Tuesday, 16 April 2024
Monday, 15 April 2024
UWT IBADAKULI WAFANYA KONGAMANO LA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA MADARAKANI NA KUMPONGEZA KUFANYA KAZI KUBWA YA KUWALETEA MAENDELEO WATANZANIA
KAMATI YA WATAALAMU WA MASUALA YA HABARI ZANZIBAR YAONGEZA KASI UFUATILIAJI MAREKEBISHO SHERIA ZA HABARI
Katika vikao mbalimbali ZAMECO ilitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya sheria hio kwa lengo la kupatikana sharia mpya na rafiki kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini.
Aidha mnamo tarehe 9/4/2024 ZAMECO wamefika katika afisi za Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar iliyopo Vuga kwa ajili ya kufuatilia hatua iliyofikiwa baada ya kupokea mapendekezo hayo mwezi wa Octoba mwaka 2023.
Mratibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa upande wa Zanzibar Shifaa Said ameeleza kuwa hatua hii ya ufuatiliaji imechukuliwa ili kuhakikisha kwamba mchakato wa kupata rasimu ya sharia ya Utangazaji unakwenda vizuri na hatimae sheria mpya itayokidhi vigezo vya kihabari ipatikane.
Kwa upande wake, Salim Said, mwandishi wa habari mkongwe amesisitiza kwamba vyombo vya habari havina nia mbaya na serikali, bali ni washirika muhimu katika kuleta maendeleo kwa jamii hivyo jitihada za ZAMECO na wengine katika kuendeleza maboresho ya sheria ya Utangazaji zinachukuliwa kama sehemu ya ushirikiano mzuri kati ya vyombo vya habari na serikali.
“Vyombo vya habari havina uadui na Serikali, sisi ni washirika wazuri na wenye lengo jema kwa jamii na nchi kwa ujumla, kwa kuzingatia vyombo vya habari ni nguzo ya maendeleo ya uchumi” Alisema Salim Said.
Katibu Tume ya Kurekebisha Sheria ndugu Mussa Kombo Bakari aliwapongeza ZAMECO kwa jitihada wanazozichukuwa kutafuta maendeleo ya tasnia ya habari na kubainisha kuwa mapendekezo waliyowasilisha yamepokelewa na kufanyiwa kazi.
“Tume imekwisha yapeleka mapendekezo hayo katika mamlaka husika na tunatumaini kwamba mapendekezo hayo yatachukuliwa kwa uzito unaostahili ili hatimaye rasimu ya mswaada wa sheria hio ipatikane , alieleza Katibu Mussa.
Nae mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa ametoa shukrani kwa katibu na wafanyakazi wote wa Tume kwa ushirikiano wao katika mchakato huu wa kupata sheria mpya huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kuhakikisha upatikanaji wa sheria mpya kwa maslahi ya Zanzibar na wazanzibari wote.
Ni takribani miaka 20 sasa wadau wa maswala ya habari Zanzibar wamekua wakipambania marekebisho ya sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu No. 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya mwaka 1997 na Sheria ya Utangazaji No. 7 ya 1997 ambayo ilifanyiwa marekebisho na Sheria No. 1 ya 2010 , ambapo Oktoba mwaka jana Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar ilipokea mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya uatangazaji lengo ni kupata sheria huru iliyokua rafiki kwa tasnia ya habari na jamii kwa ujumla.
KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024 ARIDHISHWA NA MRADI WA TANGA UWASA
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 Godfrey Mnzava katikati akifungua koki ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji wa kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Kata ya Chongoleani Jijini Tanga unaofanywa na mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya kushoto ni Mhandisi wa Miradi wa Tanga Uwasa Mhandisi Violeth Kazumba
Na Oscar Assenga,TANGA.
Mradi huo pia utahusisha kata za Mabokweni na Mzizima Jijini Tanga zenye mitaa 10 na wakazi wapatao 26,071 ambapo miundombinu inayojengwa katika mradi huo inakusudia kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma kwa wakazi wa maeneo hayo na hivyo kupata maji kwa kila siku kwa saa 24.
Lakini pia ikiwagusa watumiaji wengine ikiwemo wa viwanda,biashara pamoja na kampuni inayohusika na ulazaji wa bomba ka mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Jijini Tanga nchini Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo na kuuzindua ,Mnzava alisema wameridhishwa na mradi huo wa Tanga Uwasa kutokana na kwamba wao wamekuwa wakitekeleza maelekezo ya Serikali ya kutangaza miradi yote na zabuni kwenye mfumo wa kidigitali wa zabuni (NEST).
Alisema kwamba wanaendelea kuelekeza na kusisitiza hilo na ndio maelekezo ya Serikali miradi yote ya maendeleo ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu,wahisani,wadau wa maendeleo,mchango wa wananchi hata kama ni mapato ya ndani ya taasisi husika kama ni halmashauri na wakala wa serikali maelekezo kupitia sheria za kudhibiti matumizi ya fedha kwenye ununuzi wa umma yanawaelekeza takwimu zote zifanyike zipitia kwenye mfumo huo.
Alisema kwamba walikuwa na Tanel sasa wapo kwenye NEST lengo kubwa likiwa ni kudhibiti namna ya utoaji wa tenda ambapo mfumo huo umetengenezwa vizuri jinsi unavyoingia unakuchagua unakidhi vigezo vya kupata zabuni au haukidhi hautapata zabuni na hivyo kuondoa malalamiko na manunguniko.
Aidha alisema pia lakini hakuna upendeleo kwa hiyo katika utekelezaji wa mradi huo wamefanya hivyo niendelee kusisitiza ujumbe ufike kote nchini lazima waende kwenye mfumo wa Nest kwa sababu ndio mfumo waliopewa kwa sababu ya manunuzi ya umma kazi nzuri ya utekeleza wa mradi na mwenge wa uhuru upo tayari kufungua.
Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi huo,Mhandisi wa Miradi wa Tanga Uwasa Mhandisi Violeth Kazumba alisema utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Novemba mwaka 2022 ambapo ujenzi wake umefanywa na Mkandarasi M/S Engineerin Plus wa Jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Kazumba alisema kwamba mradi huo wa uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kata ya Mzizima,Mabokweni na Chongoleani umefadhiliwa na Taasisi inayohusika na ulazaji wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanzania.
Ambapo usanifu wake umekadiriwa kugharimu kiasi cha sh.Bilioni 2,352,201,500 na hadi sasa mkandarasi amekwisha kulipwa kiasi cha fedha taslimu sh.Bilioni 1,823,766,540 sawa na asilimia 79.46.
Alisema mradi huo umekamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kwa asilimia 100 na hadi sasa unatoa huduma kwa jamii na mamlaka hiyo inaendelea kufanya maunganisho ya maji kwenye matawi pamoja na kwa watu binafsi kwa mujibu wa maombi yanayopokelewa kutoka kwa wahitaji.
“Ujenzi wa mradi huu ulihusisha ununuzi na ulazaji wa mabomba (kipenyo cha 315mm, 250mm,200mm,150mm na 110mm) kwa urefu wa mita 24,000,ununuzi na ufungaji wa viungio vya mabomba,ujenzi wa chemba 54 na usimikaji wa alama 309 za kuonesha njia aya mabomba”Alisema.
Akizungumzia faida za mradi huo Mhandisi Kazumba alisema kwamba utawezesha wakazi wa Kata ya Mzizima,Mabokweni na Chongoleani kupata huduma ya maji safi kila siku kwa saa 24 na itawezesha uwekezaji zaidi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa Bomba la mafuta ghafi (EACOP).