Tuesday, 28 June 2022

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU BI. ZUHURA YUNUS AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bi. Zuhura Yunus akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Mafanikio ya Ziara Rasmi ya Kiserikali iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman hivi karibuni. Mkutano huo na Waandishi umefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Juni, 2022.


Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Mafanikio ya Ziara Rasmi ya Kiserikali iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman hivi karibuni.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Mafanikio ya Ziara Rasmi ya Kiserikali iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman hivi karibuni.


Katibu Mkuu wa wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Mafanikio ya Ziara Rasmi ya Kiserikali iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Oman hivi karibuni.
Share:

LG SMART HOME APPLIANCES DIGITIZING TANZANIA HOMES; SAVES USERS TIME AND ENERGY

• Top benefits of the smart home appliances include offering ease and convenience to use for TVs and refrigerators, improved performance through Artificial Intelligence (AI) technology for the washers and energy-saving for the air conditioners.

• latest core technology featuring intelligence applications hailed for helping households conserve energy and water, being environmentally friendly while being easily usable, thus promoting key sustainable development goals

DAR ES SALAAM, TANZANIA, XX JUNE 2022… 

Tanzanians can now lead an easier, more practical and convenient life with LGs recently introduced smart home appliances aimed at complementing a busy, hectic schedule and challenging daily chores.

Ranging from among others refrigerators, microwaves, televisions and washing machines, the smart home appliances seek to digitize Tanzanians’ homes turning them into an interconnected network set up that allows them to control their home appliances remotely and/or by voice demands.

Commenting on the recent innovations and smart home products, LG Electronics East Africa Managing director Sa young Kim said, “the move to digitize living rooms, the kitchen and any other room in Tanzania homes is inspired by our commitment to priorities convenience and comfort for our customers. For all of us to achieve this, there must be enough supply of smart home appliances which we have made available”.

According to a recent survey by LG ThinQ Smart Home Report, 17.3 % of surveyed users selected energy saving as the biggest smart home benefit. Other top benefits mentioned in the survey included ease and convenience to use for TVs and refrigerators and improved performance through Artificial Intelligence (AI) technology for the washers and energy-saving for the air conditioners.

Among the key smart home appliances introduced by LG in the country include the Smart OLED TVs powered by advanced artificial intelligence technologies that make homes smart and convenient. The TVs have inbuilt AI processors that analyze on-screen content to adjust it to the best possible audio, picture and video by the user’s viewing environment.

Besides, the TVs have intelligent voice recognition feature that enables users to control them with simple commands. They also provide a home dashboard that displays the status of other smart home appliances in the home and notifies users of any situation that users should be aware of, such as the fridge door being open and the remaining time for the washing cycle to end.

To help with laundry, LG has stored up Smart washing machines such as the Vivace Washing machine and other (Artificial Intelligence Direct Drive) AI DD™ / DD washing machines which identify users’ laundry’s fabric type and recommend the best laundry course for it. They also troubleshoot minor issues quickly before they escalate.

For users who want to keep foods and fruits fresh for longer periods, LG has confirmed a lineup of smart Refrigerators designed to be connected to the user’s smartphone to control the refrigerator’s temperature, control Express Freeze, and receive any diagnostics of the user refrigerator and food expiration date notifications.

 This includes the LG Net 426(L) | Slim French Door Fridge, with InstaView Door-In-Door™ which with a compatible smartphone connected to the LG SmartThinQ™ app, users can remotely adjust temperature settings so the fridge is ready to accommodate a large shopping spree.

Other outstanding features include the modern French door with innovative storage options such as a folding Shelf that can be self-folded for storing taller items and the Slim SpacePlus™ Ice System that is built into the fridge door so users can utilise the whole top shelf.

According to Sa Young Kim, this latest core technology featuring intelligence applications helps households conserve energy, and water and are environmentally friendly while being easily usable, thus promoting key sustainable development goals.
END
 
Share:

Monday, 27 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 28,2022

























Share:

SIRI YA KUTOZEEKA MAPEMA


Mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, Kiko Tanaka, alifariki akiwa na na umri wa miaka

Hapo zamani, maisha marefu yalionekana ni kitu kisichowezekana. Lakini sasa mambo yamebadilika. Je uzee kucheleweshwa au hata kuzuiwa? Je wale wenye umri wa zaidi ya miaka 100 wanasiri ambayo inaweza kumsaidia kula mtu kuishi miaka mingi?.


Ijumaa,Januari 2, 1903, mtoto mchanga wa kike anayeitwa Kiko Tanaka alizaliwa katika kijiji kidogo kilichopo katika kisiwa cha kusini mwa Japan. Katika mwaka huo huo, mashindano yam bio za baiskeli ya Tour de France yalianzishwa Paris na kampuni ya magari ya Ford iliuza gari lake la kwanza. Kiko Tanaka alifariki dunia Aprili akiwa na umri wa miaka 119, na alitambuliwa rasmi kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani.


Aliishi miaka yake ya mwisho ya maisha yake katika nyumba ya wazee, akiamka saa kumi na mbili asubuhi kila siku kufanya hesabu, kucheza michezo ya ndani ya nyumba, kula chokoleti na kunywa kahawa na soda.


Kuwapata watu wanaoishi miaka zaidi ya mia moja kama Koshi Tanaka sasa sio jambo lisilo la kawaida.

Chanzo - BBC SWAHILI

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JUNI 27,2022


















Share:

Sunday, 26 June 2022

SIMBA SC YASHINDWA KUFURUKUTA MBELE YA TANZANIA PRISONS


****************************

NA EMMANUEL MBATILO

KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta mbele ya Tanzania Prisons mara baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Sokoine mkoani Mbeya.

Simba Sc imecheza mchezo huo bila staa wao Sakho ambaye amefanya vizuri kwenye mechi za hivi karibuni kutokana na kupata majeruhi ya bega hivi karibuni na kufanya kukosa mchezo huo ambao haukuwa na faida kwao.

Tanzania Prisons imeshinda mchezo huu na kujiweka eneo zuri kuepuka kushuka daraja hivyo kusubiri mchezo wake unaofuata wa mwisho ambayo itaamua kama wataendela kusali kwenye ligi ama kushuka daraja.

Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile dakika ya 54 ya mchezo ambaye aliingia kipindi cha pili .
Share:

Saturday, 25 June 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 26,2022






Share:

ANUNUA JENEZA JIPYA LA MILIONI 1.2 AKIJIANDAA NA MAZISHI YAKE...ALISHANUNUA MENGINE MAWILI



Mzee mmoja kutoka kaunti ya Busia nchini Kenya amewaacha wenyeji vinywa wazi baada ya kujinunulia jeneza la tatu.

Alloise Otieng' Ominang'ombe mwenye umri wa miaka 87 amenunua jeneza jipya la thamani ya KSh 58,000  sawa na shilingi 1,218,000 za Tanzania na ambalo anatazamia kutumia kama gari lake la mwisho duniani.

Mzee huyo anatoka katika kijiji cha Kajoro huko Okatekok, eneo bunge la Teso Kusini kaunti ya Busia.

 Alikuwa amenunua majeneza mengine mwaka 2009 na 2012; hata hivyo alisema yalikuwa yamepitwa na wakati ikilinganishwa na mtindo wa sasa wa kuunda majeneza.

Aliambia runinga ya Citizen kwamba majeneza ya awali yatapasuliwa kuwa vipande vya kuni wakati wa mazishi yake, huku lile alilonunua jipya likitumika katika kumzika.

 "Mawili hayo yatapasuliwa vipande vipande ili vitumike kupika wakati wa mazishi yangu," alisema.

“Nataka hili liwe funzo kwa jamii yangu kwa ujumla. Unaweza kukosa mahitaji ya msingi ukiwa hai. Lakini ukifa, watu watachinja ng'ombe, watakununulia nguo nzuri na viatu wakati utakuwa umeenda kabisa. Ndiyo maana niliamua kupanga jinsi safari yangu ya mwisho itakavyokuwa inayolingana na hadhi yangu katika jamii,” aliongeza.

Katika taarifa sawia na hiyo aliyeishiwa nguvu huko Suna, kaunti ya Migori, jamaa aliyeonekana kuchoshwa na maisha alinunua jeneza nyeupe na buluu, na kulipeleka nje ya nyumba yake kisha akaingia na kujilaza ndani. Mzee huyo aliwaacha wengi vi nywa wazi wakishangaa ni vipi aliamua kufanya kitendo hicho cha ajabu.

Kulingana na Awino, alikuwa amechoshwa na mizozo ya kila mara baina yake, mkewe na wanawe na ndiposa akaamua kufanya kisa hicho cha kustaajabisha.

Akiwa amelewa kabisa, baba huyo wa watoto watatu alishtumu familia yake kwa kumsukuma ukutani huku akisema kila mara alitaka kujitoa uhai. Majirani zake walishtuka, wakatoka nje ya boma hilo mara moja na kurudi baadaye kumsihi Awino asijiue.

Chanzo - Tuko News
Share:

WANANCHI WATAKIWA KUCHUKUA HATUA KUKABILI UKATILI WA KIJINSIA


Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka TGNP Flora Ndaba akizungumza katika mdahalo wa kupinga ukatili wa klijinsia uliofanyika kijiji cha Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. (Picha zote na Fadhili Abdallah)
Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka TGNP Flora Ndaba akizungumza katika mdahalo wa kupinga ukatili wa klijinsia uliofanyika kijiji cha Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.
Polisi kata katika kata ya Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Mkaguzi wa polisi Bwire akizungumza katika mdahalo wa kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia uliofanyika kijiji cha Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma
Polisi kata katika kata ya Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma Mkaguzi wa polisi Bwire akizungumza katika mdahalo wa kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji kijinsia uliofanyika kijiji cha Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma
Viongozi wa kijiji na kata ya TITYE wakifuatilia mdahalo wa kupinga ukatli wa kijinsia ulioandaliwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP).
Wananchi wa kijiji cha Titye Halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma wakifuatilia mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia ulioandaliwa na TGNP.


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WITO umetolewa kwa jamii ya watanzania kuchukua hatua sasa katika kukabiliana na tatizo la ukatili wa kijinsia na watoto kwa kuamua kwa dhati kupambana na vitendo vya ukatili vinavyotokea kwenye maeneo yao.

Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP),Flora Ndaba alisema hayo katika mdahalo wa wananchi wa kupambana na ukatili uliofanyika kwenye kijiji cha Titye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Mratibu huyo alisema kuwa serikali na mashirika yanasaidia kukabili jambo hilo kwa kusimamia sera, sheria na taratibu za kisheria lakini katika kuhakikisha matukio yanakoma jamii inapaswa kuwa ndiyo mtekelezaji mkuu kutokana na matukio hayo kutokea kwenye maeneo yao.

Mafunzo, elimu na uhamasishaji umeshafanyika sana lakini bado wananchi wanionyoshea kidole serikali wakati wanao wajibu na jukumu kubwa katika kusimamia ukomeshaji wa vitendo hivyo.

“Ukiangalia vitendo vya ubakaji, ulawiti, mimba za utotoni kwa wananfunzi, vipigo kwa wanawake na unyanyasaji mwingine vyote vinatokea kwa watu wa familia wenye mahusiano ambao ndiyo wanapaswa kuwa walinzi wa watoto na familia zao",alisema Flora Ndaba kutoka TGNP.

Alisema kuwa serikali na mashirika wanatoa elimu na kuhamasisha kutokomeza ukatili kwa sababu inataka kuwaelimisha kujua wajibu wao kwamba suala la ulinzi, matunzo na malezi ya familia yanaanza kwa baba na mama ambao wanapaswa kusimamia jukumu lao jambo ambalo litasaidia kukabili vitendo vya ukatili kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya Kasulu, Maria alisema kuwa familia kwa kutumia serikali za vijiji ndiyo msingi wa kuzuia ukatili wa kijinsia kwa kuweka mipango ambayo wataitekeleza na kuondoa changamoto hizo,

Pamoja na hilo Maria alisema kuwa utoaji wa taarifa kwa wanajamii kwenda kwenye vyombo vya ulinzi na serikali ni muhimu ili hatua ziweze kuchukuliwa lakini wananchi wamekuwa waoga kutoa taarifa na wakati mwingine kushiriki kuwaficha wahalifu ili wasichukuliwe hatua wengi wakiwa ndugu wa karibu wanaohusika na matukio hayo.

Hata hivyo kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Titye akiwemo Mussa Ndofu ambao wamesema kuwa licha ya kuripotiwa kwa vitendo vya ukatili na mimba kwa wanafunzi lakini inashangaza kuona watuhumiwa wakikamatwa na baadaye kuachiwa bila kufanywa lolote.

Naye Isaya Haminimana alisema kuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanapewa ujauzito na walimu lakini hakuna hatua zinazochukuliwa kwa wanafunzi kuacha masomo na walimu wanaendelea kufundisha bila kufanya lolote.
Share:

CHONGOLO - CHAGUENI VIONGOZI WATAKAOKIPAMBANIA CHAMA NA SERIKALI

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akizungumza

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 

KATIBU Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amewataka wanachama wa CCM kuchagua viongozi ambao wenye dhamira ya dhati ya kukipambania chama hicho ambao wapo tayari kukilinda chama na serikali yake kwa jasho na damu.

Chongolo alisema hayo mkoani Kigoma akiwa njiani kuelekea nchini Burundi ambapo atafanya ziara ya siku tatu nchini humo ambapo pamoja na mambo mengine atafungua uwanja wa michezo na kituo cha kukuza vipaji unojulikana kama Nkurunzinza Peace Park Complex uliopo mkoa Makamba nchini Burundi.


Katibu huyo Mkuu wa CCM alisema kuwa katika uchaguzi huu wa viongozi wa ndani ya CCM ni lazima wapiga kura wazingatie kuchagua viongozi wenye mapenzi ya kweli kwa chama ambao ndiyo msingi wa viongozi wa serikali kwa siku zijazo hivyo wakati huu ni muhimu kwa wapiga kura kutoa mwelekeo wa umakini wa chama hicho.


“Ni lazima kuzingatia uchaguzi wa viongozi ambao kwa dhamira zao wanaonekana kuwa na dhamira za kuwatumikia wananchi, mkikosea sasa mtakuwa mmekosea kwa miaka yote hivyo umakini katika uchaguzi wa kiongozi anayefaa ufanyike sasa na kwa umakini mkubwa,”alisema Chongolo.


Alisema kuwa wapo wagombea wenye hila ambao wanawania nafasi za uongozi ndani ya chama kwa dhamira zao binafsi na kwamba ni vizuri wapiga kura wakaliona jambo hilo na kuwaweka kando wagombea hao.


Katibu huyo Mkuu wa CCM anafanya ziara nchini Burundi kwa Mwaliko wa Chama cha CNDD – FDD ambapo safari yake itamfikisha hadi Bujumbura mji mkuu wa Burundi ambako atakutana na viongozi wa chama hicho na serikali ya Burundi.


Chongolo alisema kuwa anafanya ziara sasa nchini Burundi baada ya Katibu Mkuu mwenzake wa CNDD – FDD, Reverien Ndikuriyo kuwa ameshafanya ziara za kichama nchini Tanzania mara tatu.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger