Thursday, 23 February 2023
MAAFISA TEHAMA, MAENDELEO YA JAMII WA HALMASHAURI WAPEWA MAFUNZO YA KANZIDATA YA TAIFA YA WANAWAKE NA UONGOZI TANZANIA
DKT. JINGU AHIMIZA UBUNIFU, UWAJIBIKAJI,UADILIFU KWA WATUMISHI WA TUME MAHALA PA KAZI
Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony Jingu wakati akifungua baraza hilo.
Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Nassoro Shemzigwa (kushoto) akiongoza baraza hilo. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Livini Avith.
Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt John Antony JinguMWANAFUNZI AMUUA KWA KISU MWALIMU WAKE

NABII MWASHA:NINAIONA NEEMA KUPITIA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MWAKA HUU

Wednesday, 22 February 2023
MAJID AUAWA AKIKABA WANAWAKE USIKU WA MANANE TINDE

MUME WANGU AKIENDA NJE KAZI HAIWEZI, ILA KWANGU MAMBO NI MOTO
AFARIKI BAADA YA KUANGUKA KWENYE MWAMBA AKIFANYA MAOMBI
Mwanaume anayesemekana kuwa na umri wa miaka 20, amefariki dunia baada ya kuanguka kutoka kwa mwamba wa Kit Mikayi eneo la Seme,kaunti ya Kisumu Kenya.
Mwanamume alifariki baada ya kuanguka kutoka kwa mwamba wa Kit Mikayi eneo la Seme, kaunti ya Kisumu.
Katika tukio hilo la Jumapili, Februari 19, mwendo wa saa nane asubuhi, marehemu alikuwa ameandamana pamoja na waumini wengine juu ya mwamba huo kuomba.
Lakini mambo yaligeuka baada ya mwanaume huyo kuteleza kutoka kwenye mwamba huo, ambao hutumika kama mahali pa maombi na kuanguka hadi kufariki, msimamizi wa eneo la Othany, Absalom Oyoo alithibitisha.
"Hakuna kitambulisho cha kumtambua marehemu ni nani na uchunguzi unaendelea," alisema Oyoo, kama alivyonukuliwa na Capital.
Msimamizi huyo alisema uchunguzi umeanzishwa ili kubaini namna marehemu alivyoanguka. Alitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Kisumu kulizungushia uzio kwenye mwamba huo ili kuzuia watu kuingia na kutoka bila kujulikana.
"Ingekuwa rahisi kuwafuatilia watu waliokuwa na marehemu kama walikuwa wametia sahihi kitabu cha wageni,” alisema.
Shughuli zozote za maombi katika mwamba huo zimesitishwa ili kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Jaramogi Oginga Odinga ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa maiti ili kubaini chanzo cha kifo chake.
CHANZO-TUKO NEWS
TENGENI MAENEO YA UWEKEZAJI – WAZIRI MABULA

Baadhi ya Wakuu wa wilaya za mkoa wa Morogoro wakiwa katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Fatma Mwasa akizungumza katika kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo.
Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mjini Rebecca Nsemwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha kujadili na kuweka mikakati ya kukwamua changamoto za sekta ya ardhi katika mkoa wa Morogoro kilichofanyika tarehe 22 Februari 2023 mkoani humo. 







