Monday, 6 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 7,2025

 

Magazeti ya leo
 
       
Share:

DUH! MREMBO ATOA KALI YA MWAKA MTANDAONI

Kuna siku mrembo mmoja aliwashangaza marafiki zake wengi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusema kuwa tangu aolewe na mumewe, hajawahi kumuita jina lolote tamu kwa ajili ya kunogesha mapenzi yao. 

Anasema walikuwa wanaishi tu kwenye ndoa lakini alikuwa na wasiwasi kutokana mumewe amekuwa akimtenga kutokana na ukweli kwamba wawili hao walikuwa wakiishi kwenye ndoa ya sogea tuishi ambayo haifuati taratibu za kidini na kimila. 

Kama alivyosema, siku zote alitamani kwamba mume wake siku moja angemwita majina kama "asali wa moyo" lakini kwa jinsi mambo yalivyokuwa yakienda, aliona angesubiri kwa miaka mingi kuona jambo hilo likitokea. 

"Tulikuwa kwenye ndoa kwa takribani miaka sita na hakuwahi kuniita jina lolote tamu. Nilikuwa nikijitahidi kadri niwezavyo lakini mume wangu alionekana kuwa mtu asiye na akili ya kujiongeza. Alikuwa akiniita kwa majina yangu kama yanavyoonekana kwenye kitambulisho changu." alisema. 

Anasema hali hii ilifanya ndoa yao kuwa ya kuchosha sana lakini kupitia mtandao wa kijamii, alifahamu kuhusu huduma za Dr Bokko ambaye ni mtaalam wa tiba asilia katika eneo zima la Afrika Mashariki na Kati. 

Mrembo huyo alipitia baadhi ya shuhuda kwenye tovuti yake na kugundua kuwa Dr Bokko ameokoa ndoa nyingine zenye hali mbaya kama yake, ndipo akaamua kuwasiliana naye kwa ajili ya huduma yake.  

Huko kwa Dr Bokko alipewa maneno ya mapenzi yenye nguvu ambayo yalikusudiwa kuamsha mapenzi katika ndoa yake. Baada ya muda anasema aliona mabadiliko makubwa kwa mume wake. Aligeuka kuwa mtu wa kimapenzi tofauti na hapo awali. 

Sasa anamwita majina matamu na pia akabadilika na kuwa mtu wa kimapenzi, jambo ambalo anasema liliifanya ndoa yao kuwa tamu ajabu. Wasiliana na Dr Bokko kwa namba +255618536050 ili nawe upate utatizo wa changamoto yako katika mapenzi. 

Mwisho.

Share:

VYANDARUA 1,542,836 VYENYE DAWA KUSAMBAZWA KATIKA MKOA WA SHINYANGA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jumla ya vyandarua 1,542,836 vyenye dawa vinatarajiwa kusambazwa katika mkoa wa Shinyanga mwezi huu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali na wadau wake kupambana na ugonjwa wa malaria. 

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 6,2025 wakati wa kikao kazi cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga juu ya kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa Mkoani Shinyanga.

Katika kikao hicho waandishi wa habari wamepitishwa katika mada mbalimbali ikiwemo hali ya malaria nchini Tanzania na mkakati wa kinga dhidi ya malaria, kampeni ya ugawaji wa vyandarua mkoani Shinyanga, mbinu bora za kuwasilisha taarifa za malaria, taarifa muhimu kwa jamii juu ya kampeni ya ugawaji vyandarua na mchango wa vyombo vya habari katika utoaji wa taarifa za kampeni ya ugawaji vyandarua.

Vyandarua hivi vitasambazwa kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, huku lengo likiwa ni kupunguza maambukizi ya malaria.

Usambazaji huu utakuwa sehemu ya mpango wa kitaifa wa kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Malari, ambao bado ni changamoto kubwa katika baadhi ya mikoa ya Tanzania.

Vyandarua vyenye dawa vimekuwa moja ya njia bora za kudhibiti maambukizi ya malaria. 

Serikali ya Tanzania inatarajia usambazaji huu utafikia kaya nyingi zaidi na hivyo kuokoa maisha ya wananchi. Usambazaji huu utafanyika kwa ushirikiano wa karibu na Serikali za Mitaa, na kwamba vyandarua vitasambazwa kwa usawa na kwa kasi ili watu wa maeneo ya vijijini wasiachwe nyuma.

Kwa sasa, wananchi wanahimizwa kutumia vyandarua vyenye dawa, na pia kuendelea kuchukua tahadhari nyingine kama vile kupiga dawa za kuua mbu katika makazi yao na kujiepusha na maeneo yenye maambukizi makubwa.


Share:

Sunday, 5 January 2025

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 6,2025

 

Magazeti ya leo
 
         
Share:

UUNGANISHAJI UMEME VIJIJINI WAFIKIA ASILIMIA 99.9



Na mwandishi wetu, Dar

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesema kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba 2024, vijiji vilivyounganishwa na umeme nchini vimefikia 12,301 kati ya vijiji 12,318 ambayo ni sawa na asilimia 99.9.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 5 Januari, 2025 na Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mha. Jones Olotu wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya upatikanaji umeme vijijini kwa Wanahabari tulipotoka, tulipo na tunapokwenda kuelekea Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati jijini Dar es Salaam.

"Vijiji 17 vilivyobakia wakandarasi wanaendelea na ujenzi wa miundombinu na vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi januari mwaka 2025," amesema Mha. Olotu.

Ameongeza kuwa, Tanzania Bara ina jumla ya vitongoji 64,359 ambapo tayari vitongoji 33,657 sawa na asilimia 52.3 vimefikiwa na umeme na vitongoji 30,702 vilivobaki vipo kwenye mpango wa kupatiwa umeme kwa kipindi cha miaka mitano.

Vile vile, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imefanikiwa kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi maeneno ya vijijini kwa kuwatengenezea fursa za uwekezaji kwa kutumia huduma ya umeme.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unaotarajiwa kufanyika januari 27 - 28 na kuhudhuriwa na watu wasiopungua 1,500 kutoka nchi mbalimbali.

Miongoni mwa washiriki ni Wakuu wa Nchi za Afrika, Mawaziri wa Nishati na Fedha, Mabalozi, Taasisi za Kimataifa, Makampuni yaliyowekeza kwenye sekta ya Nishati na watafiti.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger