Tuesday, 14 June 2022
SEKTA ZA MIFUGO SMT NA SMZ ZAENDELEA KUWEKA MIKAKATI YA MAENDELEO
Monday, 13 June 2022
JAMAA AUA MPENZI WAKE ALIYEISHI NAYE KAMA DADA YAKE KISHA NAYE KUJIUA DAR
AKIBA COMERCIAL BANK YAKUTANA NA WATEJA WAKE JIJINI MWANZA
Sunday, 12 June 2022
TGNP YATOA MAFUNZO YA BAJETI YA MRENGO WA KIJINSIA KWA WADAU NA WABUNGE VINARA WA JINSIA BUNGENI DODOMA
Mwenyekiti wa Chama cha wabunge wanawake na vinara wa jinsia Margaret Sitta akifafanua jambo kwenye mkutano wa wadau wa TGNP na kueleza kuwa Wabunge vinara wa jinsia watahakikisha wanaisemea bajeti ya mrengo wa Jinsia inafanikiwa na hatimaye makundi ya pembezoni kunufaika.
Mwezeshaji wa TGNP Deogratius Temba alisisitiza jambo kwenye mkutano uliowashirisha wananchi na wabunge vinara wa Jinsia jana Bungeni Dodoma.
HILI NDIYO KABILA AMBALO UKITAKA KUOA AU KUTOA TALAKA LAZIMA UKATWE VIDOLE
SITARUDIA TENA UKAHABA, KILICHONIPATA HUKO SIWEZI KUSAHAU!
MWILI WA PADRE WAOKOTWA UKIWA UMEFUNGWA KWENYE BLANKETI MTONI
Saturday, 11 June 2022
OJADACT YAADHIMISHA SIKU YA OPEN DATA DAY KWA KUWANOA WAANDISHI WA HABARI...YAHAMASISHA WANAHABARI KUTUMIA TAKWIMU KULINDA MAZINGIRA
COASTER ILIYOPELEKA MSIBA YAPINDUKA NA KUUA WATU WATANO KUJERUHI 9 TANGA
JKCI, HALMASHAURI YA CHALINZE WATOA HUDUMA YA MAGONJWA YA MOYO KWA WANANCHI
****
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
TAASISI ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na halmashauri ya Chalinze, Mkoa wa Pwani wametoa huduma ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wenye matatizo hayo hivi karibuni.
Huduma hiyo iliyochukua siku mbili, ikiendeshwa na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Halmashauri ya Chalinze ilihudumia wananchi kutoka mkoa wa Pwani pamoja na mikoa jirani katika hospitali ya Msoga iliyopo Chalinze.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi hiyo Dkt.Peter Kisenge alieleza kuwa zoezi hilo limefanyika katika hospitali hiyo na idadi ya watu waliofika katika zoezi hilo kwa ajili ya upimaji, wapo waliopatikana na magonjwa hayo na wengine walikuwa salama.
“Tangu tumefika hapa mpaka leo tunamalizia zoezi hili la upimaji na tumeweza kupata idadi ya watu 422, ambapo kati ya hao asilimia 60 ya wagonjwa tumewaona wana matatizo ya shinikizo la damu kwa misuli yao ya moyo kutanuka na kutofanya kazi vizuri, na tumeweza kuwapeleka wagonjwa 20 katika Taasisis yetu kwa ajili ya kupata uchunguzi zaidi”.Alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge aliwashauri wananchi kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora na kuepuka vyakula vinavochangia unene wa kupitiliza kiasi, hususani vyakula vya wanga, nyama kwa wingi, unywaji wa pombe pamoja na uvutaji wa sigara uliiokithiri.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Dkt.Allen Mlekwa aliwapongeza wananchi wa Chalinze kwa kujitokeza kupata huduma ya vipimo vya moyo pamoja na mikakati ya Halmashauri ya Chalinze juu yakuendeleza vipimo hivyo.
Dkt. Mlekwa kwa niaba ya Halmashauri ya Chalinze aliishukuru Serikali ya awamu ya sita pamoja na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa ushirikiano wa kutoa huduma hizo.
Kwa niaba ya wananchi waliopatiwa vipimo hivyo, Bi.Gabriela Mtwale aliishukuru Halmashauri ya Chalinze kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa huduma walizozipata na kuomba zoezi hilo liwe linafanyika mara kwa mara ili kuokoa maisha ya nguvu kazi ya Taifa.