Tuesday, 9 August 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 9, 2022



















Share:

Monday, 8 August 2022

Breaking News : AJALI YA MAGARI MATATU NA TREKTA USIKU HUU MWAKATA SHINYANGA


Watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha magari matatu na Trekta usiku huu katika eneo la Mwakata barabara ya Isaka Kahama.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nne usiku leo Jumatatu Agosti 8,2022 ikihusisha gari ndogo IST yenye namba za usajili T880 DUE, Hiace yenye namba za usajili T350 BDX, Lori na Trekta ambalo Plate number zake zimeng’olewa. Inaelezwa kuwa Hiace imegongana uso kwa uso na Lori.

Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde


Share:

VYAMA VYA USHIRIKA VYATAKIWA KUWA MKOMBOZI WA WAKULIMA, WAFUGAJI NA WAVUVI


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza na viongozi na wananchi kwenye siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, ambapo amewasihi wafugaji na wavuvi kujiujiunga kwenye vyama vya ushirika na kuwataka wananchi kutumia mazao ya mifugo na uvuvi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (wa nne kutoka kushoto) akisikiliza maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA), Bi. Eileen Nkondola (wa sita kutoka kushoto) kuhusu bwawa linalohamishika kwenye Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi lililopo kwenye Viwanja vya Maonesho ya Nanenane – Ngongo Mkoani Lindi.


Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Judith Nguli akito salamu za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakati wa siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo, Dkt. Erastus Mosha akiwashukuru viongozi wa Kanda ya kusini kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanapata fursa kubwa kupitia maonesho ya Nanenane kukutana na wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani wa mazao yao.


Mkurugenzi Msaidizi Utafiti na Mafunzo, Dkt. Hassan Mruttu akitoa salamu za Sekta ya Mifugo wakati wa siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiangalia viatu vya ngozi katika Banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Kulia ni mfanyabiashara wa bidhaa za ngozi, Bw. Suleiman Hassani


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizungumza wakati alipotembelea banda la Chama cha Ushirika cha TANECU kwenye siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili mkoani hapo kwa ajili ya siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akimuangalia ng’ombe aliyemkuta kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa kwenye Maonesho ya Nanenane – Ngongo mkoani Lindi.

...................................... NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amevitaka Vyama vya Ushirika vya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi nchini kuwa msaada katika kuleta maendeleo na sio kushiriki kushusha maendeleo ya wadau wa sekta hizo.

Naibu Waziri Ulega ameyasema hayo wakati wa siku ya Mifugo na Uvuvi ya Maadhimisho ya Wiki ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kusini kwenye Viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, ambapo amesema lengo la kuanzishwa kwa ushirika ni kuwasaidia wanyonge kuwa na nguvu moja itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi.

Vyama vya Ushirika ni muhimu kwa wafugaji na wavuvi kwani vinasaidia kuwakutanisha pamoja ambapo wataweza kupata fursa mbalimbali zikiwemo za mikopo na bima. Wizara inaendelea kuwahamasisha wafugaji na wavuvi kujiunga kwenye vyama vya ushirika kwa kuwa ni njia ambayo itawafanya wawe na nguvu moja kwenye maamuzi ya biashara ya mazao yao.

Naibu Waziri Ulega pia amewataka viongozi wa Vyama vya Ushirika kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwani kumekuwepo na malalamiko mengi kwenye baadhi ya vyama kutokana na ukiukwaji wa taratibu za uendeshaji kitu kinachosababisha wakulima, wafugaji na wavuvi kuilalamikia serikali.

Vilevile ameendelea kuwasihi wananchi kutumia mazao yatokanayo na mifugo na uvuvi kwa kuwa ni muhimu katika kujenga na kuimarisha afya. Pia amewashauri watanzania kuendele kutumia bidhaa mbalimbali zinazotokana na zao la ngozi kama viatu, mikanda na mikoba kwa kuwa bidhaa hizo ni bora na zinazalishwa hapa nchini.

Naibu Waziri Ulega amewasihi wafugaji kuhakikisha wanavisha hereni za kielektroniki kwenye mifugo yao kama taratibu zinavyotaka kwa kuwa mfumo huo una faida kubwa. Serikali inaendelea na uboreshaji wa mazingira ya wafugaji kwa ujenzi wa majosho, malambo na uhamasishaji wa utunzaji wa nyanda za malisho na kilimo cha malisho ya mifugo ili wakati wa kiangazi wafugaji wasiweze kupata tabu. Pamoja na mambo mengine kwa mkoa wa Lindi, Wizara inajenga Malambo kwenye Kijiji cha Kimambi (Wilayani Liwale) na Matekwe (Wilayani Nachingwea) ili wafugaji waweze kupata maji ya kunyweshea mifugo yao.

Aidha, amesema Wizara hiyo inakusudia kuanza kutoa mikopo kwa vifaa kwa wavuvi ili waendeleze shughuli zao na hatimaye kuinuka kiuchumi, ambapo pia amesema zipo boti 250 za kisasa ambazo zitakopeshwa kwa wavuvi. Huku akibainisha kwamba kipindi kirefu wavuvi wamekuwa wakitumia zana duni za uvuvi na hivyo kuvua kwa kubahatisha lakini sasa serikali imedhamiria kumsaidia mvuvi kuhakikisha anakwenda kuvua eneo ambalo samaki wanapatikana.

Pia Naibu Waziri Ulega amewataka viongozi wa vijiji kuhakikisha wanasimamia Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi ili maeneo yanayotengwa kwa ajili ya shughuli za mifugo zisiweze kuingiliwa na watumiaji wengine wa ardhi. Lakini pia amewasihi wafugaji kuto lisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kwa kuwa hiyo ni moja ya chanzo cha migogoro na ikitokea tukio kama hilo serikali itachukua hatua.

”Wakulima na Wafugaji ni ndugu kwa kuwa wote wanategemeana, hivyo ni vyema kila mmoja akaiheshimu kazi anayoifanya mwenzake ili wote kwa pamoja waweze kuendelea na kujiingizia kipato kutokana na shughuli wanazofanya,” alisema Naibu Waziri Ulega

Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Mhe. Judith Nguli amesema kuwa kupitia elimu inayotolewa kwenye maonesho ya nanenane anaamini wakulima, wafugaji na wavuvi watakwenda kutumia mbinu za kisasa kwenye shughuli wanazofanya, kitu ambacho kitawasaidia kuongeza tija katika uzalishaji na biashara ya mazao hayo.

Kwa upande wake Dkt Hasan Mruttu Mkurugenzi Msaidizi Utafiti na Mafunzo amezishauri Halmashauri kuendelea kuwahamasisha wafugaji na wavuvi kujiunga kwenye vyama vya vyama vya ushirika ili viwasaidie katika kutetea maslai yao.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo, Dkt. Erastus Mosha amewashukuru viongozi wa Kanda ya kusini kwa maandalizi mazuri waliyoyafanya kwa kuwa wakulima, wafugaji na wavuvi wanapata fursa kubwa kupitia maonesho hayo kukutana na wadau mbalimbali kwenye mnyororo wa thamani wa mazao yao.
Share:

MAADHIMISHO SIKU YA NANENANE : MKE WA JAJI WA MAHAKAMA YA TANZANIA BI.MARINA JUMA AONGOZA WAKE WA MAJAJI KWENYE MATEMBEZI

Mke wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bi.Marina Juma (katikati) akiwaongoza wake wa majaji kwenye matembezi katika kuadhimisha siku ya Nanenane, matembezi ambayo yalianzia nyumbani kwake Jaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kupitia daraja la Tanzanite, Ocean Roads na kufikia tamati Serena Hotel.
*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UMOJA wa wake wa majaji wa mahakama nchini (We are Family) wamejumuika pamoja katika kuadhimisha Siku ya Nanenane kwa kufanya matembezi ya umbali wa kilometa sita kupitia Tanzanite Bridge ambapo wake wa majaji 13 wameshiriki.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa matembezi hayo leo Jijini Dar es Salaam, mke wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bi.Marina Juma amesema wameamua kushiriki maadhimisho ya Nane nane wao kama kikundi wakaona ni muhimu kufanya matembezi ili kuimarisha afya zao.

Amesema matembezi hayo ni ya mara ya kwanza hivyo watahakikisha yanakuwa endelevu ambapo watakuwa wakikutana na kufanya mikutano ya mara kwa mara kujenga ushirikiano wa pamoja wao kama wake wa majaji nchini.

"Malengo hasa ya kikundi chetu ni kufanya mazoezi, kufahamiana na kuishi pamoja kama familia na kufanya mambo mbalimbali yenye manufaa na tija kwenye jamii". Amesema Bi.Marina Juma.

Pamoja na hayo amewakaribisha pia wake wengine wa majaji kuungana na kikundi hicho na kuweza kukutana mara kwa mara na kushiriki mazoezi kwa pamoja ili kuweza kuungana na kushirikiana kwa mambo mbalimbali.

Kwa upande wake mke wa Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Bi.Sada Othman ambaye amewawakirisha wake wa majaji wastaafu kwenye maadhimisho hayo amesema kuna umuhimu mkubwa hivyo amewataka wastaafu wengine wawe wanautaratibu wa kufanya mazoezi ili kuweka miili yao sawa kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Baadhi ya wake wa Majaji wa Mahakama ya Tanzania wakiwa kwenye matembezi katika kuadhimisha siku ya Nanenane, matembezi ambayo yalianzia nyumbani kwake Jaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kupitia daraja la Tanzanite, Ocean Roads na kufikia tamati Serena Hotel. Mke wa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bi.Marina Juma akiwaongoza wake wa majaji kwenye matembezi katika kuadhimisha siku ya Nanenane, matembezi ambayo yalianzia nyumbani kwake Jaji Mkuu wa mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma kupitia daraja la Tanzanite, Ocean Roads na kufikia tamati Serena Hotel. Wake wa Majaji wa mahakama ya Tanzania wakipata picha ya pamoja kwenye daraja la Tanzanite wakiwa kwenye matembezi katika kuadhimisha Siku ya Nane Nane ambapo wametembea kilomita sita. Wake wa Majaji wa mahakama ya Tanzania wakipata picha ya pamoja kabla ya kuanza matembezi katika kuadhimisha Siku ya Nane Nane ambapo wametembea kilomita sita wakipitia Tanzanite Bridge Jijini Dar es Salaam..

Share:

MREMBO WA MIAKA 22 ATEKWA NA PENZI LA BABU WA MIAKA 88


Chibalonza ana umri wa miaka 22, lakini moyo wake umetekwa na mapenzi ya babu mwenye umri wa miaka 88, Kasher Alphonse nchini Congo.

Babu huyo aliambia Afrimax English kuwa wanapendana na kuelewana licha ya tofauti ya umri wa miaka 66.

Kulingana na wapenzi hao ambao wamekuwa pamoja kwa miaka miwili, walivutiwa na nyoyo zao na wala sio miaka.
Alphonse alimuoa mke wake wa kwanza mwaka wa 1954 wakati alikuwa na umri wa miaka 24 na kujaliwa watoto saba pamoja.

Baada ya miongo kadhaa pamoja, mke wake wa ujana aliaga dunia kutokana na uzee, na kumuwacha babu huyo akiwa amevunjika moyo na mpweke kwani wanawe tayari walikuwa watu wazima na kuondoka nyumbani. 

Kwa kuzingatia umri wake wa uzee, Alphonse alihangaika kujifanyia mambo mengi, hivyo akatafuta mtu ambaye angemsaida. Alikuwa na bahati kukutana na Chibalonza, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 20 lakini tayari kuwa mke wake.

"Hatujafunga ndoa rasmi lakini nimefanya naye harusi ya kitamaduni. Nilipeleka hata kreti ya bia na mbuzi aliye hai kwa familia yake," alisema.

 Mzee huyo alionyesha wasiwasi kuwa hajui jinsi watoto wake watakavyoishi na mama yao wa kambo iwapo atafariki dunia.

 Anajutia kuwa hana pesa za kununua kipande cha ardhi kwingine ili mke wake mchanga awe na makazi salama mbali na familia yake ya kwanza.

Watu wengi wanaojua kuhusu mapenzi huona kama ni ajabu kwa sababu watoto wote wa Alphonse ni wakubwa kuliko mama yao wa kambo, huku mwanawe wa kwanza akiwa na umri wa miaka 66, naye kitinda mimba ana umri wa miaka 50.

 Alphonse anaweza kuonekana mnyonge na maskini kwa sasa, lakini anasema alikuwa akifanya vizuri kifedha katika siku zake za heri wakati huo akimiliki duka la jumla ambapo aliuza pombe.

 Biashara hiyo, hata hivyo, ilifungwa baada ya msururu wa wizi ambao ulimaliza hisa zake na kufanya isiweze kuendelea.

CHANZO- Tuko News
Share:

KIKWETE AKUTANA NA WAGOMBEA URAIS KENYA ODINGA NA RUTO...UCHAGUZI MKUU KESHO!

Mheshimiwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa Kiongozi ya Timu ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Kenya, ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa nyakati tofauti, amekutana na kufanya mazungumzo na Wagombea Urais William Ruto kutokea Umoja wa Vyama vya Kenya Kwanza, na Raila Odinga wa Umoja wa Vyama vya Azimio la Umoja. Mgombea wa wa Azimio la Umoja Raila Odinga, aliambatana pia na Mgombea wake Mwenza Martha Karua.

Wagombea hao Naibu Rais William Ruto na Raila Odinga, kiongozi mkongwe wa upinzani ambaye sasa anaungwa mkono na chama tawala, wanapigania nafasi ya kuliongoza taifa hilo la Afrika Mashariki.

Wapiga kura wapatao milioni 22.1 kesho siku ya Jumanne tarehe 9,2022 watamchagua rais ajaye, atakayechukua nafasi ya rais Uhuru Kenyatta anayemaliza muda wake baada ya kuliongoza taifa la Kenya kwa mihula miwili. Kwa mujibu wa katiba Uhuru Kenyatta haruhusiwi kugombea muhula wa tatu baada ya kumaliza mihula miwili. 

Vilevile wakenya watawachagua maseneta, magavana, wabunge, wawakilishi wa wanawake na idadi ya maafisa 1,500 wa kaunti.


Matokeo rasmi yatatangazwa ndani ya wiki moja baada ya zoezi la kupiga kura. Ili kushinda moja kwa moja, mgombea anahitaji kupata zaidi ya nusu ya kura zote na angalau asilimia 25 ya kura katika zaidi ya nusu ya kaunti 47 za nchini Kenya. Iwapo hakutakuwepo na mshindi wa moja kwa moja maana yake ni uchaguzi wa marudio utakafanyika ndani ya siku 30.




Share:

JINSI PICHA ZA UTUPU, VIDEO ZA NGONO ZINAPUNGUZA HAMU YA TENDO LA NDOA

Utandawazi na ongezeko la maarifa katika teknolojia ya vifaa ya mawasiliano umechangia kwa namna moja au nyingine kusambaa picha na video za ngono ambazo zinapatikana katika kanda za video, simu za mkononi na kwenye kompyuta zenye mtandao wa intaneti kwa gharama nafuu na wakati mwingine zinapatikana bure.

Wataalamu wa afya na saikolojia wanaeleza uraibu wa video za ngono ni moja kati ya sababu zinazochangia kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa, hasa kwa wanaume.

Inaelezwa kuwa mraibu wa picha za utupu anapokosa suluhisho la hisia zake kwa haraka anaweza kujikuta anajichua na akiendelea na tabia hiyo huweza kujikuta katika uraibu wa kitendo hicho hali inayosababisha kukosa hisia za kufanya tendo hadi atakapoangalia picha au video hizo. Pia anashindwa kudumu kufanya tendo la ndoa hadi aangalie picha au video za ngono.



Share:

MRADI WA TGNP KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI HARAKATI ZA MAENDELEO HALMASHAURI YA MOROGORO WALETA MANUFAA

 MRADI wa kuhamasisha wananchi kushiriki harakati za maendeleo unaotekelezwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) katika Kata tatu za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro umeleta manufaa kwa wananchi wilayani humo. 

 

Mradi huo ambao pia unalenga wananchi kujitambua, kushiriki na kuhoji matumizi ya fedha za rasilimali za nchi unatekelezwa katika Kata tatu za Kisaki, Bwakira chini na Mngazi. 

 

Asma Kilonga ambaye ni mjasiriamali na Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa (KC) Kata ya Kisaki ni mmoja wa wanufaika wa mradi huo ambaye amefanikiwa kupiga hatua kimaendeleo kupitia mradi huo. 

 

Asma anasema baada ya kupata mafunzo ya mradi kutoka TGNP kupitia Kituo cha Taarifa na Maarifa aliamua kulima shamba lake mwenyewe la viazi lishe japo alipambana katika kutafuta soko lakini kwa sasa amefanikiwa na biashara yake inakwenda vizuri.  

 

“Mimi nilithubutu kulima shamba langu mwenyewe la viazi baada ya kupata mafunzo na kupenda mradi huu wa viazi. Kwa sababu nilikuwa nalinganisha nikilima heka moja ya viazi na ufuta tayari nikaona tofauti. Kwa hiyo nikachukua mbegu nikapanda heka moja na nusu. Katika hiyo heka moja na nusu, heka moja nikawahi kupanda, hiyo nusu nikachelewa kidogo lengo ni kuangalia bei kama itakuwa na uwiano sawa. Ile heka moja niliyoipanda nikaenda nayo ilivyofika mwezi wa sita nikaangalia viazi nikavikuta viko tayari.” Anasema Asma. 

 

Asma anasema alipitia changamoto nyingi katika kuhakikisha anapata soko la viazi vyake na baada ya kupambana mwenyewe bila kukata tamaa hatimaye alipata soko na kuuza viazi vyake. 

 

Si hivyo tu, lakini mwanamama huyu pia alithubutu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo udiwani ambao hata hivyo anasema kura hazikutimia na kwamba wakati ujao anaamini zitatimia na kushika wadhifa huo. 

 

“Elimu niliyoipata TGNP, hapa nilipo kwanza ni Mjumbe wa Hlamashauri ya Kijiji niligombea, na pia nilithubutu kuchukua fomu ya udiwani wa Kata kwa bahati mbaya kura zangu hazikutosha. Kwa hiyo sasa nina uwezo wa kusimama kwenye mkutano wa Kijiji kuelimisha wat una siogopi mtu wa aina yeyote, nasimama na kuwea kuzungumza na mtu wa aina yeyote. TGNP wamenipa uraghibishi wamenijengea uwezo nawashukuru sana.” Anasema Asma. 

 

Naye Rukia Jambalaga ambaye ni mfugaji wa kuku kupitia Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Bwakira Chini anasema baada ya kupata elimu ya ufugaji wa kuku kutoka Ushirika wa Wajasiriamali Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sua (SUGECO) kupitia TGNP amepata maendeleo makubwa baada ya kuanza ufugaji na kuuza kuku ambapo alifanikiwa kujenga nyumba ya kisasa. 

 

“Kwanza tunashukuru kupata mafunzo haya ya TGNP, yametukwamua sana kimaisha. Kwanza elimu tumeenda kupata Sugeco ya mafunzo ya kufuga kuku. Kwa kweli tulipotoka na sugeco mpaka kufika hapa mafanikio tuliyoyapata ni makubwa sana kiasi ambacho tangu nilipoingia kwenye KC hii mpaka sasa hivi nina maendeleo makubwa. Tumeanza mradi wa kufuga kuku, tumeenda kuchukua kuku elfu moja tukaja tukafuga, kuku wale wakawa wakubwa na tumewauza tumepata zaidi ya mamilioni.” Anasema Rukia. 

 

Rukia anasema kuwa baada ya kupata fedha hizo waliamua kwenda kuchukua kuku wengine ili mradi wao uendelee na kuamua kwa kila mwanakikundi kujifunza nyumbani kwake namna ya ufugaji bora ili kila kila mmoja aweze kufuga. 

 

Anasema alianza kwa kufuga kuku mia tano na baada ya biashara kumwendea vizuri aliweza kujenga nyumba ya kisasa ya vyumba sit ana hivyo kuishukuru TGNP kwa kuwapelekea mradi huo. 

 

Mradi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa (KC) kupitia mpango wa uraghibishi umewasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa maeneo hayo kufahamu mambo mengi ambayo hapo awali hawakuwa wakiyafahamu.  

 

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na haki ya umiliki wa ardhi kwa wanawake, changamoto katika sekta ya elimu, uongozi na afya ambapo baada ya kupatiwa mafunzo ya uraghibishi wananchi walipata mwamko katika kupigania kuondoa changamoto hizo. 

 

Severine Henry Msohela ambaye ni mmoja wa wanachama wa kikundi cha taarifa na maarifa (KC) Kata ya Kisaki anasema baada ya TGNP kuwapatia mafunzo hayo mwaka 2013, mambo mengi yamebadilika baada ya wananchi kujengewa uwezo

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger