Tuesday, 7 February 2023
MSIGWA AELEZA SABABU MUSWADA WA HUDUMA ZA HABARI KUSHINDWA KUWASILISHWA BUNGENI
Na Dotto Kwilasa, DODOMA
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa idara ya habari Maelezo Gerson Msigwa ameeleza kushindwa kuwasilishwa kwa Muswada huduma za habari Bungeni kuwa kumetokana na ufinuyu wa muda wa shughuli za bunge zinazoendelea hapa Jujini Dodoma.
Msigwa amesema hayo kwenye Mkutano wake na Waandishi wa Habari, leo Februari 07, 2023, Saa 10:30 Jioni,katika Ofisi za Idara ya Habari-MAELEZO, Dodoma na kufafanua kuwa wabunge kujadili taarifa ya kamati za kudumu za bunge imepelekea kusogeza mbele mswada wa Sheria ya huduma ya Habari uliofanyiwa marekebisho kutopelekwa bungeni kujadiliwa kama ilivyo stahili .
Msigwa amesema kuwa Serikali ilikusudia kupeleka mswada wa Sheria ya Huduma ya Habari katika bunge ambalo linaendelea ili uweze kujadiliwa lakini kutokana na muda kuwa mfinyu hawakuweza kuwasilisha muswada huo na badala yake utawasilishwa katika bunge lijalo ambalo linatarajiwa kuwa mwezi wa nne.
Msemaji huyo wa Serikali amefafanua,"Kama mnavyojua ndugu zangu wana habari Serikali baada ya kusikiliza maoni mbalimbali kutoka kwa wadau wa habari walitaka sheria ya huduma ya habari kufanyiwa marekebisho na kweli serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hasani aliona ni jambo jema ili kila mmoja aweze kufurahi na huduma hiyo,"amesema na kuongeza;
"Kweli serikali imekusanya maoni na hata wanahabari walitoa maoni yao kwa kutokana na kupatikana mwa maoni Serikali ilikuwa imekusudia kupereka marekebisho hayo bungeni ili wabunge waweze kujadili mswada huo,"anasisitiza Msigwa.
Pamoja na hayo amesema bunge linaloendelea ni kwa ajili ya kujadili taarifa za kamati za bunge na kwa maana hiyo muda haukuweza kutosha kuweza kujadili muswada huo na kwamba mswada huo mahusu hautaweza kupelekwa bungeni kwa Sasa na badala yake utajadiliwa bunge lijalo la mwezi wa nne .
"Mswada huo utapelekwa bungeni na utajadiliwa kwani uko vizuri na umeandaliwa vizuri,maoni yote ya wadau yamezingatiwa na yamefanyiwa kazi tunataka mswada huo uweze kuwafurahisha watanzania wote ili kila mdau wa habari aweze kuwa na uhuru wa sheria hiyo na hiyo ndiyo makusudi njema ya serikali" amesema Msigwa .
"Pamoja na Sheria ya huduma ya Habari bado kuna miswada mingi ambayo ilitakiwa kupelekwa bungeni lakini kutokana na ufinyu wa muda miswada hiyo haikuweza kupelekwa bungeni na yote itapelekwa bungeni katika bunge ljalo kwa manufaa ya watanzania wote,hii haiwezi kuathiri kitu chochote,"amesema.
DUWASA YA SAINI MKATABA WA UBORESHAJI HUDUMA NZUGUNI
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri (wa tatu kulia) wakishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kulia) na Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Tanzania Steel Pipes, Mhandisi Emmanuel Mwambapa wakitia saini uboreshaji wa huduma ya majisafi eneo la Nzunguni katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya DUWASA leo Februari 7, 2023.MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri (wa tatu kulia) wakishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kulia) na Meneja Mikataba kutoka Kampuni ya Help Desk Engineer, Godfrey Peter wakitia saini uboreshaji wa huduma ya majisafi eneo la Nzunguni katika hafla iliyofanyika makao makuu ya DUWASA leo Februari 7, 2023.MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule (wa pili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri (wa tatu kulia) wakishuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kulia) na Msimamizi wa Mradi kutoka Kampuni ya Tanzania Steel Pipes, Mhandisi Emmanuel Mwambapa wakibadilishana mikataba uboreshaji wa huduma ya majisafi eneo la Nzunguni baada ya kusaini katika hafla iliyofanyika makao makuu ya DUWASA leo Februari 7, 2023.MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini uboreshaji wa huduma ya majisafi eneo la Nzunguni iliyofanyika Makao Makuu ya DUWASA leo Februari 7, 2023. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa MazingiraDodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini uboreshaji wa huduma ya majisafi eneo la Nzunguni iliyofanyika Makao Makuu ya DUWASA leo Februari 7, 2023. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri.
WAZIRI MKUU MGENI RASMI UZINDUZI WA NYARAKA ZA USIMAMIZI WA MAAFA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao na waandishi wa Habari Februari 7, 2023 kuhusu Uzinduzi wa Nyaraka za Usimamizi wa Maafa utakaofanyika Februari 9, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano Kambarage Hazina Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa pamoja na Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
******************************
Na Mwandishi wetu; Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Nyaraka za Usimamizi wa Maafa nchini tarehe 09 Februari, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kambarage uliopo Hazina Jijini Dodoma.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene alipokutana na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari Bungeni Dodoma tarehe 7 Februari, 2023 kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la uzinduzi.
Waziri Simbachawene alisema, katika kuendeleza juhudi za kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Maafa Nchini, Serikali imefanya mapitio ya Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na kukabiliana na Maafa (2012), Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano Wakati wa Maafa (2012) na Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja (2015-2020). Hivyo, mapitio hayo yamewezesha kuandaliwa kwa nyaraka tano zitakazozinduliwa ikiwemo;Mpango wa Taifa wa Kujiandaa na kukabiliana na Maafa (2022),Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wakati wa Maafa (2022) na Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja (2022-2027),Mkakati wa Taifa wa Usimamizi wa Maafa (2022-2027) na Mwongozo wa Taifa wa Kupambana na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu (2022).
“Nyaraka zote tano zimeandaliwa kwa kushirikisha wadau ndani na nje ya Serikali. Nyaraka zinazozinduliwa zimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na baadaye katika mifumo ya kitaifa, kikanda na kimataifa,”alisema Waziri.
Alifafanua kuwa, mipango na mikakati iliyoandaliwa itaimarisha usimamizi wa maafa yanayosababishwa na majanga ya nguvu za asili kama vile mafuriko na matetemeko ya ardhi na majanga yanayochochewa na shughuli za kibinadamu.
Aidha, Majukumu ya utendaji yanazingatia taasisi yenye wajibu wa kisheria, ujuzi pamoja na rasilimali zinazohitajika. Mfumo uliopo umezingatia wajibu wa sekta kutambua hatari za maafa katika eneo lake, kutenga rasilimali za kisekta kabla ya tukio kwa ajili ya kuzuia au kupunguza madhara pamoja na kujiandaa kukabili maafa endapo yatatokea.
Aliongezea kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeendelea kuimarisha shughuli za kuratibu na kusimamia shughuli za maafa kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 na Kanuni zake za mwaka 2022 pamoja na miongozo, mikakati na taratibu za kiutendaji zinazowezesha utekelezaji wa majukumu na kuimarisha uwajibikaji na ushirikiano wa wadau.
MAKUSANYO KODI YA ARDHI YAONGEZEKA KUFIKIA BILIONI 33.9
********************************
Na Munir Shemweta, WANMM
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 90.9 katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba 2022 kama kodi ya pango la ardhi sawa na asilimia 75 ya lengo la makusanyo ya shilingi bilioni 121.
Aidha, makusanyo ya mwaka wa fedha 2022/2023 yameongezeka kwa shilingi bilioni 33.9 ikilinganishwa na kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Kuongezeka kwa makusanyo kumechangiwa na msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi ambapo wananchi walio na malimbikizo walipewa nafuu ya kulipa deni la msingi kuanzia julai hadi desemba 2022 uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Hayo yalibainishwa leo tarehe 7 Februari 2023 na Waziri wa Ardhi Nyumba an Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ulipaji kodi ya pango la ardhi na maduhuli mengine ya sekta ya ardhi mkoani Dodoma.
Hata hivyo, Dkt Mabula alisema, Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuongeza kipindi cha msamaha hadi April 2023 na kubainisha kuwa, uamuzi huo ulifikiwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maombi mengi ya wananchi na taasisi yaliyoifikia serikali.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, wananchi 6,211 wameufaika na msamaha wa riba ya malimbikizo sawa na shilingi 11,931,537,409.80.
‘’Serikali inaamini kuwa fedha zilizosamehewa zimeenda kuleta nafuu kwa wahusika na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii nchini na nimshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuwasamehe kisi kikubwa hicho cha pesa kwa lengo la kuwaondolea mzigo wananchi na taasissi mbalimbali’. Alisema Dkt Mabula.
Ametoa rai kwa taasisi na mashirika ya umma na wananchi wote kutumia muda uliotolewa hadi April 30, 2023 kunufaika na msamaha wa riba uliotolewa na serikali kulipa deni la msingi (Principa amount) ili wasamehewe riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi.
Ameelekeza ofisi zote za ardhi nchini kutoa huduma siku zote hadi mwisho wa mwezi April 2023 ili kuwezesha upatikanaji huduma za ukadiriaji kodi kwa wakati na kuwasihi wananchi kuendelea kutumia njia za kielektroniki alizozieleza kuwa zimeanza kutolewa na benki washirika za CRDB na NMB katika kukadiria kulipa kodi.
‘’Waandishi wa habari wajulisheni wananchi kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameongeza muda wa msamaha wa riba ya malimbikizo na Wizara imejipanga kikamilifu ili kuwezesha wananchi kupata nafuu ya msamaha wa riba ya kodi ya pango la ardhi iliyotolewa’’ alisema Dkt Mabula.
ORODHA YA WAPISHI WA CAKE SHINYANGA 'SHY BAKERS', NAMBA ZA SIMU HIZI HAPA
Kikundi cha Wapishi wa Keki (Cake Bakers) Manispaa ya Shinyanga kimefanya Sherehe Maalum ‘Shy Bakers White Party 2023’ kufungua rasmi Mwaka 2023 na kupanga mikakati mbalimbali ya kutanua wigo wa kazi yao.
Sherehe hiyo iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 katika ukumbi wa Green View uliopo Kambarage Mjini Shinyanga imehudhuriwa na wanachama wa kikundi hicho cha Wapishi maarufu wa Keki na wapambaji wa keki katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo maarufu ‘Binti Mdongo Cake’ amesema wameamua kufanya sherehe ili kufungua rasmi mwaka 2023.
“Sisi wapambaji wa keki na wapishi wa keki za aina na shughuli mbalimbali tumekutana kwa ajili ya kufungua rasmi mwaka 2023 kwa kujadili maendeleo ya kikundi chetu lakini pia kupanga mikakati mbalimbali jinsi ya kutanua wigo wa kazi yetu. Tumekula chakula cha pamoja, tumekunywa, tumecheza muziki, kubadilishana mawazo na kupeana zawadi”,ameeleza Tabitha.
Tabitha ametumia fursa hiyo kuwaomba wateja kuendelea kupata huduma ya keki zinazotengenezwa na wanachama wa kikundi hicho huku akiwakaribisha wapishi wengine wa keki kujiunga na kikundi chao.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo akizungumza wakati wa Shy Bakers White Party 2023 iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo akizungumza wakati wa Shy Bakers White Party 2023 iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 Mjini Shinyanga.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakionesha Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakionesha Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
GGML YAKABIDHI MADARASA MAWILI KWA SHULE YA MSINGI KIZIBA
Afisa Uhusiano wa kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Dorine Denis (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa madarasa mawili yaliyojengwa na kampuni hiyo katika Shule ya Msingi Kiziba iliyopo Kijiji cha Mwenegeza wilayani Geita. Dorine alimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Terry Strong. Kushoto ni Mtendaji wa Kata ya Nyakagomba, Christopha Amos.
Na Mwandishi Wetu - Geita
KATIKA kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha elimu na kulea kizazi kijacho ambacho kitasaidia Taifa kufikia malengo ya kiuchumi na kimaendeleo, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imejenga na kukabidhi vyumba viwili vya madarasa kwa Shule ya Msingi Kiziba iliyopo Kijiji cha Mwenegeza kata ya Nyakagomba, Wilayani Geita mkoani Geita.
Madarasa hayo mawili yenye thamani ya Sh milioni 42, yanalenga kusaidia kutoa mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi ambao ufaulu wao umeathiriwa na mazingira magumu ya kujifunza.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madarasa hayo mwishoni mwa wiki mjini Geita kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Terry Strong, Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Dorine Denis alisema elimu ni nguzo muhimu ya jamii hivyo bila elimu,ni vigumu kupata maendeleo.
Alisema elimu inaweza kubadilisha maisha ya watu na ni mwelekeo wa miradi yetu ya uwekezaji wa jamii.
“GGML inaamini kuwa wananchi wa Tanzania ndio mtaji mkubwa wa kampuni hii na siku zote imekuwa ikiunga mkono juhudi za serikali za kuboresha elimu na kujenga kizazi kijacho ambacho kitasaidia taifa la Tanzania kufikia malengo yake makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.
“GGML imedhamiria kuchochea maendeleo endelevu ya jamii zinazozunguka mgodi na imedhihirisha hilo mara kwa mara kwa kushirikiana kikamilifu na serikali katika kuboresha huduma za jamii ikiwemo elimu, afya, maji na barabara pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi kwa jamii zinazozunguka mgodi huo.
“Tunakusudia kuwa na urithi uliojengwa na uchumi endelevu wa ndani unaoweza kukaa muda mrefu hata baada ya shughuli za uchimbaji madini mkoani Geita kumalizika,” alisema.
Alisema GGML inafanya kazi ya kuunga mkono malengo ya serikali ya Tanzania ya ukuaji thabiti wa uchumi na maboresho ya miundombinu ya kijamii.
“Hii inaendana na thamani yetu ya msingi ya kusaidia serikali katika kukuza ukuaji wa uchumi wa muda mrefu katika jamii tunakofanyia kazi. Kwa hiyo nimefurahishwa kwamba ujenzi wa madarasa haya umetokana na juhudi za ushirikiano kati ya serikali, jamii mwenyeji na GGML,” alisema.
Aidha, aliahidi kuwa GGML itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na wadau wengine ili kufikia lengo la sekta ya madini la kuchangia asilimia 10 katika pato la taifa ifikapo mwaka 2025.
Naye Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kiziba Beatus Mwandu aliishukuru GGML kwa ujenzi wa madarasa hayo hasa ikizingatiwa shule hiyo bado inakabiliwa na uhaba wa madarasa huku mengine yakiwa yamechakaa.
Aidha, Mtendaji wa Kata ya Nyakagomba, Christopha Amos naye aliishukuru GGML kwa msaada huo na kuahidi pia kufikisha kilio cha changamoto nyingine kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili azifanyie kazi.
WAPISHI WA KEKI MAARUFU SHINYANGA WAFANYA SHEREHE MAALUM ‘SHY BAKERS WHITE PARTY 2023'
Shy Bakers White Party 2023
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kikundi cha Wapishi wa Keki (Cake Bakers) Manispaa ya Shinyanga kimefanya Sherehe Maalum ‘Shy Bakers White Party 2023’ kufungua rasmi Mwaka 2023 na kupanga mikakati mbalimbali ya kutanua wigo wa kazi yao.
Sherehe hiyo iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 katika ukumbi wa Green View uliopo Kambarage Mjini Shinyanga imehudhuriwa na wanachama wa kikundi hicho cha Wapishi maarufu wa Keki na wapambaji wa keki katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa sherehe hiyo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo maarufu ‘Binti Mdongo Cake’ amesema wameamua kufanya sherehe ili kufungua rasmi mwaka 2023.
“Sisi wapambaji wa keki na wapishi wa keki za aina na shughuli mbalimbali tumekutana kwa ajili ya kufungua rasmi mwaka 2023 kwa kujadili maendeleo ya kikundi chetu lakini pia kupanga mikakati mbalimbali jinsi ya kutanua wigo wa kazi yetu. Tumekula chakula cha pamoja, tumekunywa, tumecheza muziki, kubadilishana mawazo na kupeana zawadi”,ameeleza Tabitha.
Tabitha ametumia fursa hiyo kuwaomba wateja kuendelea kupata huduma ya keki zinazotengenezwa na wanachama wa kikundi hicho huku akiwakaribisha wapishi wengine wa keki kujiunga na kikundi chao.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo akizungumza wakati wa Shy Bakers White Party 2023 iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo akisoma taarifa ya kikundi hicho wakati wa Shy Bakers White Party 2023 iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo akizungumza wakati wa Shy Bakers White Party 2023 iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 Mjini Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga Bi. Tabitha Mdongo akizungumza wakati wa Shy Bakers White Party 2023 iliyofanyika Jumatatu Februari 6,2023 Mjini Shinyanga.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakitoa burudani kwenye Shy Bakers White Party 2023.

Burudani ikiendelea kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Burudani ikiendelea kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakipiga picha baada ya kucheza muziki kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakionesha Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakionesha Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakionesha Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakionesha Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakikata Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakikata Keki Maalumu waliyoiandaa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Vyombo vya chakula kilichoandaliwa kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakipata chakula kwenye Shy Bakers White Party 2023.

Wanachama wa Kikundi cha Wapishi wa Keki katika Manispaa ya Shinyanga wakipiga picha kwenye Shy Bakers White Party 2023.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog