Monday, 7 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU AGOSTI 7,2023




 



Share:

Sunday, 6 August 2023

DKT SIMEO: MICHEZO NI NGUZO MUHIMU YA UTULIVU NA USALAMA KWENYE NCHI

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati alipozindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akizungumza wakati alipozindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime
Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Tanga Edgar Mdime akizungumza kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo
MKUU wa Idara ya Maabara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Sinde Mtobu akieleza umuhimu wa uchangiaji damu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt Japhet Simeo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kulia ni Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime

Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Tanga Edgar Mdime akichangia damu



Na Oscar Assenga, TANGA.

MGANGA Mkuu wa Mkoa wa Tanga Japhet Simeo leo amezindua zoezi la wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu ya Simba kuchangia damu katika Zahanati ya Kisosora Jijini Tanga huku akieleza kwamba michezo ni moja ya nguzo muhimu katika utulivu na usalama kwenye nchi.

Simeo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba kwenye uzinduzi huo alisema kwamba michezo ina tija sana katika maisha ya binadamu ikiwemo kuwaunganisha jamii na kutengeneza undugu.

Alisema kwamba uchangiaji wa damu ni muhimu ili kuokoa maisha ya wagojwa wahitaji wa damu wakiwemo waluopata ajali, wakina mama wajawazito na watoto waliopo katika hospital mbalimbali mkoani Tanga.

Mganga Mkuu huyo aliwapongeza wanachama hao kwa utayari wao wa kuona umuhimu wa kuchangia damu ambayo itakwenda kusaidia jamii yenye uhitaji huku akizitaka Taasisi, Vikundi na watu binafsi kuendelea kuwa na utamaduni huo ili kuweza kuokoa maisha ya watu wanaofika hospital kupata huduma hiyo.

"Nawapongeza mashabiki wa timu ya Simba SC kwa utayari wenu kuja kuchangia damu mimi nawaambia hii ni sadaka na thawabu kubwa sana mliyoitoa kwa wenzenu wenye uhitaji wa damu " Alisema Simeo.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Matawi ya Klabu ya Simba SC Edgar Mdime alisema kwamba zoezi la uchangiaji wa damu imekuwa ni utaratibu waliojiwekea kila mwaka lengo likiwa kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kuokoa maisha ya wahitaji.

Alisema bado wanasukumwa kuchangia damu katika hospitali wakitambua kuwa uhitaji wa damu ni mkubwa kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu hivyo licha ya kushiriki siku hiyo adhimu kwao bado wanaendelea kuhamasishana kujitoa kwa pamoja katika zoezi hilo.

Aidha alisema walianza na zoezi la usafi kubwa zaidi ilikuwa ni kuchangia damu na hamasa kubwa sana ambayo imetokea kwa mkoa huo kwa wana Simba na matawi yote wameungana kwa pamoja kwa ajili ya zoezi hili la kuchangia damu

Hata hivyo alisema kwamba wanajua damu ni muhimu sana kwa kila mmoja hasa ukizingatia wapo wakina mama wanaojifungua katika hospitali ikiwemo ajali zinatokea watu wanahitaji kuwekewa damu kwa hiyo wao wamehamasika kama wanajamii ukiachana na suala la michezo.

Tambo 

Mwenyekiti huyo alisema kwamba dhamira yao kubwa msimu huu lazima timu yao ichukue Ubingwa kutokana na uwepo wa kikosi kipana kulingana na usajili mkubwa uliofanyika wakiamini lazima timu hiyo ifanye makubwa katika mashindano ya ndani na hata kimataifa pia.

Katika hatua nyengine, Mdime alituma salamu kwa watani zao timu ya wananchi Yanga kuelekea mechi za Ngao ya jamii zitakazo chezwa Mkwakwani Tanga ambapo ametamba kwa kusema kuwa hawatakuwa tayari ngao hiyo aichukue tena mtani mbele yao.

Mchezo huo unatarajiwa kucheza Agosti 9 mwaka huu katika uwanja wa CCM Mkwakwani Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ngao ya jamii watakutana na matajiri wa Chamanzi Azam FC huku Simba SC wao wakiminyana na Singida Fountain Gate katika hatua ya nusu fainali timu zote zikitafuta nafasi ya kuanza vyema msimu 2023/2024 .
Share:

TBS yatoa elimu kwa wananchi kwenye Maonesho ya Nanenane Mwanza

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Ziwa limeshiriki maonesho ya wakulima Nanenane 2023 katika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza, kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau na wananchi kuhusu udhibiti na ubora wa bidhaa mbalimbali.

Meneja TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka amesema shirika hilo limetumia fursa ya maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali wakiwemo wazalishaji wa mazao ya chakula yatokanayo na kilimo, ufugaji pamoja na uvuvi ili kuhakikisha wanazalisha bidhaa zinazokidhi viwango.

“Kaulimbiu mwaka huu inasema ‘vijana na wanawake ni msingi imara wa uendelevu katika uzalishaji wa mifumo ya chakula’, hivyo TBS tuna jukumu la kuhakikisha chakula kinachozalishwa kinakidhi matakwa ya viwango na ni salama kwa matumizi ya bindamu” amesema Kanyeka.

Kanyeka ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo, TBS pia inatoa elimu kwa wananchi ili kutambua bidhaa zenye ubora, zinazofaa kwa matumizi na zilizopigwa marufuku ikiwemo vipodozi ili kuepuka matumizi yake kwani zina madhara makubwa kiafya.

Naye Afisa Mkaguzi TBS Kanda ya Ziwa, Musa Mayala amesema pia wanatoa elimu kwa wazalishaji na wauzaji wa bidhaa za vipodozi na chakula ili kuhakikisha wanadhibiti ubora wa bidhaa zao na kuepuka kuuza bidhaa zilizopigwa marufuku, zilizoisha muda huku pia wakizingatia utunzaji bora wa bidhaa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kwa watumiaji/ walaji.

Mayala ameeleza kuwa pia TBS inawahamasisha wajasiriamali kusajili bidhaa zao na kupata nembo ya ubora huku akiwatoa hofu kwamba Serikali imeweka utaratibu mzuri wa kuwainua wajasiriamali wadogo kwa kuwapa fursa ya kupata nembo ya ubora bure kwa kipindi cha miaka mitatu.

“Tunalenga kuwainua wajasiriamali wadogo kutoka hali ya chini kwenda hali ya juu ambapo Serikali imetoa utaratibu wa kuwasaidia kufanya shughuli zao kwa miaka mitatabu bila kulipia gharama za nembo ya ubora. Pia tunatoa mafunzo ya aina mbalimbali kuhusu namna ya kuandaa bidhaa zenye ubora na kudhibiti madhara yanayoweza kuwapata watumiaji” amesema Mayala.

Mmoja wa wananchi waliotembelea banda la TBS kwenye maonesho ya Nanenane Nyamhongolo jijini Mwanza ni David Maduhu ambaye ameshauri shirika hilo kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa bidhaa zinazozalishwa ama kuingizwa nchini ili kuhakikisha wazalishaji wanazingatia ubora uliokusudiwa.

“Nafurahi pia wamenipa vipeperushi vyenye orodha ya bidhaa ambazo hazipaswi kuwa sokoni. Nashauri waendelee kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa bidhaa zinazosajiliwa na kupewa nembo ya ubora ili kuhakikisha wazalishaji wanazingatia ubora ule ule uliokusudiwa” amesisitiza Mayala.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka akieleza kuhusu ushiriki wa shirika hilo kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kanda ya Ziwa Magharibi kwenye uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza yakishirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera.
Meneja TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka akizungumza kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Nyamhongolo jijini Mwanza.
Afisa Mkaguzi TBS Kanda ya Ziwa, Musa Mayala akieleza namna shirika hilo linavyowasaidia wajasiriamali kuboresha bidhaa zao ili kukidhi viwango na kupata nembo ya ubora.
David Maduhu ambaye no mmoja wa wananchi waliotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza akiwa na vipeperushi mbalimbali vyevye elimu kuhusu bidhaa zenye ubora na zilizopigwa marufuku sokoni.
Wananchi wakipata elimu kwenye banda la TBS kwenye Maonesho ya Nanenane 2023 Nyamhongolo jijini Mwanza.
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka (katikati) na Afisa Afisa Mkaguzi TBS Kanda ya Ziwa, Musa Mayala (kushoto) wakitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la shirika hilo kwenye maonesho ya Nanenane Nyamhongolo jijini Mwanza.
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamuge waliotembelea banda la shirika hilo.
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Happy Brown Kanyeka (wa pili kushoto waliokaa) na Afisa Afisa Mkaguzi TBS Kanda ya Ziwa, Musa Mayala (wa kwanza kushoto waliokaa) wakitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyamuge.
Wanafunzi wakipata elimu kwenye banda la TBS kwenye Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika uwanja wa Nyamhongolo jijini Mwanza yakishirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera kuanzia Agosti Mosi hadi Agosti 08, 2023.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA
Share:

SUWASA YATAJA MIKAKATI YAKE YA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA MAJI




Na Alex Sonna-SINGIDA

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA), imetaja mikakati yake ya kuimarisha upatikanaji wa maji na uondoshaji wa majitaka ikiwamo kutekelezwa kwa mradi wa maji wa Miji 28 unaogharimu Sh.Bilioni 45.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 5, 2023 mjini Singida, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA), Bw.Sebastian Warioba, amesema kuna mradi mkubwa unaoendelea kwasasa ambao umeanza utekelezaji mwezi Aprili, 2023 kupitia mradi wa Miji 28 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2024.

Amesema mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji na kuwafikia wateja kwa asilimia 90 kwenye Manispaa ya Singida.

“Kwa manispaa ya Singida tuna takribani Sh.Bilioni 45 za mradi wa miji 28, tunashukuru serikali mkandarasi ameanza kazi na anafanya kazi maeneo yote ya mradi,”amesema Bw.Warioba

Amesema kuna miradi mingine wanategemea kutekeleza kwa kupata fedha serikali kuu ili kuwafikia wananchi ambao hawajafikiwa na mtandao wa maji.

“Manispaa tuna kata 18 tumeshafikia kata 16 ambapo kuna baadhi hazijafikiwa kwa ukamilifu na zingine mbili hatujazifikia kabisa, tumewasilisha andiko Wizara ya Maji ili kupata fedha zaidi ya Sh.Bilioni tatu,”amesema.

Amebainisha kuwa Mamlaka hiyo ina wateja wa maunganisho ya maji safi 18,000 na imewafikia kwa asilimia 78.

“Eneo tunalohudumia ni Manispaa ya Singida pamoja na miji mingine saba nje ya Manispaa ambayo ni Buguno, Njia panda, Ikungi, Sepuka, Irisia, Puma na Makiungu ambapo tumewafikia wateja kwenye miji hiyo kwa asilimia 68,”amesema.Bw.Warioba

Hata hivyo, amesema suala la upotevu wa maji lipo kwa asilimia 31 na kuna mikakati ya kukabiliana na hali hiyo.

“Upotevu unachangiwa na vitu mbalimbali moja wapo ni matumizi ya yasiyosahihi au wizi wa maji, pia inasababishwa na uchakavu wa miundombinu, tunachofanya kuna maeneo tumefanya ukarabati, kubadilisha mita za zamani zinazosoma chini ya kiwango,”amesema.

Amesema mapema mwaka huu mamlaka hiyo imepata mita zaidi ya 20,000 za maji ambazo zinatumika kubadilisha na kuunganisha wateja, huku ikipewa mabomba ya zaidi ya sh. Milioni 300.

“Tunatarajia kupata mabomba mengine ya zaidi ya Sh.Bilioni moja ili kubadilisha na kuunganisha kwa wateja ili kuondokana na upotevu wa maji,”alisema.

Kuhusu uondoshaji wa majitaka, amesema Manispaa hiyo haikuwa na huduma hiyo na kuanzia mwaka huu wameanza utekelezaji wa mradi wa uondoshaji majitaka ambapo wameanza na kujenga mabwawa eneo la Manga.

“Mabwawa haya yatakapokamilika mwishoni mwa mwaka 2024 tunategemea makazi ya wananchi yatakuwa salama kwa kuondosha majitaka na kupeleka kwenye mabwawa na maji hayo yatatibiwa na baadaye yataweza kutumika kwa manufaa ya kiuchumi ya wakazi wa hapa kama vile shughuli ya kilimo,”amesema.

Kadhalika, amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Maji wameanza upembuzi yakinifu na kufanya tathmini ya athari za mazingira ili kutekeleza mradi kubwa wa majitaka wa kuweka mtandao kwenye makazi ya watu na kuongeza mabwawa ya majitaka.

“Wiki ijayo tunategemea mtaalamu mshauri atafika ili kupita maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuhuwisha study iliofanyika mwaka 2015 ili zitafutwe fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi huu maana wakati ule mradi ulikuwa wa gharama ya zaidi ya Sh.Bilioni 45 kwa kuwa muda umepita mrefu wizara imeona ufanyike upya ili kuendana na hali halisi ya sasa,”amesema.

Ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa pindi inapotokea hujuma kwenye maeneo ya miradi na miundombinu.


Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA Sebastian Warioba akiwa kwenye Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kutibu majitaka eneo la Manga Manispaa ya Singida. Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi MS. Nangai & pentels Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 1.765
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI AGOSTI 6, 2023














Share:

Saturday, 5 August 2023

PESA IPO UKICHEZA MICHEZO YA VIRTUAL NA MERIDIANBET

Michezo ya Virtual ni michezo ambayo inapatikana ndani ya Meridianbet ipo mingi sana na huchezwa kwa dakika chache na kukupatia pesa kwa muda mfupi sana yani bila kupoteza muda wako kutokana na mchezo uliouchagua.

Michezo ya Virtual safari hii imekuja na bonasi ambayo itatoka siku ya Jumatatu saa 05 asubuhi kwa wale wateja ambao watakuwa wameshinda na kwa wale wateja ambao hawajashinda, watapata rejesho la 15% ya pesa ambayo utakuwa umepoteza kulingana na dau ambalo uliweka.

Ni rahisi kabisa wewe ingia www.meridianbet.co.tz uweke pesa na uanze kucheza michezo mbalimbali ikiwemo ile ya kasino inayopatikana kwenye Virtual kama vile Luck Looty, book of gold, keno na mingine kibao.

 Aviator, poker, Roullette, Wild Icy Fruits, Piggy Party na mingine kibao upige pesa na Meridianbet. Ingia www. Meridianbet.co.tz.

Masharti ya Mchezo wa Virtual

              Promosheni hii imeanza siku ya Alhamisi tarehe 03 na itaisha hapo kesho tarehe 06 saa 6 usiku hivyo mteja wa Meridianbet kama bado hujaanza kucheza michezo ya Virtual muda ndio sasa.

              Promosheni hii itahusisha michezo ya Virtual tuu na sio mingine. Kwahiyo ukishaingia pale Meridianbet chagua michezo ya Virtual na ucheze sasa.

              Na wale ambao watakuwa ni washindi watapata bonasi zao siku ya Jumatatu saa 05 asubuhi. Ingia sasa www.meridianbet.co.tz na ucheze Virtual.

              Promosheni hii ni kwa wachezaji wote waliojisajili kwenye tovuti na APP ya Meridianbet.co.tz.

              Kwa kujisajili na Meridianbet.co.tz, kila mchezaji atakubaliana na sheria za promosheni.

              Ofa hii ni halali kwa mtumiaji mmoja, anuani ya IP au kaya.

              Meridianbet inahifadhi haki ya kubadilisha sheria za promosheni hii wakati wowote pamoja na kusitisha promosheni hii.

              Vigezo na Masharti kuzingatiwa

 

 PIGA MKWANJA NA VIRTUAL

Baada ya kusoma vigezo na masharti sasa ni wakati wa kukusanya maokoto, weka pesa kwenye akaunti yao ya Meridianbet halafu kucheza ni rahisi tuu kwani utacheza kile ambacho unakipenda.

Pesa inapatikana ndani ya saa chache sana baada ya ushindi kwani pia hauhitaji muda mrefu sana kutumia kwenye kuucheza huu mchezo. Cheza sasa Virtual na Meridianbet ujikusanyie mpunga kabla ya Ligi mbalimbali hazijaanza.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Meridianbet wameamua watoe ofa ya 15% kwa wale ambao watakuwa wamepata hasara ya kile ambacho wamekiweka, vilevile faida ni kupata bonasi siku ya Jumatatu yake baada ya kuwa wikendi umetumia muda wako vizuri kucheza Virtual.

 

Pia kumbuka kuwa kama ukiwa umeshinda Meridianbet wanakuhaikishia kuwa siku ya Jumatatu saa 5 asubuhi watakuwekea bonasi ambayo nayo pia utaitumia kuchezea michezo mingine uipendayo ndani ya Meridianbet. Kazi ni kwako wewe mteja wa Meridianbet. Muda ndio huu ingia www.meridianbet.co.tz.

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger