Wednesday, 8 March 2023

Picha : RAIS SAMIA AHUTUBIA BARAZA LA WANAWAKE WA CHADEMA MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Maridhiano kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe aliyeikabidhi kwa niaba ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023.


Viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) pamoja na Wanachama wa Chama hicho wakishangilia wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia katika Mkutano wa Baraza hilo uliofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2023.


Share:

SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI YAWATESA WANAWAKE



 Na Woinde Shizza,ARUSHA
Imebainika kuwa ugonjwa wa saratani hapa nchini umeonekana kuwa tatizo linaloongezeka kila mwaka hususani saratani ya mlango wa kizazi wa wanawake kwani kati ya wagonjwa 100 wenye saratani za aina mbalimbali wagonjwa asilimia  47% wanakutwa na saratani ya mlango wa kizazi.

Hayo yamebainishwa na meneja wa huduma ya kinga ya saratani kutoka Taasisi ya Ocean road Dr.Maguha Stephano wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mount Meru sehemu ambayo wameweka kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya saratani huduma ambazo zinatolewa na madaktari bigwa wa saratani kutoka taasisi hiyo bure .

Alisema kuwa kati ya wanawake 100 wenye magonjwa ya saratani za aina mbalimbali ikiwemo saratani ya mfumo wa chakula (koo)na saratani ya matiti , asilimia  47%  ya wagonjwa wanasaratani ya mlango wa kizazi.

Alisema kuwa saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inaongoza hapa nchini kwa kusababisha wagonjwa wengi ,pamoja na vifo ambavyo vinatokana na ugonjwa wa huo ,hivyo aliwataka akina mama wajitokeze kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wa awali ambapo alisema kinachotia moyo ni mabadiliko ya awali ya chembembe hai zilizopo katika mlango wa kizazi yanatibika kabisa .

“Tupo hapa na wagonjwa ambao tutawabaini wana mabadiliko ya awali tunawapa matibabu ya awali ya saratani ya mlango wakizazi na tangu tuanze kutoa huduma hii kwa apa Arusha juzi (jana) tumewagundua akina mama wanne wana viashiria ya mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi kwa iyo tumeshawapatia tiba kwa hiyo tuna uhakika pia tumewakinga lakini pia tuna wamama watano tumewakuta wana viashiria ya kuwa wanasaratani ya mlango wa kizazi kwa iyo tumechukuwa vinyama kwenye mlango wa kizazi tunavifanyia uchunguzi kwa sababu pia tumekuja na madaktari bigwa wa kuchunguzi wa sampuli za vinyama au majimaji /damu mwilini kuangalia uwepo wa chembechembe za saratani (Patholojia)kwa hiyo pia majibu watapata na wakithibitika kweli wana tatizo hilo tutawapeleka Ocean Road kwa ajili ya matibabu”, alisema Dr. Maguha.

Aidha alisema kuwa saratani ambayo inafuatiwa kwa kusababisha vifo vya wanawake wengi ni saratani ya matiti ,ambayo ndiyo inashika namba mbili na ya tatu ni saratani ya koo la chakula ambapo alifafanua kuwa hizi ndiyo saratani ambazo zinashika kasi na zinasababisha sana vifo vingi vya kina mama vinavyotokana na ugonjwa huo.

“Hatukuwaacha wababa nao pia tunawapa huduma na kwa upande wa kinababa saratani ambayo inaonekana ina wagongwa wengi sana kwa takwimu zetu za taasisi ya ocen road kwa mwaka uliopita ni saratani ya koo la chakula ndio inaongoza ikifuatiwa na saratani ya tezi dume ambayo hii inaadhiri wakina baba wengi lakini pia kusababisha vifo vinavyotokana na saratani kwa kina baba na niseme hizi saratani zote nilizozitaja zina kinga yake na pia zina fanyiwa uchunguzi na ndio maana tup o hapa kufanya uchunguzi wa awali na kuweza kutoa matibabu ya awali ya mabadiliko ya sawali ambapo wakina mama wataonekana wa mabadiliko ya saratani ya mlango wa kizazi", alisema Dr. Maguha.

Alisema kuwa kisababishi kinachosababisha wanawake wengi kupata saratani hii ya mlango wa kizazi ni kirusi kinachoitwa pactheloma ambacho kinasambazwa kwa njia ya kujamiana ambapo mwanamke anapokutana na mwanaume mwenye maambukizi ya kirusi hicho ndio anapopata maambukizi na baada ya muda mrefu maana tafiti zinaonyesha baada ya maambukizi ya kirusi hicho inaweza ikachukua hata miaka 10 au kumi na tano mwanamke huyo kujigundua ,hivyo aliwashauri pia wanawake kuwa na mazoea ya kwenda kupima afya zao mara kwa mara.

Alitaja baadhi ya vihatarishi vinavyompelekea mwanamke kupata hicho kirusi ni pamoja na wasichana kuanza kufanya ngono katika umri mdogo ambapo alifafanua kuwa kwa kufanya hivyo kunamuweka hatarini msichana kupata saratani hii, aidha aliongeza kuwa kuwa na mahusiano na wanaume wengi pia ni hatari pamaja na kuwa na mwanamme mwenye uhusiano na wanawake wengi pia ni hatari .

Aliwataka akina mama kujitokeza kwenda kupima saratani hii kwani haichukui muda ,pia ni rahisi ambapo alibainisha kuwa matokeo ya uchunguzi ni mazuri kwakuwa iwapo ukigundulika una tatizo utapewa tiba ya awali ikiwemo ile ya kugandisha ambayo inazuia chembe chembe hai zisiendelee kubadilika kuwa saratani lakini ukibainika pia una saratani wakati wa uchunguzi itakuwa ni vizuri maana utakuwa umeiwahi saratani ya mlango wa kizazi inatibika kabisa endapo itapatiwa matibabu mapema.
Share:

RAIS SAMIA APOKELEWA KWA SHANGWE NA WANACHAMA WA CHADEMA


Hivi ndivyo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyopokelewa na Maelfu ya Wanachama wa CHADEMA alipotua uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro tayari kwa Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Moshi Kilimanjaro.

Mamia ya Maafisa Usafirishaji (Bodaboda) wameongoza msafara wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuelekea ukumbi wa Kuringe Moshi linapofanyika Kongamano hilo.
Share:

MTANDAO WA POLISI WANAWAKE WAPELEKA FURAHA KWA WAZEE KOLANDOTO SHINYANGA


Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga  ACP Janeth Magomi akizungumza kwenye kambi ya wazee wa Kolandoto.

Na Marco Abel, Shinyanga

MTANDAO wa polisi wanawake mkoa Shinyanga wamefanya matembezi na kutoa msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwenye kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza kilichopo kata ya Kolandoto manispaa ya Shinyanga.

Mtandao huo umetoa msaada tarehe 07/03/2023 katika maadhimisho kuelekea siku ya wanawake duniani ifikapo Machi 8 mwaka huu kwenye kituo cha malezi ya wazee wasiojiweza, Kolandoto mkoani Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwenyekiti wa mtandao wa polisi wanawake mkoa wa shinyanga ambaye pia ni kamanda wa polisi mkoani humo ACP Janeth Magomi amesema wameamua kutoa msaada huo ili kuonyesha upendo na kuwathamini wazee hao kwani kwa kufanya hivyo inawatia moyo na kuona namna serikali na watu wengine wanavyothamini uwepo wao.

“Kuelekea siku ya wanawake duniani sisi kama mtandao wa polisi wanawake mkoa wa Shinyanga tumeona tufike kwenye kituo cha malezi ya wazee wasiojiweza ili kuonyesha thamani yao kwetu na kutambua uwepo wao, tumefurahi kujumuika nanyi siku ya leo”, ameseam Magomi.

Mratibu wa kituo cha makazi ya wazee na wasiojiweza Kolandoto Sophia Kang’ombe amesema wameendelea kutoa huduma za malazi, chakula na matibabu kwa wazee hao licha ya idadi yao kupungua.

 “Kipindi cha nyuma tulikuwa na idadi kubwa ya wazee lakini kutokana na jitihada za serikali kuwaunganisha wazee hawa pamoja na ndugu zao hadi sasa wameweza kupungua na kufikia wanaume 11 na wanawake 5”, amesema Sophia Kang’ombe.


Naye mwenyekiti wa makazi ya wazee kituo cha kolandoto Kija Nipuge amewashukuru Mtandao wa polisi wanawake mkoa Shinyanga kwa kuwatembelea na kutoa msaada kituoni hapo na kuomba wadau wengine kujitokeza kuunga mkono kitu hicho.


Share:

KAMATI YA SIASA CCM IMESELA YAFANYA ZIARA ,YAHIMIZA WAZAZI KUCHANGIA MADAWATI..."WATOTO WANAKAA CHINI"

Na Halima Khoya, Shinyanga.


Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Imesela Wilaya ya Shinyanga imefanya ziara ya siku tatu kwa ajili ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa ilani ya Chama hicho ili kutatua changamoto zilizopo katika miradi hiyo.


Ziara hiyo imeanza Machi 6, 2023 ambapo wametembelea miradi ya elimu katika shule ya msingi Maskati na shule ya sekondari Imesela na kujadili changamoto zinazowakabili wanafunzi na utatuzi wake.


Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika shule ya Msingi Maskati, Katibu wa CCM Kata Richard Nyanda amesema malengo ya kufanya ziara hiyo ni kutembelea miradi na taasisi zote zilizopo katika Kata hiyo ili kubaini changamoto na jinsi ya kuzitatua.


Akisoma Taarifa ya shule mkuu wa shule ya Msingi Maskati,Peter Chono Dalali amesema mwaka 2021 walisajili wanafunzi 34 waliofaulu 25 na waliofeli 9 ambayo ni sawa na 73.53%, 2022 waliosajili wanafunzi 27 waliofaulu 21 waliofeli 6 sawa na 77.78% ambapo jumla kwa miaka mitatu ilikuwa na wanafunzi 106 waliofaulu 75 na waliofeli 31 sawa na 70.75% na kufanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa kiasi kikubwa.


Dalali amebainisha kuwa katika shule hiyo imefanikiwa kuanzisha miradi miwili, ujenzi wa nyumba ya mwalimu ambapo wanamshukuru Mbunge wa Jimbo la Solwa Mhe. Ahmed Salum kwa kutimiza ahadi yake ya kutoa mifuko 200 ya saruji pamoja na ufugaji wa mbuzi ambapo wana mbuzi 13.


Hata hivyo Dalali ameeleza juu ya changamoto ya uchache wa madawati 50 ambayo yanasababisha baadhi ya wanafunzi kukaa chini hali inayosababisha wanafunzi wengi kukata tamaa na wengine kuacha shule.


"Shule ya msingi Maskati ina jumla ya madarasa 6, ofisi 3 na matundu ya vyoo 8 ambapo moja linatumiwa na walimu, thamani tuna Madawati 65 meza 9,vitu 9, kabati 1,shubaka 3,nyumba moja ya mwalimu,kuna baadhi ya wanafunzi wanakaa chini kwani inawafanya wanafunzi wengine kukata tamaa,pia kuna upungufu wa vyumba vya walimu baada ya baadhi ya nyumba kupitiwa na mradi wa reli ya kisasa, tunapungukiwa na madarasa mawili", amesema Dalali.


Mwenyekiti wa CCM Kata ya Imesela, Sebastian Mwigulu Katambi,amesema kuwa utaratibu wa kuchangia madawati ushirikishwe kwa wazazi kwaajili kuchangia haraka na kuondokana na changamoto ya kukaa chini kwa baadhi ya wanafunzi.


Monica Mshinga na Elia Emannuel ni baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ambao wameeleza uhaba wa madawati unavyopelea kufeli na hata kukosa usikizi mzuri wakiwa katika masomo yao sambamba na kukatishwa tamaa hali inayosababisha kuwepo kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Maskati,Robert Ngusa amesema kuwa awali aliitisha mkutano wa hadhara kwaajili ya kuchangia fedha za ukarabati wa madawati hayo ambapo hawakukubaliana kiasi cha kuchangia na baada ya kikao hicho wamekubaliana kuchangia elfu tatu kwa kila kaya.


Seth Msangwa ni Diwani wa Kata ya Imesela ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa amesema kuwa hali ya watoto inasikitisha baada ya kujionea baadhi ya wanafunzi wanakaa chini ambapo baada ya kuguswa na changamoto hiyo amechangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa madawati hayo.


"Niliongea na Injinia wa ujenzi akasema hizi fedha zinatoka kwa mlolongo kwamba kutoka kwenye wizara ya ujenzi ziende kwenye wizara ya ardhi kisha ziende TAMISEMI ndipo Halmashauri wailetee Taasisi husika,tuliona watujengee kwa maana thamani ya majengo ya vyumba vya walimu vinaweza kuwa na thamani kubwa,vitu ambavyo tuliwaambia watuletee fedha ni kama ardhi na miti",amesema Msangwa.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 8,2023























Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger