Friday, 19 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 20,2022










Share:

MALIMA AKUBALI KUWA MLEZI WA MWANZA PRESS CLUB

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amekubali kuwa mlezi wa chama Cha Waandishi Wa Habari Mkoa Mwanza na kuahidi kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo.


Malima amekubali kuwa mlezi Klabu hiyo baada ya kuombwa na mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari kupokea kijiti hicho kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel.


"Mimi nimevutiwa na utendaji wenu wa kazi na ndio maana mlivyoniita Leo nimekuja kuwasikiliza ila name Mimi nitawaita Ili niwaambie mambo yangu."alisema Malima


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa majadiliano juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi Mkoa wa Mwanza Edwin Soko alimuomba Mkuu wa Mkoa kuwa mlezi wa Klabu hiyo ili pamoja na mambo mengine aweze kuwa mshauri Mkuu wa Klabu hiyo.


"Mhe. Mkuu wa Mkoa,  huu umekuwa utamaduni wetu kila Mkuu wa Mkoa anayekuja Mwanza huwa tunamuomba kuwa mlezi wetu tukiamini kuwa ukaribu wetu unaweza kuwa na tija mwa Maendeleo ya Mkoa",amesema.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko

Share:

RC MALIMA : WAANDISHI WA HABARI MWANZA MKIANDIKA HABARI ZA KUCHOCHEA MAENDELEO MTAKUWA RAFIKI ZANGU

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka wanahabari wa Mkoa wa Mwanza kuwa kioo chake katika kipindi chote Cha uongozi wake.

Ameyasema hayo wakati akifungua rasmi mdahalo wa majadiliano juu ya umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19 ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Wa Habari Mkoa wa Mwanza na Internews Tanzania.

Malima amewahakikishia wanahabari ushirikiano huku akiwataka kuandika habari zitakazochochea Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza kwa ujumla.

"Mkiandika habari za kuchochea Maendeleo mtakuwa rafiki zangu lakini mkiandika habari mbaya tu kila kiku sitafanya kazi na nyie nitawatafuta wale tunaoendana."alisema Malima.

Akizungumzia zoezi linaloendelea la uchanjaji wa chanjo ya UVIKO 19 Malima amewataka wanahabari kuhakikisha wanaandika zitakazo washawishi wananchi kujitokeza kuchanja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mwanza Press Club Edwin Soko ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Mwanza katika kampeni mbalimbali ikiwemo ya chanjo ya UVIKO 19.

"Tulishiriki vema katika uzinduzi wa chanjo ya UVIKO 19 na baadhi ya Waandishi walichanja na tukaendelea kuripoti namna zoezi la chanjo linavyoendelea,huu ni utamaduni wetu tutahakikisha elimu inawafikia wananchi.alisema Soko.

Kwa upande wao washiriki wa mdahalo huo wameiomba Klabu ya Waandishi Wa Habari Mkoa Mwanza pamoja na Internews kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara kwa kuwa Mkoa wa Mwanza una waandishi wengi ambao wote wanahitajika kupewa elimu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza, Edwin Soko
Share:

RAIS AMTEUA PROF. MARK MWANDOSYA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI EWURA



Share:

DIWANI AFARIKI KWENYE AJALI BASI LILILOUA WATU WATANO SINGIDA


Diwani wa Tarafa ya Kinampanda Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Winjuka Songanieli Mkumbo, enzi za uhai wake.
Marehemu Winjuka Mkumbo enzi za uhai wake.

Na Dotto Mwaibale, Singida


WATU watano wamefariki dunia akiwamo Diwani wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Tarafa ya Kinampanda wilayani Iramba mkoani hapa, Winjuka Mkumbo na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Tanzanite kupinduka.

Kufuatia kifo cha Diwani huyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi alisema halmashauri hiyo imempoteza mtu muhimu sana ambaye mwaka huu alikuwa ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha na Mipango.

" Tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha diwani wetu huyu ambaye alikuwa msaada mkubwa katika halmashauri na ni pigo kubwa kwetu tumuombee mwenzetu kwa Mwenyezi Mungu apumzike kwa amani" alisema Msengi..

Aidha Msengi lisema marehemu enzi za uhai wake alikuwa akitoa misaada mbalimbali kwa jamii na kutokana na utendaji kazi wake ulio tukuka na makini alimteua kuwa mjumbe wa kamati hiyo ya fedha na mipango ya halmashauri hiyo.

Msengi alisema Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora tayari amekwenda mkoni Dodoma kwa ajili ya kuuchukua mwili wa diwani huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa ajali hiyo iliyohusisha basi namba T 916 DNU imetokea 9:30 alasiri katika Kijiji cha Mbwasa wilayani Manyoni Barabara ya Singida-Dodoma.

Aliwataja waliofariki kuwa ni Mwinjuka Mkumbo (40) ambaye ni Diwani wa Viti Maalum CCM wilaya ya Iramba, Alicia Flagence mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na wengine watatu ambao majina yao bado hawajambulika.

Diwani huyo alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya General mkoani Dodoma.

Kamanda Mutabihirwa alisema baada ya ajali majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya General Dodoma kwa matibabu na baada ya uchunguzi majeruhi 11 waliruhusiwa baada kupatiwa matibabu na watatu wanaendelea na matibabu huku mmoja akipewa rufaa katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.

Majeruhi wanaoendelea na matibabu ni Sharifati Mwipi (32) Rudia Kadila (59), Said Mbwana (39) na Abdul Ramadhani (32) ambao wanaendelea na matibabu katika hospitali ya General Dodoma huku majeruhi mmoja Mwamba Sita (26) amepewa rufaa kwenda hospitali ya Benyamin Mkapa.

Alisema uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi umebaini chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa basi hilo Abdul Kingwande ambaye alishindwa kulimudu kisha kuacha njia na kupinduka upande wa kulia wa barabara.

Kamanda Mutabihirwa alisema dereva wa basi hilo ambaye alitoroka baada ya ajali hiyo anatafutwa na jeshi la polisi.

"Jeshi la PolisiMkoa wa Singida linatoa wito kwa madereva wote wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani ili kuepukana na ajali zisizokuwa na ulazima," alisema.

Share:

Thursday, 18 August 2022

WIKI YA ASASI ZA KIRAIA 'AZAKI' YAZINDULIWA


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela (wa tatu kulia) akibonyeza kitufe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa wiki ya AZAKI 2022 katika hafla iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela akizungumza katika uzinduzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) 2022 leo Agosti 18, Jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutoka Ofisi ya Rais (OR TAMISEMI) Linus Kahendagaza akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela (wa tatu kusho) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society (FCS) Francis Kiwanga (wa pili kushoto) pamoja na Mratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali kutoka Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Linus Kahendagaza (wa pili kulia) katika uzinduzi rasmi wa Wiki ya AZAKI uliofanyika leo Agosti 18,2022 Jijini Dar es Salaam. (wa kwanza kushoto) ni, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundi, na (wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la CBM Nesia Mahenge.
Mratibu wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) Justice Rutenge, akizungumza katika hafla hiyo kuelezea matukio mbalimbali yatakayofanyika katika Wiki AZAKI ya 2022 yatakayofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 24, 2022 mpaka Oktoba 28, 2022.

Na: Mwandishi wetu,DAR ES SALAAM.

Imeelezwa kuwa jitihada za makusudi zinazofanywa na Asasi za kiraia katika kuimarisha ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali wa sekta hiyo zinatambuliwa na sekta binafsi kama sehemu muhimu ya kuharakisha maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 18,2022 Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela katika uzinduzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) 2022 ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Nsekela amesema kuwa ushirikiano baina ya aAasi za kirais na Sekta Binafsi unaweza kutoa suluhisho la changamoto za maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa ufanisi zaidi kuliko kila Taasisi kufanyakazi kivyake.

"Kwa bahati mbaya kumekuwepo na ushirikiano usioridhisha kati ya Asasi za kiraia na Sekta Binafsi katika kutatua changamoto za kimaendeleo nje ya ushirikiano wa kiufadhili. Hata hivyo, sisi ni wamoja. Ushirikiano kati ya sekta mbalimbali miongoni mwa mashirika, taasisi na wananchi ni miongoni mwa hatua zinazohitajika kuchukuliwa. Tunajenga Taifa moja na jamii moja ya kimataifa. Tunajenga simulizi zetu kwa ajili ya maendeleo yetu" amesema Nsekela.

Na kuongeza kuwa "Katika Sekta Binafsi tunaongelea uwekezaji unaoleta matokeo chanya. Huu ni uwekezaji unaofanywa kwa lengo la kuleta matokeo ya kijamii au kimazingira yanayopimika mbali na faida za kifedha. Lengo ni kuleta maendeleo ya kijamii na uthabiti wa kiuchumi. Msisitizo wa uwekezaji wenye kuleta matokeo chanya kijamii ni msingi muhimu wa ushirikiano wa karibu zaidi kati ya sekta binafsi na asasi za kiraia. Hii pia inaakisi Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu na Malengo Endelevu ya Maendeleo” ameongeza Nsekela.

Wiki ya Asasi za Kiraia ya 2022 inawaleta pamoja washirika muhimu wa maendeleo na ina lengo la kuimarisha ushirikiano wenye lengo la kukuza ushiriki wa Asasi za kiraia katika maendeleo ya Tanzania, kuimarisha hatua za pamoja zenye lengo la kufanyia kazi changamoto za kimaendeleo na kubadilishana mawazo kuhusu changamoto hizo.

Kuhusu Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) Nsekela amesema, “Tunaisubiri kwa hamu Wiki ya Asasi za kiraia ya mwaka huu. Tujikite zaidi katika kuoanisha uwekezaji wa Sekta Binafsi na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi. Uwekezaji wenye kuleta matokeo chanya ya kijamii ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha uwekezaji huo unaleta maendeleo endelevu.”

“Tusherehekee maendeleo ya watu kupitia simulizi za mabadiliko yaliyofanikishwa kwa kiasi kikubwa na Asasi za kiraia, lakini pia tuje na njia mpya za kuwekeza katika mipango ya kijamii kupitia ushirikiano miongoni mwa wadau mbalimbali,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga, amezungumzia kwa ufupi historia ya Wiki ya Asasi za Kiraia.

“Ujumbe wa mwaka 2018 ulikuwa ni ‘Ukuzaji wa Viwanda Tanzania: Watu, Sera na Utekelezaji’. Mwaka 2019 ujumbe ulikuwa ni ‘Maendeleo Kupitia Ushirikiano: Ushirika Kama Chachu ya Maendeleo Tanzania’, na mwaka 2021 ulikuwa ni ‘Mchango wa Asasi za Kiraia kwa Maendeleo ya Taifa’. Tangu kuanzishwa kwake, kumekuwa na utambuzi unaoongezeka miongoni mwa wadau wa umuhimu wiki hii kama jukwaa muhimu linalowakutanisha wadau mbalimbali. Sisi sote ni mashahidi wa umuhimu na matokeo chanya ya Wiki ya Asasi za Kiraia tangu ilipoanzishwa, ikiwa ni pamoja na kuimarishwa kwa umoja na mshikamano miongoni mwa wadau wa maendeleo nchini. Wiki ya Asasi za Kiraia pia imeleta mwamko mkubwa miongoni mwa washirika wa maendeleo wa umuhimu wa kuionyesha jamii mchango wao katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Wiki hii huweka msisitizo katika umuhimu wa ufanyaji kazi wa pamoja na ushirikiano katika kuwafikia wananchi,” alisema.

Naye Mratibu wa Wiki ya Asasi za Kiraia, Justice Rutenge, amesema ajenda ya wiki ya mwaka huu itajikita katika kuhakikisha washirika katika sekta mbalimbali wanakuwa ni sehemu muhimu ya ufanyaji kazi wa pamoja wenye lengo la kuleta maendeleo ambapo matukio mbalimbali ya AZAKI ya 2022 yatafanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 24, 2022 mpaka Oktoba 28, 2022.

“Tofauti na jitihada za awali zilizojikita katika kuelezea mchango wa sekta ya asasi za kiraia, ujumbe wa Wiki ya Asasi za Kiraia ya 2022, ambao ni ‘Maendeleo ya Watu, Simulizi za Watu’, una lengo la kuonyesha kwamba wananchi ndio washirika wetu wakubwa na sababu kubwa ya uwepo wa asasi za kiraia. Hii inaakisi hatua, mifumo na michakato mbalimbali inayotumiwa na asasi za kiraia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili Watanzania, hasa zile zilizoota mizizi na za muda mrefu. Hii pia inaonyesha nia ya asasi za kiraia na washirika wa maendeleo katika kuleta maendeleo chanya na kuongoza kwa mfano,” alisema.

Wiki ya Asasi za Kiraia ni tukio muhimu la kila mwaka kwa wadau wa maendeleo nchini, ikiwa ni pamoja na Asasi za kiraia, Sekta Binafsi na Serikali kwa ujumla, kwani hao wote ni washirika muhimu wa maendeleo nchini.

Wiki hii huelekeza jitihada zake katika kuhakikisha ushiriki kamili wa washirika na wadau kutoka Sekta mbalimbali.

 PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI HUO.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger