Thursday, 12 May 2022
CELINA GOMBANILLAH, MFANYAKAZI BORA MGODI WA BULYANHULU ANAYEAMINI UUGUZI NI KAZI YA WITO
WANAWAKE KAGUNGA WALIA KUTELEKEZWA
Na Fadhili Abdallah,kigoma
Wakizungumza wakati watendaji wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) wakiendesha mkutano ya uelimishaji na uhamasishaji jamii kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali na wadau wa kuzuia ukatili ikiwa ni mpango wa mtandao huo kuiongeza uelewa kwa jamii kupiga vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto.
Mmoja wa wanawake hao,Lucia Marco alisema kuwa kutokana na kutelekezwa huko familia nyingi zimekuwa zikiendeshwa na wanawake ambao wengi wao hawakuwa na shughuli za kiuchumi hivyo kusababisha hali ngumu kwa familia kupata mahitaji ya msingi sambamba na kuchangia wanafunzi kuacha kwenda shule kwa kukosa mahitaji muhimu ya shule.
“Familia nyingi zimebaki zikilelewa na wanawake ambao kulingana na Jiografia ya eneo hilo imekuwa ni vigumu kuendesha maisha kwani Shughuli kubwa ya kiuchumi inayofanyika ni Uvuvi ambao kwa akina mama imekuwa ni vigumu kujishughulisha nayo,”Alisema Licia Marco.
Naye Sabina Marco alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia wanaume kutekeleza familia kunatokana na wivu wa kimapenzi ambapo mwanaume anakuwa na wanawake wengine wan je hivyo migogoro ya kifamilia inapoanza wanaume huondoka na kuhamia kwa wanawake hao hasa wale wenye uchumi na wanajishughulisha na shughuli zinazowaingizia kipato.
waume zmmoja wa wananAidha wameeleza Ujirani na nchi ya Uburundi nao umekuwa ukichochea Familia nyingi kutengena hasa kwa wakazi wa vijiji jirani kutoka nchini humo wanapoingia katika eneo hilo na kuanzisha uhusiano na na wanaume au wanawake ambal tayari wanakuwa na familia.
Aidha inaelezwa kuwa baadhi ya wavuvi kutoka Burundi wanapofika maeneo yao kwa shughuli za uvuvi wanajenga mahusiano na kuwazalisha na baadaye kurudi kwao wakiwaacha wanawake na watoto bila msaada wowote.
Akieleza kuhusu uwepo wa changamoto hiyo Afisa maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Kigoma, George Mselem alisema kuwa katika Kukabiliana na changamoto hiyo wameanza kutoa elimu kwa wanawake kutoka makundi mbalimbali wakiwemo wajane na waliotelekezwa kujiunga kwenye Vikundi vya uzalishaji ili iwe rahisi kupata mikopo na kuanzisha shughuli za kuwaingizia kipato.
Alisema kuwa pamoja na hilo wamekuwa wakitoa elimu na kuhamasisha wakina mama hao kutoa taarifa za vitendo vya ukatili na utelekezwaji wa familia ili waweze kufuatilia waume zao waweze kuhudumia familia hata kama hawapo nyumbani ambalo ndiyo jukumu lao la Msingi.
Akizungumza katika mikutano hiyo Mratibu wa vituo vya taarifa na maarifa vinavyosimamiwa na Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Flora Ndabaniye alisema kuwa nia ya kuendesha vituo hivyo ni kuwezesha kutolewa kwa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa kwenye ngazi ya familia.
Alisema kuwa vituo hivyo vinawezesha kutolewa kwa elimu kwa jamii ili waone na kujua umuhimu kwa wahanga wa vitendo vya ukatili kutoa taarifa ili watuhumiwa wa vitendo hivyo waweze kuchukuliwa hatua.
Kata ya Kagunga inaundwa na Vijiji 13 ambavyo kwa ujumla ni wakazi 2406 ambao kwa zaidi ya asilimia 90 wanategemea uchumi wa Ziwa Tanganyika kupitia shughuli ya Uvuvi.
FAMARA ENTERTAINMENT , UVCCM MWANZA KUSHIRIKIANA KUINUA WASANII NA WACHEZAJI
WABUNGE 19 WALIOFUKUZWA CHADEMA WAFUNGUKA... HALIMA MDEE ASEMA KILICHOFANYIKA NI UHUNI MTUPU...MBOWE AJIBU UHUNI WAO
- Idadi ya wajumbe 423
- Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%
- Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%
- Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%
Breaking News : HALIMA MDEE NA WENZAKE WATIMULIWA RASMI CHADEMA.....RUFAA ZAO ZATUPILIWA MBALI
Wednesday, 11 May 2022
HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 12,2022
WAKAMATWA KWA KUBAKA NA KUUA..MFANYABIASHARA AANGUKA NA KUFARIKI
UKOSEFU WA UMEME, MIUNDO MBINU DUNI KIKWAZO KWA UWEKEZAJI NA BIASHARA KIGOMA
Tuesday, 10 May 2022
MELI KUBWA ILIYOBEBA MAGARI 4397 YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM, YAVUNJA REKODI
Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Eric Hamis, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Bw. Nicodemas Mushi alisema wanayofuraha kubwa kuipokea meli ya Meridian ACE, iliyovunja rekodi ya nyumba iliyowekwa mwezi mmoja uliopita ya kuwasili magari 4o41 mwezi Aprili 8, 2022.
Akifafanua zaidi, Bw. Mushi alisema meli hiyo imetokea nchini Japan na kupitia nchini Singapore na kuja moja kwa moja katika Bandari ya Dar es Salaam. "Kama ambavyo tumeshuhudia meli hiyo imetuletea magari 4397, huku asilimia 23 yaani magari 991 yatabaki nchini Tanzania na asilimia 77 yatakwenda nje ya nchi.
Aliongeza kuwa magari yaliyosalia yanatarajiwa kupelekwa katika nchi za Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi pamoja na DR Congo.
"Niseme kwamba hii ni hatua muhimu inayoonesha imani ya Watanzania, wateja na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi, ambao kutokana na ubora wa kazi inayofanyika na imani ya wateja wetu kwenye eneo la ulinzi na usalama, ubora wa huduma pamoja na umakini unaofanyika katika utoaji wa huduma hizi.
Aidha alisema kuwasili kwa meli hiyo kuna maana kubwa katika uchumi wa Tanzania, kwani ujio wa meli kubwa kama Meridian Ace ni ishara ya ufanisi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam. Alibainisha kuwa ili kuweza kupata makampuni makubwa na mawakala wakubwa wenye mzigo kama huo ni lazima pawepo na imani ya watumiaji wa Bandari.
Alisema ujio wa meli hiyo ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za uboreshaji shughuli za bandari na uwekezaji mkubwa wa vifaa ambayo vimewekwa ili kuboresha huduma na ufanisi wa kazi bandarini.
"...Mfano ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa vya kazi, vyote hivi vinaifanya bandari yetu sasa kutoa huduma katika kiwango cha juu kabisa cha ubora, itakumbukwa kwamba katika eneo la ulinzi na usalama tunafanya vizuri sana.
"Mizigo ya wateja wetu yote inafika katika ubora na inaondoka bandarini kwetu ikiwa salama kabisa, habari hizi njema zinawafanya wateja wapya pamoja na wasiku zote kuendelea kuiamini bandari yetu...ikumbukwe kwamba menejimenti ya TPA ikiongozwa na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na ushauri na ulezi makini kutoka Wizara yetu Mama Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi...," alisisitiza.
"...Tunafanya kampeni kubwa za kimasoko ndani ya nchi pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania lengo likiwa ni kutumia fursa zote zinazotuzunguka kuanzia nchi zote majirani zetu zinapitisha mzigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania." Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Bw. Mushi mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo.