Saturday, 4 February 2023

BENKI YA CRDB YAKABIDHI KITUO CHA MAWASILIANO OCEAN ROAD

Benki ya CRDB imekabidhi kituo cha mawasiliano katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ikiwa ni matokeo ya fedha zilizokusanywa katika mbio za CRDB Bank Marathon 2021. Kituo hicho cha kisasa na cha kwanza kwa hospitali hapa nchini kimekabidhiwa kwa uongozi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla aliekua Mgeni Rasmi katika hafla hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Mussa Nsekela amesema Benki ya CRDB ni mdau mkubwa wa maendeleo ya sekta ya afya nchini kupitia Sera ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI Policy) ambayo inaelekeza Benki kutenga asilimia moja ya faida yake kila mwaka kwa ajili ya kutatua changamoto katika sekta ya afya, elimu, mazingira, na uwezeshaji kwa wanawake na vijana.

Katika sekta ya afya Benki ya CRDB imejikita zaidi katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto na pia huduma za kibobezi (specialist services), ikiwa ni pamoja na ufadhili wa ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya, wodi za wagonjwa pamoja na utoaji wa vifaa tiba katika vituo vya afaua , zahanati na hospitali mbalimbali nchini.


“Mwaka 2020 Benki ya CRDB ilianzisha mbio za hisani zilizopewa jina la CRDB Bank Marathon kwa lengo la kusaidia jamii kwa kushirikisha wadau mbalimbali. Kupitia mbio hizi mnamo mwaka 2021, tukishirikiana na washirika wetu ambao baadhi tupo nao hapa tulifanikiwa kukusanya takribani Shilingi Milioni 500 ambapo kati ya hizo tulitenga kiasi cha Shilingi Milioni 102 kufadhili ujenzi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja chini ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ili kurahisisha ufikishwaji wa huduma, elimu na ushauri juu ya Saratani kwa watanzania wengi” aliongeza Nsekela.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage ameishukuru Benki ya CRDB kwa kusaidia ujenzi wa kituo hiko cha mawasiliano ambacho kinakwenda kuisaidia katika kutekekeleza malengo ya kuanzishwa kwake hususan upande wa kuongeza uelewa wa ugonjwa wa Saratani jambo ambalo ni muhimu katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.


“Tunaishukuru Benki ya CRDB sambamba na washirika wake Sanlam, Strategis na Alliance Insurance pamoja na wakimbiaji zaidi ya elfu 5 ambao kwa kushiriki kwao katika marathon ile ya mwaka 2021 leo tumeweza kuwa na kituo hiki cha kisasa ambacho kinakwenda kuokoa maisha ya Watanzania” alsema Dkt. Mwaiselage.
Makabidhiano hayo yalitanguliwa na matembezi ya hisani yalioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe, Amos Makalla yamefanyika katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Dar es Salaam yakilenga kuongeza ufahamu wa ugonjwa wa saratani.

Sehemu ya washiriki wa matembezi hayo walikua ni mashujaa waliopona ugonjwa wa Saratani ambapo walisisitiza umuhimu wa kupima saratani mara kwa mara kwani kugundulika kwa mapema kwa saratani kuna mchango mkubwa katika matibabu yake.
Akizungumza katika halfa hiyo Mhe. Makalla amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetenga fedha za kutosha kwenye sekta ya afya na kuhakikisha kunakua na mgawanyo mzuri wa vituo vya afya katika ngazi zote ili kuhakikisha wananchi kutoka maeneo yote ya nchi wanapata huduma bora za afya.


Kwa upande mwingine Mhe. Makalla aimeipongeza Benki ya CRDB na washirika wake kwa kufanikisha ujenzi wa kituo hiko kama walivyoahidi wakati wakihamaisha ushiriki wa mbio za CRDB Bank Marathon na kuahidi kuwa ataendelea kuwa mshiriki wa mbio hizo kama ambavyo amefanya katika miaka miwili iliyopita.
“Mimi ni shahidi mzuri wa mbio hizi na naamini CRDB Bank Marathon ya mwaka huu itakua bora zaidi ya zilizopita na natoa wito kwa wadau kushiriki kwa wingi katika mbio hizi kwani fedha zinazopatikana katika mbio hizo zinarejeshwa kwenye jamii hususan kwenye sekta ya afya” aliongeza Mhe. Makalla.


Pamoja na ujenzi wa kituo hiko, mbio za CRDB Bank Marathon kwa mwaka 2021 ziliweza kusaidia matibabu ya watoto zaidi ya 100 wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo pia kwa mwaka jana kupitia mbio hizo jumla ya Shilingi Milioni zilipelekwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Shilingi zilipelekwa katika Hospitali ya CCBRT kusaidia wanawake ambao wana ujauzito hatarishi.


















Share:

Friday, 3 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 4,2023










Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI USIKU HUU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:-

(1) Amemteua Bi Janet Zebedayo Mbene kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

(2) Amemteua Bw. James Andilile Mwainyekule kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Bw. Mwainyekule ni Mhasibu Mkuu, Tume ya Pamoja ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.

(3) Amemteua Bw. Rashid Kassim Mchatta kuwa Skauti Mkuu Tanzania. Bw. Mchatta anachukua nafasi ya Bi. Mwantumu Mahiza ambaye muda wa kutumikia nafasi hiyo umemalizika.

(4) Amemteua Bw. Gilead John Teri kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Bw. Teri ni Mshauri Mwandamizi, Umoja wa Ulaya (EU), Copenhagen, Denmark.

(5) Amemteua Bw. Damasi Joseph Mfugale kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Bw Mfugale ni Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Afrika Chapter EBI International Consulting Group, Canada.

(6) Amewateua Makamishna wa Tume wawili (2) kama ifuatavyo:-


(i) Bi. Caroline Joseph Mutahanamilwa kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania; na


(ii) Bw. Idd Ramadhan Mandi kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.



Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Februari, 2023.



Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Share:

WANANCHI WAIPONGEZA TANESCO KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA KUREJESHA UMEME, KUDHIBITI ATHARI ZAIDI MVUA YA UPEPO SHINYANGA


Mafundi wa TANESCO wakiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo  la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga 


Na Halima Khoya - Shinyanga

Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wamelishukuru Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga kwa jitihada wanazozifanya kurejesha huduma hiyo mara baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo kunyesha February 2,2023 hali iliyosababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme pamoja na nyumba kuanguka.


Wananchi hao wametoa Pongezi leo February,03,2023 wakati Wafanyakazi wa TANESCO wakiendelea na  zoezi la kurekebisha miundombinu ya umeme maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Shinyanga  yaliyoathiriwa na mvua hiyo ya upepo.

Saidi Hussein na Josephina Mondi ni miongoni mwa wateja wa TANESCO walioathiriwa na mvua ambapo wamesema ulianza upepo kisha wakasikia mtikisiko mkubwa ambao umesababisha kuanguka kwa nguzo ya umeme  na nyumba kubomoka.

Aidha wameishukuru TANESCO kuchukua hatua za haraka kuzima umeme mapema hali iliyosababisha kutokuwepo kwa madhara kwa binadamu.

Kaimu Meneja  wa TANESCO mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Leo Mwakatobe, amesema kuwa mvua hiyo imesababisha madhara ya kuanguka kwa nguzo maeneo mbal mbali katika Manispaa hiyo hali iliyosababisha wateja wao kukosa huduma ya umeme lakini pia shirika hilo kukosa mapato kwa kusambaza umeme.


Mwakatobe amesema wateja wengi wamerejeshewa huduma ya umeme na  wanaendelea kurejesha umeme kwenye maeneo yaliyobakia  huku akiwaasa wananchi waendelee kutoa taarifa mapema inapotokea changamoto ya umeme ili kitengo cha dharura kiwajibike haraka na kuondokana na madhara makubwa.


"Sisi shirika la umeme tumepata athari kubwa nguzo nyingi zimedondoka, wateja wengine mita zao zimevunjika baada ya kuangukiwa na miti kwa hiyo shirika limekosa mapato. Licha ya kutokea kwa changamoto hiyo TANESCO Shinyanga kitengo chetu cha dharura kimesimama vyema na hakuna athari iliyotokea kwa binadamu zaidi ya baadhi ya nyumba za wateja wetu kuharibika" amesema Mhandisi Mwakatobe.
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha nguzo za umeme zilizoanguka katika eneo la Nhelegani Manispaa ya Shinyanga kufuatia mvua iliyoambatana na upepo Februari 2,2023.  Picha na Kadama Malunde
Zoezi la kuchimba mashimo kwa ajili ya kuweka nguzo mpya za umeme likiendelea katika eneo la Nhelegani Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa Nguzo za umeme zilizoathiriwa na Mvua ya upepo katika eneo  la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga 
Muonekano wa Nguzo za umeme zilizoathiriwa na Mvua ya upepo katika eneo  la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga 
Fundi wa TANESCO akiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo  la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga 
Fundi wa TANESCO akiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo  la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga 
Mafundi wa TANESCO wakiendelea na kazi ya kutengeneza miundombinu ya umeme katika eneo  la Iwelyangula kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga 

Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe (katikati), Mhandisi Mkuu wa TANESCO Shinyanga, Kurwa Mangara (kulia)  na Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja Lilian Mungai wakiangalia nguzo ya umeme iliyoathiriwa na mvua ya upepo kwenye nyumba ya mteja wa TANESCO eneo la Buhangija Mjini Shinyanga
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha miundombinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua ya upepo kuangusha mti katika eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha miundombinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua ya upepo kuangusha mti katika eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe akionesha miundombinu ya umeme iliyoharibika kufuatia mvua ya upepo kuangusha mti katika eneo la Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga, Daniel Emmanuel Manga akielezea jinsi mvua ya upepo ilivyoharibu kanisa hilo.
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Muonekano wa Kanisa la EAGT Mshikamano kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga lililoanguka kufuatia mvua ya upepo iliyonyesha Februari 2,2023
Mhandisi Mkuu wa TANESCO Shinyanga, Kurwa Mangara akionesha  mita na chuma cha kupokelea umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba ya mkazi wa Lubaga Mjini Shinyanga baada ya kuathiriwa na mvua ya upepo. Kushoto ni Afisa Mahusiano na Huduma kwa wateja Lilian Mungai katikati ni Kaimu Meneja TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe
Zeozi la kurejesha huduma ya umeme likiendelea katika eneo la Lubaga Mjini Shinyanga 
Zeozi la kurejesha huduma ya umeme likiendelea katika eneo la Lubaga Mjini Shinyanga .

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger