Wednesday, 18 June 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNIB18,2025

  

Magazeti
 
Share:

MEATU MTAENDELEA KUPATA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO IKIWEMO NISHATI- DKT. SAMIA




📌Asema baada ya Vijiji vyote Meatu kupata umeme kasi inaelekea vitongojini

📌 Ataka umeme utumike kuongeza thamani ya mazao, kilimo na ufugaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani amesema Serikali imeendelea kupeleka maendeleo katika Wilaya ya Meatu ikiwemo ukamilishaji wa usambazaji  umeme katika Vijiji vyote 109 vya Wilaya hiyo.

Dkt. Samia ameyasema hayo Juni 17, 2025 Wilayani Meatu Mkoa wa Simiyu akiwa kwenye ziara ya kikazi.

"Kama tulivyoahidi, hatujaishia hapo, kazi ya usambazaji umeme sasa inaendelea kwenye vitongoji lakini pamoja na jitihada hizi zote ninafahamu kuna changamoto ya umeme kutokuwa na nguvu ambayo inatatuliwa." Amesema Dkt. Samia

Ameeleza kuwa, Wizara ya Nishati inatatua   changamoto hiyo  ya umeme kutokuwa na nguvu  kwa kujenga  njia ya kusafirisha umeme kutoka Shinyanga hadi Simiyu na ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme. 

Amesema kukamilika kwa miradi hiyo kutapelekea uwepo wa umeme wenye nguvu na wa kutosha kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo Viwanda.

Amesisitiza kuwa, lengo la Serikali ni kuona wananchi wanatumia nishati ya umeme kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuongeza thamani ya mazao, kilimo na ufugaji.






Share:

Tuesday, 17 June 2025

RUVUMA YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA KWA MSISITIZO WA HAKI NA MAADILI

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Ngolo Malenya akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika halmashauri ya Wilaya ya Madaba akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas 

Na Regina Ndumbaro Madaba -Ruvuma 

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika kwa mwaka 2025 katika Mkoa wa Ruvuma yamefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, yakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngolo Malenya, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed. 

Maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo “Haki za Mtoto: Tulipotoka, Tulipo na Tuendako”, ikiwa na lengo la kutoa hamasa kwa jamii kulinda na kutetea haki za watoto katika kila hatua ya maisha yao.

Katika tukio hilo muhimu, viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wamehudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Comrade Oddo Kilian Mwisho. 

Takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 zinaonesha kuwa Mkoa wa Ruvuma una jumla ya watoto 855,106 wenye umri wa miaka 0-17, sawa na asilimia 46.3 ya watu wote 1,848,794. 

Kati yao, wavulana ni 428,058 na wasichana 427,048. Hali hii inaonesha wazi kuwa watoto ni kundi kubwa na lenye umuhimu mkubwa katika mustakabali wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Kupitia hotuba hiyo, Malenya amesisitiza umuhimu wa kila mdau katika jamii kuhakikisha watoto wanapata haki ya kuishi, kupata elimu, ulinzi na malezi bora. 

Aidha, amesisitizwa kuwa Serikali katika awamu zote imewekeza kwa kiasi kikubwa katika kulinda amani na utulivu wa nchi, jambo ambalo ni urithi muhimu kwa watoto wetu. 

Wananchi wamehimizwa kuendeleza tunu hii adhimu kwa ajili ya ustawi wa taifa na kizazi kijacho.

Wazazi, walezi, jamii na wadau mbalimbali wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia maadili mema kwa watoto, kuzuia unyanyasaji na kutumia lugha chanya kwa kuwa watoto hujifunza kwa kuiga. 

Malenya amehimiza jamii kuepuka lugha za kichochezi au vitendo vinavyoweza kuathiri malezi ya watoto na kuharibu mustakabali wao. 

Kauli mbiu ya mwaka huu imetumika kama kichocheo cha tafakuri na hatua madhubuti katika ulinzi wa haki za watoto wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla.




Share:

BEI YA KUJAZA GESI (LPG) KWA MATUMIZI YA KUPIKIA NI HIMILIVU – KAPINGA




📌 Wizara ya Nishati na TAMISEMI zaendelea kushirikiana kuhakikisha Shule mpya zinafungwa mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema gharama ya kujaza gesi kwenye mitungi (LPG) ni himilivu ikiwa ni jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ili kuwezesha matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo Juni 16, 2025 katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Simiyu wakati wa kuzindua Shule Maalum ya Sayansi ya Wasichana ya Simiyu ambayo imefungwa miundombinu ya nishati safi ya kupikia.


“Mheshimiwa Rais ulituelekeza Taasisi ambazo zinahudumia watu zaidi ya mia moja tuzifungie miundombinu ya nishati safi ya kupikia, Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na TAMISEMI tunatekeleza agizo hilo kwa kuzifungia mifumo ya nishati safi shule mpya ambazo zinajengwa." Amesema Kapinga


Ameeleza kuwa, uwezo wa shule hiyo ni wanafunzi 800 na mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia iliyofungwa ina uwezo wa kuhudumia wanafunzi 800.


Ameongeza kuwa, kwa idadi hiyo ya wanafunzi 800 mtungi wa gesi katika Shule ya Wasichana Simiyu utakuwa ukijazwa kila baada ya miezi miwili.













Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 17, 2025

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger