• Home
  • About
  • Support
  • Contact
  • Advertise

MASWAYETU BLOG

  • Home
  • Business
    • Internet
    • Market
    • Stock
  • Downloads
    • Dvd
    • Games
    • Software
      • Office
  • Parent Category
    • Child Category 1
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • Featured
  • Health
    • Childcare
    • Doctors
  • Uncategorized
Menu
  • Home
  • Business
    • Internet
    • Market
    • Stock
  • Downloads
    • Dvd
    • Games
    • Software
      • Office
  • Parent Category
    • Child Category 1
      • Sub Child Category 1
      • Sub Child Category 2
      • Sub Child Category 3
    • Child Category 2
    • Child Category 3
    • Child Category 4
  • Featured
  • Health
    • Childcare
    • Doctors
  • Uncategorized

Saturday, 9 July 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JULAI 9,2022

 Unknown     02:51:00     NEWS     No comments   
Magazetini leo Jumamosi July 9,2022

Share:
Read More →

Friday, 8 July 2022

OFISI YA MSAJILI HAZINA YAVUKA LENGO MAKUSANYO YA MAPATO

 Unknown     15:51:00     NEWS     No comments   

************************

Na Mwandishi Maalumu

OFISI ya Msajili wa Hazina (OMH) imefanikiwa kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya jumla ya Sh bilioni 852.98 ikiwa ni asilimia 109.50 ya lengo katika Mwaka wa Fedha wa 2021/22 ulioishia Juni 30, mwaka huu.

Awali, ofisi hiyo inayosimamia Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala za Serikali na Kampuni ambazo Serikali ina hisa, katika mwaka huo ilipangiwa kukusanya Sh bilioni 779.03.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa Umma ya Ofisi ya Msajili wa Hazina iliyosainiwa na Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto, kiasi kilichokusanywa ni ongezeko la Sh bilioni 214.11 kutoka Sh bilioni 638.87 zilizokusanywa mwaka 2020/21 ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia 33.50.

Benedicto katika taarifa hiyo amesema ongezeko hilo ni matokeo ya kuimarika kwa shughuli mbalimbali za uchumi chini ya uongozi madhubuti wa Rais Samia Suluhu Hassan ambao umechochea uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini.

Alisema sababu nyingine ni uhusiano mzuri kati ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na Taasisi zote inazozisimamia; kudhibiti matumizi pamoja na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma.

Ofisi ya Msajili wa Hazina inayosimamia taasisi, mashirika ya umma, wakala za serikali na kampuni ambazo Serikali ina hisa pamoja na kupongeza kwa upatikanaji wa fedha hizo zinazokwenda kufanyakazi kuleta maendeleo ya nchi kwa kuchangia katika Mfuko Mkuu wa Serikali na hatimaye ukuaji wa uchumi wa Taifa, wameendelea kukumbusha uzingativu wa dhima ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 ambayo ni “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”.

Aidha, imetaka kuzingatiwa kwa dhima kuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2022/23 ambayo ni “Kuongeza Kasi ya Kufufua Uchumi na Kuimarisha Sekta za Uzalishaji kwa ajili ya Kuboresha Maisha”.

"Ofisi ina matumaini makubwa kwa Taasisi, Mashirika ya Umma, Wakala za Serikali na Kampuni ambazo Serikali ina hisa katika kuboresha utoaji huduma, kukuza biashara na kuhakikisha kuna tija kwenye utekelezaji wa shughuli zao zote," ilisema sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Benedicto.



Alisema ofisi yake itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu uwekezaji wa serikali kwenye taasisi, mashirika ya umma na kampuni ambazo serikali ina hisa pamoja na kuishauri serikali kuhusu uwekezaji kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za serikali.

Alitaka menejimenti zote kutambua kuwa “Uwekezaji ni Msingi wa Maendeleo Endelevu” na kuendelea kuchagiza maendeleo kwa fikra hizo.

Ofisi ya Msajili wa Hazina ndiyo msimamizi mkuu wa uwekezaji wa Serikali kwa niaba ya Rais na imekuwa pia na jukumu la kusimamia Ubinafsishaji wa Mali za Umma, Usimamizi na Ufuatiliaji wa Mashirika ya Umma, Ukusanyaji wa Madeni ya Serikali yaliyorithiwa kutoka kwa lililokuwa Shirika Hodhi la Mali za Mashirika ya Umma (CHC), na Urekebishaji na Ufilisi wa Mali zisizozalisha faida katika kampuni au mashirika yaliyobinafsishwa.

Kwa sasa, Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia Taasisi na Mashirika ya Umma 287, ikijumuisha kampuni na Taasisi 40 zinazomilikiwa na Serikali kwa hisa chache na Taasisi 10 za nje ya nchi 10.
Share:
Read More →

MISA TANZANIA YAKUTANA NA WAHARIRI…JESSE KWAYU ATAKA KELELE MAREKEBISHO SHERIA KANDAMIZI

 Unknown     13:51:00     NEWS     No comments   

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali za vyombo vya habari kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.


Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu amewataka waandishi wa habari nchini Tanzania kuungana na kuendelea kusukuma  mabadiliko ya vifungu mbalimbali vya sheria zinazosimami taaluma ya uandishi wa habari,ambavyo vinaminya utendaji na ukuaji wa vyombo vya habari.

Aidha, amewataka kuzisoma mara kwa mara sheria hizo,kutoa maoni yao kwenye mchakato wa mabadiliko uliopo sasa,kwani kwa kufanya hivyo ni kuonyesha kujali na kwa kiasi gani jambo linawagusa.


Kwayu ametoa rai hiyo leo Ijumaa Julai 8,2022 Jijini Dar es salaam wakati wa Semina kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu sheria mbalimbali za habari za vyombo vya habari nchini Tanzania, yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Jangwa la Sahara (Media Institute of Southern Africa,Tawi la Tanzania (MISA Tanzania) kwa Kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wananchi nchini (TAMWA) kupitia Mradi wa International Media Support - IMS.


Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo Wahariri wa Habari kutambua na kuchambua sheria hizo pamoja na kutoa maoni yao.


Kwa mujibu wa Kwayu, baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari , Sheria ya Takwimu na Sheria ya Udhibiti wa Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA), zinaminya uhuru wa kujieleza, upatikanaji wa taarifa na ukuaji wa vyombo vya habari nchini na kwamba zinahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuwa rafiki kwa maendeleo ya nchi.


 "Ukishakuwa na sheria mbaya huwezi jua saa ngapi itakukamata. Tusilale tusome, tupige kelele kuhusu sheria zinazotukandamiza, hizi sheria bado hazijarekebishwa,tupo kwenye mchakato ambao ni lazima tushiriki kwa kuwa inakuhusu,"amesema.


"Sheria hizi zina mamlaka makubwa sana, mfano Sheria ya EPOCA ni kubwa, inatugusa katika maisha yetu ya kila siku, kelele za kufanyia marekebisho sheria hii ziendelee kila siku. Tuna wajibu wa kupaza sauti kujitetea wenyewe juu ya sheria hizo ili pale inapowezekana ziweze kufanyiwa marekebisho ili zisiwe mwiba kwa wanahabari na vyombo vya habari", ameongeza Kwayu.


Katika hatua nyingine Kwayu amewasisitiza waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kutetea haki zao na kutetea za wananchi katika jamii, kwa kuwa wengi wamezikosa kwa kutozitambua jambo ambalo siyo sahihi.


“Waandishi wa habari ni watetezi wa haki za binadamu. Jambo linaloumiza mtu wewe mwandishi wa habari lazima likukere . Kama mwandishi wa habari hukereketwi na jambo la jamii achana na kazi ya uandishi wa habari kafanye kazi nyingine,ni lazima mjisimamie na kuwa tayari kusaidia mtu au jamii inapoumizwa”,amesema Kwayu ambaye alikuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben  amewataka waandishi wa habari kuona umuhimu wa kuzingatia utekelezaji wa masuala ya jinsia kwa kuzingatia masuala ya usawa wa kijinsia wanapoandika habari zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu Haki na Uhuru wa Kujieleza kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA leo Ijumaa Julai 8,2022 jijini Dar es salaam. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali za vyombo vya habari kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA leo Ijumaa Julai 8,2022 jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Brain Incorperated Ltd, Jesse Kwayu akitoa mada kuhusu sheria mbalimbali za vyombo vya habari kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA leo Ijumaa Julai 8,2022 jijini Dar es salaam.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben akitoa mada kuhusu masuala ya kijinsia kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mkurugenzi wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben akitoa mada kuhusu masuala ya kijinsia kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Mshauir wa Vyombo vya Habari/ Mkufunzi, Rose Haji Mwalimu akizungumza kwenye semina kwa Wahariri wa Habari iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.
Wahariri wa Habari  wakiwa kwenye semina iliyoandaliwa MISA Tanzania kwa kushirikiana na TAMWA.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Share:
Read More →

KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA UDAHILI KWA WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA KATIKA TAASISI ZA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2022/2023

 Unknown     13:51:00     NEWS     No comments   



Share:
Read More →

DIWANI AFARIKI GHAFLA MSIKITINI

 Unknown     11:51:00     NEWS     No comments   


CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepata pigo kufuatia Diwani wake wa Kata ya Mahohe Mohamed Ngonde, kufariki leo alfajiri.


Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Busoro Pazi, alisema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki akiwa katika Ibada ya alfajiri leo Julai 8, 2022 akiwa ibadani msikitini.


Katibu wa Madiwani Busoro Pazi amesema taratibu za mazishi bado kila wakati atakuwa anatoa taarifa baada kukaa na familia ya marehemu.


"Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana "amesema Busoro.


Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde amesema taarifa za Kifo cha MH, Diwani wake Mohamed Ngonde alifariki na taarifa alitoa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo amesema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki ghafla.


Mwenezi CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde amesema kila wakati taarifa kamili zitatolewa kuhusiana na msiba huo mzito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wana CCM kwa ujumla.


Alhaj Said Sidde,pia ongeza kuwa alimwelezea Mh Ngonde kuwa kada mahiri aliyekitumikia chama cha Mapinduzi kwa muda mrefu na kushikilia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti serikali ya mtaa Kichangani ,Majohe
Share:
Read More →

MWALIMU BENKI YAENDELEA KUTOA MIKOPO SABASABA

 Unknown     10:51:00     NEWS     No comments   
Mkuu wa Kitengo Cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Benki ya Mwalimu (MCB), Bi.Leticia Ndongole akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya wananchi wakipata huduma kwenye banda la Mwalimu Benki mara baada ya kutembelea banda hilo katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam Watumishi wa Mwalimu Benki wakipata picha ya pamoja katika banda lao kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam

****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANANCHI wameendelea kutembelea banda la Mwalimu Benki katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo mpaka sasa wameshawahudumia watanzania 50 waliotembelea banda hilo.

Akizungumza katika maonesho hayo leo Julai 7,2022 Mkuu wa Kitengo Cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Benki ya Mwalimu (MCB), Bi.Leticia Ndongole amesema wanatarajia idadi ya wakopaji na wateja wapya itaongezeka kwa kuwa huduma zinatolewa kwa watu wote.

“Tunaposema huduma tunatoa kwa watu wote maana yake ni walimu, wafanyabiashara, wanafunzi wa vyuo, wakulima, wafugaji, wasafirishaji, vijana na wazee... hatuachi mtu. Tunafungua akaunti za aina mbalimbali kwa hapa tumefungua akaunti 35 hivyo tunawakaribisha wote kuja kupata huduma zetu bora kwenye sekta ya benki". Amesema Bi.Leticia.

Aidha Bi.Leticia amesema wanatoa huduma kwenye mikoa yote hapa nchini kwenye matawi na kidijitali kupitia mawakala wa Mwalimu Benki, Mwalimu Mobile na Mwalimu Visa Card pia wateja wao hupata huduma zote za bima na mikopo ya vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Pamoja na hayo amewakaribisha wananchi kwa ujumla kutembelea banda lao kwaajili ya kupata huduma za kibenki hasa mikopo ambayo itawasaidia kujiinua kiuchumi binafsi na taifa kwa ujumla.
Share:
Read More →

MCHENGERWA ATEMA CHECHE KWENYE USIKU WA MASTAA WA SOKA

 Unknown     09:51:00     NEWS     No comments   

********

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amevitaka vilabu vya michezo kufanya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kujenga miundombinu ili kuinua michezo.

Mhe. Mchengerwa ametoa kauli leo Julai 7, 2022 kwenye usiku wa utoaji wa Tuzo za Mashindano ya NBC ya Shirikisho la soka nchini 2022.

Ameambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu Saidi Yakubu na watendaji wa sekta ya michezo.

Katika tukio hili lililovuta hisia za wanamichezo ndani na nje ya nchi tuzo 43 katika maeneo mbalimbali zinatolewa huku tukio hilo likirushwa mubashara na kituo cha televisheni cha Azam na mitandao mbalimbali ya kijamii kutokea jijini Dar es Salaam.

Mhe amesisitiza kuwa wakati umefika wa Vilabu vya Tanzania kumiliki viwanja vyao kama vilabu vingine duniani ambapo ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa(BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuratibu kikao baina yake na viongozi wa vilabu mapema juma lijalo ili kujadili utekelezaji wa suala hilo.

"Ninaagiza BMT na TFF wiki ijayo ratibuni kikao na viongozi wa vilabu tulimalize suala hili." Amesisitiza Mhe Mchengerwa

Aidha, amewataka viongozi wa vilabu kuzingatia maadili na kuachana na vitendo vya ukiukaji wa maadali ambapo amefafanua kwamba vilabu haviwezi kupiga hatua katika michezo endapo havitazingatia suala hilo.

" Wenzetu wanafanikiwa sana kwenye michezo kwa kuwa wanazingatia maadili" ameongeza, Mhe. Mchengerwa

Amelitaka BMT kuchukua hatua kali kwa yoyote atakaye bainika kuvunja maadili.

Pia amesema Serikali inatarajia kujenga viwanja vya michezo ya ndani na sanaa eneo la Kawe ambapo amesisitiza baada ya kukamilika utoaji wa tuzo kwa mwaka ujao utafanyika katika kumbi hizo za kisasa.

Ameongeza kuwa dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuifanya michezo kuwa uchumi.

Amesema kwa Serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kukarabati viwanja sita nchini ambapo amefafanua kuwa lengo ni kuandaa mashindano ya soka ya AFCON.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kwa maono yake makubwa ya kuendeleza michezo nchini.
Share:
Read More →
← Newer Posts Older Posts → Home
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

  • MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
    Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa na watu wengi,ni kuhusu ...
  • UPDATED:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
    Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa m...
  • NECTA:HAYA HAPA MATOKEO DARASA LA SABA 2017
    NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2017 EXAMINATION RESULTS ANGALIA MATOKEO YAKO KWA KUBONYEZA MKOA WAKO HAPO CHINI, ...
  • MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 10,027 WALIOKOSEA KUJAZA FORM ZA MIKOPO BODI YA MIKOPO 2016/2017
      KUONA MAJINA HAYO   << BONYEZA HAPA--PDF >>
  • BREAKING NEWS:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MWAKA WA MASOMO 2016/2017
      Bodi ya mikopo ya elimu ya juu wametangaza majina ZAIDI YA 20000 ya wanafunzi waliopata mkopo 2016/2017. Kama utahitaji kuangaliziwa j...
  • MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
    Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa ma...
  • MPYA:HAYA HAPA MAJINA (KATIKA PDF) WANAFUNZI SPECIAL DIPLOMA WALIOPANGIWA KURUDI UDOM &VYUO VINGINE 2016
    >>> CLICK HERE FOR LIST OF SELECTED STUDENT - UDOM (53.28 kB)<<<  CLICK HERE FOR LIST OF SELECTED STUDENTS - TEACHER ...
  • ANGALIA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWAPAMOJA NA APPLICATIONS FOR ADMISSION INTO NON DEGREE (DIPLOMA AND CERTIFICATE) PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017-NACTE
                      Nacte wametoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kuchaguliwa  katika vyuo mbalimbali  afya,ualimu ,kil...
  • MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017
    Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa ma...

Unordered List

Pages

Blog Archive

  • ▼  2026 (72)
    • ▼  January (72)
      • WAZIRI MKENDA AWAAGA VIJANA 16 WANAOKWENDA KUSOMEA...
      • NITASIMAMIA KILA MWANANCHI MWENYE UHALALI WA KUMIL...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 30, 2026
      • SERIKALI YATOA MIKOPO KIASI CHA SHILINGI MILION...
      • KIJANA APITIA MATESO MAZITO LAKINI AKAJA KUWA MTU ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 28,2026
      • TWIGA, TANGA CEMENT WAPEWA SAA 48 KUJISALIMISHA
      • WAASISI CCM RUVUMA WATOA WITO WA KUZINGATIA KATIBA...
      • CCM MIAKA 49: WAZAZI WAONGOZA MAPAMBANO YA UTUNZAJ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 27,2026
      • WAKULIMA TABORA WALALAMIKIA UPUNGUFU WA TAARIFA ZA...
      • RAIS SAMIA AMEIMARISHA UCHUMI GEITA KUPITIA UJENZI...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 25,2026
      • MV NEW MWANZA: MKOMBOZI WA UCHUMI NA BIASHARA KAND...
      • BILIONI 67 ZIMETUMIKA KUJENGA BARABARA NA MASOKO M...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 24, 2026
      • TUTACHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA TAARIFA BIN...
      • MASLAHI YA TAIFA KWANZA: MAPINDUZI YA KIFIKRA NA K...
      • ILALA TUNAJIVUNIA RAIS SAMIA, AMETULETEA MAENDELEO...
      • WANANCHI WA UKONGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUDUM...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 22,2026
      • Tanzia : MUASISI NA MWENYEKITI WA KWANZA WA CHADEM...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 21, 2026
      • KANISA LA MLIMA WA MOTO LAZINDUA MAOMBEZI YA KUIOM...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 20,2026
      • HUWEZI KUISHIWA PAWA UKIPANDA MLIMA LOLMALASIN
      • SIMBA WA TERANGA WANG’ARA MOROCCO, WANYAKUA UBINGW...
      • WANA SANTA RC BUNJU WAPIGWA MSASA MATUMIZI SAHIHI ...
      • SAUTI ZA WANANCHI: AMANI NDIO MSINGI WA MAENDELEO ...
      • WAZIRI AWESO ATAKA KAZI ZIFANYIKE USIKU NA MCHANA ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 18,2026
      • MCHINJITA AONYA SIASA ZA MIHEMKO, APINGA MIITO YA ...
      • VIJANA 5,746 WACHAGULIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UA...
      • WATUMISHI WAPYA TASAC WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 17,2026
      • HAPA KUNA MKAKATI PEKEE UNAOWEZA KUIFANYA BIASHARA...
      • WANANCHI MSATA WAFAIDIKA NA ZOEZI LA MEDANI LA EX...
      • KWA NINI UNAPOTEZA KAZI KILA MARA? USILAUMU UZEMBE...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 15, 2026
      • INAMAANISHA NINI WAKATI HUWEZI KUSHIKILIA KAZI KWA...
      • YANGA BINGWA MAPINDUZI CUP
      • MTOTO WANGU ALICHELEWA KUTEMBEA NA KUONGEA HATUA M...
      • WANAOSEMA 'SAMIA MUST GO' AKITOKA UNAMUWEKA NANI P...
      • MWANAMKE HUYU ANASIMULIA JINSI MGANGA WA JADI ALIV...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 13,2026
      • Tanzania: IPTL's Patience Pays Off in $168m Disput...
      • BILIONI 6.7 KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO KAHAMA
      • PROF. MKENDA AIPONGEZA LALJI FOUNDATION KUUNGA MKO...
      • MAKAMU WA PILI WA RAIS KUZINDUA MASHINDANO MAKUBWA...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 9,2026
      • SERIKALI IMEFANIKISHA AJIRA 1400 NJE YA NCHI: SANGU
      • KILA MTU NILIYEMWAMINI ALIISHIA KUNISALITI, HADI N...
      • HAPPY BIRTHDAY MALUNDE!
      • VETA MOSHI YATAJWA MFANO WA MAFANIKIO YA ELIMU YA ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JANUARI 8, 2026
      • KILA MTU NILIYEMWAMINI ALIISHIA KUNISALITI, HADI N...
      • SERIKALI YASEMA BARRICK NI MFANO WA KUIGWA KWA KUW...
      • START NEW YEAR 2026 WITH GOOD NEWS DOING BUSINESS ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 7,2026
      • RAIS MSTAAFU WA DKT. KIKWETE, AZINDUA JENGO LA AFI...
      • RAIS MSTAAFU WA DKT. KIKWETE, AZINDUA JENGO LA AFI...
      • CHADEMA WAJIFUNZE KUTOKA KITABU CHA HESABU: KUKIRI...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 5,2026
      • SH MILIONI 500 ZA RAIS SAMIA KWA TAIFA STARS NI UW...
      • TAHADHARI: ‘UTANDAWAZI NI CHUI’, TUJILINDE NA UTEK...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 4,2025
      • SHAMRASHAMRA ZA MWAKA MPYA 2026: AMANI YA TANZANIA...
      • CHIKAMBO AKAGUA MIUNDOMBINU KOROFI MASONYA TARURA ...
      • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 3,2026
      • WANANCHI KIJIJI CHA LAJA WILAYANI KARATU WAISHUKUR...
      • WAKAZI WA JIJI LA DODOMA WAKISHEREHEKEA MWAKA MPYA...
      • DC NKINDA ACHUKUA HATUA ZA HARAKA KUTATUA KERO YA ...
  • ►  2025 (993)
    • ►  December (73)
    • ►  November (67)
    • ►  October (72)
    • ►  September (92)
    • ►  August (82)
    • ►  July (84)
    • ►  June (76)
    • ►  May (92)
    • ►  April (86)
    • ►  March (91)
    • ►  February (83)
    • ►  January (95)
  • ►  2024 (1017)
    • ►  December (89)
    • ►  November (89)
    • ►  October (73)
    • ►  September (94)
    • ►  August (86)
    • ►  July (85)
    • ►  June (86)
    • ►  May (94)
    • ►  April (92)
    • ►  March (101)
    • ►  February (30)
    • ►  January (98)
  • ►  2023 (1772)
    • ►  December (99)
    • ►  November (101)
    • ►  October (130)
    • ►  September (102)
    • ►  August (150)
    • ►  July (162)
    • ►  June (165)
    • ►  May (178)
    • ►  April (172)
    • ►  March (188)
    • ►  February (162)
    • ►  January (163)
  • ►  2022 (1846)
    • ►  December (173)
    • ►  November (161)
    • ►  October (190)
    • ►  September (188)
    • ►  August (185)
    • ►  July (146)
    • ►  June (116)
    • ►  May (130)
    • ►  April (126)
    • ►  March (120)
    • ►  February (136)
    • ►  January (175)
  • ►  2021 (7035)
    • ►  December (284)
    • ►  November (598)
    • ►  October (641)
    • ►  September (638)
    • ►  August (619)
    • ►  July (616)
    • ►  June (617)
    • ►  May (637)
    • ►  April (581)
    • ►  March (621)
    • ►  February (539)
    • ►  January (644)
  • ►  2020 (7392)
    • ►  December (597)
    • ►  November (589)
    • ►  October (586)
    • ►  September (618)
    • ►  August (680)
    • ►  July (625)
    • ►  June (614)
    • ►  May (591)
    • ►  April (606)
    • ►  March (632)
    • ►  February (624)
    • ►  January (630)
  • ►  2019 (7895)
    • ►  December (611)
    • ►  November (643)
    • ►  October (673)
    • ►  September (664)
    • ►  August (679)
    • ►  July (677)
    • ►  June (619)
    • ►  May (725)
    • ►  April (622)
    • ►  March (477)
    • ►  February (604)
    • ►  January (901)
  • ►  2018 (409)
    • ►  December (388)
    • ►  August (1)
    • ►  July (1)
    • ►  June (2)
    • ►  May (2)
    • ►  April (7)
    • ►  March (2)
    • ►  February (1)
    • ►  January (5)
  • ►  2017 (450)
    • ►  December (1)
    • ►  November (1)
    • ►  October (119)
    • ►  September (7)
    • ►  August (2)
    • ►  July (10)
    • ►  June (23)
    • ►  May (28)
    • ►  April (39)
    • ►  March (16)
    • ►  February (77)
    • ►  January (127)
  • ►  2016 (2803)
    • ►  December (246)
    • ►  November (198)
    • ►  October (274)
    • ►  September (286)
    • ►  August (251)
    • ►  July (233)
    • ►  June (260)
    • ►  May (309)
    • ►  April (210)
    • ►  March (233)
    • ►  February (264)
    • ►  January (39)
  • ►  2015 (1416)
    • ►  December (24)
    • ►  November (102)
    • ►  October (186)
    • ►  September (89)
    • ►  August (80)
    • ►  July (229)
    • ►  June (197)
    • ►  May (61)
    • ►  April (266)
    • ►  March (105)
    • ►  February (50)
    • ►  January (27)
  • ►  2014 (1347)
    • ►  December (21)
    • ►  November (33)
    • ►  October (51)
    • ►  September (43)
    • ►  August (40)
    • ►  July (202)
    • ►  June (287)
    • ►  May (328)
    • ►  April (159)
    • ►  March (61)
    • ►  February (118)
    • ►  January (4)

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger