Friday, 7 July 2023
Thursday, 6 July 2023
KITUO CHA SAUTI YA JAMII KIPUNGUNI CHATUMIA UJASIRIAMALI KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA
KITUO cha Sauti ya Jamii Kipunguni Ukonga Jijini Dar es Salaam, kimekuwa kikitumia Ujasiriamali katika harakati za kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye jamii ambayo inawazunguka.
Akizungumza leo Julai 5,2023 wakati Kituo hicho kilipotembelewa na Wanajamii wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kutoka Mkoa wa Shinyanga na Dar es Salaam, ambao wapo katika Mafunzo ambayo yameandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, Mwanakituo wa kituo hicho Bw.Juma Masanja amesema wamekuwa wakitumia Ujasiriamali kuwaleta jamii pamoja na kutoa elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia.
Amesema kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kukusanya taka na kuzibadilisha kuwa fursa hasa kutengeneza bidhaa ambayo kwa wakati huo inahitajika sokoni kama vile taka kuzibadili kuwa mkaa wa kupikia, taka zilizooza (Matunda) kutengeneza wadudu ambao ni chakula cha mifugo.
Aidha amesema wamekuwa na klabu za kupinga ukatili ndani ya jamii ambapo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza vitendo vya ukatili katika maeneo ambayo yapo karibu na Kipunguni Ukonga Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na hayo amesema wamekuwa wakitumia kilimo cha mbogamboga kama sehemu ya kupinga ukatili wa kijinsia pale ambapo wanafanya kilimo na kukutana pamoja kwaajili ya kupeana taarifa .
Nae Mwanajamii wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kutoka Mkoa aa Shinyanga amesema kuwa maendeleo ambayo wameyaona Kipunguni, wamejifunza hivyo watakwenda kuhakikisha katika vituo vyao wanafanya maendeleo na kuhakikisha wanawaweka wanajamii karibu na kurahisisha kutoa elimu ya Kupinga Ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yao.
WADAU WA USAFIRI WAITAKA LATRA KUHARAKISHA UTOAJI RATIBA MABASI YAANZE KUSAFIRI SAA 24
WATUMIAJI wa huduma za usafiri wa Mabasi nchini wameitaka Mamlaka ya kudhibiti usafiri wa majini na nchi kavu (LATRA) kuharakisha utoaji wa ratiba itakayoyawezesha mabasi kutoa huduma za kwenda mikoani kwa Saa 24 .
Kauli ya wadau hao hususani abiria pamoja na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) imekuja siku chache baada ya Serikali kuruhusu huduma za usafiri wa Mabasi hayo kutolewa kwa Saa 24 ikisisitiza kuwa hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi wa nchi kama ilivyo kwa mataifa mengine.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Jijini Dar es Salaam, wadau hao akiwemo Mfanyabiashara wa mazao katika soko la Kariakoo Benson Maona na mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna Ibrahim, wamesema kwa kufanya hivyo pamoja na mambo mengine kwa kiasi kikubwa kutasaidia kutatua tatizo la usafiri nchini.
Akizungumzia kuhusu hilo, Maona amesema kwa kipindi kirefu hususani nyakati za msimu wa sikukuu kumekuwa kukijitokeza tatizo kubwa la usafiri wa kwenda mikoani na kuongeza kuwa hatua hiyo ya Serikali kuruhusu huduma kwa saa 24 kunaenda kumaliza kabisa tatizo hilo.
“ Tunamshukuru Waziri Mkuu kwa kutamka Bungeni hatua ya Serikali kuruhusu huduma za mabasi kwa Saa 24, hatuoni sababu gani zinazozuia huduma hiyo kutolewa hadi muda huu, Mamlaka yenye dhamana ya usimamizi wa usafiri(Latra) ione uzitoa wa kauli ya Waziri Mkuu kwa kutekeleza haraka suala hilo” amesema Maona
Kwa upande Maimuna mbali na kuipongeza Serikali amesema ni vyema Latra ikaharakisha suala hilo ili kuondoa kabisa changamoto ya abiria kulazimika kupanda magari ya mizigo yakiwemo malori hususani nyakati za usiku pale wanapopatwa na dharura mbalimbali na kulazimika kusafiri kwenda mikoani.
“Hivi sasa tunaona ratiba za mabasi zinaanza kuanzia Saa tisa usiku, bado haikakidhi matakwa yetu kama abiria, kuna wengine tunatokea maoneo ya vijijini hivyo kuwepo kwa ratiba ya saa 24 kutatusaidia kupanga vizuri muda wa kusafiri ili kufika tuendako kwa muda unaostahili Latra, Serikali iliona mbali kutaka ratiba za mabasi ziwe ndani ya muda wote mchana na usiku” amesisitiza Maimuna
Awali Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA) kupitia kwa Mwenyekiti wake Abdallah Mohamed amesema waliopokea kwa uzito mkubwa kauli ya Waziri Mkuu ya mabasi kutembea kwa saa 24 na kwamba wao kama wasafirishaji walishajipanga na suala hilo hivyo wanasubiri ratiba kamili itolewe na Latra.
"Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukisikia kilio chetu cha muda mrefu kwa kuturuhusu kutoa huduma za usafiri kwa Saa 24, ukweli kama nchi tulichelewa kutoa huduma hiyo kutokana na kuwa na manufaa mengi hasa katika eneo zima la ukuaji wa uchumi wa Taifa letu” amesisitiza.
"Aidha pamoja na Shukrani zetu kwa Rais Samia sisi kama wasafirishaji pia tunapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Spika wa Bunge Dk Tulia Akson kwa kulisimamia suala hadi leo hii tulipofika hapa, ukweli tunawashukuru sana viongozi wetu hawa kwa kuzingatia maslahi ya taifa" ameongeza
MBUNGE MTATURU AFANYA YAKE IKUNGI
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Jumanne Mtaturu Julai 5,2023, amechangia ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Ikungi ili kusaidia kukamilisha ujenzi huo.
Bingwa huyo wa siasa za "Maneno kidogo, kazi zaidi," amekabidhi Mifuko 50 ya saruji, Mbao za kufanyia blundering na kokoto lori 3 vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 3.9.
Akikabidhi kwa niaba ya mbunge, Ally Rehani ambaye ndiye katibu wa mbunge huyo, amesema amepeleka vifaa hivyo ikiwa ni muendelezo wake wa kuchangia ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ambayo ndani yake kuna ukumbi mkubwa wa mikutano.
"Kukamilika kwa Ukumbi huu itakifanya chama kuwa na uhakika wa vikao vyake sehemu salama na yenye hadhi" alisema Rehani.
Akipokea vifaa hivyo katibu wa CCM wilaya Stahmili Dendego amemshukuru Mbunge Mtaturu kwa moyo wake wa kukisaidia chama kila mara.
Ameeleza mchango wa leo ni miongoni mwa michango mingi aliyokipatia chama.
Sio mara ya kwanza kwa Mtaturu kuchangia ujenzi huo ambapo Mei 8,2023,alikabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh.Milioni 1.8 ambavyo ni Gypsum Board 75 na ndoo tano za rangi ambavyo alivikabidhi mbele ya Kamati ya Siasa ya Wilaya.
Mbali na kutoa msaada wa kifedha,Juni 15,2021,Mtaturu pia alichangia nguvu kazi kwa kushiriki uzinduzi wa ujenzi wa ofisi hiyo ambapo kwa kushirikiana na viongozi wa CCM Wilaya na Wananchi walichimba msingi wa jengo hilo.
Aidha,katika uzinduzi huo alichangia bati 100 na mifuko ya saruji 100 vyote vikiwa na thamani ya Sh Milioni 5.9.
TASAC WASHIRIKI KATIKA MAONYESHO YA BIASHARA YA SABASABA
AFISA Masoko Mwandamizi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye Banda lao katika Maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Mwananchi aliyetembelea Banda la TASAC akipatiwa zawadi katika Banda la TASAC
Watumishi \wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Martha Kelvin wa pili kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wengine wa Shirika hilo wakiwa kwenye Banda lao
Na Mwandishi Wetu,Dar es Saalam
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania, TASAC linashiriki katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa.
Maonesho hayo yenye Kauli Mbiu “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji”, yameanza tarehe 28 Juni, katika viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam na yatahitimishwa tarehe 13 Julai , 2023.
Akizungumza leo Afisa Masoko Mwandamizi wa Shirika hilo Martha Kelvin alisema lengo la kushiriki maonesho hayo ni kujenga uelewa na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kazi na majukumu yanaotekelezwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura 415 na mabadiliko yake.
Hata hivyo alisema kwamba TASAC inawaalika wananchi wote kutembelea maonesho haya na kufika katika banda la TASAC lililopo katika ukumbi wa Karume banda namba 22 na 23.
MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA CRDB ATEMBELEA MAONYESHO YA SABASABA
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto) akiwa ameambatana na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd (kulia) pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo wakati wakitembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Latifa Mohamed (wapili kulia) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Badru Idd na kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Sabasaba, Zoe Kafulusu.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Omar Said Shaban akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati walipokutana katika ukumbi maalum wa wageni katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na baadhi ya Maafisa wa benki hiyo wanaotoa huduma za kibenki katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa benki hiyo wanaotoa huduma za kibenki katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo wakati alipotembelea maonyesho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mahusiano ya Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Mashariki, Lughano Nselu wakati alipotembelea Banda la benki hiyo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanaoendelea katika viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, jijini Dar es salaam leo wakati alipotembelea maonyesho hayo.
Wednesday, 5 July 2023
HUAWEI AT MWC SHANGHAI 2023:BOOSTING 5G EVOLUTION TOWARDS 5.5G REVITALIZE THE DIGITAL ECONOMY
Huawei has shown up in full force for MWC Shanghai 2023, with their activities all falling under their theme of "GUIDE to the Intelligent World". This year, the company's activities include an experiential tour that takes audiences to multiple cities to learn about their technology and business, as well as the launch of its newest innovative products and solutions for 5GigaGreen, 5G intelligent core networks, Intelligent OptiX Networks, private line + X products, and other intelligent digital transformation solutions.
At these activities, Huawei will also host numerous roundtables and dialogues with global operators, industry partners, and opinion leaders, to explore a variety of topics which include speeding up 5G prosperity, advancing intelligent digital transformation, and striding towards the 5.5G era to realize business, industry, and social value. The company says its goal is to create new value for customers and revitalize the digital economy through sustained innovation.
Sabrina Meng, Huawei's Rotating Chairwoman and CFO, gave a keynote titled "Embracing 5G transformation". She said, "The digital infrastructure of the future intelligent world will be deeply integrated into every aspect of our lives, industry, and society. It won't be based on advancements in individual technologies, but rather on incredibly massive, complex systems – the convergence of multiple elements. It's going to require systems-level thinking and design. When watching a chess game, you can see the big picture. But when you're playing chess, you focus on the details. Likewise, systematic capabilities to integrate technology and transform management are critical for the future success of 5G. First, let's talk about integrating different technologies. We can achieve greater synergy across cloud, networks, edge, and devices through systematic design and innovation across domains. When coupled with optimization across software, hardware, chips, and algorithms, we can address the challenges associated with developing complex solutions for vastly different industrial scenarios. Next, management transformation. Digital and intelligent transformation is not just about technology itself. It's more about transforming your approach to management. Going digital requires redefining the relationships between people, events, things, and theory, and adopting a more open, forward-looking management approach to address future challenges."
There are currently over 1.2 billion 5G users worldwide, and operators who moved quickly to develop 5G are already enjoying the first wave of benefits. This is thanks to the increasing network requirements being set by new applications in various markets. In the consumer market, new services like New Calling, cloud phones, and glasses-free 3D require faster data rates and lower latency, while in the industrial market, the RedCap ecosystem has matured, the passive IoT market is expanding, and the Internet of Vehicles (IoV) requires higher uplink speeds. These all-scenario applications are expected to result in 100 billion connections. These new service models are also expected to drive industry upgrade that will create a second wave of benefits.
Commercial 5G services hit the market four years ago, and has since been introduced to more than 17,000 private-network projects around the world. Both revenue from 5G private networks and the number of industrial connections have tripled. In addition, many operators have leveraged the CNY10 billion in revenue earned from 5GtoB private networks to drive a CNY100 billion increase in DICT revenue from cloud, data storage, and platform services. While many 5GtoB services were piloted in China, they have since expanded to other parts of the world, and have been commercially replicated in Asia Pacific, Europe, the Middle East, and Africa. These services allow industry customers to reduce costs and improve efficiency, while enabling intelligent digital transformation in industries like manufacturing, ports, mines, oil fields, and healthcare.
5.5G is also rapidly approaching for the communications industry. 5.5G technologies are expected to improve network capabilities 10-fold and create 100 times more business opportunities for operators. At this year's MWC Shanghai, Huawei is showcasing four of the major features of 5.5G – 10 Gbit/s downlink, 1 Gbit/s uplink, 100 billion connections, and native AI. It is also exploring the five connectivity areas expected to go mainstream with 5.5G – connectivity for people, for things, for vehicles, for industries, and for homes. Huawei has already started helping a number of operators around the world begin commercial verification of 5.5G. The 5.5G industry will continue growing quickly as the first release of 5.5G standards is expected to be frozen in the first half of 2024 and related technologies have already been extensively verified.
MWC Shanghai 2023 runs from June 28 to June 30 in Shanghai, China. Huawei will showcase its products and solutions at stands E10 and E50 in Hall N1 of Shanghai New International Expo Centre (SNIEC). Together with global operators, industry professionals, and opinion leaders, we dive into topics such as speeding up 5G prosperity, striding towards the 5.5G era, and intelligent digital transformation. 5.5G creates new business value in areas like connecting people, Internet of Things (IoT), and Internet of Vehicles (IoV), supporting countless industries as they move towards an intelligent world
SERIKALI YAVIKUMBUKA VYUO VYA UALIMU NCHINI
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya uwekezaji mkubwa kwenye Vyuo vya Ualimu nchini kwa kujenga majengo mapya, kukarabati pamoja na kuweka vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Akikagua utekelezaji wa Miradi ya Elimu katika Chuo cha Ualimu Kasulu na Kabanga yote ikiwa wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Franklin Rwezimula amesema lengo ni kuhakikisha walimu tarajali wanapata mafunzo katika mazingira bora.
Amesema maboresho hayo yamekwenda sambamba na kuweka mifumo inayotumia nishati asilia kupikia akitolea mfano Chuo cha Ualimu Kabanga ambacho kimejengewa mifumo hiyo na kupunguza matumizi ya kuni.
“Chuo cha Ualimu Kabanga ni kielelezo cha utunzaji wa mazingira katika ujenzi wa miundombinu yake kwa kuwa imewekewa mifumo ya kuchakata maji taka na kupata mbolea huku maji yakitumika tena kumwagilia na hapo hapo kupata gesi inayotumika kupikia,” amesema Dkt. Rwezimula
Nae Mratibu wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Cosmas Mahenge amesema Chuo cha Ualimu Kabanga na kile cha Kasulu ni moja ya Vyuo vilivyonufaika na Mradi huo kwa kujengewa miundombinu mipya na kuwekewa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Amesema katika Chuo cha Ualimu Kabanga majengo yake yamejengwa upya na kuwa Chuo cha mfano katika kutunza mazingira kwa kuwa kinatumia biogas huku kile cha Kasulu kikijengewa maabara ya Fizikia, Kemia, Bailojia pamoja na Maktaba.
“Kwa ujumla Mradi huu ni mkombozi wa elimu ya ualimu kwa kuwa pamoja na kujenga na kukarabati umetoa mafunzo kwa wakufunzi, ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, vifaa vya kufundishia na kujifunzia,”ameongeza Mratibu Mahenge.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Ualimu Kabanga Edward Wawa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kufanikisha ujenzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu Kabanga na kuahidi kuleta ufanisi zaidi katika utendaji.