Sunday, 8 January 2023

HAPPY BIRTHDAY CEO WA MALUNDE 1 BLOG



Leo Januari 8 ni Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Mkurugenzi na Mmiliki wa Mtandao wa Malunde 1 blog (www.malunde.com), ndugu Kadama Malunde mkazi wa Shinyanga Tanzania. Happy Birthday!!
Share:

KAMATI YA UTATUZI WA MIGOGORO VIJIJI NA MITAA 975 NCHINI YAHITIMISHA KAZI DAR ES SALAAM.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendelo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam. Waziri wa TAMISEMI Angela Kairuki akiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam. Sehemu ya viongozi wa Wizara na wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini maamuzi ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendelo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula katikati, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amosi Makala kushoto na Waziri Kairuki kulia wakiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu zoezi la utatuzi wa migogoro ya ardhi ya Mitaa na Vijiji 975 zoezi ambalo limehitimishwa leo Mkoani Dar es Salaam.

Picha na Anthony Ishengoma

****************************

Na Anthony Ishengoma.

Kamati ya Mawaziri nane ya kutatua migogoro ya ardhi kati ya Vijiji na Mitaa 975 imehitimisha kazi yake katika Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kamati hiyo na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kukutana jana Mkoani Dar es Salaam na kukubaliana kuwa wananchi wa kata ya Zingiziwa sasa ni wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Awali akiongea na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema kuwa kumekuwepo na migogoro ya mipaka kati ya baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam na Pwani jambo ambalo limekuwa likizua taharuki kwa wananchi wa maeneo hayo ikiwemo suala zima la huduma za msingi ambazo zimekuwa zikitolewa katika mikoa yote miwili.

Waziri Mabula akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kuhitimisha mkutano huo alibainisha kuwa baada ya zoezi hilo kuhitimishwa Mkoani Dar es Salaam maeneo mengine ambayo Rais wa Tanzania ameridhia yachukuliwe au yagaiwe kwa wananchi zoezi la kuyatambua na kuyawekea mipaka linaendelea katika maeneo hayo.

Aidha Dkt. Angeline Mabula aliongeza kuwa zoezi la utambuzi wa maeneo hayo litajulikana mpaka ifikapo mwezi Machi mwaka huu na kwa yale maeneo ambayo yatakuwa bado yana mkanganyiko wa mipaka Waziri mwenye dhamana atayapitia na kuyatolea majibu baada ya masuala ya kiutaalam kuwa yamefanyiwa kazi.

Waziri Mabula aliongeza kuwa kamati yake imebaini kuwa kuna sababu tatu zilizochangia Migogoro ya ardhi hiyo kuwepo mojawapo likiwa la wananchi kutotii sheria kuvamia maeneo ambayo hayaruhusiwi kuingia akiyataja maeneo ya ifadhi pamoja na maeneo ambayo yanamilikiwa na Taasisi mbalimbali ambazo zimeshindwa kulinda maeneo yake na hatimaye kuvamiwa wananchi na kujimilikisha kama vile ni mali yao.

Mbali na uvamizi wa ardhi Waziri Mabula alibainisha kuwa kuna baadhi ya maeneo baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia ardhi kinyume na sheria za kutunza mazingira ikiwemo kutofanya kilimo ndani ya mita sitini ya vyanzo vya maji hivyo watu kuendeleza kilimo katika kingo za mito na maziwa akibainisha kuwa wananchi wanafahamu kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu zilizopo.

Waziri Mabula aliongeza kuwa kamati yake imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa vyanzo maji nakuongeza kuwa kila Waziri mwenye dhamana alikuwa akiongea na wananchi kuhusiana na eneo lake na Rais ameridhia maeneo ya ifadhi ambazo zimekosa sifa kugaiwa kwa wananchi kwa utaratibu maalum uliotolewa na serikali.

Waziri wa TAMISEMI Bi. Angela Kairuki alihitimisha majadiliano kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kwa kutumia mamlaka aliyonayo kama Waziri mwenye dhamana kwa kuamua wananchi wa Zingiziwa kubakia Mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka viongozi wa Dar es Salaam kujipanga ili kuwatangazia wananchi wa Zingiziwa kwamba ni wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri huyo wa TAMISEMI aliwaagiza wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani Kwenda mapema kwa wananchi wa Zingiziwa ili kuwatangazia tamko la serikali wakati taratibu nyingine zikifuata zikiwemo taratibu za kitafsiri tamko la kiserikali kuhusu mipaka ili kuondoa mgogoro uliopo kiutawala.

Waziri Kairuki alibainisha kuwa maamuzi yake yamezingatia busara ikiwemo huduma za elimu, na masuala mengine kama vile huduma za sensa, usalama, utaratibu wa uandikishaji anwani za makazi lakini pia uzoefu wa maeneo ambaya awali yalikuwa na migogoro kama hii ya kiutawala.

Wizara vya Ardhi kwa kushiruikiana na Wizara za kisekta kwa muda sasa wamekuwa katika zoezi la utatuzi wa Migogoro ya Ardhi hususani kwa wananchi ambao wamekiuka taratibu za matumizi ya ardhi au kumiliki ardhi bila kuzingatia sheria na sasa kamati hiyo imehitimisha zoezi hili katika Mkoani Dar es Salaam.
Share:

Saturday, 7 January 2023

MINZA MAYENGA; MAMA ALIYEKATWA MAPANGA NA MUMEWE KISA NG’OMBE NA MASHAMBA


Minza Mayenga (47) mkazi wa Mkoa wa Simiyu ambaye ni mama wa watoto tisa aliyekatwa mapanga na mme wake sehemu za kichwa na mkono Novemba 30,2022 akiwa katika hospitali ya wilaya mji wa Bariadi Somanda.

Na Mwamvita Issa 

Kwa siku za hivi karibuni wanandoa wamekuwa ni wahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili kwa vazi wanaloliita uvumilivu ili kulinda heshima ya ndoa katika jamii.


Pamoja na mikakati mbalimbali iliyowekwa na serikali ili kukabiliana na vitendo vya ukatili, bado wanawake wamekuwa na mwitikio mdogo katika kutoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa ikilinganishwa na taarifa zinazotolewa juu ya wanawake na watoto.


Imekuwa ni nadra kwa wanawake kutoa taarifa za vitendo vya ukatili ambavyo wamekuwa wakifanyiwa kwa kujali kulinda mahusiano na kuogopa mtazamo hasi wa jamii baada ya kutoa taarifa hizo.


Katika taarifa ya haki za binadamu kwa mwaka 2021 iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) mwezi Mei mwaka 2022 ilionesha matukio ya ukatili dhidi ya wanawake yalifikia 23, 685 kwa mwezi, ambapo mikoa inayotajwa kuongoza ni pamoja na Arusha, Manyara, Lindi, Tanga na Mkoa wa Kipolisi Temeke.


Baadhi ya sababu zinazochochea kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake zimetajwa kuwa ni pamoja na kuendelea kushikiliwa kwa mila na desturi zilizopitwa na wakati,elimu duni na mfumo dume wanawake kutomiliki mali katika familia.


Licha ya serikali na wadau wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kutoa elimu hadi vijijini lakini hali bado vitendo hivyo vinaendelea kutokea,kama anavyosimulia Minza Mayenga (47) mkazi wa Mkoa wa Simiyu ambaye ni mama wa watoto tisa aliyekatwa mapanga na mme wake sehemu za kichwa na mkono Novemba 30,2022.


Anasema tukio hilo lilitokea siku mbili baada ya amri ya mwisho ya mahakama juu ya shauri la ndoa namba 112/2022 lilitotolewa na mahakama ya Mwanzo ya Bariadi kituo cha Mhango mkoani Simiyu ikiamuru kupewa stahiki alizokuwa anadai kwa mumewe ili kujikimu pamoja na wanae.


Alikuwa akidai ng’ombe wanne kati ya 11 waliopatikana baada ya kuozesha binti yao pamoja na ekari 8 kati ya 20 walizokuwa wanamiliki.


Minza anasimulia chanzo cha ugomvi kuwa ni baada ya binti yake mkubwa kumjengea nyumba ya kuishi kipindi ambacho mme wake alimuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine.


Anasimulia kuwa, ugumu wa maisha na kukosa matunzo vilimfanya kuhamia kijiji cha Katoryo Kata ya Tegeruka wilaya ya Musoma Mkoani Mara ili kukabiliana na umasikini aliokuwa nao alipokuwa akiishi kijiji cha Ngulyati walayani Bariadi mkoa wa Simiyu.


“Tulivyohamia huko alifika na kunitelekeza nikaanza kuishi nikisaidiwa na kaka zangu hadi binti yangu mkubwa alipokuja na kunijengea nyumba, baada ya miaka mitatu alirudi na alipokuta ile nyumba ugomvi ukaanzia hapo,”anasimulia akiwa na maumivu makali.


“Alikuwa hataki niishi kwenye ile nyumba alikuwa ananipiga na kunitishia kunichoma kisu, baada ya mateso kuzidi ilibidi nihame mimi na watoto tukajenga kijumba kidogo pembeni ya makazi ya kaka yangu na yeye akabaki nyumba kubwa”,anaeleza.


Baada ya muda kidogo kupita mume wake aliuza nyumba ile pamoja na magunia 60 ya mpunga ambayo Minza alilima kwa ajili ya chakula wakati ambao mme wake hakuwepo.


“Maisha yalikuwa magumu sina makazi sina chakula na ninawatoto ilibidi nisafiri hadi Ngulyati kwenda kumuomba anipe ng’ombe wawili wa kulimia na ekari 4 za shamba nipate sehemu ya kulima”,anaeleza.


Anasema mume wake alikataa kumpa kitu chochote ndipo alipofungua kesi katika mahakama ya Mwanzo,kesi ambayo alishinda na hukumu ikatolewa kuwa apewe alichokuwa anakihitaji.


“Baada ya hukumu hakunipa chochote nikawa bado nipo Ngulyati kwa dada yangu ndipo siku moja jioni alinivizia na kunikata mapanga,ninadhani lengo lake lilikuwa ni kuniua kwa sababu nilipoteza fahamu lakini bado aliendelea kunikata hadi watu walipomkamata”,anasimulia Minza.


Minza yupo katika hospitali ya wilaya mji wa Bariadi Somanda, akiendelea kupatiwa matibabu huku sura yake ikiwa imeshonwa na nyuzi nyingi ambazo ni ngumu kuzihesabu, mme wake Buluba Nkalango anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Simiyu.


Wakati vitendo vya ukatili wa kijinsia vinazidi kuongezeka nchini Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na makundi maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Januari 22, 2022 akiwa katika hafla ya uzinduzi wa dawati la jinsia katika Taasisi za elimu ya juu na Kati,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alitaja jitihada sita ambazo Wizara yake imeanzisha ili kupambana na hali hiyo.



Anasema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA),ambapo jitihada hizo zimewezesha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaotoa taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia kwa vyombo husika na kwa kipindi cha mwaka 2020/21 jumla ya matukio 20,025 ya ukatili yaliripotiwa ikilinganishwa na matukio 18,270 yaliyoripotiwa kwa mwaka 2019/20.


Waziri Gwajima alisema baadhi ya wanawake wameendelea kuwa waathirika wa vitendo vya ukatili kwa kuendelea kuamini kuwa ni wajibu wao kuendelea kuwa katika ndoa hata kama wanakumbana na mateso na manyanyaso pia kuogopa maneno ya watu katika jamii pale wanapoondoka kwenye ndoa.


Emmanuel Martine ni mdau wa kupinga ukatili kwa wanawake na watoto kutoka katika shirika lisilo la kiserikali la World Vision linaendesha mradi wa maendeleo katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu anasema imekuwa ni kichaka cha wanaume kuwatendea maovu kwa sababu katika jamii hiyo inaamini mwanamke anayeachika kwenye ndoa anakuwa hana maadili.


“Kuna haja ya wadau kutafuta namna na njia mbalimbali za kuwaelimisha wanawake pamoja na wanamme ambao wamekuwa wakifanya ukatili huo ili kila mmoja awe ni mlinzi wa mwenzake”,anasema.


Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Ushirika wa Tumaini Bariadi Prosper Shayo anasema ni wajibu wa jamii kuangalia ni vitu gani vinapunguza upendo baina yao hali inayochochea migogoro na ukatili uliopitiliza.


“Ningeomba jamii kujifunza mambo matatu ambayo ni upendo uvumilivu na uaminifu, tuwafundishe upendo ili kila mmoja akipenda mwenzake hatutaona ukatili huu unaoendelea,” anasema mchungaji Shayo.

Share:

WADAU SMZ NA SMT WAJADILI ANDIKO LA MAPENDEKEZO YA SHERIA YA UTAFUTAJI NA UOKOAJI


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Zanzibar, Ndg. Shomari Omar Shomari (katikati), akizungumza na wadau wa usafiri kwa njia ya anga na maji kutoka SMZ na SMT wakati wa kujadili mapendekezo ya andiko la sheria ya Utafutaji na Uokoaji katika ukumbi wa ZURA, Zanzibar.

Dkt. Devotha Mandanda, Mwanasheria kutoka TASAC akifanya wasilisho la mapendekezo ya andiko la Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Ndg. Shomari Omar Shomari (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pampja na baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao cha kujadili andiko la mapendekezo ya Sheria ya Utafutaji na Uokoaji. 

Na: Mwandishi wetu, ZANZIBAR 

Wadau mbalimbali wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji na anga wamekutaka kwa siku mbili kujadili kuhusu andiko la mapendekezo ya sheria ya utafutaji na uokoaji katika ukumbi wa ZURA uliopo Zanzibar tarehe 5 na 6 Januari, 2023.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wakati wa kikao hicho Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Usafirishaji na Mawasiliano Zanzibar Ndg. Shomari Omar Shomari amesema sheria hiyo ni mihimu kwa pande zote mbili kwani usafiri wa anga  na majini umeongezeka kwa kasi kikubwa  hivyo ni wakati muwafaka kukamilisha sheria ya utafutaji na uokoaji.

“Kutokana na majanga yanayotokea majini na angani basi hivyo matoke yanayotokea ni muongozo mzuri wa kufanya na kufuatia miongozo hiyo ya utafutaji wa anga na kubainika kuwepo na changamoto katika anga na bagarini" alisema Bw.Shomari.

Aliongeza kuwa anatambua juhudi za Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi kupitia katibu Mkuu kwa utamaduni wake wa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na kuwezesha kufanyika kikao hiki muhimu Zanzibar ili kupata maoni ya pande zote mbili.

“Tunafahamu changamoto kwa sheria kama hizi zinazohusu Muungano kupata maoni mpaka kukamilisha utaratibu wa kutunga sheria, jambo hili alilolifanya ni muhimu sana pia inaonyesha ushirikiano wetu ulivyozidi kuimarika, aliongeza" Bw. Shomari.

Pia alisema mbali na kuwa kumekuwa utungaji wa sheria hii unafuatia makubaliano na maelekezo yaliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Majini (IMO), hivyo kuwataka washiriki kuhakikisha sheria hiyo inasimamia masuala ya utafutaji na uokoaji kwa kuzingatia miongozo ya kimataifa.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti kutoka Wizara ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi - Zanzibar, Bw. Makame Machano Haji amesema ni vyema kuwe na mfumo rasmi wa kisheria utakao toa nguvu kwa pande zote mbili kushirikiana kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pindi kunapotokea janga katika anga au majini.

“Suala hili linahitaji rasilimali fedha, watu na vifaa, nguvu ya upande mmjoja haiwezi kufamikisha kutatua tatizo hili hivyo tukiungana pamoja tunaweza kutatua tatizo kwa pamoja" alisema Bw. Machano.

Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Bw. Maseke Mabiki amesema jambo la muhimu ni wadau kuwa wazi kuelezea changamoto ili kuweza kuwa na sheria itakayosaidia pande zote mbili.

Wadau mbalimbali wa Sekta ya usafiri kwa njia ya anga na maji kutoka Serikali ya Muungano Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambao ni Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi – Zanzibar, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA) pamoja na Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar (KMKM) wamekutana kujadili andiko la Mapendekezo ya Sheria ya Utafutaji na Uokoaji.

Share:

HISTORIA YA MANJU MADEBE JINASA...."NILIWAHI KUFA"

Mwandishi Nguli /Mwandamizi Shija Felician amekutana na Manju Madebe kutoka Nzega Tabora ambaye ameelezea Historia yake... Manju huyu maarufu anasema Aliwahi Kufa, pia alikuwa analima na kuvuna muda huo na alikuwa anaita nyuki na kulina asali.. Fuatilia hapa maajabu ya Msukuma huyu
Share:

RAID YAKUBALI MWALIKO WA MUDA MREFU WA KUTEMBELEA MGODI WA NORTH MARA

Share:

CCM SHINYANGA WAJIPANGA MIKUTANO YA HADHARA..."HII PIN ILITUATHIRI PIA... SASA VYAMA RAFIKI VIKASEME UKWELI VISIFUNIKE MIWANI YA MBAO"

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga kimempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya kwa Watanzania ikiwemo kupanua wigo wa Demokrasia Diplomasia huku kiviomba vyama vya Upinzani nchini kusema ukweli kuhusu maendeleo yaliyofanywa na serikali.


Pongezi hizo z imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mabala Kashindye Mlolwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Januari 7,2023 katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga.

“Tunampongeza sana Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anazozifanya kwa Watanzania hasa kwenye suala la Demokrasia na Diplomasia kwa ujumla, hivi karibuni ametoa tamko la kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vyote vya siasa ikiwa ni moja ya tunda la maridhiano, jambo ambalo litaleta chachu ya Demokrasia na Ushindani wa kisiasa kwa hoja katika nchi yetu”.

"CCM Mkoa wa Shinyanga tunampongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupanua wigo wa Demokrasia Tanzania, ameruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya upinzani (Vyama Rafiki). Mikutano hii ya hadhara italeta chachu, twendeni tukashindane kwa hoja, sisi tumejipanga kwa mikutano, Moto umeshawashwa tutawapa ratiba ya mikutano, sisi tumejipambanua kwa Ilani yetu, hatuna Presha".

"Siasa siyo uadui, siasa ni kujenga amani ya nchi. Vyama vya siasa vikifika kwenye maeneo waseme tu ukweli wa mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali. Vyama Rafiki wakiri ukweli wa mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali visifunike miwani ya mbao kwenye ukweli, waseme tu ukweli mambo makubwa yamefanyika", amesema Mlolwa.


"Hili la vyama vya siasa visifanye mikutano kwamba tulikuwa na hofu gani, hata sisi CCM lilituathiri na CCM. Hii Pin ya kutofanya mikutano ilituhusu pia, sasa tupo tayari kwenda kufanya mikutano ya hadhara na hili ni agizo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kilichobaki sasa ni utekelezaji tu Sisi tuna Ilani ya Uchaguzi ya CCM tunayoisimamia kazi yetu ni kutekeleza tu", ameongeza Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Shinyanga.


Ameeleza kuwa, mbali na kupanua wigo wa Demokrasia, Pia Rais Samia amefanya mambo makubwa kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisas itakayonufaisha pia wakazi wa Shinyanga na mambo kadha wa kadha.

“Tunampongeza Mhe. Rais Samia kwa mvua ya maendeleo mkoa wa Shinyanga. Mama Samia ni kiongozi na Rais wa mfano, ni mama mwenye huruma mwenye upendo mkubwa kwa Watanzania, amejenga shule za watoto wa kike waweze kusoma hata waliopewa ujauzito na kujifungua, ameleta tumaini kwa watoto wa kike Tanzania”,amesema.


“Miradi yote ya kimkakati inaendelea kwa kiwango cha hali ya juu. Pia tunampongeza Mhe. Rais Samia kwa miradi inayoendelea kujengwa nchi nzima. Hivi karibuni tumeona ujazaji wa maji katika bwawa la kufua umeme la Mwl. Nyerere huko Rufiji. Pia tumeshuhudia ujenzi wa madarasa mbalimbali kwenye maeneo yenye uhitaji nchi nzima, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya,ujenzi wa barabara za rami,kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita, kujali maslahi ya watumishi wa umma na mengine mengi”,ameongeza Mabala.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 7,2023












































Share:

Friday, 6 January 2023

Video Mpya : BUGANGA - KAMA MBWA

 

Share:

WAHUNI WASHIRIKIANA NA WANAFUNZI KUVUTA BANGI SHINYANGA MJINI

Mfano mwanafunzi akivuta bangi
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Najulwa akizungumza kwenye kikao cha mtaa huo

Na Suzy Luhende, Shinyanga Press Club Blog

Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Solomon Najulwa amewataka wanafunzi wote wa mtaa wa Dome waliofaulu kuingia kidato cha kwanza kujiepusha na uvutaji wa bangi na madawa mengine ya kulevya kwa sababu yanavuruga ufahamu wa akili.

Hayo ameyasema Januari 5,2023 kwenye kikao cha kuwajengea uwezo wazazi na watoto wanaoingia kidato cha kwanza na wanaoanza chekechea kilichofanyia ofisini kwake kikiwahusisha wazazi wenye watoto hao, ambapo amewataka watoto kujiepusha na uvutaji wa bangi na utumiaji wa madawa mengine ya kulevya.

Najulwa amesema kuna vijana wengi wamemaliza darasa la saba wamejiingiza kwenye makundi mabaya ya uvutaji bangi, hivyo si vyema kujiingiza kwenye makundi hayo kwani yanaharibu tabia njema.

"Nawaombeni sana watoto wangu msijichanganye na makundi mabaya ya uvutaji bangi na madawa ya kulevya kwani yanaathiri nguvu kazi ya Taifa letu, mnatakiwa kusoma kwa bidii ili kwa baadae tujenge Taifa lenye umoja na lenye uelewa na nyinyi ndiyo mtakuwa sadaka nzuri kwa Taifa na kupata viongozi wazuri kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu,"amesema Najulwa.

"Pia nawaomba wazazi msiwaruhusu kulala kwa muda wanaotaka wao wenyewe lazima wapate muda mzuri wa kujisomea masomo ya kujikumbusha, aidha wazazi tusiwatume kupita kiasi watoto wetu na kukosa muda wa kujisomea,"amesema Najulwa.

"Baadhi ya watoto wetu wamekuwa wakijifungia ndani na simu kubwa wanajifunza mambo yasiyofaa na wanachati yasiyowafaa na wanaangalia mambo mabaya yasiyowahusu hayo yanapeperusha elimu yenu acheni kabisa, pia wazazi naomba muwe na ushirikiano na walimu toeni mchango wa chakula ili watoto waweze kupikiwa chakula kizuri na waweze kuwasilikiza walimu wanachokifundisha," ameongeza.

Mwalimu mkuu wa shule ya Bugoyi A Alex Juma amesema vijana wengi waliomaliza darasa la saba wanavuta bangi na wanavuta sana hadi wanaanguka na wanarudi shuleni hapo kuvutia, hivyo wazazi wanatakiwa kukaa karibu na watoto hao ili kuweza kuwabadilisha.


"Ni jambo la kusikitisha sana pale tunapoona mtoto mdogo namna hii akivuta bangi na hawaogopi hata mchana kweupe wanakuja hapo Bugoyi na wengine wamemaliza shule ya msingi mwaka jana tu nawaomba wazazi tuwasaidie watoto hawa hata wanapotoka nyumbani tuwafuatilie wameelekea wapi,"amesema Mwalimu Juma.


Mwalimu mkuu wa shule ya Bugoyi B Elisiana Mlangeni amesema watoto hao wamekuwa ni shida  katika eneo la Bugoyi, kwani wanakaa pale karibu na jiko wanaanza kuvuta bangi. "Siku moja walifukuzana na polisi lakini wanaendelea kuja tu imekuwa ni kero kubwa sana".


" Najiuliza hili ni kosa la wazazi au la mwanafunzi, naomba wazazi mfuatilie watoto hawa kwani tunajenga kizazi kibaya hawa watoto wakiendelea hivyo watakuja kuvunja maduka ya watu watakuwa wezi, wasaidieni mapema zungumzeni nao walekezeni watabadilika,"amesema Mlangeni.

Kwa upande wake mgeni rasmi wa kikao hicho mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mazinge James Msimba ambaye alikuja kwa niaba ya mratibu elimu kata amesema ugumu wa maisha kwa wazazi sio kipimo cha kushindwa kulea watoto, kwani watoto wengi wamejikuta wakiwa katika mazingira mabaya kwa sababu wazazi wamewaacha na kuwa busy na maisha.

"Watoto hawa wanaosemekana wanavuta bangi wengi wao wanakuja shuleni kwangu Mazinge, hivyo wakileta mambo ya bangi shuleni kwangu nawafukuza, hivyo kabla hawajaja wazazi kaeni nao wakija huko waje wamebadilika wakiwa na maadili mema waje wapate haki yao ya elimu,"amesema mwalimu.

Baadhi ya wazazi Joseph Malale na Rea Enosi wamesema wanashukuru kukumbushwa, hivyo wameahidi kufuatilia watoto wao na kuwaelekeza, pia wameahidi kushirikiana na walimu ili kujua maendeleo ya watoto wao shuleni, lakini pia wamewaomba walimu pale watoto wao wanapoonekana wanakosea shuleni waonywe ili wasiendelee kufanya makosa.

Naye kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi ameahidi kulifuatilia suala la watoto wanaovuta bangi wiki ijayo ataanza msako ili kuhakikisha anawakamata watoto hao na wale wanaosababisha kuvuta bangi watakamatwa.
Wakazi wa mtaa wa Dome wakimsikiliza mwenyekiti akizungumza na kuwaasa wanafunzi waache kuvuta bangi
Wazazi na wanafunzi wakimsikiliza mwenyekiti wa mtaa wa Dome akiwataka washirikiane na walimu

mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mazinge James Msimba akizungumza kwenye kikao cha mtaa wa Dome cha kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza
Mwalimu mkuu wa shule ya Bugoyi (A) Alex Juma akizugumza kwenye kikao cha mtaa wa Dome
Mwalimu mkuu wa shule ya Bugoyi B Elisiana Mlangeni akiwaasa wanafunzi kutojiingiza kwenye makundi yasiyofaa

Wanafunzi wakiapa watasoma kwa bidii hawatajiingiza kwenye makundi yasiyofaa

Wanafunzi wakiapa watasoma kwa bidii hawatajiingiza kwenye makundi yasiyofaa

Share:

AJALI YA BASI LA LORI YAUA WATU 16


Takriban watu 16 wamepoteza maisha wakati basi la abiria lilipogonga lori moja Ijumaa asubuhi kwenye barabara kuu ya Uganda inayounganisha mji mkuu, Kampala, na mji wa kaskazini wa Gulu.

Polisi wanasema watu 12 walifariki papo hapo huku wengine wanne wakifariki baadaye hospitalini. Wasafiri wengine kadhaa kwenye basi hilo walijeruhiwa.

Lori hilo lilisemekana kuegeshwa na kupakia mizigo takriban kilomita moja kutoka Kamdini Corner - kituo maarufu cha kusimama na ukaguzi kaskazini mwa nchi.

Kumekuwa na viwango vya kutisha vya ajali za barabarani nchini katika wiki za hivi karibuni na haswa katika msimu wa sikukuu.

Ripoti ya polisi wa trafiki mapema wiki hii ilifichua kuwa ajali 104 za barabarani zilirekodiwa kati ya 30 Desemba na 1 Januari.

Takriban watu 35 waliuawa katika ajali hizi za barabara pekee.

Ajali za barabarani zimekuwa janga la muda mrefu nchini. Polisi wa trafiki walisajili zaidi ya ajali 4,000 kote nchini Uganda mnamo 2021, nyingi zikiwa mbaya.

Chanzo - BBC SWAHILI


Share:

IGP WAMBURA AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa mitatu.


Kupitia taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 06, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, IGP Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

IGP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Aidha amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.
Share:

BABA AJIUA BAADA YA KUUA MKE, MAMA MKWE NA WATOTO WATANO


Michael Haight mwenye umri wa miaka 42 nchini Marekani amemuua mke wake, mama mkwe na watoto wake 5 na yeye kujiua baada ya mke wake kuwasilisha ombi la talaka jambo ambalo yeye hakulitaka.

Tukio hilo limetokea katika jimbo la Utah nchini Marekani ambapo miili ya watu hao imepatikana ndani ya nyumba ya mashambani katika Jiji la Enoch wakati wa ukaguzi katika boma lao.

Waliofariki ni mke wake Tausha mwenye umri wa miaka 40, mama mkwe wake Gail Earl mwenye umri wa miaka 78 na watoto wake watano pamoja na mhusika huyo Michael Haight.

Polisi wamesema chanzo cha mauaji hayo ni mwaume huyo kutofurahishwa na ombi la talaka lililowasilishwa na mke wake tarehe Desemba 21/2022.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger