Sunday, 21 April 2024
RAIS SAMIA AFANYA MAGEUZI HUDUMA BORA ZA AFYA, KILIMO
Na Mwandishi Wetu,
Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya afya pamoja na ruzuku ya mbolea kwa wakulima katika Mkoa wa Ruvuma.
Mhe. Jenista ameyasema hayo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi, Dkt. Emmanuel Nchimbi mkoani Ruvuma.
MSAJILI WA HAZINA AZUNGUMZA NA KAMPUNI YA UCHIMBAJI MADINI YA PERSEUS
DODOMA
Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, Aprili 20, 2024 amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka Kampuni ya uchimbaji Madini ya Perseus ya nchini Australia iliyowakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Jeff Quartermaine pamoja na Afisa Fedha Mkuu wa kampuni hiyo, Lee Anne de Bruin.
Kampuni ya PERSEUS imenunua hisa za Kampuni ya ORECORP iliyokua inamiliki mgodi wa Nyanzaga uliopo Geita.
Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine, Perseus imekubali kuongeza asilimia 4 ya hisa za Serikali "Free Carried Interests" na kuifanya Serikali ya Tanzania kumiliki asilimia 20 ya mgodi huo kutoka asilimia 16 za awali.