Monday, 15 August 2022
Sunday, 14 August 2022
BENKI YA NMB YAKUTANA NA KLABU YA BIASHARA KIGOMA...MAGESE ASEMA 'MAFUNZO YAMEWAJENGA WAFANYABIASHARA KWENYE MAFANIKIO'
Meneja wa kanda ya magharibi wa benki ya NMB Sospeter Magesse (aliyesimama kushoto) akitoa maelezo kwa wanachama wa klabu ya biashara ya benki hiyo wa wilaya ya Kasulu na Kibondo kuhusu matumizi ya simu na kadi za kielektorniki zinavyotumika kufanya miala na huduma za kifedha ikiwemo ya mikopo inayotolewa na benki ya NMB na manufaa ya huduma hiyo kwa wateja wakati wa kikao cha wanachama hao kilichofanyika wilayani Kasulu mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita. (Picha na Fadhili Abdallah).
Mkuu wa idara ya Biashara wa benki ya NMB makao makuu Alex Mgeni (kushoto) akizungumza na kutoa maelekezo mbalimbali ya namna ya kufanya biashara kwa ufanisi na kukabili changamoto za kibiashara wakati wa kikao na wanachama wa klabu ya biashara ya wateja wa benki hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Wanachama wa klabu ya biashara ambao ni wateja wa Benki ya NMB wilaya za Kasulu na Kibondo wakifuatilia mada zilizokuwa ikiwasilishwa katika mkutano wa wanachama hao uliofanyika wilayani Kasulu mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki.
***
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
BENKI ya NMB imesema kuwa semina na mafunzo yanayotolewa kwa wateja wa benki hiyo kupitia klabu za biashara za benki hiyo zimeleta mafanikio makubwa katika kuzingatia taratibu na miongozi ya huduma za kibenki nchini.
Meneja wa Kanda ya Magharibi wa benki ya NMB, Sospeter Magesse alisema hayo wakati wa kikao cha wanachama wa klabu ya biashara kutoka wilaya ya Kasulu na Kibondo kilichofanyika wilayani Kasulu.
Magesse alisema kuwa moja ya mambo ambayo yamesaidia wanachama wa vilabu hivyo ambao ni wateja wa benki ya NMB ni pamoja na kujua taarifa za huduma zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo upatikanaji wa mikopo, taratibu za upatikanaji wa mikopo hiyo na namna ya kufanya marejesho kulingana na taratibu zilizowekwa.
Meneja huyo wa kanda ya Magharibi wa benki ya NMB alisema kuwa kufanyika kwa mikutano hiyo kumesaidia kuimarisha huduma za benki kwa maana ya kuongeza wateja, ongezeko kubwa la wateja wanaochukua mikopo lakini pia imepunguza changamoto kubwa zinazojitokeza baina ya wateja na benki hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya biashara wa benki ya NMB Makao makuu, Alex Mgeni alisema kuwa kufanyika kwa mikutano hiyo kupitia vilabu vya biashara vya benki hiyo vimewezesha wateja wa benki hiyo kuzifikia fursa mbalimbali zinazotolewa ikiwemo mikopo kwa ajili ya kuimarisha biashara zao na shughuli za kiuchumi.
Mgeni alisema kuwa zipo fursa nyingi za mikopo na huduma nyingine ambazo wafanyabiashara na wateja wa benki hiyo wanaweza kuzifikia ambazo hazijatumika kikamilifu na ambazo zinaweza kusaidia kuinua biashara na kuchangia kuongeza ukusanyaji wa mapato wa serikali.
Sambamba na hilo Mkuu wa kitengo cha Bima kutoka NBM Makao makuu, Martin Masawe aliwaasa wateja wa benki hiyo kuweka bima za biashara zao, majengo ya vitega uchumi, nyumba na vyombo vya o vya usafiri ili waweze kuondokana na hasara majanga yanapotokea.
Baadhi ya wanachama wa vilabu vya wafanyabiashara vya benki ya NMB waliohudhuria mkutano huo walisema kuwa mikutano hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao ikiwemo kujua namna ya kuchukua hatua kukabiliana na changamoto za kibiashara zinapojitokeza na urejeshaji mikopo.
Mmoja wa wateja hao Zaitun Buyogera alisema kuwa mikutano hiyo imewawezesha kukutana na wataalam wa masuala ya biashara sambamba na viongozi wa benki hiyo ambao wamewapa ufafanuzi wa mambo mengi ambayo yanawasaidia kuendesha biashara zao kwa ufanisi.
NAIBU WAZIRI SAGINI ATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ENDAPO WAKIGUNDUA CHOMBO CHA MOTO WANACHOSAFIRIA KINA HITILAFU.

Naibu Waziri Jumanne Sagini akizungumza na abiria waliopata ajali ya basi la Shaloom Express iliyotokea jirani na Daraja la Mto Wami,mkoani Pwani 13/08/2022.

Naibu Waziri Jumanne Sagini akikagua na basi la Kampuni ya Shaloom Express lililopata ajali jirani na Daraja la Mto Wami,mkoani Pwani
..........................................
Na Mwandishi wetu,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amesikitishwa na ajali ya basi la Kampuni ya Shaloom Express linalotoka jijini Arusha kuelekea Dar es Salaam iliyotokea jana Agosti 13 jirani na Daraja la Mto sambasamba na ajali nyingine zinazojitokeza nchini kwa ujumla na kuwataka abiria wanaotumia vyombo vya moto vinavyosafiri masafa marefu kutoa taarifa mapema kwa askari Polisi wa usalama barabarani endapo watakapoona basi au chombo chochote cha usafiri kinahitilafu ili kuepuka ajali.
Akizungumza na abiria walionusurika katika ajali hiyo, Naibu Waziri Sagini amesema kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kujilinda na ajali zinazotokea barabarani na kusema kuwa wakiona hitilafu yoyote kwenye chombo wanachosafiria na dereva mwenyewe basi ni bora kutoa taarifa mapema kwa askari polisi wa usalama barabarani ili hatua zingine zichukuliwe.
“Tunashukuru Mungu kwamba abiria wote wametoka salama na ni wape pole sana abiria waliojeruhiwa. Naomba mtambue kuwa Serikali ipo pamoja nanyi na niwaombe abiria watusaidie kuwa walinzi wa usalama wao wenyewe.Toeni taarifa endapo mnaona basi linahitilafu”
Aliyasema hayo jana, Agosti 13, 2022 baada ya kukagua basi lililopata ajali jirani na Daraja la Mto Wami la Kampuni ya Shaloom Express linalotoka jijini Arusha kuelekea Dar es Salaam.
Aidha Naibu Waziri Sagini amemuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani kuhakikisha mizigo yote ya abiria ya waliojeruhiwa ambayo imebaki inahifadhiwa ili waweze kupata mizigo yao.
Mmoja wa manusura katika ajali hiyo aliyefahamika kwa jina la Shaban Abdala aliishukuru Serikali kwa kujitokeza mapema na kusema gari hilo lilikuwa bovu na kwamba baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya basi hilo walikuwa wakilalamika uchakavu wa gari hilo.
“Naishukuru Serikali kwa kujali na kujitokeza mapema na basi hilo lilianza kuwa na tabu ya usalama kuanzia mapema na kwamba lilifikia hatua kwenye mlima ilishindwa kupanda.”
BENKI YA NBC YAKABIDHI MATREKTA YA MIKOPO KWA WAKULIMA
Wakulima wakiwa na Matrekta ya Mikopo ambayo wamekopeshwa na Benki ya NBC.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Shinyanga, imekabidhi Matrekta Mawili ya Mikopo kwa Wakulima ili kuunga juhudi za Serikali kukuza Sekta ya Kilimo na uchumi wa Taifa.
Matreka hayo yamekabidhiwa leo Agosti 13 ,2022 na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, hafla iliyo hudhuliwa pia na Kampuni ya usambazaji wa zana za Kilimo Agricom.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga Joyce Chagonja, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Matreka kwa wakulima, amesema Benki hiyo ina fursa nyingi za mikopo kwa ajili ya wakulima ikiwamo kuwakopesha zana za kilimo, pamoja na Bima za mazao.
Amesema ukopeshaji wa Matrekta hayo hakuna masharti magumu, bali ni Mkulima anatakiwa awe na Shamba, pamoja na kuchangia asilimia 25 ya Mkopo wake, huku wao wakichangia asilimia 75 na Marejesho yake ni nafuu hayambani Mkulima.
“Matrekta ambayo tumekabidhi wakulima hawa leo gharama zake ni Sh. milioni 40.7 kwa kila Moja na wakulima hawa wamechangia asilimia 25,”amesema Chagonja.
“Benki ya NBC tupo pamoja na Serikali kukuza Sekta ya Kilimo sababu tunatambua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo asilimia 80, na ndiyo maana leo tumekabidhi Zana hizi za kilimo kwa wakulima,”ameongeza.
Naye wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ameipongeza Benki hiyo ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kukuza Sekta ya kilimo na kutoa mikopo Zana za kilimo kwa wakulima, huku akitoa wito kwa wakulima kuzitumia zana hizo kufanya kilimo chenye tija na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao.
Nao baadhi ya wakulima walionufaika na mikopo hiyo ya Matrekta akiwamo Golea Kamata na Bujiku Fumbuka, amesema Zana hizo za kilimo zitakwenda kuwa chachu ya mabadiliko na kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla kupitia Sekta hiyo ya Kilimo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) Tawi la Shinyanga, imekabidhi Matrekta Mawili ya Mikopo kwa Wakulima ili kuunga juhudi za Serikali kukuza Sekta ya Kilimo na uchumi wa Taifa.
Matreka hayo yamekabidhiwa leo Agosti 13 ,2022 na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, hafla iliyo hudhuliwa pia na Kampuni ya usambazaji wa zana za Kilimo Agricom.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga Joyce Chagonja, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Matreka kwa wakulima, amesema Benki hiyo ina fursa nyingi za mikopo kwa ajili ya wakulima ikiwamo kuwakopesha zana za kilimo, pamoja na Bima za mazao.
Amesema ukopeshaji wa Matrekta hayo hakuna masharti magumu, bali ni Mkulima anatakiwa awe na Shamba, pamoja na kuchangia asilimia 25 ya Mkopo wake, huku wao wakichangia asilimia 75 na Marejesho yake ni nafuu hayambani Mkulima.
“Matrekta ambayo tumekabidhi wakulima hawa leo gharama zake ni Sh. milioni 40.7 kwa kila Moja na wakulima hawa wamechangia asilimia 25,”amesema Chagonja.
“Benki ya NBC tupo pamoja na Serikali kukuza Sekta ya Kilimo sababu tunatambua kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo asilimia 80, na ndiyo maana leo tumekabidhi Zana hizi za kilimo kwa wakulima,”ameongeza.
Naye wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, ameipongeza Benki hiyo ya NBC kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kukuza Sekta ya kilimo na kutoa mikopo Zana za kilimo kwa wakulima, huku akitoa wito kwa wakulima kuzitumia zana hizo kufanya kilimo chenye tija na kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao.
Nao baadhi ya wakulima walionufaika na mikopo hiyo ya Matrekta akiwamo Golea Kamata na Bujiku Fumbuka, amesema Zana hizo za kilimo zitakwenda kuwa chachu ya mabadiliko na kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla kupitia Sekta hiyo ya Kilimo.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Shinyanga Joyce Chagonja, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Matrekta kwa wakulima.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi Matrekta kwa wakulima
Meneja wa Kampuni ya Agricom Kanda ya Ziwa Christina Mabula, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Matrekta kwa wakulima.
Muonekano wa Matrekta ya Mikopo kwa wakulima.
Wakulima wakiwa na Matrekta ya Mikopo ambayo wamekopeshwa na Benki ya NBC.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kulia) akikabidhi funguo kwa Mkulima Golea Kamata ambaye amekopeshwa Trekta na Benki ya NBC.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko (kushoto) akikabidhi funguo kwa Mkulima Bujiku Fumbuka ambaye amekopeshwa Trekta na Benki ya NBC.
Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya wakulima kumaliza kukabidhiwa Matrekta ya mikopo na Benki ya NBC.
BENKI YA NBC YASISITIZA DHAMIRA YAKE KUKUZA SEKTA YA MICHEZO,SANAA NA UTAMADUNI
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (Kulia) akisalimiana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja Ofisa Mkuu wa Uendeshaji Benki ya NBC Bi Alelio Lowassa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa NBC, Godwin Semunyu
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wageni waalikwa wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi akizungumza na wageni waalikwa wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (Kulia) akisalimiana na wageni mbalimbali akiwemo Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar (katikati) wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi (Kulia) akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Muheza Mkoani Tanga Mhe, Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mkuu wa Uendeshaji Benki ya NBC Bi Alelio Lowassa (kulia) akisalimiana na baadhi ya wageni wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya michezo, sanaa na utamaduni nchini wakati hafla ya jioni iliyolenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza iliyoandaliwa kwa ushirikiano na benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
..............................................
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu adhma yake ya kukuza na kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini kwa kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo inayokua kwa kasi.
Akizungumza kwenye hafla ya jioni iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam ikilenga kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika hivi karibuni Birmingham, Uingereza, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw. Theobald Sabi alisema sekta ya michezo, sanaa na utamaduni ina mchango muhimu katika suala zima la ajira pamoja na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa ujumla.
“Pamoja na kuitikia wito wa serikali katika kuinua sekta hii muhimu, benki ya NBC tumebaini kwamba sekta hii ni eneo la kimkakati kiuchumi iwapo sisi kama wadau muhimu tutaiunga mkono,’’ alisema Bw Sabi kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakiwemo viongozi waandamizi wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Bw Sabi alibainisha kuwa benki hiyo Ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na wadau wa sekta michezo, sanaa na utamaduni na dhamira hiyo inapimwa kwa namna ambavyo taasisi hiyo hiyo inadhamini matukio mbalimbali ya kimichezo hapa nchini ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League), NBC Dodoma Marathon, mashindano mbalimbali ya mchezo wa golf pamoja na kuunga mkono jitihada za ujenzi wa miundombinu ya michezo ikiwemo ujenzi wa viwanja vya mpira katika maeneo mbalimbali nchini.
“Hivyo basi kwetu NBC milango ipo wazi wa wadau mbalimbali wa sekta ya michezo, sanaa na burudani ili tuweze kushirikiana katika kukuza sekta hii muhimu lengo likiwa ni kukuza ajira ambayo ni nyenzo muhimu kiuchumi na ustawi wa sekta ya fedha nchini,’’ alisema.
Pamoja na kuwapongeza na kuwakaribisha wanamichezo wa Kitanzania walioshiriki kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola hafla hiyo pia ilihusisha makabidhiano ya taarifa ya namna bora ya kusimamia HAKIMILIKI na ugawaji wa Mirabaha kwa wamiliki wa kazi za sanaa nchini.






































