Saturday, 11 May 2024

TIGO YAKUTANA NA WADAU WAKE KWENYE JUKWAA LA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI SHINYANGA


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya TIGO Tanzania imekutana na wadau wake Mkoa wa Shinyanga katika Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali lenye lengo la kutoa fursa kwa wafanyabiashara kujua huduma na bidhaa za Kibiashara, Kifedha na za dukani zilizoambatana na uboreshaji wa mtandao wa 4G+ kimkoa na Kanda ya ziwa kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa Jukwaa hilo lililofanyika Ijumaa Mei 10,2024 usiku katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga, Mkurugenzi wa Kampuni ya TIGO Tanzania Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa amesema TIGO imeendelea kuboresha huduma za kuingiza sokoni bidhaa mpya hivyo kuwaomba wadau kuchangamkia fursa zinazopatikana katika Kampuni hiyo.

Amesema Kampuni  ya TIGO imetoa elimu ya bidhaa na  huduma  zake zinazorahisisha biashara kwa taasisi mbalimbali ili kuweza kukuza biashara zao na kuongeza wateja.

"Tumekutana na wadau wetu wakiwemo wafanyabiashara na wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga ili kuwaeleza na kuwatambulisha bidhaa zetu pamoja na huduma zetu zikiwemo za Mobile solutions, APN, Bulk sms, E1, Toll-free, Mjasiriamali box, 5G standalone, Collection account, Disbursement account, Huduma za kikoba, Lipa kwa Simu, Huduma simu za mkopo, Huduma za kurudisha number (simswap) na Huduma za kuoanisha number (special number)",ameeleza Mutalemwa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya TIGO Tanzania Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kampuni ya TIGO Tanzania Kanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Meneja wa Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga Sadock Mahundo akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Meneja wa Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga Sadock Mahundo akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Meneja wa Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga Sadock Mahundo akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Meneja wa Mauzo  Taasisi Ndogo na Kati wa Kampuni ya TIGO Kanda ya Ziwa, Paschal Mathew akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Meneja wa Mauzo Mashirika na Taasisi Kubwa wa Kampuni ya TIGO Kassongo Faraji akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Meneja wa Kampuni ya TIGO Tanzania Kanda ya Ziwa, Christopher Charles akizungumza wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Msimamizi wa Duka Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga, Pendo Ally akieleza kuhusu Simu za mkopo zinazouzwa katika duka hilo wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Msimamizi wa Duka Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga, Pendo Ally akieleza kuhusu Simu za mkopo zinazouzwa katika duka hilo wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania
Msimamizi wa Duka Kampuni ya TIGO Mkoa wa Shinyanga, Pendo Ally akieleza kuhusu Simu za mkopo zinazouzwa katika duka hilo wakati wa Jukwaa la Wafanyabiashara na Wajasiriamali Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Kampuni ya TIGO Tanzania



Share:

MAENEO YALIOATHIRIWA NA MVUA BARABARA YA DAR-LINDI-MTWARA YOTE NI SHWARI


Barabara ya Dar es salam-Lindi-Mtwara sasa imerejea katika hali ya kupitika baada ya kukamilika urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo yote yaliyokuwa yamekatika.

Mvua kubwa zilizoambata na Kimbunga Hidaya ziliharibu miundombinu ya barabara hiyo katika eneo la Mikereng’ende, Songas, Somanga na Matandu-Nangurukuru ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Juzi tarehe 9 Mei 2024 Magari ya Mizigo, Mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama yalianza kuruhusiwa kuendelea na safari jambo ambalo liliamsha hisisa mseto kwa wananchi kuwapongeza wataalamu wa Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) kwa kazi waliyoifanya usiku na mchana katika kurejesha miundombinu hiyo.

Wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali, wananchi, wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara wanapaswa kusafiri kwa tahadhari kwani maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.
Share:

Friday, 10 May 2024

BARAZA LA USHINDANI LATOA ELIMU KWA WADAU DODOMA



KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,akisisitiza jambo wakati akifungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.


KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,akizungumza wakati akifungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.





Kaimu Msajili wa Baraza la ushindani (FCT) Be.Kunda Mkenda,akizungumza wakati wa semina ya baraza hilo kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma yenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.

Mkuu wa Idara ya Uchumi FCT, Kulwa Msogoti ,akizungumza wakati wa semina ya baraza hilo kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma yenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.


BAADHI ya washiriki wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,(hayupo pichani) wakati akifungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.


Ofisa Sheria Mkuu Hafsa Said,akichangia mada wakati wa semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.


WADAU mbalimbali wakichangia mada wakati wa semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.


KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Bw.Kaspar Mmuya,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya baraza la ushindani (FCT) kwa wadau wa Mkoa wa Dodoma lenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji leo Mei 9,2024 jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu
BARAZA la ushindani (FCT) limetoa elimu kwa wadau mkoani Dodoma yenye lengo la kukuza na kulinda ushindani wa kibiashara na kumlinda mlaji.

Akifungua semina hiyo jijini Dodoma Mei 9, 2024, Katibu Tawala wa Mkoa huo, Kaspar Mmuya, amepongeza baraza hiyo kwa kutoa elimu hiyo itakayowasaidia watanzania kwenye biashara zao kwa kuongeza kasi ya uwajibikaji ili kujiepusha na migogoro ya kiushindani.

“Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuunda chombo hichi na Rais Samia Suluhu Hassan ametoa nafasi kupitia FCT kutoa maoni ili kudhibiti soko na ushindani na kuleta usawa,”amesema.

Awali, Kaimu Msajili wa Baraza hilo, Kunda Mkenda amesema elimu inayotolewa na FCT ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kisheria kwa kuwa ni chombo cha rufaa kilichoanzishwa chini ya kifungu cha 83(1) cha Sheria ya Ushindani namba nane ya Mwaka 2003.

Kwa upande wao, Mkuu wa Idara ya Uchumi FCT, Kulwa Msogoti na Ofisa Sheria Mkuu Hafsa Said, wameeleza namna baraza linavyoendesha mashauri yake na kwamba kwa kipindi cha Mwaka 2007 hadi Machi, 2024, mashauri 443 yalisajiliwa kati ya hayo 429 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi huku 13 yakiwa kwenye hatua mbalimbali za usikilizwaji.

Aidha, washiriki wa semina hiyo, Faustine Mwakalinga na Grace Onea, wamepongeza baraza kwa kutoa elimu hiyo na kuahidi kuwa mabalozi kwenye maeneo yao ili kuepuka migogoro ya kiushindani.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger