Monday, 20 February 2023

AMUUA KWA RISASI MKE WAKE WA ZAMANI NA WENGINE WATANO


Mwanaume mmoja aliyekuwa na bunduki tatu amempiga risasi mke wake wa zamani na watu wengine watano wakati wa ghasia katika mji mdogo wa vijijini katika jimbo la Mississippi nchini Marekani.

Polisi wanasema Waathiriwa waliuawa katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na duka na nyumba mbili, huko Arkabutla, ambapo kuna jamii ya watu wasiozidi 300.

Polisi wamemfungulia mashtaka mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 52 kwa mauaji ya kiwango cha juu na anashikiliwa katika gereza la kaunti hiyo.Hakuna sababu ya shambulio lake hadi sasa
Share:

WAHUNI WAMVAMIA KAMANDA WA POLISI, WAPORA REDIO NA BUNDUKI

Polisi katika kaunti ya Busia nchini Kenya wanatafuta bunduki iliyoibwa kutoka kwa kamanda wa polisi usiku wa Jumamosi, Februari 18,2023.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, wezi walivunja nyumba ya kamanda huyo na kuichakura kabla ya kuiba redio na bastola yake aina ya Czeska.

Wezi hao pia walivamia nyumba ya wafanyakazi wake na kuiba mtungi wa gesi na redio.

 Polisi pia wanashuku kuwa wezi hao walinyunyiza dawa ya kulewesha kupitia kwa dirisha la chumba cha kulala ambacho kilikuwa wazi huku kamanda huyo akilalamikia kuwa na maumivu ya kichwa na kizunguzungu alipoamka.

"Iliripotiwa na Kamanda wa CIPU wa kaunti hiyo ya Busia, Bishar Muhumed SSP kwamba jana mwendo wa saa 9.30 usiku, alifunga nyumba yake katika makao ya serikali, Milimani Estate iliyoko takriban mita 300 kutoka mpakani na kulala," taarifa hiyo ya polisi ilisoma kwa sehemu. 

"Leo mwendo wa saa 0335 aliamka akihisi maumivu ya kichwa na kizunguzungu baada ya kuona sanduku lake limetupwa chini karibu na kitanda chake huku nguo zikiwa zimetawanyika kote. Bastola yake ya Czeska Pistol no.F8457 ikiwa na risasi 15 kwenye koti moja haipo," taarifa imeongezwa.

Maafisa wa usalama wa eneo hilo walitembelea eneo la tukio na kikosi cha wapelelezi. "Mbwa wa kundi la K9 aliletwa kwenye eneo la tukio na kuchukua harufu ambayo ilitupeleka kwenye barabara inayoelekea Uganda lakini harufu ilitoweka kabla ya kufika kwenye mpaka. Kikosi cha maafisa wa polisi walivamia eneo hilo ili kupata bunduki hiyo. Hakuna aliyekamatwa au kupatikana hadi sasa,” iliongeza taarifa hiyo.
Share:

WANAFUNZI NCHINI UGANDA KUSOMA KIDATO CHA 5 NA 6 KWA MIAKA MITANO







Wanafunzi kote nchini Uganda ambao watahitimu kujiunga na elimu ya A-Level, sasa watatakiwa kusoma kwa hadi miaka mitano, ikiwa serikali itaidhinisha mtaala mpya wa A-Level .

Awali, wanafunzi wamekuwa wakisoma Senior Five na Six katika kipindi cha miaka miwili kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.

Naibu mkurugenzi wa mapitio ya mitaala na uendelezaji wa vifaa vya kufundishia katika Kituo cha Taifa cha Maendeleo ya Mitaala (NCDC), Bi Bernadette Nambi, alisema sehemu ya miaka mitano ni kumwezesha mwanafunzi ambaye hataweza kumaliza A-Level ndani ya miaka miwili kufanya mitihani yote atakayofeli.

Pia Wanafunzi watakaofeli mitihani ya Uganda Advanced Certificate of Education (UACE) sasa watatakiwa kurudia somo lililofeli tu. Awali, ikiwa mwanafunzi atashindwa kufikia kanuni mbili kupita, atatakiwa kurudia mtihani mzima.A
Share:

MCHENGERWA, AKUTANA NA MENEJIMENTI YAKE, ATOA MIEZI MIWILI KUPATA MAPINDUZI


Na John Mapepele

Waziri mpya wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerewa leo. amekutana kwa mara ya kwanza na Menejimenti ya Wizara yake na ametoa miezi miwili kwa watendaji kuleta mapinduzi yanayosubiriwa na watanzania.

Mhe. Mchengerwa amesema haya mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma wakati alipoambatana na Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi ambapo amefafanua kuwa yeye kwa kushirikiana na Viongozi wenzake walioteuliwa hivi karibuni atahakikisha wanafanya mabadiliko na mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii ili ichangie zaidi uchumi wa nchi.

Baada ya tukio hilo Waziri Mchengerwa amefanya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Balozi Dkt. Pindi Chana.

‘’Tunahifadhi na kutangaza utalii nchini.Lakini pia twende tukadhibiti ujangili tunataka tudhibiti kwelikweli ili kuhakikisha kwamba vitendo vya hovyo hovyo havitokeo. Na mimi kwenye kipindi changu sitataka kusikia vitendo vya hovyo hovyo,’’ amesema Mchengerwa wakati wa makabidhiano hayo.

Aidha, Mchengerwa ameagiza kupatiwa taarifa za idara na taasisi za Wizara ifikapo Jumatatu, Februari, 20, 2023 ili aweze kuzipitia.

‘’Nataka kupitia taatifa hizi halafu tutaitana kwa ajili ya kupanga kazi tuweze kujua ndani ya kipindi cha miezi miwili tumekwendaje kwenye Wizara yetu ili tuweze kutimiza zile ndoto ambazo tunazo za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,’’ ameongeza Mchengerwa.

Waziri huyo pia amehimiza ushirikiano baina yake na Waziri aliyekuwepo Balozi Dkt. Pindi Chana. ‘’Naomba sana tushirikiane pale ambapo kuna jambo ambalo mnadhani nahitaji kulipitia wakati wowote . Nitaomba na wengine wakati wowote nitaomba mnipigie kama kuna taarifa ambazo ni za muhimu ili kuboresha zaidi.’’ amesisitiza Mchengerwa.

Katika hafla hiyo pia yamefanyika makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.Eliamani Sedoyeka na Katibu Mkuu wa sasa Dkt. Hassan Abbas 
Share:

MWALIMU ALIYESHAMBULIA MWANAFUNZI TUHUMA ZA KUIBA MAANDAZI AKAMATWA



Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia mwalimu wa shule ya Sekondari Loiler iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi mkoani Mbeya,Peter Emmanuel (29),kwa tuhuma za kumshambulia fimbo mwanafunzi kwa madai ya kuiba maandazi matano.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, amesema kuwa tukio hilo limetokea Februari 10,2023 katika Shule ya Sekondari Loiler mkoani Mbeya.

Kamanda amesema kuwa mtuhumiwa huyo pamoja na mlinzi wa shule hiyo Haruna Issa (30),mkazi wa Iwala walimshambulia kwa viboko sehemu mbalimbali za mwili mwanafunzi huyo wa kidato cha IV mwenye umri wa miaka 16,mkazi wa Mwangake na kumsababishia madhara.

Kamanda amesema kuwa watuhumiwa hao walimtuhumu mwanafunzi (jina linahifadhiwa) kuiba maandazi matano ambayo kila andazi ni linauzwa sh.300 hivyo jumla ya maandazi yote ni sh.1,500 katika duka la shule hiyo.

Kamanda amesema kuwa na mwalimu na mlinzi huyi walimshambulia kwa viboko na kumsababishia majeraha sehemu ya paji la uso, mkono wa kushoto na magoti yote mawili.

“Baada ya kumshambulia na kumjeruhi,siku hiyo ya tukio majira ya saa 5:00 usiku walimkimbiza Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya matibabu.

“Jeshi la Polisi kupitia wasiri wake lilipata taarifa na kufanya ufuatiliaji na kubaini kutokea kwa tukio hilo na hatimaye kuwakamata watuhumiwa wote wawili,” amesema kamanda.

Kamanda amesema kuwa upelelezi wa shauri hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa jamii kuacha mara moja tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria.



Via: Jamhuri
Share:

Sunday, 19 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU FEBRUARI 20,2023









Share:

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAMUUUNGA MKONO RAIS SAMIA, YATOA MILIONI 2 KWA USHINDI WA YANGA.


Na John Mapepele

Wizara ya Maliasili na Utalii, imemuunga mkono Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuipongeza Yanga katika ushindi wake wa leo dhidi ya TP Mazembe katika Kombe la Shirikisho.

Katika mechi ya leo iliyochezwa katika Uwanja wa Benjamini timu ya Yanga imeweza kujinyakulia pointi zote tatu baada ya kuibamiza TP Mazembe mabao matatu kwa moja.

Kutokana na kupata magoli matatu, Yanga imejinyakulia milioni 15 kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alizoahidi ikiwa ni shilingi milioni 5 kila goli baada ya kumalizika kwa mchezo usiku huu ambapo Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa shilingi milioni 2.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa amefafanua kuwa Wizara yake itaendelea kutumia Michezo kuendeleza Utalii duniani.

" Na sisi Wizara ya Maliasili na Utalii tutatumia michezo kama hii kutangaza vivutio vya nchi yetu katika mabara yote, tunataka kuwajaza watalii hapa nchini ili wachangie kwenye uchumi wetu" amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Wizara nyingine zilizotoa fedha ni Ardhi, Fedha na Utamaduni Sanaa na Michezo ambazo pia kila moja imetoa milioni 2.

Ushindi huo unaifanya Yanga kushika nafasi ya tatu katika kundi D la mashindano hayo.

Katika mchezo huo Viongozi mbalimbali wa Serikali wamehudhuria wakiwemo Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe, Pindi Chana Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekul, Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt.Hassan Abbasi na Katibu Mkuu wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu.
Share:

MCHUNGAJI KIMARO ASAMEHEWA


Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa leo Jumapili ametangaza msamaha kwa Mchungaji wa Ushirika wa Kijitonyama, Dk Eliona Kimaro ambaye alipewa likizo ya siku 60.


Usiku wa Januari 16, 2023 ilisambaa video ikimuonyesha mchungaji Kimaro akiwaeleza waumini wake kuwa amepewa likizo ya siku 60 baada ya kuitwa katika ofisi ya msaidizi wa askofu na kufanya kikao na mkuu wa jimbo.


Likizo hiyo ilikuwa inamalizika Machi 17, 2023 na Mchungaji Kimaro alipokuwa akiwaaga Washirika wa Kijitonyama alisema baada ya likizo hiyo hatarudi hapo, alielezwa akaripoti Makao Makuu ya Dayosisi.


Katika msamaha huo wa leo Februari 19, umetangazwa katika Ibada iliyofanyika Ushirika wa Kinyerezi, Tabata na kuongozwa na Askofu Malasusa ambapo ametangaza uamuzi huo Kanisani baada ya Mchungaji Kimaro kupewa fursa ya kuwasalimia waumini na akaomba radhi kwa yote yaliyotokea.

"...Mchungaji Kimaro kama ulivyoomba umesamehewa, endelea kutafakari, endelea kukaa karibu na Mungu wako," amesema Askofu Malasusa huku akiwaomba waumini washirika mbalimbali kuwatunza na kuwaombea wachungaji wao.


Akizungumza wakati wa ibada hiyo Mchungaji Kimaro ameomba radhi kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo kwa usumbufu wowote uliojitokeza wakati huu ambao amekuwa likizo.

“Naomba radhi kwa mkuu wa kanisa Askofu, Dk Fredrick Shoo kwa usumbufu wowote ambao ulijitokeza katika mitandao na kwenye vyombo vya habari kwa wakati huu ambao nimekuwa likizo ya faragha,” amesema Dk Kimaro.




Pia, amemshukuru Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Alex Malasusa kwa upendo na kazi kubwa ya kumtunza kichungaji
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 19,2023



















Share:

Saturday, 18 February 2023

EWURA YAIBUKA KIDEDEA UHUSIANO MZURI NA VYOMBO VYA HABARI, KAGUO MTENDAJI BORA


Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeibuka mshindi wa kwanza kwa Taasisi zenye uhusiano mzuri na vyombo vya habari, TRA imeshika number mbili na CRDB imekuwa ya tatu, Tuzo hiyo imetolewa leo Tar.18/02/2023 na Chama cha Maafisa Uhusiano Tanzania, Dar es Salaam.

Sambamba na hilo pia Meneja wa Mawasiliano EWURA, Bw. Titus Kaguo, ameibuka kuwa mtendaji bora wa Mawasiliano na Uhusiano katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.

Tuzo hizo zimefunguliwa na na Naibu Waziri wa Habari, Mhe. Kundo Mathew na kuhudhuriwa na Wataalamu wa Habari na Mawasiliano wa Serikali na sekta binafsi.
Share:

MCHENGERWA, DKT. ABBASI WASHIRIKI MCHEZO WA SSC NA RAJA.


*************

*Mchengerwa asisitiza kutumia Utalii wa Michezo kuitangaza Tanzania.

Na John Mapepele

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi leo ni miongoni mwa viongozi na wadau wa Soka ambao wameshiriki kwenye mpambano baina ya Simba SC na Raja CA katika mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika katika kundi C.

Mchezo huu umechezwa katika Uwanja wa Mkapa ambapo hadi mwisho wa mchezo Raja imeongoza kwa mabao matatu kwa nunge

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan alitangaza kutoa shilingi milioni tano kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Simba leo ambapo pia atatoa fedha hiyo hiyo kesho kwa timu ya Yanga endapo itaifunga timu ya TP Mazembe katika Kombe la Shirikisho.

Mhe. Mchengerwa alikuwa waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Dkt. Abbasi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo hadi Februari 14, 2023 ambapo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan aliwateua tena kuendelea kuhudumu kwa nafasi hizo hizo kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa Wizara yake imedhamiria pamoja na mikakati mingine kutangaza utalii ikiwa ni pamoja na Utalii wa Michezo na Utamaduni ili uweze kuchangia kwenye pato la Taifa.

Aidha, akiongea na Menejimenti ya Wizara yake jana, Mhe. Mchengerwa amesisitiza sekta ya Utalii inatakiwa kuchangia kiasi kikubwa kwenye uchumi na pato la Taifa kwa kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi na ambavyo havipatikani katika sehemu mbalimbali duniani.

Naye Dkt. Abbasi ameongeza kuwa tayari Mhe. Rais Samia Suluhu ameshafanya kazi kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia Filamu ya Royal Tour hivyo watanzania wanatakiwa kuunga mkono jitihada hizo.

Hadi sasa katika kundi Hilo timu ya Raja, inaongoza ikifuatiwa na Horoya, Vipers na Simba inashika nafasi ya mwisho.

Mchezo huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Pindi Chana na viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.
Share:

SIMBA SC YACHAKAZWA 3-0 DHIDI YA RAJA CASABLANCA




NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imeshindwa kupata pointi kwenye mechi yake ya pili hatua ya makundi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo imepokea kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Raja Casablanca ya nchini Morroco.

Katika mchezo huo ambao Simba Sc alikuwa mwenyeji ambapo mechi ilichezwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, Raja Casablanca walifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 30 kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Hamza Kabba.

Bao la pili la Raja Casablanca limefungwa na Soufiane Benjdida dakika 83 ya mchezo baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kufanikiwa kuweka kambani.

Raja Casablanca walipata bao la tatu kwa mkwaju wa penati kupitia kwa beki wao Ismail Mokadem

Hii ni mechi ya pili Simba Sc haijaambulia chochote kwenye michuano hiyo kwani mechi ya kwanza waliookea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya.




Share:

KILICHOMPATA ALIYETAKA KUNITAPELI SHAMBA LANGU

Kuwa na makazi mazuri ni sehemu ya mambo matatu ya muhimu (basic needs) kwa binadamu yeyote ukiachilia mbali chakula na mavazi, hivyo katika kutafuta kwangu maisha, nilijitahidi sana niweze kujenga nyumba.


Hiyo ni kwa sababu wazazi wangu wenyewe hawakuwahi kuwa na nyumba yao hadi tunazaliwa na kuwa watu wazima, nao walitulea kwenye nyumba hizo za kupanga toka tunazaliwa hadi tukawa watu wazima na kuanza kujitemea na kufanya maisha yetu.

Siku zote ndoto yangu ilikuwa ninunue shamba halafu nijenge nyumba ili wazazi wangu waje kuishi hapo na baadaye nijenge hapo pembeni nyumba yangu na familia yake.

Kwa kweli sikupenda kuona wazazi wangu wanafikia hatua ya uzee wakiwa kwenye nyumba za kupanga kwani itafikia muda watakosa nguvu za kufanya kazi na watashindwa kulipa kodi.

Hatimaye nilifanikiwa kununua shamba heka moja na mara moja nilianza ujenzi kutokana nilikuwa nimejipanga kisawasawa, mafundi walifanya kazi usiku na mchana hadi kazi hiyo ikaisha na nami na wazazi wangu tukahamia katika nyumba hiyo.

Hata hivyo, siku moja nikiwa nyumbani, alijitokeza mtu mmoja na kudai eneo lile shamba ni la kwake pia, nilimwambia nina hati ya kumiliki ardhi hiyo naye akasema anayo pia, nilipojaribu kuulizia kwa mtu aliyeniuzia akasema siyo kweli, huyo ni tapeli.

Baada ya wiki kama mbili, mtu yule naye akaleta vifaa na mafundi mara moja ili kuanza ujenzi, jambo hilo lilinichanganya sana hasa pale niliposikia mtu huyu ana nguvu kubwa kifedha, huvyo anaweza kusema mimi ndio nimevamia eneo lake.

Kwa kutambukua uzito wa jambo hilo, niliamua kuwashirikisha ndugu zangu kadhaa ili wanipe ushauri wa kufanya, sitomsahau rafiki yangu Moses aliyenipatia namba ya Dr. Kiwanga, nilipiga na kuwasiliana naye na kumuomba ananifanyie dawa ya kuondoa tatizo hilo.

Basi, Dr. Kiwanga aliniambia ndani ya siku tatu nitapata majibu sahihi, lakini kabla ya siku tatu kuisha nilipigiwa simu na kuambiwa
yule aliyevamia eneo langu amepata ajali mbaya ya gari na kwamba amelazwa Hospitali, licha ya kuwa alikuwa amenitendea ubaya, kweli kama binadamu nilishtuka sana.

Alikaa Hospitali kwa muda mrefu sana, zaidi ya miezi miwili, akiwa huko alituma watu waje nyumbani kuniomba msamaha kwa kile alichonifanyie na kuahidi hataendelea na ujenzi huo. Nami niliamua kumsamehe na sasa naendelea vizuri na maisha yangu na tayari nimejenga nyumba yangu ya pili.

Kumbuka kuwa Dr. Kiwanga ana uwezo wa kuwezesha kuwa mtu wa bahati maishani, ana uwezo wa kukukinga na adui zako wanaokutakia mabaya kwa wakati wowote ule kwa muda wa siku tatu utaona matokeo yake utayaona.

Kwa mengi zaidi wasiliana nao kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com au kwenye wavuti www.kiwangadoctors.com au waweza kuwasiliana nao kupitia namba ya simu +254 769404965.


Share:

MWANDISHI WA HABARI EDWIN SOKO ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MTENDAJI WA TAASISI YA TMFD



Taasisi ya Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development (TMFD) inayofanya kazi katika eneo la vyombo vya habari na uvuvi hapa Tanzania imepata Mkurugenzi wake mpya.


Mwandishi wa habari mkongwe Bwana Edwin Soko ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa taasisi hiyo.


Uteuzi huo umetangazwa kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya (TMFD) Bwana Tumaini Mbibo jana Februari 17, 2023 na uteuzi huo umeanza rasmi jana.
Share:

SIBTAIN MURJI, ZAMEEN MURJI WAFIKISHWA MAHAKAMANI WAKIKABILIWA NA MASHTAKA MATATU IKIWEMO KUKWEPA KODI


Sibtain Murji 43(Kishoto) na Zameen Murji 47 (Kulia) wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kabla ya kusomewa mashtaka matatu likiwemo la kukwepa kodi kiasi cha Sh. Bilioni sita jijini Dar es Salaam jana Februari 17,2023.


************* 

WATU wawili, Sibtain Murji 43 na Zameen Murji 47 wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kukwepa kodi kiasi cha Sh. Bilioni sita. 

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Sylivia Mitanto akisaidiana na wakili Emmanuel Medalakini imedai kuwa tarehe isiyojulikana kati ya Januari 2021 Desemba 2022 jijini Dar es Salaam washtakiwa walishindwa kupeleka tamko la Mapato la biashara iliyosajiliwa kwa jina la Murji Brothers na kupelekea kukwepa kodi ya Sh. 6,224,341983.09/= 

Pia inadaiwa, siku na mahali hapo washtakiwa hao kwa pamoja kwa makusudi, walikwepa kodi kwa njia ya udanganyifu na kuisababishia Mamlaka ya Mapato (TRA) hasara ya kiasi cha fedha zaidi ya Sh. Bilioni 6/= 

Katika shtaka la utakatishaji fedha inadaiwa, Siku na mahali hapo washtakiwa hao walijipatia kiasi hicho cha fedha cha sh. bln 6/- huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kukwepa kodi. 

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. 

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, 2023.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger