Wednesday, 11 January 2023

MAKAMANDA WA POLISI WATANGAZA KIAMA KWA WEZI WA MAFUTA, VIFAA VYA UJENZI RELI YA KISASA 'SGR'


Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Januari 1,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu matokeo ya Operesheni ya kubaini na kukamata wezi wa mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akielezea hatua zinazochukuliwa na Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza katika kulinda Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Isaka- Mwanza. Wa kwanza kushoto ni  Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akifuatiwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akiongozana na makamanda wa Polisi mikoa ya Shinyanga na Simiyu, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta na maafisa mbalimbali wa jeshi la Polisi katika kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza wametoa onyo kali kwa watu wanaohujumu Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Isaka hadi Mwanza kwa kuiba mafuta ya dizeli na vifaa vya ujenzi wakisisitiza kuwa ni lazima mradi huo uwe salama muda wote.

Onyo hilo limetolewa leo Jumatano Januari 11,2023 na Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga (ACP Janeth Magomi), Simiyu (ACP Blasius Chatanda), na Mwanza (SACP Wilbroad Mutafungwa) walipotembelea Kambi Kuu ya Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi CCECC kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ili kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi.
Akizungumza kwa niaba ya Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa amesema kamwe hawapo tayari kuona mradi huo unahujumiwa na baadhi ya wafanyakazi waliopo ndani ya mradi huo na wananchi walio nje ya mradi huo.


Kamanda Mutafungwa amesema Jeshi la Polisi katika mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza wanaendelea na msako mkali na Operesheni ya Pamoja ‘Joint Operation’ ya kuwabaini na kuwakamata watu wote wanaohujumu ujenzi wa mradi huo wa Reli ya Kisasa kwa namna yoyote iwe kuiba,kupokea, kushiriki kuiba mafuta na vifaa vingine vya ujenzi.
Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa SGR (Isaka – Mwanza) upande wa Mkandarasi Kampuni ya CCECC – CRCC JV, Bw. Wang Chao.

“Operesheni hii ni endelevu, tutahakikisha tunawakamata watu wote waliopo ndani ya mradi na walio nje ya mradi ambao kwa namna yoyot wanafanya uhalifu kwa kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi. Tunaomba wananchi endeleeni kushirikiana na Polisi kutupa taarifa fiche, na tayari tumekamata baadhi ya wahalifu,madumu,baiskeli na pikipiki wanazotumia kuiba”,amesema Mutafungwa.

“Huu ni Mradi Mkubwa sana na ni mali ya Watanzania wote, hivyo ni lazima kila mmoja ashiriki kuulinda. Tutatumia nguvu zote kuulinda, tunatuma salamu kwa wahalifu wakafute kazi nyingine ya kufanya siyo kuhujumu mradi huu. Tupeni taarifa tushughulike na wahalifu”,ameongeza Kamanda Mutafungwa.

Kamanda huyo wa Polisi Mwanza ametumia fursa hiyo kuyatahadharisha baadhi ya Makampuni ya Ulinzi yanayofanya kazi ya ulinzi kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kuzingatia maadili na uadilifu .

“Tunafuatilia pia kuhusu Makampuni ya ulinzi yenye ulegevu, haiwezekani vifaa vya ujenzi viibiwe Site. Sisi tunafuatilia pia, tupeni taarifa ili tufanye mapitio ya maadili na uadilifu. Pia tuendelee kutoa elimu kwa wananchi kwenye kata zote ambako mradi huu unapita,huko kuna Mkaguzi wa kata, tunataka wananchi wawe wamiliki wa mradi, waulinde”, amesema Mutafungwa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema Makamanda wa Polisi wataendelea kushirikiana katika Operesheni ya kuwabaini na kuwakamata wahalifu wote ili mafuta na vifaa vya ujenzi visiibiwe kwa kupambana na baadhi ya wafanyakazi waliopo ndani ya mradi na waliopo nje ya mradi wanaoshirikiana katika wizi huo.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Blasius Chatanda amesema ana furahi kuona wimbi la wizi wa mafuta na vifaa vya ujenzi limepungua ukilinganisha na siku za mwanzo wakati ujenzi unaanza mnamo mwaka 2021.

“Nafurahi kuona wimbi la wizi limepungua, mwanzo hali ilikuwa mbaya, kulikuwa na udokozi uliohusisha wafanyakazi ndani ya mradi na waliopo nje ya mradi. Hali hiyo tumeidhibiti wamebaki wachache walio nje ya mradi ambao ni rahisi kupambana nao. Tuendelee kupeana taarifa na kushirikiana, haiwezekani mradi uhujumiwe na sisi tupo”,amesema Chatanda.



Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa SGR (Isaka – Mwanza) upande wa Mkandarasi Kampuni ya CCECC – CRCC JV, Bw. Wang Chao, Mwanasheria wa Mradi Akida Majenga na Meneja Usalama wa Mradi huo, Wilbert Sichome wamesema licha ya maendeleo mazuri ya mradi, changamoto iliyopo ni udokozi wa mafuta na vifaa ambapo vifaa vimekuwa vikiibiwa Site na vibaka huku wakiomba kuwepo kwa magari ya doria ili kuimarisha hasa wanapoelekea kuongeza vifaa.
Madumu, mipira, baiskeli, pikipiki zilizokamatwa zikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi

Naye Afisa Rasilimali kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Cornel Kyai amesema hali ya wizi wa vifaa vya ujenzi imepungua huku akiipongeza Operesheni inayoendelea kufanywa na Kikosi cha Polisi Reli na Jeshi la Polisi kuendelea kudhibiti vitendo vya wizi ambapo mpaka sasa mafuta zaidi ya lita 10,000 yameokolewa,pikipiki,baiskeli na watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Akizungumzia matokeo ya Oparesheni inayoendelea, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta amesema
tarehe 9 Januari 2023 majira ya saa 10:50 jioni katika eneo la Seke kwenye barabara ya mradi wa ujenzi wa reli wakiwa kwenye doria na misako ya wahalifu walimkamata Abel Luekila (22) mkazi wa Ngudu Kwimba akiwa na amepakia madumu 9 ya mafuta ya dizeli kwenye pikipiki aina ya Kinglion isiyo na usajili ambapo kila dumu la mafuta lilikuwa na ujazo wa lita 20 jumla lita 180.

Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta.

“Kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi sasa jumla ya mafuta ya dizeli lita 520, ukiongeza lita 180 na kufanya idadi kuwa lita 700 yameokolewa na askari polisi wa reli ambapo wahalifu waliyaficha mafuta hayo kwenye vichaka”, ameeleza Mbuta.

“Vitu vingine vilivyotelekezwa na wahalifu kwa lengo la kukwepa mkono wa sheria ni pamoja na pikipiki zaidi ya 20, baiskeli 8, madumu tupu zaidi ya 120 yatumikayo na wahalifu kuiba mafuta na mipira 22 ya kunyonyea mafuta”,ameeleza Mbuta.

Amefananua kuwa kwa kipindi cha Mwezi Januari hadi Novemba 2021 walifanikiwa kukamata lita za mafuta 5820 yenye thamani ya shilingi 18,328,870/=.

“Kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba 2022 tulikamata mafuta ya dizeli lita 13,922 yenye thamani ya shilingi 43,589,782/= ambapo thamani ya mafuta yote ni shilingi 61,918,652/=. Hii ni thamani ya mafuta kabla ya matukio mapya. Tayari watu 21 wamefungwa jela”,amesema.


“Tumejipanga vizuri, hakuna mhalifu atabaki salama. Kwa yeyote atakayeingiwa na tamaa ya kuiba vifaa vya ujenzi, mafuta tutamfikia popote alipo, tutamkamata na kumfikisha mahakamani., kikubwa tuendelee kupeana taarifa”,amesema Mbuta.


“Mradi huu wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) ni wetu Watanzania hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi wa reli hii, vifaa vinavyotumika na mafuta. Wenyeviti vitongoji, mitaa na viongozi wote kwa kushirikiana na wananchi kila mmoja anatakiwa kuwa mlinzi na kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha reli yetu muda wote inakuwa salama”, ameongeza Mbuta.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu leo Jumatano Januari 11,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Januari 1,2023 wakati akitoa taarifa kuhusu matokeo ya Operesheni ya kubaini na kukamata wezi wa mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Maafisa wa Polisi wakiwa katika kituo cha Seke Stesheni
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akionesha madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akionesha madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akionesha madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta akionesha madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Sehemu ya madumu, baiskeli, pikipiki, mipira iliyokamatwa ikitumika kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi kwenye mradi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka - Mwanza. 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa (kushoto)  akizungumza na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta, Makamanda wa Polisi na maafisa wa polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza namna ya kulinda Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Isaka- Mwanza.
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta,  akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) 
Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta,  akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa SGR (Isaka – Mwanza) upande wa Mkandarasi Kampuni ya CCECC – CRCC JV, Bw. Wang Chao akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Meneja Usalama wa Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka- Mwanza Wilbert Sichome akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Meneja Usalama wa Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Isaka- Mwanza Wilbert Sichome (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Mwanasheria wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Akida Majenga akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Mwanasheria wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Akida Majenga akizungumza wakati wa kikao cha Makamanda wa polisi na maafisa wa polisi mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Simiyu na Uongozi wa Kampuni ya CCECC – CRCC JV inayotekeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR)
Afisa Rasilimali kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Cornel Kyai 
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza SACP Wilbroad Mutafungwa akiongozana na makamanda wa Polisi mikoa ya Shinyanga na Simiyu, Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Tanzania, ACP Sebastian Mbuta na maafisa mbalimbali wa jeshi la Polisi katika kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:

ASKARI POLISI AKUTWA AMEFARIKI KWENYE NYUMBA YA KULALA WAGENI ARUSHA NDUGU WAKIMUUA KIJANA ALIYETUKANA MAMA YAKE MZAZI

Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi

Jesh la Polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa tarehe 08 Januari mwaka huu Jeshi hilo lilipokea taarifa ya matukio ya watu wawili kufariki dunia katika maeneo tofauti tofauti katika Mkoa wa Arusha.


Akitoa taarifa hiyo  leo Januari 11 kamanda wa Palisi Mkoa wa Arusha kamishina Msadizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa Tarehe 08.01.2023 muda wa saa 08:30 usiku Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilipokea taarifa ya uwepo wa mtu mmoja ambaye alifariki maeneo ya nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Mrina Shine iliyopo kata ya Levolosi Jijijini Arusha.


Kamanda Masejo amebainisha kuwa mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Polisi walifika eneo hilo na kuukuta mwili huo ambao waliutambua kuwa ni Mkaguzi wa Polisi Stewart Kaino (47) Askari Polisi wa wilaya ya Arumeru.


Aidha amesema kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira mazima ya kifo hicho.


Sambamba na hilo Kamanda Masejo ameelezea tukio jingine ambapo amesema  kuwa Tarehe 08.01.2023 huko katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha mtu mmoja aitwaye Nelson Mollel (33) mfanyabiashara, mkazi wa kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa.


ACP MASEJO amebainisha kuwa Uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa mtu huyo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa ni ndugu zake tarehe 03.01.2023 wakimtuhumu kumtukana mama yake mzazi (jina limehifadhiwa) na kumuibia.



Kamanda Masejo aliendelea kufafanua kuwa baada ya kupigwa, ndugu hao waliendelea kukaa na majeruhi bila kumpeleka hospitali hadi ilipofika tarehe 08.01.2023 alifikishwa hospitali akiwa mahututi na kufariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.


Amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo ambao walikimbia baada ya kuona hali ya marehemu kuwa mbaya.


Share:

DKT MABULA ATAKA WANA CCM KUTUMIA FURSA YA MIKUTANO YA HADHARA KUJIBU HOJA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa Scarf mara baada ya kuwasili ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza ilipofanyika sherehe ya kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januri 2023. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa tarehe 11 Januari 2023 mkoani Mwanza. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa Bi. Ellen Makungu Bogoje akizungumza kwenye sherehe za kuwakaribisha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023. Baadhi ya wana CCM waliojitokeza katika sherehe za kuwakaribisha wajumbe wa NEC Taifa ambao ni Dkt Angeline Mabula na Ellen Makungu Bogoje tarehe 11 Januari 2023. Vijana wa hamasa wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakifurahia wakati wa sherehe za kuwapokea wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM Taifa zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023. Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima akizungumza katika sherehe za kuwapokea wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM zilizofanyika ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tarehe 11 Januari 2023.

**************************

Na Mwandishi Maalum, MWANZA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanachama wa Chama cha Mapinduzi nchini kutumia fursa ya kuruhusiwa mikutano ya hadhara kama njia ya kujibu hoja kwa kuelezea mafanikio ya yaliyofanywa na chama hicho.

Dkt Mabula amesema hayo tarehe 11 Januari 2023 katika ofisi ya Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza wakati wa mapokezi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa waliochaguliwa hivi karibuni kwenye mkutano mkuu wa 10 wa CCM.

Amesema, wana CCM wasiangalie sasa ambapo mikutano imeruhusiwa na kuanza kubishana huku wakiacha kuangalia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuifanya kasuasua.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Chama cha Mapinduzi kinayo matawi, Mashina pamoja na Kamati zake zake za siasa katika ngazi zote na kinachotakiwa ni kurudi kwa wanachama na kuhamasisha maendeleo huku wakikagua utekelezaji wa ilani ya CCM.

‘’Lazima kwenda kila ngazi kwa kukagua na kuangalia kama ilani inatekelezwa lakini siyo kwa kunyanyasa watumishi, hoja ya msingi hatutakiwi kuzifanya hoja zinazokuja kama kero za kujibishana na kila changamoto itakoyokuja igeuzwe kama fursa ya kusonga mbele.

Aidha, alimsifu na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na kueleza kuwa kama kuna mtu ambaye watanzania watamkumbuka basi ni yeye kutokana na hekima na busara zake hasa kwa serikali yake ya awamu ya sita kuwa kiungo kizuri cha kuendeleza yale mazuri yote ya serikali ya awamu yaliyopita

‘’kikubwa anachokifanya kama mama ni hekima, busara na maamuzi yake ni furaha kwa watanzania suala la mariasdhiano lililofanyika ninachotaka kuwaomba wana ccm wenzangu maridhaino ni mchakato, hoja ya msingi hapa tusizifanya hoja zinazoibuliwa katika mikutano kama hoja za kubishana bali ziwe za kutoa majibu kwa yale yaliyofanyika’’ alisema Dkt Mabula

Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi Taifa alieleza kuwa, wanachotakiwa wana CCM kufanya ni kuisimamia serikali kwa kujibu hoja na kuangalia yale yote yaliyoelekezwa na chama kama yanafanyika kama ilivyopangwa.

Naye Mjumbe wa Halamshauri Kuu ya Taifa Bi. Elen Makungu Bogoje amesema Chama cha Mapinduzi kimeendelea kuisimamia serikali kila mahala na kusisitiza kuwa ipo haja kwa viongozi wa CCM katika kila ngazi kwenda kuisimamia serikali katika miradi yote iliyopo maeneo yao.

‘’Niwaombe viongozi wa CCM katika kila ngazi kwenda kuisimamia serikali ili wapinzani wakose hoja za kusema katika mikutano ya hadhara na kazi hii ya kuisimamia serikali tumeifanya na tunaendelea kuifanya’’. Alisema Ellen

Wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt Angeline Mabula ambaye ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Ellen Makungu Bogoje waliwasili kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Mwanza ambako ndiko wanakotokea tangu wachaguliwe kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM katika Mkutano Mkuu wa Cahama cha Mapinduzi uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni.
Share:

MWONGOZO WA KUDHIBITI VVU, UKIMWI NA MAGONJWA YASIOMBULIZWA WAHUISHWA KULINDA AFYA ZA WATUMISHI


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agness Meena akizungumza na Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu walioshiriki kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza mahali pa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya wadau kutoka katika Wizara mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agness Meena (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza mahali pa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.


Mratibu wa Kinga na Mwitikio wa kitaifa dhidi ya VVU, Dkt. Hafidh Ameir akitoa taarifa ya hali ya VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agness Meena (hayupo pichani) kufungua kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza mahali pa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Charles Kato akitoa neno la utangulizi kabla ya Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agness Meena kufungua kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza mahali pa kazi kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Anuai za Jamii na Mratibu wa VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Mwanaamani Mtoo akiwasilisha mada kuhusu Umuhimu wa Ujumuishwaji wa Anuai za Jamii mahali pa kazi wakati wa kikao kazi cha kujadili Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza kilichofanyika jijini Dodoma.

*******************************

Na. Veronica E. Mwafisi-Dodoma

Tarehe 11 Januari, 2023



Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Agness Meena amesema Serikali imehuisha Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Sugu Yasiyoambukiza (MSY) mahali pa kazi wa mwaka 2014 ili kulinda afya za watumishi wa umma, kuimarisha afya ya akili na kudhibiti msongo wa mawazo, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa watumishi katika kutoa huduma bora kwa wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.



Bi. Meena amesema hayo jijini Dodoma, wakati akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu cha kupitia na kuthibitisha rasimu ya Mwongozo wa Kudhibiti VVU, UKIMWI na Magonjwa Yasiyoambukiza (MYA) mahali pa kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.



Bi. Meena amewaasa wakurugenzi hao, kutumia kikao kazi hicho kujadili na kutoa michango itakayoboresha rasimu ya mwongozo huo uliohuishwa, ili kufikia malengo ya Serikali ya kuwa na watumishi wenye afya nzuri ya akili na mwili itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao kikamilifu.



“Nawasihi mpitie kwa makini mwongozo huu ili mtoe maoni yatakayokidhi mahitaji ya sasa na baadae katika kukabiliana na changamoto za kiafya ambazo watumishi wa umma wamekuwa wakikabiliana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao, changamoto ambazo zimekuwa zikikwamisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi,” Bi. Meena amesisitiza.



Bi. Meena ameongeza kuwa, mwongozo huo utasaidia Serikali kupunguza gharama za kuwahudumia watumishi wa umma wanaopata magonjwa yasiyoambukiza pamoja na kupunguza vifo vya watumishi wa umma ili kulinda nguvukazi ya taifa.



Kwa upande wake, Mratibu wa Kinga na Mwitikio wa kitaifa dhidi ya VVU, Dkt. Hafidh Ameir amesema, endapo elimu itaendelea kutolewa kwa watumishi wa umma watapata uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya VVU na UKIMWI na watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kujilinda dhidi ya maambuzi ya VVU ikiwa ni pamoja na kwa hiari yao kumueleza mwajiri kuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI na hatimaye kupatiwa huduma stahiki.



Dkt. Ameir amesema, bado kuna baadhi ya watu wanadhani mtu mwenye virusi vya UKIMWI anaweza kumuambukiza mtu mwingine kwa kupiga chafya, kuchangia vyombo na vifaa vya kazi hivyo kuna kazi ya ziada kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa kiasi kikubwa katika maeneo ya kazi.



Naye, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Uchambuzi Sera, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Charles Kato amesema, Mwaka 2014 ilionekana kuna umuhimu wa kujumuisha magonjwa sugu yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiendelea kuisumbua jamii wakiwemo watumishi wa umma ambayo ndio sababu pia iliyofanya Ofisi ya Rais-UTUMISHI kupitia Idara ya Uendelezaji Sera kukutana na Wakurugenzi wa Utumishi na Utawala ili kupitia na kuthibitisha rasimu hiyo ya Mwongozo wa VVU na Ukimwi.



Dkt. Kato amesema, utumishi wa umma unakabiliwa na changamoto ya uwepo wa magonjwa yasiombakuza ambayo yanaathiri utendaji kazi, hivyo Ofisi ya Rais-UTUMISHI kupitia Idara ya Uendelezaji Sera iliona kuna umuhimu wa kukutana na Wakurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu ili kupitia na kuthibitisha rasimu ya Mwongozo wa VVU na UKIMWI uliohuishwa ili uweze kuwa na tija na manufaa katika kulinda rasilimaliwatu Serikalini.



Kikao kazi hicho cha siku moja kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kupitia Idara ya Uendelezaji Sera kimehudhuriwa na Wakurugenzi wa Idara za Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara mbalimbali.

Share:

Tuesday, 10 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 11,2023

























Share:

NAIBU WAZIRI KASEKENYA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI MAGOMENI

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya (kulia mwenye miwani) akiwa pamoja na watumishi wa Wakala wa majengo (TBA) akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro (kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro (kushoto) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, Arch.Bernard Mayemba akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, Arch.Bernard Mayemba akimueleza jambo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 10,2023 Jijini Dar es Salaam mara baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***************

SERIKALI Imeeleza kuwa itaendelea kushirikiana na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) katika Sera pamoja na kuingia mikataba na taasisi za kifedha ili kuwapa nguvu kutokana na kazi bora wanayoifanya ya kuwasaidia watanzania katika kubuni, kusimamia na kujenga majengo mbalimbali ya makazi na biashara.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi ' Magomeni Kota Phase 2 A' uliokamilika kwa asilimia 96 Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi. Godfrey Kasekenya amesema mradi huo wa kisasa utaanza matumizi yake kufikia mwezi ujao.

"Mradi huo wa kisasa una ghorofa nane utabeba Kaya kumi na sita kwa kaya mbili kila ghorofa ambazo zina huduma zote muhimu umebuniwa na kutekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) ambayo Serikali imeiamini zaidi katika kujenga majengo kwa ajili ya makazi na biashara". Amesema

Kuhusiana na uhitaji wa nyumba hizo za makazi Kasekenya amesema, hadi sasa watumishi wengi wamejitokeza kuomba kupanga nyumba hizo hali inayoashiria uhitaji mkubwa wa majengo ya makazi kwa watumishi na wasio watumishi na kuiagiza TBA kushirikiana na taasisi binafsi katika kupunguza changamoto hiyo na Serikali itashirikiana nao hususani katika Sera na kuingia mikataba na taasisi za kifedha.

"Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa tayari na mstari wa mbele katika kuanzisha na kuendeleza miradi ambayo anaamini itawasaidia wananchi wakiwemo watumishi... Serikali imejipanga katika hili na Wizara hatujakwama fedha zinakuja na miradi inatekelezwa." Amesema Kasekenya.

Aidha, ameeleza kuwa mradi huo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi Bilioni 5.6 na majengo mengine matano yanajengwa katika eneo hilo kwa ajili ya watumishi ambapo wa ujumla Kaya 80 zitaishi katika eneo hilo huku mradi unaotekelezwa katika eneo la Temeke Mwisho ukitegemewa kubeba Kaya 148.

Pia ameitaka TBA kupitia watendaji wake kuwa waadilifu kwa kujenga majengo yenye thamani ya fedha inayotolewa na Serikali na kutotumia fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo vinginevyo.

"Ikiwezekana endeleeni kutumia vifaa vya ujenzi vya hapa Tanzania, wataalam tuwe wabunifu wa vifaa vya ujenzi bila kutegemea kuagiza kutoka nje... Na watakaopata nafasi ya kuishi katika nyumba hizi watunze mazingira haya ili kupunguza gharama ya kuyatengeneza mara kwa mara." Amesema.

Vilevile amesema mradi huo unategemewa sana na wananchi wakiwemo watumishi ambao wanahitaji makazi bora na salama ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na TBA wamekuwa wakipunguza changamoto hiyo ya makazi kwa kutekeleza miradi hiyo kwa ubunufu na usasa zaidi.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro amesema uhitaji wa nyumba za makazi kwa wananchi wakiwemo watumishi bado ni changamoto na Wakala hiyo inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa nyumba za makazi na biashara kupitia fedha za ruzuku.

Arch. Kondoro amesema, TBA inazingatia matumizi fedha kwa kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika ipasavyo kwa kuzingatia thamani na wanazingatia muda wa utekelezaji kwa kukamilisha mapema na kwa ubora wa hali ya juu.

Kuhusiana na gharama za nyumba hizo Arch. Kondoro amesema, Serikali imetoa mwongozo wa kodi kwa ajili ya watumishi wa Umma ni theluthi mbili ya soko (kodi zinazotozwa mtaani.)

Awali msimamizi wa mradi huo Arch. Benard Mayemba amesema miradi ya Magomeni Kota Phase 2A na kuendelea na mradi wa Temeke Mwisho inatekelezwa kwa fedha za ruzuku na gharama za ujenzi katika eneo la Temeke Mwisho utagharimu Bilioni 17 hadi 19 na utachukuwa Kaya 148 na inategemewa kujengewa majengo 7 zaidi yatakayobeba Kaya 1000.
Share:

ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMTISHIA KUMUUA MTOTO WAKE WA KUZAA MWENYEWE



Na Walter Mguluchuma -Katavi .

Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Agustino Mikese Mkazi wa Kijiji cha Isinde Kata ya Mtapenda Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumbaka na kumtishia kumuua mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa).

Mtuhumiwa huyo amekamatwa Januari 6,2023 baada ya mtoto huyo kuona vitendo hivyo vya kubakwa na baba yake kuwa vimemzidia .

Mtoto huyo baada ya kuona baba yake amekuwa akimfanyia vitendo hivyo vya kikatili mara kwa mara na kumtishia kumuua aliamua kwenda kutoaa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji cha Isinde .

Baada ya tukio hilo kufikishwa katika uongozi wa Serikali ya Kijiji ndipo walipotoa taarifa kwa Jeshi la Polisi.

Polisi baada ya kuwa wamepokea taarifa hizo walianza kufuatilia na ndipo hapo Januari 6 mwaka huu walipomkamata mtuhumiwa huyo akiwa kijijini hapo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Isinde Hamis Rashid Mbogo amesema kuwa kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa ndugu wa mtuhumiwa huyo walikuwa wameshasikia tuhuma za ndugu yao kuwa na tabia ya kumfanyia ukatili huo mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.

Amesema mtoto huyo alikuwa akiishi nyumbani kwao akiwa na wazazi wake wote wawili ambapo mama yake mzazi kwa sasa ni mjamzito.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amesema kuwa mtuhumiwa huyo bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tuhuma hizo.

Amesema wamefanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo kwa kumfanyia mtoto huyo vipimo vya kidaktari.

Kamanda Makame ameeleza kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote ili akajibu tuhuma zinazomkabili .


Share:

PROF. NDALICHAKO ATAKA SERA YA VIJANA 2023 IENDANE NA MAHITAJI YA SASA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika leo Januari 10,2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof.Jamal Katundu,,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika leo Januari 10,2023 jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako,wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo lililofanyika leo Januari 10,2023 jijini Dodoma.

.........................

Na Mwandishi Wetu, DODOMA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Prof.Joyce Ndalichako, amelitaka Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kutoa maoni yanayoendana na mahitaji ya sasa kwenye Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2023. Prof.Ndalichako ametoa kauli hiyo leo Januari 10, 2023 alipokuwa akifungua mkutano wa Baraza hilo jijini Dodoma ambao pamoja na mambo mengine unajadili na kutoa maoni kuhusu sera hiyo. Amesema vijana ndiyo nguzo ya maendeleo ya taifa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine jukumu lake kubwa ni kusimamia masuala ya vijana nchini. “Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2021 inaonesha kuwa kundi la vijana kati ya miaka 15 hadi 35 linajumuisha watu wapatao Milioni 20.73 sawa na asilimia 34.9 ya watu wote. Hili ni kundi muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu, vijana wanapaswa kujengewa misingi ya kulinda amani, umoja na kuendeleza mshikamano katika taifa letu,”amesema.

Aidha, amesema maandalizi ya kuandaa Sera ya Maendeleo ya Vijana bado yanaendelea na hatua kadhaa zimeshakamilika ikiwa pamoja na kufanya tathmini ya Sera ya mwaka 2007, kuandaa rasimu ya Sera ya Mwaka 2023,kuandaa rasimu ya mkakati wa utekelezaji na kupata maoni ya Menejimenti na Wakurugenzi wa sera na mipango wa Wizara.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya teknolojia na utandawazi, Prof.Ndalichako amesema mfumo wa maisha duniani umebadilika sana ikiwemo makuzi na tabia ya vijana.

“Tuangalie ni kwa namna gani vijana wetu watanufaika na fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia.Ni namna gani wanaweza kutumia maendeleo ya Teknolojia ya habari na mawasiliano kama fursa ya kuwapatia ajira na kipato,”amesema.

Awali, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Prof.Jamal Katundu, amemhakikishia Waziri Ndalichako kuwa sera hiyo itakamilika ili itumike kwa maendeleo ya vijana nchini.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger