Sunday, 12 February 2023

RAIS WA BUNGE LA AFRIKA 'PAP' CHIFU CHARUMBIRA AHUTUBIA BUNGE LA KIARABU, AHAMASISHA UWEKEZAJI BARANI AFRIKA

Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament (PAP) , Mhe. Chifu Fortune Charumbira akihutubia Mkutano wa Tano wa Maspika wa Mabaraza ya Kitaifa ya Kiarabu ya Bunge la Kiarabu mjini Cairo, Misri
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament (PAP) , Mhe. Chifu Fortune Charumbira (juu) akihutubia Mkutano wa Tano wa Maspika wa Mabaraza ya Kitaifa ya Kiarabu ya Bunge la Kiarabu mjini Cairo, Misri
Rais wa Bunge la Afrika (Pan African Parliament (PAP) , Mhe. Chifu Fortune Charumbira amehutubia Mkutano wa Tano wa Maspika wa Mabaraza ya Kitaifa ya Kiarabu ya Bunge la Kiarabu.



Mhe. Chifu Charumbira alikuwa mgeni rasmi katika Mkutano huo uliofanyika Februari 11, 2023 mjini Cairo, Misri.


Charumbira ametumia fursa hiyo kuwahamasisha na kuwaomba Waarabu kuwekeza barani Afrika hasa katika nyanja za miundombinu na kilimo.


"Bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa maliasili. Wawekezaji huja barani Afrika kutoka nchi za Magharibi, lakini kuna haja ya uwekezaji wa Waarabu na kusisitiza kuwa kuwe na nafasi ya uratibu kati ya Mabunge ya Kiarabu na Bunge la Afrika ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande zote mbili", alisema.


Pia alisisitiza haja ya kuja na mbinu za kiubunifu za kufadhili uchumi wa pande zote mbili kupitia ushirikiano mahiri kwa misingi ya mafanikio ili kuhakikisha kuwa uchumi wa mikoa yote miwili unachochewa kufikia uwezo wa juu wa kiuchumi.


Hatua hizi zote kwa mujibu wa Chifu Charumbira, zinapaswa kufanywa katika muktadha wa ramani zilizoainishwa vyema zinazojumuisha Ajenda 2063 na Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA). Bunge la Kiarabu na Bunge la Afrika lazima lifanye kazi kwa umoja katika utekelezaji wa ramani za barabara zinazoweza kusaidia eneo letu kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya haraka, aliendelea.


Alimpongeza Rt. Mhe. Spika AlAsoomi na timu yake sio tu kwa ajili ya kuwaleta pamoja Maspika wa Mabaraza ya Kitaifa ya Waarabu na Mabaraza, bali pia kwa kufanya hivyo chini ya kauli mbiu ambayo ni muhimu sana na kwa wakati muafaka hasa kwa Afrika na Ulimwengu wa Kiarabu, yaani, “Dira ya Bunge ya Kuimarisha Chakula. Usalama katika Ulimwengu wa Kiarabu."


Chifu Charumbira alieleza kuwa muundo wa mkutano huo na kauli mbiu hiyo inatambua mambo matatu: kwanza, Mabunge hayo yana jukumu kubwa la kuhakikisha usalama wa chakula katika Nchi Wanachama, mikoa na mabara; pili, kwamba Mabunge ya Mikoa, jumuiya za kiuchumi za kikanda na vyombo vya mabara vinaweza tu kufaulu kwa ushirikiano wa karibu baina yao; na, tatu, Waheshimiwa Maspika kama wakuu wa kisiasa wa Mabunge ya nchi zao wanapaswa kuwa mstari wa mbele wakati Mabunge yanatekeleza wajibu wao katika kuimarisha usalama wa chakula katika Ulimwengu wa Kiarabu na Afrika.


Chifu Charumbira alitoa wito wa wazi wa kuchukua hatua kwa kusisitiza kwamba hatua za maana lazima zifuate maazimio ambayo mkutano huo unapitisha na kuwakumbusha maneno ya Benjamin Franklin aliyosema kwa usahihi kwamba "Kufanya vizuri ni bora kuliko kusemwa vizuri."


"Maneno yaliyosemwa katika mkutano huu yanaweza kutia moyo, lakini ni hatua tu ndizo zitaleta mabadiliko", alisema Chifu Charumbira.

Share:

Saturday, 11 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 12,2023









Share:

CPB YAJIPANGA KUPAMBANA NA UPANDAJI WA BEI ZA MAZAO


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BODI ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB),imesema imejipanga kuhakikisha wanapambana katika kupunguza upandaji wa mazao mbalimbali kwa kuwasaidia wakulima upatikanaji wa mbolea kwa wakati,

Hayo yamebainishwa leo Februari 11,2023 Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB), Salum Hagan,wakati wa mkutano wa wadau wa bodi hiyo ulifanyika Ubungo jijini hapa .

Hagan amesema kupanda kwa chakula kinatokana na changamoto mbalimbali ikiwe upatikanaji hafifu kwa mbolea kunakochangiwa na hali ya Vita ya Ukrani na Urusi hivyo baada ya kuliona ilo Bodi hiyo na kusaidia upatikani wa mbolea kilahisi kwa wakulima na kupelekea kufanya kilimo kwa wingi na kusaidia kupungua kwa upandaji wa vyakula.

Mbali na jitihada hizo,Hagan amesema kwa sasa bodi inapanga kununua mazao kwa wingi kutoka kwa wakulima na kuweka ziada ya chakula ambapo amesema bodi hiyo inaweza kununua mazao yenye thamani ya bilioni 50 huku ikitarajia kuongeza kiasi hicho cha fedha na kufikia bilioni 100.

Hata hivyo,Hagan,amesema baada kuteuliwa kuongoza bodi hiyo kwa kipindi kifupi wameweza kubadili mifumo mbalimbali ndani ya bodi pamoja na kuwaita wadau kufanya kazi na CPB.

Kwa Upande wake Mstahiki Meya wa Ubungo na Diwani wa Kata ya Ubungo. Mh.Mwasha Hassan Siraju,ambaye alikuwepo kwenye mkutano huo na amempongeza mwenyekiti wa bodi ya CBP kuteuliwa kwenye nafasi na kusema bodi itakwenda kutatua changamoto ya upandaji wa mazao unaendelea hapa nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB), Salum Hagan akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa bodi hiyo ulifanyika leo Februari 11,2023 Ubungo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB), Salum Hagan akisisitiza jambo wakati akizungumza katika mkutano wa wadau wa bodi hiyo ulifanyika leo Februari 11,2023 Ubungo jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB), Salum Hagan akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa bodi hiyo ulifanyika leo Februari 11,2023 Ubungo jijini Dar es Salaam.

Wadau wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko(CPB) wakifuatilia mkutano ambao umefanyika leo Februari 11,2023 Jijini Dar es Salaam
Share:

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUACHA UHOLELA MITANDAONI

Msemaji wa Serikali na Idara ya habari- MAELEZO Gerson Msigwa  akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa TOMA.


Na Dotto Kwilasa,Malunde1 Blog,DODOMA

MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya habari-MAELEZO Gerson Msigwa amezindua Taasisi ya Waandishi wa habari mtandaoni (TOMA)huku akiwataka waandishi wa habari hizo kufanya kazi kwa kufuata misingi ya uandishi ili kuondokana na uholela .

Msigwa ameyasema hayo Februari 10,2023 Jijini Dodoma wakati akizindua Taasisi hiyo (TOMA)na kueleza kuwa uholela wa uandishi wa habari unadumaza taaluma hiyo na kusababisha kutoaminika na jamii hivyo kuwataka wanahabari mtandaoni kuzingatia weledi na kutokubali kutumika.

"Zingatieni weledi kuondokana na uholela holela uliopo miongoni mwenu,andikeni kwa kufuata kanuni na kataeni kutumika kwani mkifanya hivyo mtapoteza dhana ya uwepo na ukuaji wa sekta hii,"amesema

Amesema kutokana na kukua kwa matumizi ya TEHAMA,mitandao ya kijamii imerahisisha habari kufika kwa urahisi na kuwa chanzo kikuu cha habari hivyo kuwataka Waandishi wa habari kutumia kigezo hicho kukua kiuchumi na kijamii kwa kuzingatia maadili ya mtanzania. 

"Tasnia ya habari mtandao ipo mikononi mwa vyombo vya habari Mtandaoni, kwa sasa vyombo vya habari Mtandaoni ni  nguzo kubwa kwa sekta ya habari nchini,nitoe tu angalizo kwa sababu kadri zinavyoongezeka inaonekana kama weledi wake unapungua,

Niwatake TOMA kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni wanakuwa na uelewa mkubwa juu ya maudhui wanayoandikà wasiharibu utu wa mtu wala kukiuka haki za binadamu, kinachosumbua Media house nyingi ni weledi, kumeibuka watu ambao wanazusha tu habari zao bila kuzingatia maudhui uandishi hauko hivyo,"amesema

Kutokana na hayo Msigwa amewataka wamiliki wa vyombo vya habari hivyo  kuzingatia weledi katika utendaji kazi wao hasa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya teknolojia kwa kuhakikisha wanazingatia maudhui yanayoendana na taaluma hiyo.

"Sisi tujitahidi kujitofautisha na hao ili tulinde taaluma yetu na Serikali sio kwamba haioni juhudi za vyombo vya habari inaona na ndio maana imetoa uhuru wa kutosha kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo cha habari ila changamoto inatokea namna gani ya kuchuja kipi kiende hewani na kipi kisiende kulingana na maudhui yake,"amesema Msigwa 

Aidha, uzinduzi huo wa TOMA umeratibiwa na Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Arusha (APC) na kuhudhuriwa na wanahabari kutoka mikoa mbalimbali nchini.


Share:

WAENDESHA BODABODA WACHAFUKWA UJENZI BARABARA YA LUBAGA KUCHUKUA MUDA MREFU..."NJIA YA MCHEPUKO HATARI...TUNATOZWA FAINI KIHUNI"

Vifusi vikiwa barabarani

Na Halima Khoya - Malunde 1 blog
Waendesha pikipiki maarufu 'Bodaboda' katika Manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa barabara ya kutoka Shinyanga Mjini kuelekea Old Shinyanga (Lubaga) ili kutokana na kwamba njia ya mchepuko iliyowekwa kwa ajili ya kutumia siyo salama na ni hatari kwa watu na mali zao.


Wakizungumza na Malunde 1 blog wamesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo umetumia muda mrefu tangu Oktoba 2022 hadi sasa hivi mwezi Februari, 2023 na kwamba njia ya mchepuko iliyowekwa kwa ajili ya kutumia siyo salama na ni hatari kwa watu na mali zao.


Waendesha bodaboda hao akiwemo Juma Pius na Hamis Mathayo wamesema matengenezo ya barabara hiyo ni changamoto kwao kwani wanatozwa faini zisizo na ulazima (50,000 hadi 500,000) ambazo ni kinyume na sheria huku akiiomba serikali kumaliza haraka ujenzi huo ili kufanya kazi kwa uhuru.

"Nilikuwa na mteja nimempakia nikawa nimepita barabarani ghafla nikakutana na mkandarasi amesimama mbele yangu ikabidi nikatishe, katika harakati za kujitetea nikakunja pembeni wakati huo katikati ya barabara wamefunga waya kiasi kwamba hata ukienda vibaya unakufa,ikabidi nisimame wakachukua pikipiki wakapeleka kituoni, wakasema faini laki 5 ndipo alikuwepo kiongozi mwingine akasema faini ya ardhi ya TANROADS ni elfu 50,ikabidi nilipe nikapewa risiti ndiyo nikarudishiwa pikipiki yangu", amesema Pius.


Nao wajasiriamali wa vyakula na matunda Lubaga, Magret Samwel na Johan Shilla wamesema kuwa adha wanayokumbana nayo ni kukosa wateja hali inayosababishwa na kizuizi cha kukatisha barabara kwenda upande mwingine ili kutoa huduma zao hali inayorudisha nyumba mzunguko wa biashara zao.


"Mfano nina mteja kando ya barabara inanibidi nizunguke umbali mrefu sana ili nifike alipo hivyo tunakosa wateja wengi, tunaiomba mamlaka husika ifanye haraka kukamlisha ujenzi huu ili tuendelee na biashara zetu zinazotupatia kipato",amesema Shilla.


Kwa upande wake Meneja TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi  amesema kuwa Mkandarasi aliyechukua kazi hiyo yupo ndani ya muda ambapo mkataba wake ni wa miezi 8 na anatarajia kumaliza ujenzi huo mwezi wa 6 mwaka huu sambamba na kwamba hakuna faini inayotozwa kwa wananchi.


Ndirimbi amesema kuwa baadhi ya malighafi zinazotumika katika ujenzi huo zikiwemo kokoto zinatoka  nje ya Shinyanga ambapo amebainisha kuwa wakandarasi wanaofanya ujenzi huo wametoka ndani ya nchi ya Tanzania hivyo vifaa anavyotumia katika ujenzi huo ni vichache.


"Mkandarasi yupo ndani ya mkataba wa siku 240 ambayo ni miezi 8,hivyo tunaomba muwe wavumilivu, pia wakandarasi waweke tahadhari kwa wananchi pia wakandarasi wawasikilze wananchi bila kugombana", amesema Ndirimbi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger