Friday, 18 July 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 19,2025

Magazeti
 


















Share:

AFISA MTENDAJI AKUTWA AMEFARIKI KWA KUNYWA SUMU YA PANYA

Aliyekuwa afisa mtendaji wa kijiji cha Kangeme kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama Julian Mkumbo (35) amekutwa amefariki dunia ndani ya chumba alichokuwa akiishi mara baada ya kutoonekana kwa siku kadhaa.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP. Janeth Magomi amesema Aprili 16, 2025 marehemu alikutwa akiwa amefariki na mara baada ya uchunguzi kufanyika na madaktari walibaini kuwa amefariki kwa kunywa sumu ya panya.

SACP. Magomi amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na upelelezi wa tukio hilo huku akitoa wito kwa wananchi na kutoa pole kwanndugu jamaa na marafiki na kuisihi jamii kumrudia MUNGU kwa imani yake na kuachana na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Share:

RAIS SAMIA ATOA BIL 19.6 UJENZI WA MIRADI YA ELIMU (SEQUIP) MKOANI NJOMBE



Na mwandishi wetu, Njombe

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa shilingi Bilioni 19.6 kwa ajili ya Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari SEQUIP mkoani Njombe.

Kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Bilioni 4.360 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya madarasa, maabara, mabweni, Bwalo la chakula Jengo la Utawala na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya wasichana ya mkoa wa Njombe ambayo imekamilika.

Hayo yamebainishwa tarehe 17 Julai 2025 na Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Njombe Mwl Nelasi Mulungu ambapo amesema pia Bilioni 1.6 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Mkoa ya Amali ambayo inaendelea na ujenzi katika Wilaya ya Ludewa.

Mwl Mulungu amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Bilioni 12.638 kwa ajili ya ujenzi wa shule 20 za kata katika mkoa huo wa Njombe.

Pia amesema kuwa serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika mkoa wa Njombe ikiwemo ujenzi wa Mabweni, Nyumba za walimu, na Matundu ya vyoo.








Share:

Thursday, 17 July 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 18,2025


Magazeti


















Share:

Wednesday, 16 July 2025

NM-AIST YASHEREHEKEA WIKI YA UBUNIFU KWA KUCHOCHEA SAYANSI YA AFRIKA KUJITEGEMEA



Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula( kulia) akimsikiliza mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya St. Joseph akielezea kuhusu ubunifu wa ndege nyuki (drone) yenye uwezo wa kupanda mbegu shambani kwa kutumia mfumo wa kisasa unaopima ukubwa wa shamba na kusambaza mbegu kwa usahihi na haraka wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela Julai 16,2025.

Na.Mwandishi Wetu_Arusha

Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imeadhimisha Wiki ya Ubunifu kwa lengo la kuendeleza maono ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela, aliyetamani bara la Afrika lijitegemee kielimu na kiteknolojia kwa kuzalisha wataalamu wake wa ndani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo Julai 16,2025 katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo, Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Maulilio Kipanyula, alisema Wiki ya Ubunifu inalenga kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa sayansi, uhandisi, teknolojia na ubunifu kama nguzo kuu za maendeleo ya kweli.

“Maendeleo hayawezi kupatikana bila sayansi na teknolojia. Tumejikita pia katika matumizi ya sayansi shirikishi, hasa akili bandia (AI), kama sehemu ya kukuza maarifa ya vijana wetu,” alisema Prof. Kipanyula.

Shughuli hiyo imeambatana na mihadhara ya kitaalamu kutoka kwa wazungumzaji wa kitaifa na kimataifa, pamoja na maonesho ya bunifu kutoka kwa wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vya ufundi. Kila kundi lilipewa nafasi kuonesha vipaji vyao kupitia uvumbuzi unaolenga kutatua changamoto za kijamii.

Miongoni mwa bunifu zilizovutia wengi ni drone iliyoundwa na wanafunzi wa shule ya sekondari ya St. Joseph, ambayo ina uwezo wa kupanda mbegu shambani kwa kutumia mfumo wa kisasa unaopima ukubwa wa shamba na kusambaza mbegu kwa usahihi na haraka.

“Nimefurahishwa sana na ubunifu huu. Teknolojia hii ni msaada mkubwa kwa wakulima wetu kwani inapunguza gharama, muda, na upotevu wa mbegu. Ni aina ya bunifu zinazofaa kuendelezwa,” aliongeza Prof. Kipanyula.

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Taasisi anayeshughulika na Taaluma, Utafiti na Ubunifu, Prof. Anthony Mshandete, alisema taasisi hiyo inaendelea kuibua vipaji kuanzia shule za sekondari hadi vyuo vikuu kwa lengo la kukuza teknolojia zinazoibuka na kuliletea taifa maendeleo.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mandela Wiki, Prof. Linus Munishi, alisema wiki ya ubunifu imehusisha wadau kutoka ngazi mbalimbali kuanzia shule za sekondari, vyuo vya kati na vikuu, hadi mashirika ya umma, sekta binafsi, wajasiriamali na viwanda.

“Tunapenda kuona kizazi cha ubunifu kinaanza kuibuliwa mapema kabisa, ndiyo maana tumeshirikisha hata shule za awali na zile zilizoko karibu na taasisi,” alieleza Prof. Munishi.

Maadhimisho hayo yamekuwa jukwaa muhimu la kukuza mawazo mapya na kushirikisha jamii katika safari ya mabadiliko ya kiteknolojia, kwa kuzingatia dira ya Hayati Nelson Mandela ya Afrika yenye kujitegemea kielimu na kisayansi.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula akizungumza na wanafunzi, wabunifu na wasayansi wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela Julai 16,2025.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula( kulia) akimsikiliza Dkt Esther Kimaro ( kushoto) akielezea kuhusu miradi ya ushirikishwaji wa jamii kwa ajili ya usimamizi endelevu wa magonjwa ya mifugo katika jamii za wafugaji wakatinwa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela Julai 16,2025.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula( kulia) akimsikiliza mwanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya St. Joseph akielezea kuhusu ubunifu wa ndege nyuki (drone) yenye uwezo wa kupanda mbegu shambani kwa kutumia mfumo wa kisasa unaopima ukubwa wa shamba na kusambaza mbegu kwa usahihi na haraka wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela Julai 16,2025.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula akitembelea wabunifu mbalimbali walikuwa wakionyesha bunifu na Teknolojia ikiwa ni Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela julai 16,2025.


Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula( kushoto ) akipokea zawadi kutoka kwa waalimu shule ya Sekondari ya Shepherd wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela Julai 16,2025.


Wahudhuriaji wa maadhimisho ya wiki ya Ubunifu ya Nelson Mandela ikiwa ni wiki ya kuonyesha ubunifu katika masuala ya sayansi na teknolojia kwa lengo la kumbukizi ya aliyekuwa Rais wa Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela inayoadhimishwa katika wiki ya kuazimishwa siku yake ya kuzaliwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.
Share:

NILIZIKA MIMBA TATU BILA MAELEZO LAKINI BAADA YA TIBA YA KIROHO, SASA NIMESHIKA MIMBA YANGU YA KWANZA KWA AMANI


Kila mwanamke mwenye ndoto ya kuwa mama anajua uchungu wa kuiona mistari miwili ya ujauzito, kisha wiki chache baadaye, damu inaanza kutoka.

Nilipitia hilo mara tatu. Mara ya kwanza nilifikiri ni bahati mbaya. Mara ya pili nikaambiwa na daktari labda mimba hazishikiki kwa sababu ya homoni. Mara ya tatu, nililia hadi sauti ikanikata. Nilijifungia ndani siku tatu bila kula. Soma zaidi
Share:

KAMPENI YA “TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA” YAENDELEA SEKONDARI ROBANDA, SERENGETI

Katika mwendelezo wa kampeni ya kitaifa ya TUWAAMBIE KABLA HAWAJAHARIBIWA, Sajenti Emmanuel kutoka Jeshi la Polisi, kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto, ametembelea Shule ya Sekondari Robanda iliyopo Kijiji cha Robanda, Kata ya Ikoma, Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na wanafunzi wa kidato cha tano.

Akiwa shuleni hapo, Sajenti Emmanuel amewahimiza wanafunzi hao kujitambua na kuelekeza nguvu zao katika masomo ili kufikia malengo yao ya kitaaluma na maisha kwa ujumla, amesisitiza umuhimu wa kuepuka mahusiano ya kimapenzi wakiwa bado shuleni, akieleza kuwa vitendo hivyo vimekuwa chanzo kikuu cha kukatisha ndoto za wanafunzi wengi nchini.

Aidha, amewataka wanafunzi kuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kutoa taarifa mapema kwa mamlaka husika, amebainisha kuwa taarifa zinaweza kutolewa katika ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto iliyo katika kituo cha polisi, kwa Afisa wa Ustawi wa Jamii, au kwa viongozi wa serikali ya kijiji na kata.

Kampeni hiyo inalenga kuwafikia vijana walioko mashuleni na katika jamii kwa ujumla, ikiwa ni jitihada za pamoja kati ya serikali, vyombo vya dola, na wadau wa maendeleo katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na kusaidia vijana kufikia ndoto zao kwa usalama.
Share:

Tuesday, 15 July 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 16,2025



Magazeti










Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger