Friday, 1 July 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI MOSI, 2022

Share:

Thursday, 30 June 2022

OJADACT YAADHIMISHA SIKU YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA NA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

Mwandishi wetu - Mwanza.

Chama Cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT )kwa kushirikiana na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeadhimisha siku ya kupiga vita dawa za kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu kwa kuwahimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuielimisha jamii athari za dawa za kulevya.

Mgeni rasmi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesisitiza waandishi wa habari kuwa daraja la kuelimisha jamii juu ya athari za dawa.

Dkt. Rutachunzibwa pia ameishukuru OJADACT kwa kuandaa maadhikisho hayo kwa kuwaleta waandishi pamoja na kuwapitisha kwenye kujifunza athari za dawa za kulevya na kusema kitendo cha OJADCT kuwepo Mwanza kunasaidia kwenye mapambano ya dawa za kulevya.

Mwenyekiti wa OJADACT Bwana Edwin Soko amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni tukubaliane na dawa za kulevya kwa ustawi wa jamii itumike kwenye kuielimisha jamii juu ya athari za dawa za kulevya nchini.

Pia mtoa mada Dkt. Eunice Masangu amesema kuwa, kwa sasa hospitali ya Mkoa ya Sekeouture inatoa huduma ya methadone kwa watumiaji wa dawa za kulevya za iroine kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

OJADACT inajikita kwenye mapambano ya dawa za kulevya nchini hivyo kila mwaka inaadhimisha siku hiyo.

Share:

Wednesday, 29 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JUNI 30,2022

Share:

NAIBU WAZIRI MASANJA AKUTANA NA WATENDAJI WA KAMPUNI YA REO YA HONGKONG YA UTANGAZAJI WA MAENEO YA UWEKEZAJI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watendaji wa kampuni ya REO Communications kuhusu kutangaza maeneo ya uwekezaji ya kitalii jijini Dodoma leo.

***********************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa Kampuni ya REO Communications kutoka Hongkong inayojishughulisha na utangazaji wa maeneo ya uwekezaji ya nchi mbalimbali barani Afrika kwa njia ya majarida.

Kikao hicho kimefanyika leo Juni 29, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.

Mhe. Masanja amewapongeza watendaji hao kwa nia nzuri ya kutaka kutangaza maeneo ya uwekezaji pamoja na vivutio vya utalii vya Tanzania.

Aidha , ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanafanikiwa katika adhima hiyo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya REO Communications nchini Tanzania, Xhovana Kelmendi alisema lengo ni kuhakikisha wanatangaza maeneo ya uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Utalii, Kilimo na Madini.

Amesema wameshafanikiwa kutangaza maeneo ya uwekezaji katika nchi ya Indonesia na wana miradi ya aina hiyo ambayo inaendelea katika nchi za Kuwait, Morocco, Nigeria, Malta na Tokyo.

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya kukutana na wadau wa Sekta ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka.
Share:

MAFUNZO YA UJUZI TEPE KWA MAKUNDI MAALUMU YA VIJANA YAZINDULIWA RASMI SHINYANGA…WAPEWA MBINU ZA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza wakati akizindua Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.

Na Chiku Makwai Shinyanga.

OFISI ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), imetoa mafunzo ya ujuzi tepe (Soft Skills) kwa makundi maalumu ya vijana, wakiwamo wenye ulemavu, wamama wadogo (Young Mothers) na wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU) katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuwawezesha kujitambua na kujitathmini.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo vijana takribani 75 wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo ujasiriamali usimamizi wa biashara, kujitambua, Afya ya uzazi na ujinsia.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu (Juni 28,2022 hadi Juni 30,2022, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata amesema suala la vijana kutokuwa na elimu ya ujuzi tepe, limekuwa likisababisha vijana kukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwamo za kiuchumi, kiafya pamoja na kupata mimba katika umri mdogo na kupoteza dira ya maisha yao.

Amesema kuwa mafunzo hayo ya ujuzi tepe yatakuwa msaada mkubwa kwa vijana hao katika kujitambua, na kufanya maamuzi sahihi juu ya masuala mbalimbali katika maisha yao na kuweza kuzifikia ndoto zao.

Aidha ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuanzisha Programu ya kutoa Mafunzo ya Ujuzi tepe kwa makundi maalumu ya vijana ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa maisha ya vijana.

“Programu hii ya ujuzi tepe ni muhimu sana kwa Taifa letu, itawasaidia vijana waondokane na mazingira ambayo huwapelekea kutokuwa na mwelekeo wa maisha, ambapo watasimama imara na kutimiza ndoto zao” amesema Chamatata.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Rajabu Masanche, amewaasa vijana hao watakapomaliza mafunzo yao na kuunda vikundi vya ujasiriamali, watumie pia fursa za kupata mikopo ya Halmashauri asilimia 10, ambapo asilimia nne hutolewa kwa wanawake na 4% kwa vijana, na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu, ili wapate mitaji na kuanzisha biashara zao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Julius Tweneshe, amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuwawezesha vijana kiuchumi pamoja na kuwaonyesha fursa mbalimbali ambazo zinapatikana zikiwemo za mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana uliopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Nao Baadhi ya vijana ambao wamepata mafunzo hayo, akiwamo Happnes Kasembo, amesema mafunzo hayo yamewasaidia kupata elimu ya kujitambua, pamoja na kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa wa maisha yao, na kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato na kuacha kuwa tegemezi ikiwa tayari wameshapatiwa mwanga wa maisha na kuziishi ndoto zao.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza wakati akizindua Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata akizungumza wakati akizindua Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe akizungumza wakati Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.

Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Idara ya Maendeleo ya Vijana Godfrey Massawe akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Rajabu Masanche akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (WAVIU) na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia uliofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Godfrey Kajia akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Mafunzo Tepe, Rose Joel akizungumza wakati wa Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Beda Chamatata (kushoto) Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Julius Tweneshe (katikati) na Mwenyekiti wa Mafunzo Tepe, Rose Joel  wakiwa kwenye Uzinduzi Mafunzo Tepe (Soft Skills) yaliyofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya Vijana Waliohudhuria Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, WAVIU na Wamama Wadogo (Young Mothers) yanayohusu masuala ya Ujasiriamali, Usimamizi wa Biashara, Kujitambua, Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa lengo la kuwajengea uelewa kwenye masuala hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Liga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tarehe 29 Juni, 2022.
Sehemu ya Vijana Waliohudhuria Uzinduzi wa Mafunzo Tepe (Soft Skills) kwa Makundi Maalumu ya Vijana Wenye Ulemavu, WAVIU na Wamama Wadogo (Young Mothers)

PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU,
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Share:

UTEKELEZAJI WA MRADI WA TIMIZA MALENGO KUDHIBITI VVU KWA VIJANA BALEHE.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene.
Na Dotto Kwilasa,DODOMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi na mashirika ya kimataifa kuhakikisha inafikia azma ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU)kwa asilimia 100  kwa vijana ili kuwapa nafasi ya kutimiza malengo yao.

Hayo yamebainishwa Jijini hapa wakati wa uzinduzi wa ugawaji na usambazaji wa vishikwambi kwa ajili ya kufundishia elimu ya VVU na ugonjwa wa  Ukimwi, afya ya uzazi na ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa timiza malengo kwa wasichana balehe na Wanawake vijana.

Simbachawene amesema, maendeleo ya nchi yanategemea nguvu kazi ya rasilimali watu na nguvu kazi hiyo kwa sehemu kubwa inafanya na vijana hivyo 
utekelezaji wa mradi wa timiza malengo kwa wasichana balehe na Wanawake vijana utasaidia kwa kiasi kikubwa kunusuru kundi hilo kwenye maambukizi ya VVU.

"Pamoja na  jitihada zinazofanywa na serikali kulinda kundi hili yapo masuala kadhaa ikiwemo maambukizi ya VVU na UKIMWI  ambayo yamekuwa ni kikwazo kikubwa Kwa ustawi wa Vijana na Taifa kwa ujumla,ugonjwa wa  UKIMWI umeendelea kuwa tishio la uchumi na maendeleo ya nchi na madhara yake yanaendelea kuwa ni changamoto katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa,"amesema

Pamoja na hayo amesisitiza kuwa kama Taifa kuna kila sababu ya kuhakikisha kundi la vijana linalindwa ili kuimarisha nguvu kazi ya Taifa,kukuza uchumi,na kujenga Taifa lenye nguvu na kuongeza kuwa yapo mengi ambayo serikali inafanya kuhakikisha kundi hilo linawekewa mazingira wezeshi na salama yanayolinda ustawi wa akili  na miili yao.

Ameeleza kuwa njia muhimu zitakazoweza kudhibiti maambukizi ya VVU Kwa vijana ni Kwa njia ya elimu  kuhusu masuala ya UKIMWI ili kusaidia kundi hilo kutimiza malengo.

"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaridhishwa sana na namna mradi wa timiza malengo unavyotekelezwa kwa maslahi mapana ya Taifa mradi huu ulianza katika mikoa mitatu na halmashauri 10 wamepanua wigo hadi kufikia mikoa mitano na halmashauri 18,"amesema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania  (TACAIDS) Dk. Leonard Maboko amesema mradi wa timiza malengo  unagharimu fedha sh.bilion 55.2  na unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa UKIMWI, Kifua kikuu na Malaria (Global Fund) katika mikoa mitano.

Amefafanua kuwa mradi huo unatarajia kuwafikia wasichana belehe na wanawake vijana walioko nje na ndani ya mfumo wa shule wapatao million 1 lengo ikiwa ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu maambukizi ya UKIMWI ili kukuza nguvu kazi ya Taifa.

"Msingi wa utekelezaji wa mradi huu ni kusaidia kupunguza maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kwa wasichana balehe na wanawake vijana wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24 ili waweze kutimiza Malengo na ndoto zao pasipo kikwazo chochote,"amesema Maboko

Sambamba na hayo amefafanua kuwa mradi huo unalenga kusaidia wasichana walio ndani na nje ya mfumo wa shule kwa kuwajengea uwezo kifikra ,maarifa na maadili ili wakati wote wabaki salama dhidi ya maambukizi ya VVU  na waweze kutumika na kulijenga Taifa.

Mmoja wa Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya Sekondari Mtumba aliishukuru serikali kwa kuendelea kuwajali vijana kwani wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali ambazo zimepelekea wengine kukatisha ndoto zao.

"Elimu ya ukimwi ni muhimu kwetu kama vijana kwa sababu itatusaidia kujielewa,pia kwa wanafunzi ambao wapo katika umri wa kubalehe ambao mara  nyingi huharibikiwa maisha kwa kujiunga na makundi yasiyoeleweka watanufaika ikiwa wataelimishwa kuhusu ukimwi bila kificho,"amesisitiza 

Mwisho.

Share:

Tuesday, 28 June 2022

SHULE AMBAYO WANAFUNZI WAVULANA WANAVAA NGUO KAMA SKETI

Wanafunzi wa kiume wakiwa katika monekano wa kike baada ya kuvaa sketi
**
NYAKASURA ni shule ya mchanganyiko ya bweni, ya kata ya upili iliyopo huko magharibi mwa nchi ya Uganda ambayo wanafunzi wa kiume wanavaa sare za ‘Kilt’ zenye muonekano wa sketi.

Unaambiwa shule hiyo ilianzishwa miaka 96 iliyopita na Missionari wa Scotland Kamanda Enest Calwell ambaye inasemekana ndio ameanzisha utamaduni wa kuvaa sare hizo.

Mkuu wa Shule hiyo amekanusha kwa kusema sare hizo za ‘Kilt’ sio sketi na huvaliwa kwa kawaida huko nyanda za juu Scotland.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive

Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger