Friday, 10 November 2023
Thursday, 9 November 2023
BODI YA TASAC YAUNGA MKONO NA KUPONGEZA JITIHADA ZA TPA KUJENGA BANDARI YA KUHUDUMIA MZIGO MCHAFU KISIWA CHA MGAO
BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeunga mkono na kupongeza jitihada za Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kujenga Bandari ya kuhudumua mizigo Mchafu eneo la Kisiwa -Mgao.
Ujenzi huo unatarajiwa kufanyika katika kisiwa hicho kilichopo katika Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Mkoani Mtwara ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma karibu na wananchi.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Capt. Mussa Mandia akiwa katika ziara hiyo ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAC chini ya usimamizi wa Bodi hiyo.
Wednesday, 8 November 2023
REA YATENGA BILIONI 10 KUSAMBAZA MITUNGI YA GESI VIJIJINI
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (kulia), akiwasilisha Taarifa ya Utendaji Kazi wa Wakala hiyo kwa Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga (katikati), Novemba 7, 2023. Naibu Waziri alitembelea Makao Makuu ya REA jijini Dodoma na kuzungumza na Menejimenti ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwe kushika wadhifa huo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka.
Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge anayewakilisha Vijana Mbinga, Judith Kapinga akiwasha jiko la gesi muda mfupi kabla ya kugawa majiko hayo kwa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma hivi karibuni. Mheshimiwa Kapinga aligawa majiko hayo ikiwa ni sehemu ya Mpango Maalumu wa Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuwawezesha wananchi wa vijijini kupitia Wabunge wao, kutumia nishati safi ya kupikia.
Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakiwa katika picha ya pamoja. Wanawake hawa wamejiwekea utaratibu wa kuchanga fedha na kununua majiko na mitungi ya gesi ambapo hugawa katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha wanawake waishio vijijini kutumia nishati safi ya kupikia.