Monday, 23 June 2025

NSSF TUNAENDELEA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII: KARIBU TUKUHUDUMIE

NSSF TUNAENDELEA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII: KARIBU TUKUHUDUMIE
Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata elimu ya hifadhi ya jamii katika banda la NSSF wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili kwa wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiri wenyewe, pia wanapewa elimu jinsi wanavyoweza kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja na elimu kuhusu huduma za kidijiti (NSSF Portal).


Share:

MDEMU AWATAKA WANAWAKE KUPENDANA, KUSHIKAMANA NA KUPEANA SAPOTI KATIKA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI

Na WMJJWM – Iringa

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Felister Mdemu, ametoa wito kwa wanawake nchini kupendana, kushikamana, na kupeana taarifa kuhusu fursa zinazotolewa na serikali ili kujikwamua kiuchumi na kushiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali za kijamii na kisiasa, ikiwemo kugombea nafasi za uongozi.

Mdemu ametoa kauli hiyo Juni 22, 2025 wakati wa hotuba yake kwenye kongamano la kuelekea kilele cha Siku ya Wajane na Wagane Duniani, linalotarajiwa kufanyika Juni 23, 2025, mkoani Iringa.

Katika hotuba hiyo, amesisitiza umuhimu wa wanawake kuelimishana na kupeana taarifa kuhusu mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kama njia ya kuwawezesha kiuchumi.

“Kinamama tupendane, tuache chuki na wivu wa maendeleo. Tushikane mikono, tupeane fursa. Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametupatia mikopo na fursa nyingi kwa ajili ya kutuinua kiuchumi. Naomba tupeane habari na tushirikiane kuzifikia,  tuache kukwamishana,” amesema Mdemu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jinsia, Badru Abdunur, ametoa pongezi kwa uongozi wa mkoa wa Iringa kwa kuandaa kongamano hilo muhimu ambalo limewakutanisha wajane na wagane ili kujadili changamoto na fursa zinazowahusu.

“Ni faraja yetu kukutana nanyi leo, na tumeweza kujifunza mambo kadhaa. Tuna matumaini kuwa mtayafanyia kazi mafunzo mliyopata ili yakawasaidie kukabiliana na changamoto na kukimbilia fursa mbalimbali. Serikali imeendelea kupokea na kutatua changamoto za makundi maalum, ikiwemo wajane na wagane,” amesema Badru.

Aidha, Afisa Maendeleo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Saida Mgeni amewataka wanawake kuwa na nidhamu ya fedha na kujifunza tabia ya kujiwekea akiba, hata kama ni kidogo, ili waweze kujitegemea kiuchumi. Pia aliwasihi kusimamia kwa uadilifu mali walizoachiwa na wenza wao waliotangulia mbele za haki.

Baadhi ya wajane na wagane walioshiriki kongamano hilo waliishukuru Serikali kwa kuwatambua na kuwaandalia siku maalum inayolenga kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili.
Share:

NSSF TUNAENDELEA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII: KARIBU TUKUHUDUMIE

NSSF TUNAENDELEA KUTOA ELIMU YA HIFADHI YA JAMII: KARIBU TUKUHUDUMIE
Wananchi mbalimbali wakiendelea kupata elimu ya hifadhi ya jamii katika banda la NSSF wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma.

NSSF inashiriki maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa ujumla ikiwemo elimu kuhusu mafao, jinsi ya kujisajili kwa wanachama wapya kutoka sekta binafsi na wananchi waliojiri wenyewe, pia wanapewa elimu jinsi wanavyoweza kujichangia kupitia simu ya mkononi popote walipo, fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba na viwanja na elimu kuhusu huduma za kidijiti (NSSF Portal).


Share:

Sunday, 22 June 2025

MATI SUPER BRANDS YADHAMINI MASHINDANO YA WEST KILI TOUR CHALLENGE 2025

 



Na Ferdinand Shayo ,Kilimanjaro .

Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited imedhamini mashindano ya West Kili Tour Challenge 2025 msimu wa 5 yanayojumuisha mbio za riadha,baiskeli na piki piki yaliyofanyika katikati ya Hifadhi ya shamba la Miti la West Kilimanjaro kwa lengo la kukuza utalii wa michezo na kuunga mkono juhudi za Rais Dr.Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.

Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo Brayson Mnene amesema wamekuwa wakidhamini mashindano hayo kwa miaka miwili mfululizo kwa lengo la kuunga mkono utalii wa michezo na shughuli za uhifadhi zinazofanywa kwa lengo la kutunza ekolojia ya Mlima Kilimanjaro.

Mkuu wa Wilaya ya Siha Dkt. Christopher Timbuka amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kufanya utalii katika hifadhi ya shamba la miti la West Kilimanjaro lenye vivutio mbali mbali vya utalii ikiwemo wanyamapori,ndege na miti ya asili.

Mkuu wa Hifadhi ya West Kilimanjaro Robert Faida ameyataka makampuni mbali mbali kuunga mkono mashindano hayo yanayolenga kutangaza utalii na fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta hiyo .

Kwa Upande wake Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godifrey Mzava amewapongeza Waandaaji wa mashindano hayo pamoja na wadhamini kwa kushiriki kwenye tukio hilo kubwa lililowakutanisha mamia ya wananchi na wadau wa utalii







Share:

UNATIA NIA UBUNGE AU UDIWANI UCHAGUZI MKUU 2025?

 

Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, Mtandao wa Malunde 1 Blog  unawakaribisha wote wanaotangaza nia ya kugombea Ubunge au Udiwani kupitia vyama vya siasa kutangaza nia na kurusha habari zao kupitia blog hii maarufu.

Tunatoa nafasi ya:

✅ Kutangaza nia yako rasmi

✅ Kurusha habari, picha na video za kampeni

✅ Kufanya mahojiano maalum

✅ Kuwafikia wananchi kwa haraka na weledi


📱 🥏 +255 757 478 553 au 0688 864 294

🌐 Tovuti: www.malunde.com


👉🏾 Tangaza kupitia Malunde 1 Blog!

#Uchaguzi2025 #Malunde1Blog #TangazoLaNia #Udiwani #Ubunge

Share:

WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI MAGEREZA NA VYUO VYA MAFUNZO WANOLEWA


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.


Meza kuu ikiwa katika mkutano huo.Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza jambo wakati wa mafunzo ya siku tatu ya Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.



Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma.
Hakimu Denis John Mpelembwa akiwaapisha washiriki
Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya Waratibu, Waandishi Wasaidizi na Waendesha vifaa vya Bayometriki wa Magereza kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 mkoani Dodoma wakila kiapo cha kutunza siri kabla ya kuanza mafunzo hayo.
Mratibu wa Uandikishaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mafunzo , akizungumza jambo.

Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji, Caroline Ruben akiwasilisha mada kuhusu uraia kwa washiriki wa mafunzo hayo.
****************
Na. Waandishi Wetu
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaasa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo kwa Tanzania Zanzibar kufanya kazi kwa weledi.

Wito huo umetolewa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa watendaji hao ambayo yameanza leo tarehe 22 Juni, 2025 Mkoani Dodoma kwa Magereza sambamba na Unguja kwa Vyuo vya Mafunzo.


Akifungua mafunzo kwa watendaji hao yaliyofanyika Mkoani Dodoma kwa watendaji wa Magereza, Tanzania Bara, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Jacobs Mwambegele amesema Tume imewateua watendaji hao kutokana na weledi wao.

“Sina shaka kuwa kuteuliwa kwenu kunatokana na ujuzi, uwezo na weledi mlionao katika kutekeleza majukumu ya kitaifa likiwepo zoezi la uboreshaji wa Daftari ambalo ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,” amesema Mhe. Mwambegele.

Amewahakikishia watendaji hao kuwa kwenye mafunzo hayo ya siku tatu Tume itawapa ujuzi wa kutosha kwa nadharia na vitendo kuwawezesha kutekeleza jukumu lao kwa weledi.

Akifungua mafunzo kama hayo Kisiwani Unguja, Zanzibar kwa watendaji wa Vyuo vya Mafunzo, Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufani Mstaafu, Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk ametoa wito kwa watendaji hao kuvitunza vifaa vya uboreshaji wa daftari.

“Ninatoa wito kwenu kuhakikisha mnavitunza vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi la uboreshaji wa Daftari na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili muweze kuyafanyia kazi kwa usahihi wakati wote wa utekelezaji wa zoezi hilo,” amesema.

Jaji Mbarouk pia amewahakikishia watedaji hao kuwa maafisa kutoka Tume watakuwepo muda wote wa zoezi na kwamba endapo watapata changamoto ya aina yoyote wasisite kuwasiliana nao.

Kwa mujibu wa ratiba zoezi hilo la uboreshaji wa Dafatri kwenye Magereza na Vyuo vya Mafunzo linafanyika kwa siku saba kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 04 Julai, 2025 ambapo watakaohusika ni mahabusu na wafungwa walihukumiwa kifungo chini ya miezi sita.
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe, Jaji wa Rufani (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya waratibu, waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki wa Vyuo vya Mafunzo kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yaliyoanza leo Juni 22 -24, 2025 Mjini Unguja Zanibar.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Adam Mkina akizungumza wakati wa Mafunzo hayo.

Meza Kuu ikiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger