Sunday, 22 June 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 22,2025


 Magazeti       





Share:

Saturday, 21 June 2025

TBA YAHIMIZWA KUWAFIKIA WATUMISHI WA UMMA KUPITIA MAONESHO



Na Mwandishi wetu,Dodoma

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umetakiwa kuyatumia vyema maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kuelimisha watumishi wa umma juu ya huduma na miradi mbalimbali inayotekelezwa na taasisi hiyo, hususan katika sekta ya makazi na ujenzi wa ofisi.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Selemani Mkomi, alipotembelea banda la TBA katika viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma, ambako maonesho hayo yanaendelea.

“Kwenye maonesho haya mmekuja kuonesha huduma mnazotoa, ambazo zinawahusu sana watumishi wa umma. Hao ndio wahitaji wakuu wa makazi, ofisi na maeneo mengine ya matumizi. Ni vyema mkatoa maelezo ya kutosha kuhusu huduma zenu ili ziweze kufahamika kwa urahisi,” amesema Bw. Mkomi.

Ameongeza kuwa bado kuna changamoto ya uelewa kwa baadhi ya watumishi wa umma kuhusu mahali wanapoweza kupata nyumba za makazi, hivyo amesisitiza TBA kuongeza jitihada za kuhamasisha na kutoa elimu kwa watumishi kuhusu upatikanaji wa huduma hizo.

Kwa upande wake, mmoja wa watumishi wa umma waliotembelea banda hilo, Bw. Hussein Mzee Mussa, amesema ameridhishwa na miradi mbalimbali ya nyumba inayotekelezwa na TBA, ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba 3,500 za makazi unaoendelea katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.

“Mradi huu ukikamilika utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto ya makazi kwa watumishi wa umma hapa mkoani Dodoma,” amesema Bw. Mussa.

TBA inaendelea kutumia maonesho ya wiki ya utumishi wa umma kama jukwaa la kuelezea miradi ya ujenzi na ushauri inayoitekeleza, ikiwemo ya nyumba za makazi kwa watumishi wa umma, ujenzi wa ofisi za serikali, pamoja na ujenzi wa mji wa serikali unaoendelea jijini Dodoma.


Share:

WAZALISHAJI UMEME MKOANI NJOMBE WATAKIWA KUSHIRIKIANA


-Washauriwa kuunda umoja wa kusaidiana na kubadilishana uzoefu

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu ametoa wito kwa waendelezaji wa miradi ya Nishati Jadidifu Mkoani Njombe kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuongeza tija kwenye shughuli zao na kuwa mfano bora kwa waendelezaji wa miradi katika mikoa mingine.

Ametoa wito huo Juni 20, 2025 akiwa katika ziara ya kukagua mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko ya maji uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Kata ya Ukwama, Wilaya ya Makete Mkoani Njombe unaomilikiwa na Dayosisi ya Kusini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)kupitia Kituo cha Udiakonia Tandala.

"Kwa wingi wa rasilimali ya maji iliyopo Mkoani hapa ni dhahiri uwezo wa kuzalisha zaidi ya megawati 50 ndani ya Mkoa huu pekee upo, ni suala la nyinyi waendelezaji wa miradi kuunganisha nguvu kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana," alisisitiza Mhe. Balozi Kingu.

Hata hivyo alipongeza kwa jitihada zinazochukuliwa na waendelezaji wa miradi ya kuzalisha umeme katika miradi aliyoitembelea na aliwasisitiza kutoridhika na kiasi kidogo wanachozalisha badala yake wafikirie namna ya kutanua wigo wa uzalishaji ili watanzania waweze kunufaika na umeme wanaozalishwa.

Alisema Taifa linahitaji kuwa na umeme mwingi ili kuwezesha maendeleo ya kichumi na kijamii hasa ikizingatiwa kuwa umeme ni injini ya uchumi.

Aliwakumbusha kuwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) upo kwa ajili ya kuwaendeleza hivyo wahakikishe wanafanya kazi kwa karibu na Wakala ili kurahisisha shughuli zao na kufikia malengo waliyojiwekea.

"Serikali kupitia REA ipo kwa ajili yenu, hakikisheni kila hatua mnayopiga mnashirikiana kwa karibu na REA ili miradi iweze kwenda kwa kasi na kuleta tija inayokusidiwa," alisisitiza Mhe. Balozi.

Kwa upande wake Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Wilson Sanga alishukuru Serikali kwa kuchangia uendelezaji wa mradi huo unaozalisha kilowati 360 ambazo zote zinaingizwa katika Gridi ya Taifa kwa makubaliano maalum ya kimkataba na TANESCO. Aliishukuru sana Serikali kupitia REA kwa mchangio uliotolewa katika kufanikisha Mradi huo.

Naye Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema mradi huo wa Ijangala umenufaika na ruzuku ya Jumla ya Shilingi Milioni 996.

Mbali na uwezeshwaji huo, Mhandisi Mwijage alisema Mwendelezaji mradi amewezeshwa na REA kupata mkopo nafuu wa muda wa miaka 12 uliyotolewa kupitia Benki ya Uwekezaji ya Tanzania (TIB) wenye thamani ya Shilingi Milioni 922 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji umeme na utekelezaji wa mradi kwa ujumla.

Mha. Mwijage alisisitiza kuwa milango ya Wakala ipo wazi kwa waendelezaji miradi ya Nishati Jadidifu na kwamba wasisite kuwasiliana na Wakala kwa jambo lolote linalokwamisha uendelezaji wa miradi.

Vilevile aliwasisitiza wazalishaji umeme kuhakikisha mazingira yanatunzwa ili kuwa na miradi endelevu.
Share:

Thursday, 19 June 2025

ICTC NA THN WASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO KUINUA VITUO VYA UBUNIFU TEHAMA


Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam

Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICTC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Vituo vya Ubunifu Tanzania (Tanzania Hubs Network - THN) wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati kwa lengo la kuimarisha uwezo wa vituo vya ubunifu nchini katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Makubaliano hayo yaliyofikiwa jijini Dar es Salaam yameelezwa kuwa ni hatua mpya katika kuimarisha uratibu wa ukuaji na matumizi ya TEHAMA nchini, hasa katika kuchochea ubunifu miongoni mwa vijana na wajasiriamali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dk. Nkundwe Mwasaga alisema ushirikiano huo utaisaidia Tume kuwa karibu zaidi na vituo vya ubunifu nchini kote, hali itakayorahisisha kutambua na kuendeleza bunifu mbalimbali zinazochangia kwenye uchumi wa kidijitali.

“Hii ni hatua muhimu kwa Tume ya TEHAMA. Ushirikiano huu utasaidia kuhamasisha maendeleo ya TEHAMA kupitia bunifu mbalimbali zinazotoka kwenye vituo hivi, ambavyo mara nyingi vinabeba mawazo na suluhisho ya changamoto zinazowakabili Watanzania,” alisema Dk. Mwasaga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mtendaji wa THN, Kiko Kiwanga alisema kuwa makubaliano hayo yatafungua milango ya ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na vituo vya ubunifu, hatua itakayosaidia kubaini na kutatua changamoto zinazokwamisha vijana na wajasiriamali nchini kutumia TEHAMA kuibua fursa za kiuchumi.

“Makubaliano haya ni jukwaa la pamoja kati yetu na Serikali, si tu kwa ajili ya kuboresha mazingira ya ubunifu, bali pia kusaidia vijana kufanikisha mawazo yao ya kiteknolojia na kuyageuza kuwa miradi yenye tija,” alisema Kiwanga.

Makubaliano hayo yamekuja wakati ambapo Serikali inaendelea kusisitiza umuhimu wa TEHAMA kama nyenzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya uchumi wa kidijitali na kuongeza ushindani wa taifa katika soko la kimataifa.

















——
Kwa habari zaidi kuhusu TEHAMA na maendeleo ya ubunifu nchini, endelea kutembelea Torch Media
Share:

Wednesday, 18 June 2025

WANANCHI WANUFAIKA NA ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA




Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo Juni 18 umeendelea kutoa elimu kuhusu nishati safi ya kupikia kwa wananchi waliotembelea banda la Wakala huo katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.

Maadhimisho hayo ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23 yameanza Juni 16 yakiwa na kauli mbiu inayosema “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji”.

Wananchi wa rika zote kutoka Mkoani Dodoma na Mikoa ya karibu wameonekana kuvutiwa na banda la REA ambapo wataalam kutoka REA wamewapa taarifa kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wakala pamoja na kupata elimu kuhusu nishati safi ya kupikia.

Wananchi hao wamepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia REA za kuhakikisha wananchi wanaachana na matumizi ya nishati zisizo safi na salama kwa kupikia.
Share:

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA PBPA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DODOMA





WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Logistiki wa Mafuta Bi. Hilda Kowero mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akipokea zawadi katika banda la PBPA mara baada ya kutembelea banda la Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



WANANCHI mbalimbali wakipata elimu katika banda la Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.
Share:

WAZIRI SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA RAIS,MIPANGO NA UWEKEZAJI WIKI YA UTUMISHI WA UMMA






WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini Raymond Mtani,mara baada ya kutembelea banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.





WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.



WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mhe. George Simbachawene,akiwapongeza watumishi wa Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji ,mara baada ya kutembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ametembelea na kukagua banda la tume ya taifa ya Mipango na Uwekezaji katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yanayofanyika katika viwanja vya Chinangari Park Dodoma.

Akitoa maelezo mbele ya Waziri huyo leo Juni 17,2025 Mkuu wa Kitengo cha Habari na mawasiliano Serikalini Raymond Mtani amesema ofisi hiyo ina jukumu la kuratibu mipango ya kitaifa na kusimamia shughuli za sekta za uwekezaji wa ndani.

“Tangu kuanzishwa kwake ofisi hii imekuwa na mafanikio makubwa, katika mpango wa kitaifa imeratibu zoezi kubwa la uandikaji wa dira ya taifa ya 2050 ambapo mchakato huo ulishirikisha wananchi wote zaidi ya Milioni 1 ambao walitoa maoni yao na waliyaridhia,”amesema.

Aidha, ameongeza kuwa kwasasa wanalo zoezi la kuandaa mpango wa pili wa maboresho ya mazingira ya biashara.

“Hili ni zoezi muhimu kwasababu tunakwenda kwenye uchumi wa Trilioni moja kwa maono ya dira ya taifa ya 2050, kwahiyo sekta binafsi zinatarajiwa kuchangia zaidi ya asilimia 50 ili tuweze kufikia hayo malengo,”ameongeza.

Wiki ya Utumishi kitaifa imeanza Juni 16 mpaka Juni 23,2025 ikiwa inajumuisha taasisi na Wizara mbalimbali hapa nchini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger