Saturday, 4 March 2023

MAZISHI YA MANJU JAMES MAKUNGU SOMBI YATIKISA, NI MSIBA USIO NA VILIO! MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA...NI MAAJABU

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu James Makungu Sombi
Picha iliyotumika kuaga mwili wa James Makungu Sombi

TAZAMA VIDEO AKIAGWA KIMILA...NI MAAJABU
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi
Mwili wa James Makungu Sombi ukiagwa kwa ngoma za kimila

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Ni msiba usio na vilio!!, Kuaga kwa picha tu bila kuona mwili wa marehemu!! Ndivyo mwili wa aliyekuwa Manju maarufu James Makungu Sombi (89) ulivyoagwa na kuzikwa huku ngoma za utamaduni wa Kabila la Wasukuma ( Bhugobogobo na Bhununguli) zikichezwa ikiwa ni kutimiza agizo la manju huyo,ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utamaduni na miongoni mwa waanzilishi wa makumbusho ya utamaduni wa Wasukuma Bujora mkoani Mwanza.

Mazishi ya James Sombi yamefanyika leo jioni Jumamosi Machi 3,2023 katika kitongoji cha Shikoba kijiji cha Mwamanga kata ya Mwamanga wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Awali mwili wa marehemu JameS Makungu Sombi uliagwa katika Makumbusho ya Bujora Ijumaa na leo Jumamosi kuagwa na mamia ya waombolezaji nyumbani kwake Kissa Mwanza ikiwa ni siku tano zimepita tangu afariki dunia Februari 27,2023 mchana baada ya kuanguka ghafla nyumbani kwake akisumbuliwa na Presha.

Enzi za uhai wake, James Sombi maarufu Ng’wana Sombi aliagiza kuwa akifariki dunia asizikwe hadi siku tano zipite na wakati wa kuaga mwili wake na wakati wa mazishi ngoma za utamaduni zichezwe na asiyepo mtu yeyote wa kulia bali zinazopaswa kulia ni ngoma pekee lakini pia hakutaka waombolezaji waage mwili wake kwa kuangalia mwili bali picha tu, na ameagwa kwa picha tu.

James Makungu Sombi aliyezaliwa tarehe 05.02. 1934 Mwamanga Magu ambapo alisoma shule ya msingi Kitongo kisha kuanza kujishughulisha na kilimo na ufugaji huko Shikoba- Mwamanga Simu Magu (zamani Kwimba) na baadaye alihamia Kisesa Mwanza akifanya kazi MWATEX baadaye kwenye makumbusho ya Bujora baada ya kufahamiana na Padre Clement waliyefahamiana tangu mwaka 1954 akawa anatangaza utamaduni wa Kabila la Wasukuma hadi Ulaya hasa Denmark na mwaka 2005 alistaafu kazi hapo kwenye Makumbusho ya Bujora.

James Sombi ameacha mjane, watoto 31, wajukuu 81 na vitukuu 72.

TAZAMA KILA KITU HAPA
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi ukiwa nyumbani kwake Kisesa Mwanza

Historia fupi ya marehemu James Makungu Sombi ikisomwa
Ngoma ya kimila Bhugobogo ikichezwa kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 

Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye ni mdau wa masuala ya utamaduni kupitia mtandao wa Malunde 1 blog akitoa pole na salamu za rambirambi kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 

Kiongozi w dini akitoa neno kwenye msiba wa  James Makungu Sombi 
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu James Makungu Sombi  likiwa na picha ya kimila, kitambaa cheusi na chekundu wakati wa kuaga 
Msaidizi wa Mtemi wa Bhuhungukila, Fumbuka Samson Lubasa ambaye ni mwalimu wa utamaduni katika chuo cha Butimba TTC na mwanakamati wa Bujora Research Committee akiongoza zoezi la kuaga kimila mwili wa marehemu James Makungu Sombi 

 Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea

Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea kwa ngoma za kimila

Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea
Zoezi la kuaga mwili wa marehemu James Makungu Sombi likiendelea
Wajukuu wa marehemu James Makungu Sombi wakiwa wamebeba jeneza la babu yao

Wacheza ngoma ya Bhununguli wakipanda gari  liliobeba mwili wa marehemu James Makungu Sombi 
Mwili wa marehemu James Makungu Sombi ukiwa ndani ya gari baada ya kuwasili kijijini kwao Mwamanga Magu kwa ajili ya mazishi
Ngoma ya kimila ikiendelea wakati wa mazishi ya marehemu James Makungu Sombi  katika kijiji cha Mwamanga Magu 

Mwili wa marehemu James Makungu Sombi  ukiagwa katika kijiji cha Mwamanga Magu 

Share:

WASABATO SHINYANGA WAENDESHA CHANGIZO UNUNUZI BASI LA SHULE, WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS SAMIA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

Wasabato wakiwa katika Changizo la ununuzi wa Basi la Shule ya Awali na Msingi SAPPS.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

KANISA la Waadventista Wasabato Shinyanga, wameendesha zoezi la changizo kwa ajili ya kununua Basi la Shule katika Shule ya Awali na Msingi ya Kanisa hilo iliyopo Ndala Manispaa ya Shinyanga 
(SAPPS) Shinyanga Advetist Pre and Primary School,  ili kuboresha huduma za usafiri kwa wanafunzi katika shule hiyo.

Zoezi la Changizo hilo limefanyika leo Machi 4, 2023 katika Kanisa la Mtaa wa Shinyanga Mjini, na kukutanisha Makanisa ya Wasabato Mitaa Mitano, ukiwamo Mtaa wa Mwasele, Lubaga, Ushirika, Ndembezi na Mwenyeji Shinyanga Mjini.

Askofu wa Jimbo la Nyanza ukanda wa dhahabu Enock Sando, akizungumza wakati wa Ibada ya Sadaka ya kumtolea Mungu kununua Basi la Shule hiyo ya (SAPPS), amesema kuunga mkono elimu (Support) ni kumuunga mkono Mungu, pamoja na Juhudi za Serikali chini ya Rais Samia katika uboreshaji wa Sekta ya elimu ili wanafunzi wasome katika mazingira Rafiki.

“Unapounga mkono elimu una muunga Mkono Baba wa Mbinguni na Rais Samia, sababu katika shule yetu hii ya Awali na Msingi ya (SAPPS) hawasomi tu watoto wa Wasabato bali wa jamii nzima,”amesema Askofu Sando.

“Mabadiliko katika Jamii yana anza na mtu mmoja, na pia Tanzania itajengwa na Watanzania wenyewe, hivyo nawaomba waumini tujitoe kuchangia fedha ili basi la shule lipatikane, Mungu ameshawekeza kwako kwa kukupatia Ajira, Ofisi, Miradi mbalimbali, Biashara, sasa anahitaji umtolee ili uendelee kupalilia Mibaraka,”ameongeza.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Awali na Msingi (SAPPS) Elijah Wadea Waritu ambaye pia ni Mchungaji, amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 170 na wana Mabasi Mawili tu, huku uhitaji ni kuwa na Mabasi Mawili tena yafike Manne, na katika ombi hilo la changizo wameomba angalau kupata Basi moja ili yafike matatu na kuboresha zaidi huduma ya usafiri kwa wanafunzi.

Aidha, Changizo hilo endelevu na mtu yeyote ambaye ataguswa kuchagia upatikanaji wa Mabas katika Shule hiyo ya SAPPS ili kuunga mkono uboreshaji Sekta ya Elimu na kupalilia Mibaraka yake kwa Bwana.
anaweza kutuma pesa yake kupitia Account hizi.

024103007194-Benki ya NBC

30710056115-Benki ya NMB

Jina la Account Shinyanga Adventist Pre and Primary School.

Askofu wa Jimbo la Nyanza ukanda wa dhahabu Enock Sando, akitoa neno wakati wa Ibada ya kutolea Bwana Sadaka ya ununuzi wa Basi la Shule ya Wasabato SAPPS ya Awali na Msingi.

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakiwa katika Ibada ya kumtolea Bwana Sadaka ya ununuzi wa Basi la Shule ya SAPPS.

Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wwasabato Mtaa wa Shinyanga Mjini Razalo Mbogo akiwa katika Ibada ya kumtolewa Bwana Sadaka ya ununuzi wa Basi la Shule.

Mama Mchungaji akiwa katika Ibada ya kumtolewa Bwana Sadaka ya ununuzi wa Basi la Shule ya SAPPS.

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakiwa katika Changizo la Basi la Shule ya SAPPS.

Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato wakiendelea na Changizo la Basi la Shule ya SAPPS.

Wanakwaya wakiimba nyimbo kwenye Ibada ya kumtolea Bwana Sadaka ya kununua Basi la Shule ya SAPPS.

Wanakwaya wakiendelea kuimba nyimbo kwenye Ibada ya kumtolea Bwana Sadaka ya kununua Basi la Shule ya SAPPS.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 4, 2023

Share:

Friday, 3 March 2023

SHINDANISHENI TAFITI ZENU ILI ZIWEZE KUPATA SOKO EAC-PROF.MSHANDETE

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Utafiti na Ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa Shindano la Wazo la Kibiashara lililoandaliwa na Ndaki ya Biashara na Sayansi ya Jamii (BuSH) kwa udhamini wa Taasisi hiyo na Chuo cha Washington State cha nchini Marekani Machi 3,2023.

Washiriki wa Shindano la wazo la Kibiashara lililoandaliwa na Ndaki ya Biashara na Sayansi ya Jamii (BuSH) kwa udhamini wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela na Chuo cha Washington State cha nchini Marekani wakifuatilia matukio katika shindano hilo lilifanyika Machi 3,2023.

Washindi wa kwanza katika Shindano la wazo la biashara la Kifaa Kinachotumia nishati ya mwanga wa jua kutambua uwepo wa vimelea vya TB kwenye mazingira hatarishi ambao ni Clarence Rubaka, Happiness Mkumbo, Angela Aluko na Kelvin Makuki wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shindalo hilo.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Utafiti na Ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa wazo la Kibiashara.

Na.Mwandishi Wetu-ARUSHA

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Utafiti na Ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Anthony Mshandete ametoa wito kwa watafiti na wanazuoni kushindanisha tafiti zao ili ziweze kuwa bidhaa na huduma zenye ushindani wa soko la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Profesa Mshandete ameyasema hayo Machi 3,2023 Jijini Arusha wakati akifungua shindano la Ubunifu wa Biashara liloshirikisha makundi manne ya watafiti wanafunzi kutoka taasisi hiyo chini ya uratibu wa Ndaki ya Biashara na Sayansi ya Jamii (BuSH) kwa udhamini wa Taasisi hiyo na Chuo cha Washington State cha nchini Marekani.

“Shindano hili ni muhimu katika kuwahamasisha watafiti walioko vyuoni na katika taasisi kutoa tafiti zenye kukidhi viwango, na kuzitoa katika maabara ziwe bidhaa zitakazoingia sokoni ili kuleta ajira kwa vijana na ushindani katika soko la Afrika Mashariki” amesema Profesa Mshandete.

Amesema kuwa washiriki hao wanatakiwa kutumia fursa hiyo, katika kutoa tafiti zenye kuleta matokeo chanya ili kupata suluhisho katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Naye Mmoja wa Majaji katika shindano hilo Privanus Katinhila ameipongeza Taasisi ya Nelson Mandela, kwa kuratibu shindano hilo katika tasnia ya viwanda, biashara na uwekezaji na kutoa rai kwa wafanyabiashara wa jiji la Arusha, kuitumia Taasisi hiyo kujifunza fursa mbalimbali zinazopatikana ikiwemo tafiti na bunifu ili kuwezesha bidhaa zao kuwa na ubora zaidi.

Washindi wa kwanza katika Shindano hilo ni Clarence Rubaka, Happiness Mkumbo, Angela Aluko na Kelvin Makuki wenye wazo la kibiashara la Kifaa Kinachotumia nishati ya mwanga wa jua kutambua uwepo wa vimelea vya TB kwenye mazingira hatarishi ambapo wamejipatia zawadi ya shilingi milioni tatu pamoja na nafasi ya mafunzo ya wiki mbili katika Chuo cha Washington State nchini Marekani ili kuboresha zaidi wazo hilo la Kibishara huku washindi wa pili wakipata shilingi milioni mbili na washindi wa tatu shilingi milioni moja.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger