Saturday, 18 June 2022

Breaking : UHALIFU MKUBWA WA MAZINGIRA MUDA HUU MJINI SHINYANGA....SHUHUDIA HAPA KIZAA ZAA BOMBA LA SHUWASA

Haya siyo mafuriko! Bali ni Bomba la Maji la Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) linalopita katika eneo la Soko Kuu Mjini Shinyanga likiwa limepasuka baada ya mtambo wa kuchonga barabara (Greda) uliokuwa unang’oa kisiki katika eneo ambalo ujenzi wa stendi ya mabasi unaendelea.

Tukio hilo lililozua kizaazaa limetokea jioni hii leo Jumamosi Juni 18,2022 majira ya saa 12 jioni ambapo maji hayo yanayotiririka kuelekea maeneo mbalimbali yameendelea kupotea kwa zaidi ya saa moja na kusababisha uharibifu/uhalifu wa mazingira na upotevu mkubwa wa maji.

 Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Tazama Video hapa chini


















Share:

AMUUA MKEWE KWA KUMKATA JEMBE KICHWANI...AMPONDA PONDA




JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamsaka fundi wa majokofu, Godbles Sawe (47), anayetuhumiwa kumuua mke wake Ester Gadau.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, amesema kuwa mauaji hayo yametokea Jumanne Juni 14, 2022 eneo la Kibamba wilayani Ubungo.

Kamanda Muliro mesema kuwa Sawe ambaye ni mkazi wa Kimara Suka mkoani Dar es Salaam, anatuhumiwa kumuua mke wake, Ester Gadau, kwa kumkata kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia umauti kisha kukimbia baada ya mauaji hayo.

Akisimulia tukio hilo Diwani wa Kibamba, Peter Kilango amesema kuwa mtuhumiwa alifanya tukio hilo majira ya saa 12.30 jioni kwa kumlima na jembe kichwa kisha kukimbilia kusikojulikana kwa kutumia usafiri wa bodaboda.

Diwani Kilango amesema mtuhumiwa huyo ambaye ni Mchaga wa Machame anajishughulisha na kazi ya kutengeneza friji ambapo siku ya tukio mtuhumiwa alitoka nyumbani na kumuacha mkewe akikanda unga wa ngano kwa ajili ya kuchoma maandazi.

“Mke wake ni mjasiriamali anafanya kazi ya kuchoma maandazi na vitumbua na wakati anatengeneza vitu vyake kwa ajili ya kuchoma maandazi na vitumbua, alitoka na kwenda kununua mkaa,” alisema Kilango.

Aliongeza kuwa baada ya Ester kurudi alikuta mlango umefungwa na kushangaa kuwa nani amefunga, mwanamke huyo aliwauliza majirani na kujibiwa kuwa mume wake ambapo alivyogundua ni mume wake aliamua kwenda kwa mjumbe kwa kuwa hawakuwa na uhusiano mzuri na mumewe.

Alieleza kuwa baada ya mjumbe kuelezwa, alikuja na kugonga mlango na mtuhimwa akafungua na kumuamuru mkewe aingine ndani lakini mkewe akakataa kuingia. Aliongeza kuwa kwa kuwa majirani wanafahamu ugomvi wao waliondoka wakiamini kuwa wataelewana tu.

“Wakati wakiwa nje ya nyumba yao mtuhumiwa akamwita mtoto wao anaitwa Ben anasoma darasa la saba Kibamba, lakini mke akamjibu kuwa Ben hayupo nimemtuma dukani. Jibu hilo lilimkasirisha yule bwana wakati ameshikilia jembe anajifanya analima ghafla akamkimbiza mkewe na kumpiga na jembe kichwani,” aliongeza Kilango.

Baada ya mkewe kuanguka chini mtuhumiwa alianza kumponda kichwa mithili ya kulima hali iliyosababisha kupasua kichwa na kukiharibu kabisa. 

Wananchi waliposhtuka na kujaribu kumkata alikimbia na kufika barabarani na kupanda bodaboda na kutokomea kusikojulikana.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JUNI 18,2022













Share:

Friday, 17 June 2022

SERIKALI KUTATUA KERO ZA VIWANDA VYA KATANI TANZANIA

Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji azungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akitoka katika ofisi za kiwanda cha 21st Century Textiles Limited mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji (hayupo pichani) baada ya kufanya ziara kwenye kiwanda hicho leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge leo Juni 17,2022 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Waziri wa Viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji amesema serikali ishaanza kuchukua hatua za kutatua changamoto za viwandani vinavyozalisha bidhaa za katani hapa nchini ili viweze kujiendesha katika mazingira sahihi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha 21st Century Textiles Limited kinachojihusisha na kuchakata mkonge, Dkt Kijaji amesema katika kutatua changamoto hizo serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mazao yote yanayotokana na zao hilo ikiwa ni lalamiko lao kubwa la wenye viwanda.

Pia Amesema wameona ushindani ambao si mzuri unatokana na mazao ya nyuzi za lailoni na zingine zinatoka nje ya nchi hivyo wizara inaendelea kulishughulikia ili kuweza kuliondoa tatizo hilo ambalo linasababisha viwanda hivyo kutokufanikiwa ipasavyo.

Aidha amesema kuwa changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa viwanda hivyo nazo wanazighulikia ili kuweza kuhakikisha kila mfanyakazi anafanya kazi katika mazingira mazuri na kazi kuendelea.

Amewahakikisha wafanyakazi wa kiwanda hicho cha 21st Century Textiles Limited kwamba kiwanda hicho hakitafungwa kwani changamoto zinazowakabili wanaenda kuzitatua mara moja hivyo kila mfanyakazi atapata haki yake na kuendea na kazi.

"Katika Mwaka wa fedha ujao Serikali inatarajia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili sekta ya Viwanda ili kila muhusika wa eneo hiyo ananufaika katika sekta hiyo hatimaye kuongeza ajira na uchumi kwa ujumla hapa nchini". Amesema Waziri Kijaji.
Share:

TBS YATEKETEZA BIDHAA ZISIZO NA UBORA NA USALAMA MKOANI RUKWA.


****************************

SHIRIKA la Viwango Tanzania( TBS) ,Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na taasisi za serikali mkoani Rukwa limeteketeza bidhaa za vyakula na vipodozi visivyo na Ubora na Usalama vya uzito tani tatu na thamani ya Sh. milioni 25. Bidhaa hizo ziliteketezwa Alhamisi Juni 16, mwaka huu katika tanuru la kuchomea taka la kituo Cha Afya Cha Mazwi na dampo vilivyopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuteketezwav kwa bidhaa hizo, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi Rodney Alananga alisema bidhaa hizo zilikamatwa katika kaguzi na operesheni zilizofanyika Februari hadi Mei, 2022 katika maeneo ya vijijini na mijini ya mipakani na kwenye masoko.

Alisema bidhaa hizo za vyakula na vipodozi zilikutwa zimekwisha muda wa matumizi, huku zingine zikiwa zilmepigwa marufuku na hivyo kuuzwa kinyume cha sheria ya Viwango Na.2 ya Mwaka 2009 na hivyo kuhatarisha afya ya walaji na watumiaji, kuathiri mazingira na uchumi wa nchi.

Alifafanua kuwa bidhaa hizo zilitaifishwa,na wamiliki walilipishwa gharama zote za uteketezaji kwa mujibu wa sheria na kupewa onyo kali kutorudia Tena.

"Hivyo wadau wote wakiwemo waingizaji bidhaa hizo nchini, wasambazaji, wauzaji na watumiaji na walaji wameshauriwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo ikiwemo kuendelea kutoa ushirikiano kwa TBS na serikali kwa ujumla kwa lengo la kuhakikisha bidhaa tunazotumia ni bora na salama.," Alananga
Share:

ABUBAKAR KARSAN ATANGAZA KUSTAAFU UKURUGENZI UTPC


Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan (kushoto) akifungua Mkutano wa Kupitia na Kuthibitisha Kanuni za Maadili ya Uandishi wa Habari Mtandaoni leo Jijini Mwanza. 
***

BAADA ya kuutumikia Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Clubs (UTPC) kwa zaidi ya miaka 19 kama mkurugenzi mtendaji, Abubakar Karsan ametangaza rasmi kustaafu kuitumikia taasisi hiyo ifikapo Desemba mwaka huu 2022.

Karsan ameitumikia taasisi hiyo kama Mkurugenzi mtendaji toka mwaka 2003, ambapo amesema kufikia mwezi Desemba 2022 atastaafu rasmi kuitumikia UTPC ambayo ameeleza imekuwa taasisi imara na kubwa nchini.


Akifungua mkutano wa kupitia kanuni za maadili ya vyombo vya habari mtandaoni jijini Mwanza leo, Karsan ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari na kubainisha kuwa, ameamua kwa hiari yeye mwenyewe kustaafu.

“Toka mwaka jana niliomba mimi mwenyewe kwenye bodi ya wakurugenzi nistaafu, nikapumzike na niweze kuwaachia vijana, lakini bodi ilikataa wakaniomba niendelee mwaka mmoja hadi mwaka 2022,” amesema Karsan.


“Niliwakubalia bodi na sasa ule mwaka mmoja utamalizika mwezi Desemba, mwaka huu, nami nakwenda kupumzika ili niwaachie wengine waweze kuendeleza taasisi hii,”ameeleza Karsan.


Mkurugenzi huyo amesema kuwa, UTPC tayari imefanya mchakato wa kumpata mkurugenzi mpya, ambapo amewaomba waandishi wa habari nchini kutoa ushirikiano mkubwa kwake.

“Mchakato wa kumpata Mkurugenzi mpya wa UTPC ulianza muda mrefu na tayari amepatikana, hivyo niwaombe waandishi wa habari nchini kutoa ushirikiano mkubwa kwake,” amesema Karsan.


Amesema kuwa, tangu kuanzishwa kwa UTPC wamepitia changamoto nyingi sana, ambazo zimefanya taasisi hiyo kusimama na kuwa imara zaidi.

Soma pia:
Share:

Thursday, 16 June 2022

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO MADOGO YA MAKATIBU WAKUU


Share:

IGP SIMON SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya maofisa wa polisi wa mikoa.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Juni 16, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP David Misime,imeeleza kuwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Tarime Rolya Kamishna msaidizi wa polisi ACP William Mkonda anakwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani kanda Maalum ya Dar es Salaam akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi ACP Abdi Isango ambaye atakuwa Mkuu wa Opereshen Mkoa wa Mbeya..



Share:

WAHARIRI WA REDIO ZA JAMII WANOLEWA KUHUSU SENSA 2022


Na Mwandishi Wetu, Iringa

Wahariri wa Radio Jamii hapa nchini wameaswa kushiriki kikamilifu katika kuwaelimisha na kuwahamasiha wananchi ili waweze kushiriki Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Said Ameir leo Juni 16, 2022 wakati wa ufunguzi wa siku ya kwanza ya mafunzo kwa wahariri wa Redio Jamii yanayofanyika mjini Iringa kwa siku mbili.


" Baada ya mkutano na Wamiliki wa Vyombo vya Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, tumefanya mafunzo kwa Wahariri wa Mitandao ya Kijamii na sasa Wahariri wa Redio za Kijamii", alisisitiza Bw. Ameir.


Akieleleza zaidi amesema kuwa mafunzo kwa makundi mbalimbali ya wadau ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Uelimishaji na Uhamasishaji.


Aidha, amesema kuwa wahariri hao wanalo jukumu kubwa katika kutoa elimu na kuhamasisha wananchi wote ili washiriki kikamilifu katika Sensa ya watu na Makazi Agosti 23, 2022.


Kwa upande wake mmoja wa watoa mada kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Hellen Hilary amesema Sensa ya Watu na Makazi itasaidia Serikali kupanga mipango ya Maendeleo kwa kuzingatia takwimu zitakazokusanywa.


Baadhi ya mada zitakazotolewa kwa Wahariri hao ili kuwajengea uwezo ni pamoja na; Sensa na Sheria ya Takwimu, Umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi na Maandalizi yake, Sensa na Mbinu za Uripoti kwenye Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na Matumizi ya Mitandao ya Kijamii.


Sensa ya Watu na Makazi itafanyika Agosti 23, 2022 kote nchini ikilenga kusaidia kuongeza kasi ya maendeleo.
Share:

TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KUKUZA TEHAMA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na mgeni wake Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian muda mfupi baada ya kuhitimisha mazungumzo yaliyolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akipokea utambulisho wa wasaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati alipokutana nae kwa mazungumzo. Mazungumzo yalilenga kutazama maeneo ya ushirikiano ili kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam. Picha: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akisisitiza jambo mbele ya Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati wawili hao walipokutana kwa mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam

**************

Na Mwandishi Wetu

Tanzania na China zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kukuza usambaza wa TEHAMA nchini ili kuhakikisha azma ya Serikali kujenga Uchumi wa Kidijitali inafikiwa.

Makubaliano hayo ya ushirikiano yamefikiwa baina ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian mkutano uliofanyika jijini Dar es salaa.

Kuhusu kupeleka huduma za mawasiliano maeneo yasiyofikiwa hasa maeneo ya vijijini China imekubali kuwa itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.

“Tutaendelea kuwahamasisha wawekezaji wa sekta ya mawasiliano nchini Kwetu ili waweze kufikisha huduma za mawasiliano kama ambavyo umeeleza” alitoa hakikisho Balozi Ke katika kikao chake na Waziri Nape.

Pamoja na kukubali kwamba suala la usalama mtandaoni linazo changamoto lukuki ambapo China imekuwa ikikabiliana nazo kila uchao Balozi Ke amesisitiza kuwa China bado inaona umuhimu wa kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha usalama mtandaoni unakuwa wa uhakika kwa kuweka mazingira na Miundombinu itakayowezesha Tanzania kukabili majanga ya kimtandao.

“Kimsingi tumekubaliana kuboresha zaidi suala la usalama mtandaoni hasa kwenye eneo la capacity building (kujenga uwezo) kwa wataalam wetu wa TEHAMA, kubadilishana programu za kiteknolojia zitakazowezesha ukuzaji wa sekta mtambuka za maendeleo kiuchumi kwa mfano kilimo, afya, biashara mtandao nakadhalika” alibainisha Waziri Nape.

Katika mkutano huo pande hizo mbili pia zimekubaliana namna zitakavyowezesha Tanzania kupokea na kukuza teknolojia mpya za mawasiliano ikiwemo Teknolojia ya mawasiliano ya kasi ya 5G.

Ili kuhakikisha Wizara inatekeleza majukumu yake hasa kupitia Idara ya Habari-Maelezo pande hizo mbili zimekubaliana kuboresha Miundombinu ya Idara hiyo itakayowezesha kuongeza ufanisi wa utoaji huduma, hasa kwa kuzingatia kuwa Idara hiyo inahusika kutoa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi.

Kuhusu uungwaji mkono katika Ujumbe wa Baraza-Tendaji la Shirika la Mawasiliano Duniani ITU ambapo Tanzania mwaka huu inawania kuchaguliwa tena kuingia kwenye Baraza hilo katika Mkutano Mkuu wa ITU unaotarajiwa mwezi Septemba baadae mwaka huu, China imekubali kuwa itaiunga mkono Tanzania, ikitumia fursa hiyo kuomba Tanzania pia iiunge mkono katika Nafasi mbalimbali inazowania.

Balozi Ke ametoa hakikisho kuwa atafikisha ujumbe pia kwa nchi nyingine Rafiki kuiunga mkono Tanzania kuwania Nafasi hiyo ambayo itashuhudia nchi 13 za Afrika zikichaguliwa katika nafasi za ITU katika mkutano wa jijini Bucharest nchini Romania utakaoketi Septemba na Oktoba mwaka huu.

Mara baada ya mkutano huo pande za wataalamu kutoka pande mbili za makubaliano zitaketi na kuja na mpango thabiti wa ushirikiano ili utekelezaji uanze mara moja.
Share:

DKT. JIM YONAZI AKAGUA MAENDELEO YA UWEKAJI MNARA WA MAWASILIANO KATIKA KIJIJI CHA MSOMERO MAKAZI MAPYA YA WANANCHI WANAOHAMIA KUTOKA NGORONGORO

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (wa tatu kushoto) akitoa miaelekezo kwa Mwakilishi wa moja ya kampuni za watoa huduma za mawasiliano wakati wa ziara yake na ujumbe wa viongozi wa taasisi za mawasiliano katika kijiji cha Msomero kilichopo Wilaya ya Handeni, Tanga eneo la makazi mapya ya wakazi wanaohamia kutoka Hifadhi ya Ngorongoro. Pamoja nae ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mheshimiwa Siriel Mchembe (wa pili kushoto), Meneja wa Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)-Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum (wa kwanza kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kulia). Picha: TCRA

Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Kaskazini Mhandisi Imelda Salum kuhusu maendeleo ya uwekaji mnara wa mawasiliano katika kijiji cha Msomero kilichopo Wilaya ya Handeni, Tanga. Mradi huo unatekelezwa na Shirika la Mawasiliano (TTCL). Wengine pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (wa tatu kutoka kushoto), Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote Bi. Justina Mashiba (wa nne kutoka kushoto) na Meneja wa TTCL, Tanga Humphrey Ngowi (wa sita kutoka kushoto). Picha: TCRA
Share:

UMOJA WA WABUNGE WANAWAKE WA EALA WAKUTANA ARUSHA KUBADILISHANA UZOEFU


Mbunge wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wanawake kutoka nchi za Afrika katika mkutano ulionza Juni 15,2022 jijini Arusha.
Na Rose Jackson,Arusha

Umoja wa wabunge wanawake wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na viongozi kutoka Afrika wamekutana jijini Arusha katika mkutano wa kimataifa wa wabunge wa kikanda ili kubadilishana uzoefu na mawazo haswa wa wabunge wanasiasa.


Akizungumza Juni 15,2022 katika ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu ulioandaliwa na bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Idea International na kufanyika Arusha Mwakilishi wa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye ni mbunge wa bunge hilo Anastazia Wambura alisema ni vyema wanawake wakawa mstari mbele katika kuwania nafasi ya uongozi wa kisiasa kutokana na eneo ambalo maamuzi hufanyika.


Alisema wanawake wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufikia ajenda ya usawa katika utoaji wa maamuzi kuanzia ngazi ya jamii hadi taifa.


Wambura alibainisha baadhi ya changamoto zinazomkwamisha mwanamke kutowania nafasi ya uongozi ikiwemo majukumu ya kifamilia katika malezi pamoja na mila na desturi zinazowaonyesha kuwa wanawake ni duni.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa wabunge wanawake wa Bunge la Afrika mashariki, Fatuma Ndangiza alisema lengo la mkutano huo ni kuwapa kipaumbele wanawake viongozi kubadilisha uzoefu wa masuala ya uongozi haswa wale wanaoshiriki maswala ya ngazi za siaasa.


"Wabunge wataweza kujadili changamoto na Mafanikio ili waweze kusaidia wanawake vijana ili nao watambue kuwa Wana uwezo wa kufanya Siasa na kuwa na familia kwa wakati mmoja ikiwa ni pamoja na kubaini changamoy zinazowakumba wanawake wanasiasa", aliongeza Fatima.


Mmoja wa wadau wanaopigania haki za binadamu kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo,Agnes Sadiki alisema ni anashukuru kukutana na wanawake kutoka nchi mbalimbali kwani itasaidia kuhamasisha wanawake kuwania nafasi za uongozi mbalimbali na kuweza kufanya maamuzi.


Naibu Waziri anayeshughulika na Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda, Dk.Rebecca Kadaga alisema mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo kwa jamii ni pamoja na kuzingatia usawa katika ngazi za maamuzi hivyo ni vyema wanawake wakapewa kipaumbele.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger