Tuesday, 14 May 2024

TRA YATOA ELIMU YA KODI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO SHINYANGA

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga imetoa elimu ya Kodi kwa Wanafunzi wanachama wa Vilabu vya Kodi kutoka shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea uwezo na ufahamu wa masuala mbalimbali ya kodi.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Ijumaa Mei 10,2024 katika Ukumbi wa Makindo Hotel Mjini Shinyanga yakishirikisha wanafunzi kutoka shule ya Msingi Little Treasures, Shule za Sekondari Old Shinyanga, Uhuru na Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy Com) na Chuo cha St. Joseph.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo, Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea ufahamu wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali ya kodi.

“Mafunzo ambayo tunayaandaa yanalenga kuwafundisha vijana wetu wakiwa wadogo hasa wanafunzi wa shule za Msingi, Sekondari na vyuoni kujua maana ya kulipa kodi, umuhimu wa kodi ni nini, kwanini serikali zote duniani zinaweka kodi. Kodi ni malipo ya lazima ambayo mwananchi mzalendo anatozwa kwa ajili ya kuisaidia serikali yake iweze kuendesha majukumu yake kwa wananchi”,amesema David.

“Ni muhimu sisi wananchi kuhakikisha tunapokwenda kupata huduma yoyote tupewe risiti ya EFD na wafanyabiashara watoe Risiti. Na nyinyi ni mabalozi wazuri kwa sababu msingi mzuri kwa sababu tunaamini tukiwafundisha mngali wadogo mtakuwa wazalendo wazuri wa nchi hii”,ameongeza.

Kwa upande wake, Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi amesema kodi ndiyo chanzo kikubwa cha mapato ya taifa, inasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi, ujenzi wa miundombinu na huduma za kijamii hivyo kuwashauri wafanyabiashara kujisajili TRA ili wapate namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN), kufanyiwa makadirio ya kodi kila mwaka, kuwasilisha Return na kulipa kodi sahihi na kwa wakati sahihi.

Nao wanafunzi kutoka Vilabu vya kodi wameishukuru TRA kwa kuwapatia elimu ya masuala ya kodi na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kueneza elimu hiyo kwa jamii ili kuhakikisha kila mwananchi anawajibika kulipa kodi.
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga leo Ijumaa Mei 10,2024 - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Shinyanga, Makwabe David akizungumza wakati akifungua mafunzo ya elimu ya mlipakodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga

Afisa Huduma na Elimu Kwa Mlipa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Semeni Selemani Mbeshi akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga

Afisa Kodi TRA Mkoa wa Shinyanga, Joel Elias akitoa elimu ya kodi kwa wanafunzi kutoka Vilabu vya Kodi shule za msingi, sekondari na vyuo Mkoa wa Shinyanga

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 14, 2024

Share:

Monday, 13 May 2024

MKUU WA ULINZI WA RAIS AFUKUZWA KAZI

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amemfukuza kazi mkuu wa shirika linalohusika na ulinzi wake baada ya maafisa wake wawili kukamatwa kuhusiana na madai ya njama ya mauaji dhidi yake.

Kufutwa kazi kwa mkuu wa idara ya ulinzi wa taifa (UDO) Serhii Rud kulifichuliwa katika amri iliyochapishwa kwenye tovuti ya rais. Hakuna sababu ya kufukuzwa kazi.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Ukraine Ukrinform, Rud aliteuliwa kuwa mlinzi wa juu wa Zelensky mnamo Oktoba 2019. Nafasi bado haijatajwa.

UDO ina jukumu la kuhakikisha usalama wa rais wa Ukraine na maafisa waandamizi wa serikali, pamoja na ulinzi wa majengo ya utawala.

Mapema wiki hii ilibainika kuwa Ukraine iliwakamata maafisa wawili wa usalama wanaodaiwa kuhusika katika njama ya Urusi ya kumuua Zelensky.

Makanali wawili wa kijesho katika UDO walishutumiwa kwa kufanya "shughuli za uhaini dhidi ya Ukraine ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Ukraine ilisema Jumanne.

Makanali wote wawili walishtakiwa kwa uhaini; Mmoja pia alishtakiwa kwa kuandaa kitendo cha kigaidi.
Idara ya usalama wa taifa ya Kyiv (SBU) imesema "imezuia" mipango ya kumuua Zelensky na maafisa wengine waandamizi wa Ukraine, akiwemo mkuu wa SBU, Vasyl Maliuk, na mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Ulinzi ya Ukraine, Kyrylo Budanov.
Share:

DKT BITEKO: WAUGUZI NI KADA MUHIMU KWA MAENDELEO YA HUDUMA ZA AFYA NCHINI

NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu 
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu 
NAIBU Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel  akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu 
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza 

Na Oscar Assenga, TANGA

NAIBU Waziri Mkuu Dkt Dotto Biteko amefunga kilele cha  maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani huku akieleza wauguzi ni kada muhimu kwa sababu maendeleo ya huduma za afya nchini hayawezi kufikiwa bila uwepo wao.

Dkt Biteko ambaye pia ni Waziri wa Nishati aliyasema hayo leo wakati akifunga maadhimisho hayo yaliyokuwa yakiendelea kwenye ukumbi wa Hotel ya Regail Naivera Jijini Tanga ambapo alimwakilisha Rais Dkt Samia Suluhu.

Alisema kwamba wauguzi wanafanya nzuri na kwamba asilimia 100 ya watumishi wa sekta ya afya nchini asilimia 60 ni wauguzi na shughuli zinazowapeleka kazini watoa huduma za afya asilimia 80 ya kazi hizo zinafanywa na wauguzi lakini changamoto zilizongumza na wauguzi niungane nanyi ni za kweli ni lazima kuona namna ya zifanyiwe kazi.

“Leo mnaposheherekea siku ya wauguzi mnakazi kubwa ya kukumbushana wajibu wenu na kurejea viapo vyenu mtumie siku ya leo muendelee kukumbushana kutekeleza wajibu wenu”Alisema

Aidha aliwaambia kwamba wao ni kundi muhimu na wanatambua mchango wao kwa jamii na kwamba hata watoto wanapozaliwa mtu wa kwanza kumpokea mkononi hata kaba ya mzazi ni muunguzi.

“Watu wanakuja kwenu wakiwa na maumivu wengine wamezimia kutokana na maradhi mbalimbali waliyyapata wengine kwa ajali wanakuja wakiwa na tumaini moja tu afya zao na maumivi yao kuwatoka wanawategemea nyie hivyo muuguzi ukimtaja kuwa daraja la pili utakuwa umetenda dhambi “alisema

“Niwahakikishie kwamba Serikali inatambua mchango wenu kama wauguzi wapo asilimia 60 na ndio wanafanya kazi asilimia 80 ni kweli lazima miundo yenu tuiangalie hivi ni sayansi gani inayohusika na utawala ambayo muuguzi mwenye uzoezi mkubwa kwenye sekta hawezi kuwa kiongozi kwenye eneo la uongozi?Alisema

“Kwamba zipo taaluma ambazo mtu atasoma kazi yake ni kuuongozwa na hawezi kupata nafasi ya kuongoza na hata ikitokea kwa wauguzi wenzake hilo jambo sio sawa hivyo Naibu Waziri wa Afya nielekeze hilo jambo mlifanyia kazi mliangalie sitaki kuingilia misingi taaluma lakini nazungumzia logiki ya kawaida ya misingi ya utawala lazima haki ya uongozi kuna watu wengine wanaipata “Alisema Naibu Waziri Mkuu.

“Kama kuna kiongozi mzuri wa uongozi anauwezo wa kufanya kazi vizuri kwanini umuondoe kwenye vikao vya uongozi kwa sababu eti yeye ni muuguzi na uuguzi ugeuke kuwa ni mtu wa kutumwa na kushurutishwa na mtu mwengine jambo hilo sio sawa”Alisisitiza Naibu Waziri Mkuu Dkt Biteko.

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Molel aliwataka watumishi wasikubali kugawanywa hakuna cha nesi, daktari, maabara na kada nyengine kwani wao ni kitu kimoja.

“Kwa sababu kila mtu anaweza kuwa DMO kwenye suala la uongozi lakini uthibiti namba moja imetokea wizara ya afya wametokea mawaziri maprofesa lakini amekuja dada yetu mwanasheria Ummy Mwalimu leo na anafanya vizuri sana tunahaangaika kuna wauguzi na wakunga msikubali watu wawatawale ishu tupige mzigo Dkt Samia atape kura zake nyie mnaonaje hiyo”Alisema Dkt Molel

Katibu Mkuu wa Chama cha Wauguzi Tanzania Samweli Mwambopa alisema kwamba wanaishukuru Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini kiwemo ujenzi wa miundombinu, uwekezaji vifaa tiba ambayo ndio msingi wa utoaji wa huduma bora za afya.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho hayo inawakumbusha viongozi wa Serikali na wananchi kwamba wanapowekeza kwenye uuguzi unasaidia kuboresha huduma za afya na kuwepo kwa huduma bora.

Aidha alisema huduma bora katika Hospitali kwa asilimia 80 hutegemea huduma za uuguzi ndio maana wanahimiza kufanya uwekezaji kwenye eneo hilo kwenyey sekta ya afya na kutambua hiyo ni taaluma inayojitegemea.

Hata hivyo alisema wauguzi wapo mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanapata huduma wakati wote hivyo wapo kwenye kutoa ufumbuzi katika kusaidia wagonjwa.

Alisema mafaniko ya chama hicho ni wauguzi wamekuwa mstari wa mbele kutoa huduma za VVU ikiwemo kutoa ushaauri nafasi upimaji na uanzishaji wa dawa kwa wapokea huduma
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger