadhihirisha umakini, weledi, na ustadi wa hali ya juu wa Mkandarasi."

Naibu Waziri aliendelea kusema kuwa kazi hiyo iliyotukuka ya mkandalasi inawapa tumaini kubwa Serikali na watekelezaji wa mradi huo, kuwa kazi itakamilika kwa wakati na kwa viwango tunavyotarajia. 

"Kwa kasi hii mliyoionyesha, Watanzania wana uhakika wa kuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027, nasi tunajivunia kusimama mbele yao tukiwadhihirishia, kwa vitendo, kuwa shauku yao itatimia. Mradi unatazamiwa kukamilika tarehe 24 mwezi wa 7 mwaka kesho, na tunaamini hilo linawezekana. Hii itatuwezesha kuutumia uwanja, kuujua na kujiandaa vizuri kabla ya mashindano ya AFCON."

Mwana Fa alieleza kuwa, mafanikio na kasi ya CRCEG mpaka kufikia hatua hii ni kutokana na ushirikiano ambao kwanza Serikali, kupitia Wizara yake ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, unauonyesha kwa kufanya malipo kwa wakati na kutoa ushirikiano katika vyombo vingine mbalimbali vya kiserikali vinavyosimamia shughuli hii pale unapohitajika. 

"Aidha, kwa kurahisisha shughuli za Mkandarasi za kitaalamu na usimamizi, natambua mchango mkubwa unaowekezwa katika utekelezaji wa mradi kupitia Mshauri Elekezi, Dar Al-Handasah, pamoja na Ofisi ya Msimamizi wa Wizara iliyopo hapa hapa site, yaani Clerk of Work. Vile vile tunatambua kuwa kuwepo kwa ofisi hizi katika mradi kunasaidia kuzitatua changamoto kwa wakati pindi zinapojitokeza, lakini pia kurahisisha utekelezaji na kusababisha Mkandarasi kujielekeza mojakwa moja katika utekelezaji wa mradi, " alisema Naibu Waziri na kusisitiza.

"Ushirikiano huu unazidi kujenga mahusiano yetu, kati ya mtu mmoja mmoja, makampuni ya kichina na ya wazawa kupitia mikataba midogo, wafanyabiashara na wataalamu wa ndanii inasaidia kuhamisha ujuzi na kubakiza ufanisi nchini, na pia inazidi kuimarisha mahusiano kati ya Serikali ya Tanzania na China.."

Mwana Fa ambaye pia ni Mbunge wa Muheza alisema kuwa mradi huo ni mmoja wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan. "Pongezi na asante nyingi zimfikie, anapoona juhudi hizi bila shaka zinamtia moyo na kuzidi kumuhakikishia kuwa thamani ya pesa na maono ya Serikali yake yana tija na kuwapa tumaini watanzania."

Alimalizia kwa kusema kuwa mradi huo ni wa kimkakati, unaodhamiria kuongeza chachu ya michezo nchini, ikiwa ni jitihada za makusudi kulea vipaji na kutengeneza jamii yenye nguvu na afya borakupitia michezo. 

"Niwatie moyo wakandarasi na wadau wote wanaohusika katika utekelezaji wa mradi huu; historia inajengwa, na tunayo kila sababu ya kujivunia kuwa miongoni mwa watekelezaji. Mradi huu ukaweke alama nyingine kubwa katika uhusiano kati ya Tanzania na China.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Kenani Kihongosi amesema: "imekuwa nikiufuatilia kwa ukaribu sana mradi huu wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa michezo jijini Arusha tangu ulipoanza kutekelezwa mwaka jana(2024). Sababu ya kuufuatilia mradi huu kwa ukaribu huo ni kutokana na kuwa miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 338 za Kitanzania zinawekezwa katika utekelezaji wa mradi huu."

RC aliongezea: "Lakini pia, mimi ni mdaumkubwa wa michezo, nikiamini kuwa michezo ni nguzo mojawapo ya kuimarisha afya na nguvu kwa vijana ambao ni taifa la kesho, na kwa Watanzania wote kwa ujumla."

Amesema kuwa anatambua kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 24 mwezi wa saba mwaka kesho. ", Mimi, kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu, nafurahishwa na juhudi zinazofanywa na mkandarasi katika utekelezaji wa mradi.

Kwa kasi ninayoiona, ni wazi kuwa mradi utakamilika ndani ya wakati, ili wakazi wa Arusha wawe wa kwanza kuutumia uwanja huu na kuonajuhudi inayofanywa na serikali yao,si kwa maneno tu bali kwa vitendo."

Aliongezea kuwa Arusha ni kitovu cha utalii, na uwanja huu ni kivutio kingine cha utalii wa michezo.

"Hivyo, naendelea kuwaasa wakandarasi na wadau wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma ili kukamilisha mradi kama inavyotarajiwa. Kiuchumi, natambua jinsi ambavyo shughuli za ujenzi wa uwanja huu umetengeneza ajira kwa vijana na wanawake wengi," alisema.

RC Kihongosi alisistiza; "Lakini pia, utakapokamilika, uwanja huu utazalisha ajira zaidi, kuibua biashara mpya zinazohusiana na michezo na burudani, kukuza sekta ya utalii, na kuchangia katika pato la taifakwa ujumla. Kwa hiyo, kwangu mradi huu ni wa muhimu sana, na nausubiria kwa hamu kubwa."

Aliwaeleza wakandarasi wanatekeleza mradi huo kuwa atendelea kuwapa ushirikiano katika masuala yote ya kiutawala, utaratibu, vigezo, na usimamizi unaotarajiwa kutolewa na ofisi yangu pamoja na taasisi zilizo chini yake ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa mafanikio na viwango.

"Aidha, nitoe rai kwa wadau wote wa utekelezaji wa mradi huu kusimamia kwa umakini, kwa uadilifu, na kwa uwajibikaji mkubwa fedha na muda wa utekelezaji, ili thamani ya fedha ionekane na maono ya Serikali yatimie. Mafanikio ya mradi huu yatakuwa sababu nyingine ya kuendeleza mahusiano kati ya Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China, " alisema.

Vilevile, amesema kuwa mradi huo umefungua fursa za kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo baina ya wataalamu na wakandarasi wa ndani, katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa maslahi ya Taifa la leo na la vizazi vijavyo.

Alimalizia kwa kusema: "Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha itaendelea kutoa ushirikiano wake kikamilifu ili kuhakikisha maandalizi ya mashindano ya AFCON yanafanyika kama yanavyotarajiwa, na kwa viwango vinavyokidhi matarajio ya nchi yetu.

"Kwa dhati kabisa, nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa busara na wa kizalendo wa kuwekeza kwenye miundombinu ya michezo nchini,ikiwa ni sehemu ya kukuza vipaji, kuimarisha afya za Watanzania, na kulinda heshima ya nchi kimataifa."

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampuni ya CRCEG Wang Yusheng amesema: "Kwa niaba ya CRCEG, napenda kutoa shukrani kubwa kwa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na serikali ya Tanzania kwa ukarimu, upendo, na msaada wao wakati wote tangu kuanza kwa mradi. Pia, nawashukuru vyema washauri elekezi, na timu zote zilizoshiriki katika ujenzi huu mpaka kufikia hapa. Zaidi ya hayo, ninawapongeza wafanyakazi wote waliojitoa usiku na mchana kwenye mradi huu mpaka kupelekea kazi hii kufikia hapa, tunawashukuru sana."

Yusheng aliongezea: " Tangu kuanza kwa ujenzi wa Uwanja huu wa Michezo mnamo tarehe 25 Julai 2024, chini ya uangalizi wa viongozi wetu na msaada wa wadau mbalimbali, tumeshinda changamoto nyingi. Kwa bidii ndani ya siku 360, tumefanikiwa kumaliza kazi ya zege kwa siku ishirini kabla, na haya ni mafanikio makubwa ya awali."

Amesema kuwa ujenzi wa uwanja huo ni mfano mzuri katika kuonyesha ushirikiano wa nchi ya China na Tanzania, na uthibitisho wa jitihada za CRCEG katika kuijenga "Mpango wa Mkanda Moja na Njia Moja”. Hii ni kuhakikisha uwanja unakamilika kwa ubora. Uwanja huu utakuwa jukwaa jipya la michezo wa mpira wa miguu, likisaidia Tanzania kukua kimichezo, kuboresha sura ya jiji, na kuvuta fursa za maendeleo. Pia kuleta mchango mpya kwenye uchumi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

"Tunatambua kuwa hii ni hatua moja, lakini bado kuna hatua nyingine zaidi ili kukamilisha mradi huu. Hatua hii ya mwanzo ni mwendelezo wa jitihada mbalimbali ambazo tayari tumezianzisha. Huu ni ushaidi wa dhamira yetu ya kusonga mbele ili kufanikisha malengo ya mradi huu. Kwa dhima ya "Uhuru, Umoja na Kazi" ya Reli ya TAZARA, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, kupanua mipango, na kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati mnamo Julai 2026.

"Mwisho, Nawatakia kila la kheri, katika majukumu yenu ya kujenga Taifa, na tunatarajia uwanja huu kukamilika ili utumike kama ilivyopangwa. Hii itachochea kuimarika kwa urafiki kati ya nchi ya China na Tanzania mara dufu. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, Naibu waziri na wageni wote, nawatakia Afya njema na mafanikio makubwa.Asante".



Share:

VIONGOZI VIJANA NA WANAWAKE KUKUTANA MOROGORO KWA AJILI YA MDAHALO WA KITAIFA KUHUSU USHIRIKI WA KIRAIA KWA KUTUMIA SIMULIZI ZA HADITHI NA TEKNOLOJIA BUNIFU TANZANIA

Taasisi ya Youth Environmental Justice and Gender Equality (YOGE) kwa kushirikiana na  Ona Stories wanatarajia kufanya Mdahalo wa Kitaifa kuhusu Ushiriki wa Kiraia kwa kutumia simulizi za Hadithi na Teknolojia Zinazochipukia ili kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana katika nafasi za uongozi nchini Tanzania.

Mdahalo huo unatarajiwa kufanyika Julai 22, 2025 mkoani Morogoro, utawakutanisha viongozi 30 kutoka sekta mbalimbali zikiwemo siasa, biashara, dini, vyombo vya habari, sanaa na utamaduni kutoka mikoa mbali mbali ikiwemo ya Rukwa, Katavi, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam washiriki wakiwemo viongozi wanawake, wazee na vijana.

Katika kikao hicho, washiriki watapata fursa ya kutazama Filamu ya kumbukizi ya maisha na kazi za Bibi Titi Mohamed, mtetezi na kiongozi mwanamke aliyetoa mchango mkubwa katika kuhimiza ushiriki wa wanawake na vijana katika uongozi na nafasi za maamuzi nchini. 

Filamu hiyo inalenga kuonesha mchango wake chanya na mkubwa katika kuchochea na kuhakikisha ushiriki endelevu wa wanawake na vijana katika nafasi za juu za uamuzi nchini.

Mdahalo huo unafanyika wakati muafaka hususani kufuatia uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alisisitiza kubuni mipango na sera zinazoshabihiana na utekelezaji wa dira hiyo kupitia vipaumbele mbali mbali vya kimkakati ikiwemo utawala ushiriki wa masuala ya kiraia, ujumuishaji na ushiriki wa wanawake, vijana na makundi maalum ili kuhakikisha tunatimiza lengo kuu la kubadilisha nchi yetu kuwa taifa la kipato cha juu, shirikishi na lenye maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2050.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Mussa Kilakala, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kikao hicho.


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 20,2025

Magazeti

 


Share:

Saturday, 19 July 2025

ALIKUWA MBABE WA KUCHEAT, SASA ANAOGOPA KUCHATI NA SHAMBA GIRL



Kabla sijajua nini maana ya amani ya ndoa, nilijua uchungu wa usaliti. Mume wangu alikuwa mwanaume wa heshima mbele za watu, lakini ndani ya nyumba aligeuka kuwa mtu tofauti kabisa. Simu yake ilikuwa kama kifaru haiwezi kuguswa, kuangaliwa wala kuulizwa. 

Usiku wa manane alikuwa akiandika meseji kwa kucheka kimya, mchana alikua akijifanya kazini, kumbe yuko na wake wa watu. Soma zaidi
Share:

SERIKALI YAANZISHA OPERESHENI KABAMBE KUONDOA WAFUGAJI WALIOINGIA MAENEO YA KILIMO TUNDURU

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Denis Masanja akizungumza na wananchi wa kijiji cha Cheleweni kata ya Sisi kwa Sisi kuhusu operesheni kabambe ya kuwaondoa wafugaji wote waliovamia maeneo ya wakulima wilayani Tunduru 

Na Regina Ndumbaro- Tunduru

Serikali wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma, imetangaza kuanza rasmi operesheni kabambe ya kuwaondoa wafugaji wote waliovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo na uhifadhi. 

Hatua hii inalenga kudhibiti migogoro ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Cheleweni, kata ya Sisi kwa Sisi, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amesema kuwa operesheni hiyo itaanza rasmi Julai 21, na inalenga kuhakikisha kuwa wafugaji wote wanafuata sheria kwa kufanya shughuli zao kwenye maeneo rasmi ya ufugaji. 

Amesisitiza kuwa baada ya operesheni hiyo, wafugaji watatakiwa kuripoti katika ofisi za serikali za vijiji husika ili kuelekezwa maeneo wanayopaswa kwenda.

Katika hatua ya kudumu ya kutatua migogoro hiyo, Masanja ameeleza kuwa serikali itaunda kamati ya pamoja itakayojumuisha wafugaji, wakulima na baadhi ya wananchi waliopendekezwa na vijiji. 

Kamati hiyo itakuwa na jukumu la kutafuta suluhisho la kudumu la kuzuia muingiliano wa makundi hayo mawili, ambao mara nyingi huibua migogoro mikubwa.

Mkuu huyo wa wilaya ametaja kuwa chanzo kikuu cha migogoro hiyo ni baadhi ya viongozi wa vijiji na wananchi wanaopokea fedha kutoka kwa wafugaji kwa maslahi binafsi na kuwakaribisha kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa shughuli za ufugaji. 

Amewaonya kuwa tabia hiyo inachochea migogoro na kuwataka wananchi kuacha kuwapokea watu wasiofahamika kiholela bila kufuata taratibu za kisheria.

Kuhusu changamoto ya miundombinu, Masanja ameahidi kuwa serikali itashughulikia tatizo la barabara inayounganisha kijiji cha Cheleweni na makao makuu ya kata ya Sisi kwa Sisi, ambayo imeharibiwa vibaya na mvua za masika. 

Amesema ukarabati huo utafanyika haraka ili kurudisha huduma za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa eneo hilo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Chiza Marando, ameeleza kuwa jumla ya vitalu 221 tayari vimetengwa kwa ajili ya wafugaji, hivyo amewataka wafugaji waondoke katika maeneo ya wakulima na kuelekea kwenye vitalu hivyo vilivyopangwa rasmi.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Cheleweni, Mustafa Ponera, amefafanua kuwa kutokana na ubovu wa barabara, wananchi hulazimika kutembea kwa miguu zaidi ya kilometa 7 hadi kijiji cha Sisi kwa Sisi kufuata magari ya usafiri kwenda Tunduru mjini. 

Amesema wamiliki wa magari wameacha kabisa kupeleka magari yao kijijini hapo kwa kuhofia kuharibika kutokana na hali mbaya ya barabara hiyo.

Katika kutatua tatizo hilo, Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wilayani Tunduru, Silvanus Ngonyani, amebainisha kuwa serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 155 kwa ajili ya ukarabati wa barabara hiyo. 

Ameahidi kuwa kabla ya mwezi Agosti, barabara zote zenye changamoto zitafanyiwa matengenezo, huku akiwaomba wananchi kuwa wavumilivu.

Mkuu wa Wilaya Masanja amewasihi wananchi kushirikiana na serikali katika ujenzi na utunzaji wa miradi ya maendeleo kama vile vyumba vya madarasa, badala ya kuiachia serikali pekee jukumu hilo, kwani maendeleo ni jukumu la kila mmoja.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger