Saturday, 16 July 2022

HATIMAYE NANDY NA BILLNAS WAFUNGA NDOA



Msanii William Lyimo maarufu Billnass na nyota wa muziki wa Bongofleva Faustina Mfinanga maarufu Nandy wamefunga ndoa.

Wawili hao wamefunga pingu za maisha leo Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Billnass na Nandy ni wapenzi wa muda mrefu na siku za hivi karibuni waliutangazia umma kuwa muda si mrefu watakuwa wazazi baada ya kupost picha zikimuonyesha Nandy akiwa mjamzito.

Picha: Clouds Digital










Share:

MWANRI AIPONGEZA SERIKALI KUONGEZA MSULI SEKTA YA KILIMO…ATAKA KUZALISHA VYA ZIADA


Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri akionesha jembe la palizi kwa ajili ya zao la pamba na mazao mengine
Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri akielezea kuhusu jembe la palizi kwa ajili ya zao la pamba na mazao mengine
Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) waliotembelea wadau wa pamba Kanda ya Ziwa, Julai 15,2022 mkoani Shinyanga.
Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) waliotembelea wadau wa pamba Kanda ya Ziwa, Julai 15,2022 mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Balozi wa zao la Pamba nchini Aggrey Mwanri ameipongeza serikali kwa namna ilivyofanya mabadiliko makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuongeza bajeti ambapo bajeti hiyo italeta mabadiliko makubwa kwa wakulima.

Katika mwaka 2022/2023, Bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kutoka Shilingi 294,162,071,000 hadi Shilingi 751,123,280,000 sawa na ongezeko la asilimia 155.34 225 429 ambapo Sehemu kubwa ya fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, miundombinu ya uhifadhi wa mazao, kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao, kuimarisha utafiti wa kilimo, uzalishaji wa mbegu na utoaji wa ruzuku.

Akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) waliotembelea wadau wa pamba Kanda ya Ziwa, Julai 15,2022 mkoani Shinyanga, Mwanri amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeonesha jitihada na mabadiliko makubwa katika kusimamia sekta ya kilimo kwa kutenga bajeti kubwa, ambayo itatoa ruzuku za pembejeo na kuendelea kutoa elimu ya kilimo chenye tija ili kubadilisha Kilimo kiwe na tija zaidi.

“Tuna Serikali iliyo makini ‘serious’ na inachokifanya kwenye kilimo, ni vyema vijana wakachukua fursa kwenye kilimo kwani kilimo ni biashara. Fursa hazitolewi, fursa zinachukuliwa. Wananchi waunge mkono mambo mazuri yanayofanywa na serikali kwa kufanya kazi kwa vitendo kwa kulima kwa tija ili tupate malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda vyetu na kwa upande wa zao la pamba tutapata mafuta mengi ili kutatua changamoto ya uhaba wa mafuta nchini”,amesema.

“Wakulima wetu wanatakiwa kuzalisha mazao kwa ziada. Huwezi kupata maendeleo kama huzalishi vya ziada. Usilime kwa ajili ya kula tu, Kilimo cha mazao yote Tanzania sasa ni biashara, sasa hakuna zao la chakula tu. Lima kwa tija kibiashara”,ameongeza Mwanri.

Aidha amewataka vijana kuchangamkia fursa kwa kujiajiri katika kilimo akisisitiza kuwa ajira ya kweli ni kujiajiri katika kilimo na kwamba wananchi wakilima kibiashara maisha yao yatabadilika.


Katika hatua nyingine Mwanri amesema bei ya zao la pamba katika msimu huu inaridhisha tofauti na misimu mingine kwani wanunuzi wananunua kilo moja ya pamba zaidi ya bei elekezi ya serikali ambayo ni shilingi 1560 ambapo baadhi yao sasa wananunua zaidi ya shilingi 1600 na kuna kipindi bei ilifikia hadi shilingi 2020 kutokana na bei ya pamba kupanda katika soko la dunia.

Mwanri amewashauri vijana kuachana na dhana ya kwamba zao la pamba wanalima wazee.

“Kwenye zao la pamba vijana wapo wachache wanaoonekana sana kulima pamba ni wazee, lakini kwenye zao la pamba kuna ajira nyingi, vijana changamkieni fursa hii, kilimo ni biashara kinalipa na mwajiri mkuu ni kilimo”,amesema.
Share:

MAMA ALIYETUMIA VIDONGE VYA ARV KWA MIAKA 6 KISHA KUJA KUBAINIKA HANA UKIMWI AFUNGUA KESI KUDAI FIDIA


Faridah Kiconco (37); ni mama alitumia dawa za ukimwi kwa miaka sita

FARIDAH Kiconco (37); ni mama aliyeambiwa kwenye kituo cha afya kuwa ana Virusi Vya Ukimwi (HIV) kisha akatumia dawa kwa miaka sita, kumbe hana Ukimwi.

Faridah amefungua kesi akidai fidia baada ya dawa alizopewa kunywa kwa miaka hiyo kumletea matatizo ya kiafya kwenye figo na ini.

Faridah, raia wa nchini Uganda, akihojiwa kwa masikitiko amesema, mwaka 2011 alikwenda kituo cha afya cha Kabwohe kupima mimba, lakini pia akaambiwa apime na Virusi Vya Ukimwi ambapo majibu yalikuja akaambiwa ameathirika hivyo akapewa dawa za kuanza kutumia.

Anasema mwaka 2012 alijifungua mtoto wake wa kwanza na 2017 akajifungua mtoto wake wa pili, lakini mwezi mmoja tu baada ya kujifungua mtoto wa pili, ngozi yake ikaanza kubadilika rangi kuwa ya njano.

Anasema alirudishwa kituo husika cha afya kisha baadaye alikwenda Hospital ya Rufaa ya Mbarara ambapo huko alifanyiwa vipimo upya kwa kina na kuonekana hana Virusi Vya Ukimwi bali ogani zake muhimu figo na ini hazifanyi kazi vizuri kama kawaida na sababu ikiwa ni dawa hizo za Virusi Vya Ukimwi alizopewa kutumia kwa miaka 6 kuanza kumletea madhara (side effects).

Mwaka 2018 alifungua kesi dhidi ya Serikali kuhusu kituo husika cha afya kumsingizia kuwa ameathirika ambapo hadi sasa takriban miaka 4 kesi haijasikilizwa hata mara moja licha ya kuwa ilifika mahakamani tangu muda huo.

Kituo husika kilichompakazia Faridah kuwa ana ‘ngoma’, daktari alipoulizwa amesema yeye ni mgeni hapo kikazi ana miezi tu, hajui kilichotokea muda huo kwani hakuwepo.

Kwa upande wa mahakama wanasema jaji husika aliyekuwa asikilize kesi hiyo alistaafu hivyo anasubiriwa jaji mwingine.

Stori: Sifael Paul
Global Publishers 
Share:

TARURA YALETA FARAJA KWA WANANCHI MOMBA



Wananchi Wilayani Momba, Songwe wanefarijika baada ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa daraja la muda katika mto Nkana Kata ya Chilulumo.


Hatua hiyo imechukuliwa baada ya daraja la awali kuvunjika na kusababisha mawasiliano ya Kata za Chilulumo,Nkulwe,Kamsamba,Mkomba Ivuna na makao makuu ya Wilaya ya Momba kukatika.



Akitoa taarifa kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA, wakati wa ziara yao mkoani Songwe, Meneja wa TARURA Mkoa wa Songwe Mhandisi Killian Haule alisema kuwa TARURA kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Songwe,Jeshii la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamejipanga kurejesha mawasiliano ndani ya muda mfupi kwa kujenga daraja la chuma (TRUSS Bridge) ili wananchi wapate huduma ya Usafiri na Usafirishaji.



Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Mhandisi Florian Kabaka amesema kuwa daraja hilo ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi na amewataka wananchi kulitunza pindi litakapo kamilika.


Mkurugenzi wa barabara kutoka TARURA Mhandisi Venant Komba ameeleza kuwa licha ya ujenzi wa daraja la muda, TARURA inafanya maandalizi ya ujenzi wa Daraja la kudumu katika mto Nkana.


"Maandalizi ya ujenzi wa daraja la kudumu hapa mto Nkana yanaendelea maana eneo hili ni muhimu sana kwa wananchii ili kuwawezesha kusafirisha mazao hasa zao la mpunga,” alisema mhandisi Komba.


Kwa upande wake Mhe. Sabasi Semfukwe, diwani wa kata ya Chitete alisema kuwa walikuwa wanapata changamoto kubwa sana kutokana daraja kuvunjia, kwa kuzingatia kuwa njia hiyo ni ya kimkakati kwa ukuaji wa uchumi wa maeneo yao.


“ Tumefarijika sana sababu kujengwa kwa daraja hili kwetu ni kufungua ukuaji wa kiuchumi kwa kusafisha mazao yetu. Mawasiliano sasa yatakuwepo na itaongeza tija kwa wananchi katika maswala ya uzalishaji,” alisema Mhe. Semfukwe.


Naye Rehema Kipubile mkazi wa Kanyala alisema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwaletea daraja hilo kwani wamepata tabu sana baada ya mawasiliano kukatika kuzifikia huduma muhimu za kijamii.


“Sisi wakinamama hasa tukiwa wajawazito tumepata tabu sana kuvuka hapa kwenda hospitali, tunashukuru sana kwa daraja hili jipya linalojengwa tutapata nafuu, “ alisema Rehema


Bodi ya Ushauri ya TARURA imekamilisha ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi katika Mikoa ya Iringa,Mbeya na Songwe ambapo imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi na kuleta matokeo chanya ndani ya kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa wakala
Share:

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA BANDA LA TVLA MAONESHO YA MIFUGO KIBIASHARA CHALINZE

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba M. Ndaki (MB) akipata maelezo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kutoka kwa Afisa Utafiti Mifugo wa TVLA Ndg. Msafiri S. Kalloka kwenye uzinduzi wa maonesho ya Mifugo kibiashara yaliyofanyika kwenye uwanja wa maonesho Highland Estate LTD, Ubena Zomozi, Chalinze Julai 15, 2022.Ndg. Msafiri S. Kalloka Afisa Utafiti Mifugo wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) akitoa maelezo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Wakala kwa wanananchi waliotembelea banda la TVLA kwenye uzinduzi wa maonesho ya Mifugo kibiashara yaliyofanyika kwenye uwanja wa maonesho Highland Estate LTD, Ubena Zomozi, Chalinze Julai 15, 2022
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 16,2022













Share:

Friday, 15 July 2022

JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAJIPANGA KUBORESHA USHINDANI KIELIMU

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema hayo jana Jijini Dodoma wakati akiongea kwenye kikao cha Wakuu wa shule za Umoja wa Wazazi jijini Dodoma. 
Na Dotto Kwilasa,DODOMA

JUMUIYA ya Umoja  wa wazazi ,
 Chama  cha Mapinduzi (CCM) imeazimia kuboresha shule zote zinazomilikiwa na Jumuiya hiyo kuwa zenye viwango,vigezo, vipimo  na utofauti ili kuingia kwenye ubora wa ushindani sawa na shule nyingine.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akiongea kwenye kikao cha Wakuu wa shule za Umoja wa Jumuiya ya wazazi Tanzania na kutaka maboresho hayo kuhusisha makundi  kundi yote ikiwemo wanafunzi wenye ufaulu mzuri,ufaulu wa kati na wale wasiojiweza kabisa .

Amesema ili kuendana na malengo ya kuanzisha shule hizo inatakiwa  kila kundi lipewe dozi kulingana na hali halisi
ya madaraja yao na kwamba kila jambo linahitaji msukumu zaidi wa mafanikio .

"Sasa hivi hatupo tena kwenye giza, 
tunatakiwa kuongeza bidii kwenye haya mafanikio tuliyoyaleta wenyewe
na lazima mfahamu kuwa hakuna muujiza kwenye mafanikio,"ameeleza

Katibu Mkuu huyo pia amesema kulingana na mwenendo  wanaoenda nao shule hizo zinahitaji mabweni hivyo kuweka wazi kuwa yeye kwa nafasi yake atahakikisha anatekeleza jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya walimu na wale wanafunzi wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki.

"Ahadi yangu ipo  palepele kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri zaidi ili kuendana na hadhi ya Jumuiya hii ikiwa ni apamoja na kuongeza madarasa mawili mawili,tutaangalia pia uhitaji wa shule husika hali itakayoongeza ufanisi na  kupekelea shule zetu kuwa kimbilio kwa kila mtu,"amesisitiza Chongolo 

Sambamba na hayo Chongolo ameeleza malengo ya kuanzisha Shule za Jumuiya hiyo kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa elimu kwa wananchi waliokosa fusra kwenye machaguo mbalimbali ya serikali,kupanua wigo na kupata wasomi wengi kwenye nchi na kuongeza kiwango chenye elimu yenye tija nchini.

"Kazi bado haijaisha,tuna kazi nyingine ya ziada,bado lengo kuu la elimu bora na kufanikisha kuendelea liko pale pale 
kufanikisha misingi ya uanzishaji wa shue zetu kwa kuwaandaa na kuwajengea msingi wanafunzi walioshindwa na wale wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki,"amesema Katibu huyo

"Tumewapa jukumu hili la kuboresha mazingira ya elimu,nendeni  mkalifanye kwa dhamira ya dhati,mengi mmefanya kwa kujitolea,mafanikio yanatafutwa na ili kufanikiwa lazima uweke juhudi zako ninyi ni watu wa msukuko tambueni heshima ya Mwalimu ni matokea,ukitaka kuheshimiwa tengeneza matokeo yako vizuri,"amesema na kuongeza;

Heshima ni gharama,na ninyi mmeonesha namna mnavyodhamiria kuitafuta heshima kwa gharama yoyote,sina shaka dhamira yenu ni kujaza kibaba"amesisitiza

Katibu huyo pia alitoa wito kwa Wakuu wa Shule  hizo za Jumuiya ya wazazi kuwapa motisha walimu na wanafunzi ili kufanya vizuri zaidi na kwamba awamu ijayo hawatatoa zawadi kwa usawa bali  watatoa kutokana na ushindi wa matokeo 

"Tutatumia ushindani wa vigezo,vipimo, viwango na utofauti,tusilazimishe mambo makubwa tuendelee kuweka msukumo na viwango vyetu  ili tupate ubora tunautaka,"amesisitiza

Pamoja na hayo Katibu huyo Mkuu wa CCM ametumia nafasi hiyo kuwataka Wakuu hao kupenda kufanya kazi kwenye mazingira yanayohitaji mafanikio na kukemea tabia ya baadhi ya walimu kutamani shule zilizofanikiwa.

"Mwalimu mwenye uwezo apelekwe kwenye shule inayohitaji mafanikio,hali hiyo itawaheshimisha walimu,kila mtu atafute mafanikio ya shule yake nisione mtu anataka kuhamia shule yenye mafanikio waliyoyaanzisha wenzie  wakati yeye ameshindwa huo ni ubinafsi mkubwa,"amesema

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi taifa Dkt.Edmund Mndolwa ametumia  nafasi hiyo kuwataka Wakuu wa Shule hizo kuacha kuingiza siasa kwenye Jumuiya hiyo huku akiwataka kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadali na uzalendo.

"Siasa ina mahali pake hatupaswi kuiingiza kwenye utendaji,lazima tujue kutofautisha vitu hivi,najua kuna wakati mnafanyia kazi katika mazingira magumu lakini msikate tamaa ili muendelee kuijenga heshima yenu,"amesema

Amesema shule za wazazi nchini kwa sasa zina utulivu wa kutosha tofauti na ilivyokuwa mwanzo na kueleza kuwa hali hiyo imetokana na maelekezo ya uongozi uliopo na kufanya matokeo mazuri 
kwa shule zote za wazazi licha ya wanafunzi waliopo ni wale wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki.


Mwishoo



 Kwilasa ,DODOMA

JUMUIYA ya Umoja  wa wazazi ,
 Chama  cha Mapinduzi (CCM) imeazimia kuboresha shule zote zinazomilikiwa na Jumuiya hiyo kuwa zenye viwango,vigezo, vipimo  na utofauti ili kuingia kwenye ubora wa ushindani sawa na shule nyingine.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema hayo jana Jijini Dodoma wakati akiongea kwenye kikao cha Wakuu wa shule za Umoja wa Jumuiya ya wazazi Tanzania na kutaka maboresho hayo kuhusisha makundi  kundi yote ikiwemo wanafunzi wenye ufaulu mzuri,ufaulu wa kati na wale wasiojiweza kabisa .

Alisema ili kuendana na malengo ya kuanzisha shule hizo inatakiwa  kila kundi lipewe dozi kulingana na hali halisi
ya madaraja yao na kwamba kila jambo linahitaji msukumu zaidi wa mafanikio .

"Sasa hivi hatupo tena kwenye giza, 
tunatakiwa kuongeza bidii kwenye haya mafanikio tuliyoyaleta wenyewe
na lazima mfahamu kuwa hakuna muujiza kwenye mafanikio,"ameeleza

Katibu Mkuu huyo pia alisema kulingana na mwenendo  wanaoenda nao shule hizo zinahitaji mabweni hivyo kuweka wazi kuwa yeye kwa nafasi yake atahakikisha anatekeleza jambo hilo ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira ya walimu na wale wanafunzi wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki.

"Ahadi yangu ipo  palepele kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri zaidi ili kuendana na hadhi ya Jumuiya hii ikiwa ni apamoja na kuongeza madarasa mawili mawili,tutaangalia pia uhitaji wa shule husika hali itakayoongeza ufanisi na  kupekelea shule zetu kuwa kimbilio kwa kila mtu,"amesisitiza Chongolo 

Sambamba na hayo Chongolo ameeleza malengo ya kuanzisha Shule za Jumuiya hiyo kuwa ni pamoja na kuongeza wigo wa elimu kwa wananchi waliokosa fusra kwenye machaguo mbalimbali ya serikali,kupanua wigo na kupata wasomi wengi kwenye nchi na kuongeza kiwango chenye elimu yenye tija nchini.

"Kazi bado haijaisha,tuna kazi nyingine ya ziada,bado lengo kuu la elimu bora na kufanikisha kuendelea liko pale pale 
kufanikisha misingi ya uanzishaji wa shue zetu kwa kuwaandaa na kuwajengea msingi wanafunzi walioshindwa na wale wanaodhaniwa kuwa hawafundishiki,"amesema Katibu huyo

"Tumewapa jukumu hili la kuboresha mazingira ya elimu,nendeni  mkalifanye kwa dhamira ya dhati,mengi mmefanya kwa kujitolea,mafanikio yanatafutwa na ili kufanikiwa lazima uweke juhudi zako ninyi ni watu wa msukuko tambueni heshima ya Mwalimu ni matokea,ukitaka kuheshimiwa tengeneza matokeo yako vizuri,"amesema na kuongeza;

Heshima ni gharama,na ninyi mmeonesha namna mnavyodhamiria kuitafuta heshima kwa gharama yoyote,sina shaka dhamira yenu ni kujaza kibaba"amesisitiza

Katibu huyo pia alitoa wito kwa Wakuu wa Shule  hizo za Jumuiya ya wazazi kuwapa motisha walimu na wanafunzi ili kufanya vizuri zaidi na kwamba awamu ijayo hawatatoa zawadi kwa usawa bali  watatoa kutokana na ushindi wa matokeo 

"Tutatumia ushindani wa vigezo,vipimo, viwango na utofauti,tusilazimishe mambo makubwa tuendelee kuweka msukumo na viwango vyetu  ili tupate ubora tunautaka,"amesisitiza

Pamoja na hayo Katibu huyo Mkuu wa CCM ametumia nafasi hiyo kuwataka Wakuu hao kupenda kufanya kazi kwenye mazingira yanayohitaji mafanikio na kukemea tabia ya baadhi ya walimu kutamani shule zilizofanikiwa.

"Mwalimu mwenye uwezo apelekwe kwenye shule inayohitaji mafanikio,hali hiyo itawaheshimisha walimu,kila mtu atafute mafanikio ya shule yake nisione mtu anataka kuhamia shule yenye mafanikio waliyoyaanzisha wenzie  wakati yeye ameshindwa huo ni ubinafsi mkubwa,"amesema

Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi taifa Dkt.Edmund Mndolwa ametumia  nafasi hiyo kuwataka Wakuu wa Shule hizo kuacha kuingiza siasa kwenye Jumuiya hiyo huku akiwataka kufanya kazi kwa kufuata misingi ya maadali na uzalendo.

"Siasa ina mahali pake hatupaswi kuiingiza kwenye utendaji,lazima tujue kutofautisha vitu hivi,najua kuna wakati mnafanyia kazi katika mazingira magumu lakini msikate tamaa ili muendelee kuijenga heshima yenu,"amesema

Amesema shule za wazazi nchini kwa sasa zina utulivu wa kutosha tofauti na ilivyokuwa mwanzo na kueleza kuwa hali hiyo imetokana na maelekezo ya uongozi uliopo na kufanya matokeo mazuri 
kwa shule zote za wazazi licha ya wanafunzi waliopo ni wale wanaodhaniwa kuwa hawafundishika.



Share:

ADAKWA NA TANI MOJA YA BANGI


Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Ramadhani Kingai akitoa maelezo kuhusu kukamatwa kwa madawa ya kulevya aina ya bangi yanayokadiriwa kuwa na uzito wa tani moja yaliyokamatwa kijiji cha Kabulanzwili wilayani Kasulu mkoani Kigoma. (Picha na Fadhili Abdallah)


*****


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Polisi mkoani humo imemtia mbaroni mtu mmoja mkulima na mkazi wa kijiji cha Kabulanzwili wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma akituhumiwa kupatikana na madawa ya kulevya aina ya bangi yanayokadiriwa kuwa na uzito wa tani moja.



Kamanda mkoa Kigoma Ramadhani Kingai akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma alimtaja mtu aliyekamatwa kuwa ni Lije Nicholous maarufu kama Madeberi (48) mkulima na mkazi wa kijiji cha Kabulanzwili wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Kamanda kingai alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa na polisi waliokuwa doria akiwa kwenye harakati za kusafirisha madawa hayo ya kulevya kwenda kuuza ambapo haijalezwa mara moja yalikuwa yakipelekwa wapi.

Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa kwa sasa mtuhumiwa huyo anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mkoa Kigoma sambamba na magunia ya bangi yaliyokamatwa na kwamba upelelezi unaendelea ili kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Katika tukio lingine Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa polisi mkoani humo imewatia mbaroni watu watatu kati ya wanne wanaotuhumiwa kutekeleza mpango wa kumbaka msichana mmoja mwanafunzi katika chuo cha waganga kilichopo mkoa Tanga akiwa mwaka wa kwanza ambapo vijana hao walimbaka msichana huyo kwa wakati mmoja.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Ramadhani Kingai akizungumza mjini Kigoma leo asubuhi aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Julius Yelenimo (25), Hemed Miosho (24), Bakari Hassan (21) na mthumiwa wanne ambaye amekimbia jina lake halikuweza kupatikana.

Maelezo ya Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma yanaeleza kuwa watuhumiwa kwa pamoja walimkamata msichana huyo na kumuingiza ndani ambapo walifungulia muziki kwa sauti kubwa ili kufanya sauti ya msichana huyo kuomba msaada isisikike hivyo kutekeleza kitendo chao na baadaye kukimbia hadi walipotiwa mbaroni na polisi.


Share:

GGML WANG'ARA MAONESHO YA SABASABA, WAIBUKA MUAJIRI BORA







 Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Geita Gold Mine Limited (GGML), imeendelea kung'ara baada ya kuibuka mshindi katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara - Dar es Salaam maarufu kama sabasaba kwa kunyakua tuzo ya muajiri bora na msafirishaji bora wa madini nje ya nchi. 

Pia GGML imepata tuzo ya mlipa kodi bora wa pili na muajiri bora anayezingatia taratibu za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Tuzo zote zimetolewa Julai 13 na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango ( wa pili kulia) na kupokewa na Mwanasheria Mwandamizi wa GGML, David Nzaligo (wa pili kushoto waliosimama nyuma) kwa niaba ya uongozi wa kampuni. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji.
Share:

MGODI WA MWIME WAJENGA SHULE MPYA


Muonekano wa majengo ya shule mpya kijiji cha Mwime.
Jengo la matundu 12, ya choo.
Muonekano wa majengo ya shule mpya kijiji cha Mwime.
Jengo la matundu 12, ya choo.
Meneja wa kikundi cha umoja wa wamiliki wa mashamba Kabela, Joseph Andrea Nalimi.


Na Paul Kayanda -  Kahama

MGODI wa Mwime uliopo Kata ya Zongomela Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga chini ya umoja wa kikundi cha wamiliki wa mashamba (KABELA) wamenunua ekari 5 kwa thamani ya Shilingi Milioni 10 na kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya Msingi.

Kikundi hicho kimechukua uamuzi huo baada ya kuona shule ya Msingi Ilindi iliyopo mtaa wa Mwime kuwa na wingi wa watoto wanaosoma shuleni hapo ambao nni zaidi ya 2000 ukilinganisha asilimia kubwa umoja ya wanakikundi ni wazawa na eneo lao limebarikiwa na Mungu kuwa na Madini ya Dhahabu.

Meneja wa umoja wa wamiliki wa mashamba wa mgodi wa Mwime Joseph Nalimi aliyasema hayo juzi alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari waliotembelea Mgodi huo ili kujionea hali halisi ya maendeleo ya Mtaa wa Mwime kufuatia uwepo wa mgodi huo.


“Baada ya kukaa na serikali ya mtaa huu,tuliona kwenye suala la elimu shule yetu ya msingi imezidiwa sana na wanafunzi,tumejaribu kuwa tunajenga madarasa pale lakini hayawezi kutosha na tukabaini kuwa hata tukijenga madara 50 bado mwalimu mkuu atakuwa na mzigo mzito,” alisema Jeseph Nalimi meneja kikundi na kuongeza.

“Tuliona dawa ni kujenga shule mpya, kwa mana hiyo tukaomba mpango kazi ambapo mgodi tukalinunua eneo kwa gharama ya shilingi Milioni 10, tukalikabidhi kijiji na hati wanayo, wakampa taarifa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ambaye akawapa milioni 120 za madarasa sita,” alisema.

Meneja huyo alisema kuwa mgodi unaunga mkono juhudi za mkurungenzi wa halmashauri kwa kujenga madarasa mawili ili kuongeza pamoja na ofisi mbili za walimu, na wakachimba karo na kujenga boma la choo matundu 12 wasichana 6 na wavulana 6 na kwamba tayari wamemkabidhi mkurugenzi kwa ajili ya umaliziaji.

Pamoja na mambo mengine meneja huyo alisema kuwa waliamua kujenga pia choo cha walimu matundu mawili na kukarabati ofisi ya kijiji kwa kuiezua paa na kuianza kuijenga upya mpaka rangi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ilindi Dogo Mheziwa alipongeza Mgodi huo kupitia kikundi cha umoja wa wamiliki wa mashamba kusaidia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wake huku akisema kuwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya manispaa ya Kahama Anderson Msumba ameunga mkono juhudi za mgodi huo kwa kuchangia shilingi Milioni 120 za umaliziaji katika shule mpya ya msingi Mwime.

Kufuatia hali hiyo Mheziwa alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kuupandisha hadhi mtaa wa Ilindi kuwa Kata ya Mwime badala ya Kata ya Zongomela kutokana na maendeleo kuwa ya kasi kwenye eneo hilo kufuatia uwepo wa mgodi.

“Sensa ya watu na makazi kwa mtaa wa Ilindi na Mwime itasaidia kujua idadi ya watu na kupata Kata, kutoka mtaa wa Ilindi kwenda makao makuu ya Kata Zongomela ni lazima uvuke kata jirani ya Mhungula ndipo ufike kata ya Zongomela naomba serikali iliangalie hilo,” alisema Mheziwa.

Alisema kuwa wananchi wanapata adha ya kupata huduma ya kiofisi huko Zongomela kwani wanatembea umbali mrefu kilomita tatu ndipo unafika makao makuu, kwa wazee wajawazito ni changamoto lakini iwapo serikali itasikia kilio hicho itakuwa imesogeza huduma karibu.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger