Wednesday, 11 May 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 11,2022

Magazetini leo Jumatano May 11 2022












Share:

UKOSEFU WA UMEME, MIUNDO MBINU DUNI KIKWAZO KWA UWEKEZAJI NA BIASHARA KIGOMA


Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo. (Picha na Fadhili Abdallah)
Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo.
Washiriki wa kongamano la biashara na uwekezaji kutoka nchi tano zinazozunguka ziwa Tanganyika na nchi za maziwa makuu wakifuatilia mwenendo wa mada zinazowasilishwa kwenye kongamano hilo.



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

CHAMA cha Wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) kimesema kuwa kuondolewa kwa changamoto ya miundo mbinu ya usafirishaji kwa njia ya barabara na meli kutawezesha biashara baina ya mkoa Kigoma nan chi za maziwa makuu kuwa na tija kubwa.

Mwenyekiti wa TCCIA mkoa Kigoma,Abdul Mwillima akizungumza katika kongamano la biashara la nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika na ukanda wa maziwa makuu ambapo amesema kuwa ukosefu wa meli za uhakika na barabara kutokuwa za viwango vya lami inakwamisha biashara na uwekezaji kufanyika vizuri.

Mwillima alisema kuwa ukosefu wa umeme wa kutosha ni kikwazo kingine ambacho kinasababisha wafanyabiashara na wawekezaji wenye nia ya kujenga viwanda mkoani Kigoma kushindwa kufanya hivyo pamoja na kuwepo kwa fursa kubwa ya biashara na uwezekaji mkoani humo.

Pamoja na hilo alisema kuwa kongamano linalofanyika litatoa changamoto nyingi ambazo zitajadiliwa na kuzitafutia njia za kuzitatua na kwamba mkoa Kigoma utafaidika kiasi kikubwa na kongamano hilo ambao kwa sasa umekuwa kama kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashairiki na ukanda wa maziwa makuu.

Akifungua kongamano hilo MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amesema kuwa kongamano la biashara baina ya nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika na ukanda wa maziwa makuu ni fursa kubwa kwa nchi hizo katika kukuza uchumi ili kufikia uchumi wa kati.

Alisema kuwa kongamano hilo linaongeza msukumo ya malengo ya serikali ya awamu ya sita kuhusu kujenga uchumi wa viwanda kwa kutumia rasilimali za ndani ili kufikia uchumi wa kati mwaka 2025.

Kuwepo mpakani kwa mkoa Kigoma kunatoa fursa kubwa kuhakikisha mpango huo unatekelezeka kwa mafanikio na serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara na kupunguza gharama za uwekezaji na biashara.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Serikali inaendelea kutatua kero za uwekezaji nchini kupitia TIC na inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo sekta binafsi ambao ndiyo wadau wakubwa kwenye kutoa ajira na uwekezaji na biashara.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD-FDD cha nchini Burundi, Reverien Ndikuriyo alisema kuwa serikali ya Burundi imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa reli iendayo kasi kwenda Gitega nchini humo lengo likiwa kurahisisha usafirishaji na biashara kuelekea bandari ya Dar es Salaam.

Ndikuriyo alisema kuwa kwao Burundi Kongamano hili ni muhimu sana katika kuona namna gani wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania, Burundi nan chi nyingine za Afrika Mashairiki zinashirikiana katika biashara na uwekezaji huku akieleza umuhimu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki na namna itakavyowezesha kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwepo awali kwa nchi nyingine kufanya biashara na nchi hiyo.

Akitoa salam kwa niaba ya Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi zinazoshiriki nchi hizo, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Yahaya Simba alisema kuwa hatua ya mkoa Kigoma kuandaa kongamano hili inatoa fursa chanya kwa balozi mbalimbali kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa mafanikio na kuahidi kuunga mkono jitihada hizi zinazofanyia ili ziweze kuleta matokeo chanya.
Share:

Tuesday, 10 May 2022

MELI KUBWA ILIYOBEBA MAGARI 4397 YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM, YAVUNJA REKODI


Muonekano wa mbele wa Meli ya Meridian ACE ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam leo mchana.
Meli kubwa ya shehena ya magari inayojulikana kama Meridian ACE ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Nicodemas Mushi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA, mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo.
Meli kubwa ya shehena ya magari inayojulikana kama Meridian ACE ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam.
Muonekano wa nyuma wa Meli ya Meridian ACE ilipokuwa ikiwasili katika Bandari ya Dar es Salaam leo mchana.

MELI kubwa ya shehena ya magari yapatayo 4397 imewasili katika Bandari ya Dar es Salaam. Meli hiyo ya MERIDIAN ACEyenye idadi kubwa ya magari imewasili leo majira ya saa sita mchana na kuvunja rekodi, ikiwa na idadi kubwa ya magari kuwasili kwa mara moja katika Bandari hiyo. 

Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Eric Hamis, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Bw. Nicodemas Mushi alisema wanayofuraha kubwa kuipokea meli ya Meridian ACE, iliyovunja rekodi ya nyumba iliyowekwa mwezi mmoja uliopita ya kuwasili magari 4o41  mwezi Aprili 8, 2022.

Akifafanua zaidi, Bw. Mushi alisema meli hiyo imetokea nchini Japan na kupitia nchini Singapore na kuja moja kwa moja katika Bandari ya Dar es Salaam. "Kama ambavyo tumeshuhudia meli hiyo imetuletea magari 4397, huku asilimia 23 yaani magari 991 yatabaki nchini Tanzania na asilimia 77 yatakwenda nje ya nchi. 

Aliongeza kuwa magari yaliyosalia yanatarajiwa kupelekwa katika nchi za Zambia, Malawi, Rwanda, Burundi pamoja na DR Congo.

"Niseme kwamba hii ni hatua muhimu inayoonesha imani ya Watanzania, wateja na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi, ambao kutokana na ubora wa kazi inayofanyika na imani ya wateja wetu kwenye eneo la ulinzi na usalama, ubora wa huduma pamoja na umakini unaofanyika katika utoaji wa huduma hizi. 

Aidha alisema kuwasili kwa meli hiyo kuna maana kubwa katika uchumi wa Tanzania, kwani ujio wa meli kubwa kama Meridian Ace ni ishara ya ufanisi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam. Alibainisha kuwa ili kuweza kupata makampuni makubwa na mawakala wakubwa wenye mzigo kama huo ni lazima pawepo na imani ya watumiaji wa Bandari.

Alisema ujio wa meli hiyo ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za uboreshaji shughuli za bandari na uwekezaji mkubwa wa vifaa ambayo vimewekwa ili kuboresha huduma na ufanisi wa kazi bandarini. 

"...Mfano ujenzi wa miundombinu, ununuzi wa vifaa vya kazi, vyote hivi vinaifanya bandari yetu sasa kutoa huduma katika kiwango cha juu kabisa cha ubora, itakumbukwa kwamba katika eneo la ulinzi na usalama tunafanya vizuri sana. 

"Mizigo ya wateja wetu yote inafika katika ubora na inaondoka bandarini kwetu ikiwa salama kabisa, habari hizi njema zinawafanya wateja wapya pamoja na wasiku zote kuendelea kuiamini bandari yetu...ikumbukwe kwamba menejimenti ya TPA ikiongozwa na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na ushauri na ulezi makini kutoka Wizara yetu Mama Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi...," alisisitiza.

"...Tunafanya kampeni kubwa za kimasoko ndani ya nchi pamoja na nje ya mipaka ya Tanzania lengo likiwa ni kutumia fursa zote zinazotuzunguka kuanzia nchi zote majirani zetu zinapitisha mzigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania." Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Bw. Mushi mara baada ya kuwasili kwa meli hiyo.

Share:

Monday, 9 May 2022

MISA TANZANIA YATOA MAFUNZO YA SHERIA ZA HABARI KWA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA


Rose Jackson,Arusha

Waandishi wa habari mkoani Arusha wamepatiwa semina ya kuwajengea ufahamu wa Sheria mbalimbali ambazo zinagusa uendeshaji wa Tasnia ya habari nchini Tanzania.


Semina hiyo imeandaliwa  MISA Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo Wana habari kuhusu Sheria mbali mbali ambazo zimekuwa zikiminya Uhuru wa habari


Akitoa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari mwezeshaji wa mafunzo Jesse kwayu amesema lengo la semina hiyo pia ni kutoa mafunzo kuhuusiana na Uhuru wa kujielezaa kwa wanahabari hapa nchini


Amesema kulingana na katiba ya jamuhuri ya Muungano wa watazania ya mwaka 1977 ibara 18 inasema wandishi wa habari ni wawezeshaji wa umma wa kutumia haki ya kujielezaa na Uhuru wa kutoa maoni pamoja na Uhuru wa kuchakata na kusambaza habari kupitia vyombo mbali mbali vya habari na kuweza kuwafikia wananchi.


Naye mjumbe wa bodi wa MISA Tanzania Musa Juma amesema katika semina hiyo wameweza kujadili na kupata maoni ya waandishi kuhusu maboresho ya Sheria ya huduma ya habari na namna wanavyoweza kushawishi kuwepo kwa Sheria rafiki kwa wandishi wa habari.


Kwa upande wao waandishi wa habari Jamila omary aliyeshiriki semina hiyo ametoa wito kwa waandishi wa habari kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria na kuwataka kujitokeza kutoa maoni kuhusiana maboresho ya Sheria ya huduma ya habari ili waweze kufanya kazi za kiuandishi na kuelimisha jamii.
Share:

AJABU, MPANGAJI ATAKA KUMDHULUMU NYUMBA MMILIKI WAKE

Hakuna kitu kinampa mtu uhakika wa maisha mjini kama kumiliki nyumba yake binafsi, maisha ya kulipa kodi mjini yamekuwa yakiumiza watu wengi hadi wengine kuamua kurejea vijijini.

Wamiliki wa nyumba wengi huwa hawana subra kwa wapangaji wao linapokuja suala la kodi, hutaka fedha zao mara moja na pale wanapozikosa huwataka wapangaji kuondoka mara moja ili kupangisha watu wengine.

Kutokana na hilo Baba yetu aliamua kujenga nyumba kubwa mbili kwa ajili ya watoto wake ili hapo baadaye tusije kuteseka katika maisha ya kulipa kodi, kila mtoto alipewa yake, mimi na kaka yangu.

Niliamua kupangisha ile nyumba yangu wakati naendelea na masomo na fedha ya kodi niliyopata nilikuwa nalipa nayo ada ya chuo na matumizi mengine. Mara kwa mara nilikuwa naenda kuwatembelea wapangaji wangu kujua changamoto zao kama ukosefu wa maji na maeneo ambayo yanatakiwa kufanyiwa ukarabati.

Baada ya kumaliza shule nilitaka kuhamia katika nyumba yangu hiyo, hivyo niliwapa wapangaji taarifa kuwa baada ya miezi sita wanatakiwa kuhama ili niweze kuhamia. Uzuri wote walielewa na kunihakikishia baada ya kipidi hicho watakuwa wamehama nami nitaendelea na maisha yangu.

Cha kusikitisha ni kwamba ilipotimia miezi sita kuna mpangaji mmoja aligoma kuhama na kudai nyumba ni yake, nilishangaa sana pale alipoamua kutoa nyaraka kuwa anamiliki nyumba hiyo. Ugomvi ulikuwa mkubwa hadi Baba yangu alikuja lakini mpangaji yule aligoma kabisa kuondoka.

Nilitaka kwenda Mahakamni kufunga kesi, lakini rafiki yangu mmoja Seif aliniambia kuna mtu mmoja anaitwa Dr. Kiwanga ambaye anaweza kunisaidia.

Seif alinipa namba za Dr. Kiwanga ambazo ni +254 769404965 na kuniambia niwasiliane naye mara moja, nilimpigia Dr. Kiwanga na kueleza kuwa mpangaji wangu wanataka kinidhulumu nyumba yangu. Dr. Kiwanga aliniambia nisijali kwani ndani ya siku tatu atakuondoka mwenyewe.

Baada ya siku tatu nilienda katika ile nyumba yangu na kukuta kumetawaliwa na ukimya mwingi, nilijaribu kuita lakini hakuna ambaye aliitika. Nilipoingia ndani nipo nikagundua kuwa ameshahama, na hapo nakajua kuwa dawa ya Dr. Kiwanga imeshafanya kazi yake ipasavyo.

Hadi sasa ninapoandika stori hii nimeshahamia kwenye nyumba yangu na yule aliyetaka kunidhulu kwa sasa yupo jela baada ya kumtapeli mtu mwingine kiwanja chake maana ndio ulikuwa mtindo wake wa maisha.

Kwa kipekee namshukuru sana Dr. Kiwanga kwa tiba hii aliyonipatia, natamani sana kila mtu anayesumbulia na utapeli au kudhulumiwa awasiliane naye mara moja na atapata ufumbuzi mkubwa.

Mimi nilikuwa nawaza kwenda Mahakamani kufungua kesi ambapo ningetumia gharama kubwa kuwalipa wanasheria lakini Dr. Kiwanga kaniokoa na masumbuko yote hayo.

Habari nyingine ni kwamba Dr. Kiwanga anaweza kukuwezesha kushinda bahati nasibu, kukuondolea migogoro ya mashamba, migogoro ya mapenzi, kuikinga biashara yako na kukupa mvuto wa kimapenzi.

Pia Dr. Kiwanga anatibu magonjwa kama presha, kifafa, kisonono, kaswendwe, upungufu wa nguvu za kiume na mengineo, watembelee leo upate suluhu kwa matatizo yanayo kutatiza

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yake; www.kiwangadoctors.com, pia waweza kumpigia simu kwa namba +254 769404965 au tuma barua pepe kupitia kiwangadoctors@gmail.com




Share:

RAIS SAMIA AITISHA KIKAO CHA DHARURA KUJADILI BEI ZA MAFUTA



RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitisha kikao cha dharura usiku wa kuamkia leo Mei 9,2022 katika Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.


Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.
Share:

ROYAL TOUR YAMUIBUA LEMBELI



WAKATI Serikali ikiendelea na uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour,aliyoshiriki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan,kutangaza utalii nchini,aliyekuwa Mbunge wa Kahama mwaka 2005 hadi 2015,James Lembeli,ameibuka na kutoa ushauri.


Lembeli ambaye katika kipindi chake cha Ubunge alipata kuhudumu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,alisema Filamu hiyo ingependeza kuzinduliwa huku kukiwa na mkakati endelevu wa kuikuza sekta hiyo kwa kufungua Ofisi za Bodi ya Utalii ( TTB )katika nchi zenye kuleta watalii wengi Nchini.


Alizitaja nchi ambazo zitastahili kufunguliwa ofisi hizo kuwa ni ,Ujerumani,Marekani,Uingereza,China na Ufaransa,kama ambavyo nchi za Afrika Kusini,Rwanda,Kenya na Zimbabwe zilizofanya,hivyo kusaidia ushindani katika sekta ya utalii duniani.

Pia alishauri kuwepo umuhimu wa kutenga bajeti ya fedha za kutosha kwa ajili ya Bodi ya Utalii zitakazowezesha kuziendesha ofisi katika nchi hizo na kuondokana na kasumba ya kutegemea ofisi za Ubalozi zenye majukumu ya kidiplomasia kutekeleza majukumu hayo.


Alifafanua kuwa Maafisa wa Ubalozi kwa asilimia kubwa hawana taaluma ya uhifadhi na utalii,jambo ambalo kwa mara kadhaa wamejikuta wakitoa taarifa zisizo sahihi pindi watu wanapofika ubalozini kupata taarifa za vivutio mbalimbali vilivyopo nchini.


“Kadhia hii ilipata kutokea mwaka 2003, nikiwa miongoni mwa maafisa wa Wizara ya Maliasili Utalii katika maonyesho ya Berlin, Ujerumani.Wakala mmoja mkubwa wa utalii nchini humo alilalamika kutopewa taarifa sahihi za idadi kamili ya Faru walioko Ngorongoro",alisema Lembeli.


Aliendelea kusema, “wakala huyo aliambiwa na maafisa wa ubalozi wako faru 300 ,na wageni walipofika Ngorongoro walibaini kwamba wamedanganywa hivyo kutaka kumshitaki kwa uongo na udanganyifu.”


Alibainisha watendaji wengi wa serikali kuu na katika balozi zetu,hawajawahi kufika katika hifadhi zetu na hata Zanzibar,hivyo kuhoji wanawezaje kutoa taarifa sahihi za maeneo hayo huku taarifa walizonazo wakisoma kwenye vitabu,majarida,vipeperushi au kuona katika “Safari Chanel”.


Lembeli aliyepata kuhudumu Hifadhi ya Taifa,akiwa Meneja Mawasiliano kwa zaidi ya miaka 15,kupitia taaluma yake ya uandishi wa habari,akihamasisha na kuitangaza Tanzania duniani,alipongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan,na kudai pasipo mikakati thabiti haitokuwa na tija


Alionesha khofu yake pasipo mkakati maalumu filamu hiyo,kuishia katika kabati za kutunza nyaraka za serikali,hivyo kumuomba Rais Samia kuhakikisha inasimamiwa kikamilifu na serikali na Taasisi husika kwa kuona Filamu ya Royal Tour ikiendelea kutangazwa duniani kote.


Lembeli alijinasibu kufanya kazi iliyotukuka ya kuutangaza utalii akiwa na Waziri wa Maliasili wa wakati huo,Zakhia Hamdani Meghji,na kupongeza hatua ya Rais Samia juu ya hatua ya filamu hiyo ambayo imeanza kuleta tija nchini.


Aidha aliifananisha filamu ya Royal Tour na inayoitwa Serengeti haitakufa ( Serengeti shall never die) iliyotengenezwa mwaka 1956 na Mjerumani,Michael Girmick,ambayo kwa kipindi cha miaka 65 tangu kutengenezwa ikiendelea kutangaza maajabu ya Hifadhi ya Taifa Serengeti na Tanzania,duniani.

Aliendelea kusema kuwa filamu hiyo ya Serengeti Shall Never Die haitakufa imeendelea kudumu miaka yote 65 kutokana na serikali ya Ujerumani kupitia Taasisi ya Frankfurt Zoological Society kila mwaka kutenga fedha ya kutosha kuhakikisha filamu hiyo inatangazwa na kuongeza watalii katika nchi yetu.


Aidha alibainisha kama ilivyo kwa filamu hiyo ya Serengeti, Royal Tour itadumu kuwa nyenzo muhimu kwa kuitangaza Tanzania duniani kwa miaka 100 ijayo huku akitaka Wanaobeza kazi na uamuzi uliofanywa na Rais Samia,kuelimishwa.


Alisema watu hao hawaijui tasnia ya utalii sambamba na kutofahamu gharama na jasho linalotumika na serikali za nchi na wadau,hasa wafanyabiashara wa sekta hiyo kuleta watalii nchini,hivyo kueleimishwa kutasaidia kuona umuhimu wa filamu hiyo kwa Taifa.
Share:

Sunday, 8 May 2022

WAZIRI DKT MABULA ATAKA WANASIASA KUWA WAKWELI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

Sehemu ya washiriki wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja akizungumza wakati wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.


Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akizungumza wakati wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

****************************

Na Munir Shemweta, WANMM MBEYA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanasiasa nchini kuwa wakweli wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuepuka kuleta migongano baina ya Serikali na wananchi.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo Mei 6, 2022 mkoani Mbeya wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipokutana na uongozi wa mkoa na wilaya kwa lengo la kutoa mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

‘’Tusitafute kura kwa kudanganya wananchi halafu mwisho wa siku tunakosa maneno mazuri ya kuwaambia kutokana na kuwaaminisha kuwa ukiwa kiongozi hawataondoka eneo fulani hivyo kupatwa na kigugumizi utaenda kusema nini wakati ushawaaminisha’’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri Dkt Mabula, wanasiasa wanatakiwa kuwa wakweli kwenye masuala ambayo ni kwa ajili ya ulinzi, maendeleo na mustakabali wa nchi na kama kuna makosa yalifanyika huko nyuma kwa kusajiliwa vijiji maeneo ya hifsadhi basi wakaeleze ukweli na na kusisitiza serikali haiko tayari kurudia makosa.

Akigeukia uamuzi wa serikali kuhusu vijiji 975, Dkt Mabula alisema serikali ya mkoa wa Mbeya inalo jukumu la kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa kushirikiana na taasisi na mamlaka zote zilizopo ndani ya mkoa.

Mkoa wa Mbeya unahusisha vijiji/Mitaa 58 yenye migogoro ya matumizi ya ardhi ambapo vijiji 31 kati ya hivyo vitabaki kwenye maeneo yake huku vijiji/ mitaa 21 wataalamu wakifanyia tathmini na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua migogoro iliyopo kwa manufaa ya Taifa.

‘’Nitoe angalizo maeneo yote ambayo wataalam wanafanyia kazi serikali imekwisha chukua picha za anga za maeneo husika hivyo hatutegemei kuona shughuli mpya zikifanyika katika maeneo yote ambayo wataalam wanapita’’ alisema Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Share:

Video Mpya : KISIMA 'NYANDA MAJABALA' - MAMA.....INA UJUMBE MZITO MAMA NA VIJANA WASIO NA AJIRA


Hii hapa Ngoma nyingine Msanii Kisima 'Nyanda Majabala' kutoka Bariadi Mkoani Simiyu inaitwa Mama...

AJIRA NGUMU...Wazazi nao wanataka UWAHUDUMIE

Wimbo huu ni maalumu kwa MAMA na vijana wote waliosoma ,wanatafuta maisha Mjini lakini ajira hakuna, wanahangaika tu, wazazi nao wanataka huduma😭😭😰😰

Video hii imetengenezwa Mbasha Studio na Director Migera ..Tazama Hapa chiniTazama hapa chini
Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG UWE UNAPOKEA HABARI KWA URAHISI ZAIDI


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:

Saturday, 7 May 2022

WANAKIJIJI WAUA MAJAMBAZI WALIPORA MILIONI 1.2


Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi
**
Majambazi wawili ambao majina yao hayajafahamika wameuawa na wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi, baada ya kuvamia duka la mfanyabiashara mmoja na kupora fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1.2.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 5, 2022, majira ya saa 2:00 usiku katika Kijiji cha Kisongo Pande wilayani kilwa mkoani humo.

"Watu hawa walikuwa wanne, wawili waliingia ndani na wawili walibaki nje na kupiga risasi juu ili kuwatisha wananchi na yule aliyevamiwa walioingia ndani walipora milioni 1.2, kutokana na Polisi Kata na ulinzi shirikishi wananchi waliweza kujikusanya na kuwadhibiti majambzai hao,"amesema Kamanda Kitinkwi.

CHANZO - EATV
Share:

WANAWAKE WASUSIWA MAZISHI GEITA


Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye mazishi Geita
**
Wanawake katika kijiji cha Imaramawazo mtaa wa Ibongo kata ya Ludete wilayani Geita wamesusiwa kuchimba kaburi na kufanya mazishi ya Zawadi Mchele mkazi wa kijiji hicho aliyefariki kwa kuugua ghafla, huku wanawake hao wakihusishwa na tuhuma za mauaji ya wanaume katika kijiji hicho.

EATV imefika kijijini hapo na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo la wanawake kuchimba kaburi ambapo wamesema kwamba, wanawake hao walisusiwa zoezi hilo baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki bila kuugua ikilinganishwa na wanawake kijijini hapo.

"Leo wanawake ndio wamechimba kaburi, na hii inatokana na kwamba wanaume wamechoshwa na matukio ya wanaume pekee kufaliki ghafla wakati mwingine hata bila kuugua. Kwahiyo hii imefanywa kwama adhabu kwa wanawake kwamba kama wanaua basi waajibike kufanya mazishi"- Eunice Mabula, Mkazi wa Kijiji cha Imaramawazo.

Aidha, mwenyekiti wa mtaa huo Coronel Petro anasema alishangaa kupigiwa simu za jeshi la Polisi juu ya sintofahamu ya wanaume kwenye kijiji hicho kutoshiri mazishi ndipo yeye pamoja na Jeshi la Polisi wakafika kwenye kijiji hicho na kuwaamuru wanaume kijijni hapo kushiriki mazishi.

Hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kuamuru mazishi yafanywe na wanaume, wakazi wa mtaa huo (wanaume) kwa kushirikiana na wanawake kutoka kijiji cha jirani wakafanikisha mazishi hayo ambayo wanawake wa kijiji husika hawakushiriki kutokana na kuogopa kususiwa tena mazishi.

CHANZO - EATV
Share:

NEMC WAJUMUIKA NA WANANCHI WA MTAA KISUTU KUFANYA USAFI

Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akikabidhi gloves kwa wananchi ambao wamefanya usafi katika mtaa wa Kisutu leo Jijini Dar es Salaam katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama
Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja mara baada ya kufanya usafi katika mitaa ya Kisutu leo Mei 07,2022 jijini Dar es Salaam.  Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akikabidhi fagio kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri katika mtaa wa Kisutu leo Jijini Dar es Salaam katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu kama kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu kama kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi Serikali ya mtaa wa Kisutu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri akizungumza mara baada ya kupokea vifaa vya usafi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) limekabidhi vifaa vya kufanyia usafi katika serikali ya mtaa wa Kisutu pamoja na kujumuika na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

Akizungumza katika zoezi hilo leo Mei 07,2022, Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John amesema jukumu lao ni kuhakikisha mji unakuwa safi na salama, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kwa ujumla ili kuona mji unakuwa safi na salama.

"Tukihakikisha mji unakuwa safi na salama hatutaona magonjwa kama kipindupindu na magonjwa mengine ya mripuko, lakini pia miili yetu itakuwa na afya njema na kuongezeka kwa nguvu kazi ambazo ndo tegemezi katika kukuza uchumi". Amesema Bi.Irene.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri amewapongeza NEMC kwa kuhakikisha Jiji linakuwa safi na salama ambapo wamepokea vifaa vya kufanyia usafi ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza juhudi kuhakikisha mji unakuwa safi.

Nae Mtaribu wa zoezi la Usafi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa Bw.Moses Mwakiborwa amesema kutokana na Rais wa nchi kuhakikisha anatuletea wageni wa kutosha kuna umuhimu wa mji kuwa safi na salama kwasababu ndo kitovu cha biashara na utambulisho wa nchi yetu.

Amesema zoezi hilo la kufanya usafi kwao litakuwa ni endelevu mpaka watakapohakikisha jiji linakuwa safi na salama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama walivyofanya leo NEMC.

Pamoja na hayo NEMC imetoa wito kwa taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kuhakikisha wanafanya kila namna ili kuhakikisha jiji linakuwa safi na salama maana hii ni njia ya kuunga juhudi za Serikali la kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

Share:

MAPACHA 9 WASHEREHEKEA SIKU YAO YA KUZALIWA....



Ni seti mbili ya mapacha kama hawa ambao wamewahi kurekodiwa katika historia, lakini hakuna walioishi zaidi ya siku chache.
 ***

Mapacha tisa wa kipekee waliozaliwa wakati mmoja (wasichana watano na wavulana wanne) wako "katika afya kamilifu" wanaposherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza, baba yao ameambia BBC.


"Sasa wanatambaa. Wengine wanaketi na hata kutembea wakijishikilia mahali," alisema Abdelkader Arby, afisa wa jeshi la Mali.


Bado wako katika uangalizi wa kliniki nchini Morocco walikozaliwa.


Alisema mama yao Halima Cissé, 26, pia anaendelea vyema.


"Sio rahisi lakini twamshukuru Mungu. Hata kama inachosha wakati mwingine,unapowaona watoto wote wakiwa na afya njema, [kwenye laini]kutoka kulia kwenda kushoto tunafarijika.Tunasahau kila kitu," aliambia BBC Afrique.


Ndio amerejea nyumbani kutoka Morocco kwa mara ya kwanza ndani ya miezi sita, akiwa na mtoto wake wa kwanza, Souda, mwenye umri wa miaka mitatu.


"Nafurahi sana kujumuika na familia yangu - mke wangu, watoto."


Watakuwa na sherehe ndogo tu ya kuzaliwa wakiwa na wauguzi na watu wachache kutoka kwa jengo lao la ghorofa, Bw Arby alisema.


"Hakuna kilicho bora kuliko mwaka wa kwanza. Tutakumbuka wakati huu mzuri tunaoenda kuupata."


Watoto hao walivunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa watoto wengi zaidi kuzaliwa kwa wakati moja na kuishi.


Kabla ya kujifungua mnamo Mei 4, 2021, Bi Cissé alisafirishwa hadi Morocco na serikali ya Mali kwa uangalizi maalum.


Kuzaa watoto wengi ni hatari na akina mama walio na zaidi ya vijusi wanne kwa wakati mmoja wanashauriwa kuavya mimba hiyo hasa katika nchi ambazo utoaji mimba ni halali.


Pia kuna hatari ya watoto kupata matatizo ya kiafya kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, kama vile sepsi s(kuvimba tishu na viungo) na kupooza kwa ubongo.


Bi Cissé na watoto hao kwa sasa wanaishi katika kile ambacho baba yao alikitaja kama "gorofa yenye tiba" ambayo ni ya wamiliki wa kliniki ya Ain Borja huko Casablanca ambako watoto hao walizaliwa.


"Kuna wauguzi ambao wako hapa, pamoja na mke wangu, ambao husaidia kutunza watoto," Bw Arby alisema.


"Kliniki imewapa menyu ambayo inasema nini cha kuwapa kula wakati wote - usiku na mchana," aliendelea.


Abdelkader Arby, Halima Cissé binti ya Soudawalifurahi san akuwa na familia kubwa hivyo

Watoto hao  wasichana watano na wavulana wanne  alizaliwa wakiwa na wiki 30 kulingana Waziri wa Afya wa Mali, Fanta Siby. Walikuw ana uzani wa kati ya gramu 500 na kilo moja (1.1lb na 2.2lb), Profesa Youssef Alaoui, mkurugenzi wa matibabu wa kliniki ya Ain Borja clinic aliambia shirika la habari la AFP wakati wa kuzaliwa kwao.


Walizaliwa kupitia njia ya upasuaji.


Wavulana wanaitwa Mohammed VI, Oumar, Elhadji, Bah, nao wasichana wakapewa majina ya Kadidia, Fatouma, Hawa, Adama na Oumou.


Kila mmoja wao ana kitu cha kipekee, baba yao alisema.


"Wate wana tabia tofauti. Wengine ni wapole, huku wengine wakipiga kelele na kulia sana. Wengine wanataka kuokota kila wakati. Wote ni tofauti sana, jambo ambalo ni la kawaida kabisa."


Bw. Arby pia lishukuru serikali ya Mali kwa usaidizi wake.


"Serikali ya Mali ilitayarisha kila kitu kwa ajili ya matunzo na matibabu ya watoto hao tisa na mama yao. Sio rahisi hata kidogo, lakini ni nzuri na ni jambo la kufariji," alisema.


Hawajafika Mali lakini tayari ni maarufu sana nchini humo, baba yao alisema.


"Kila mtu ana shauku kubwa ya kuwaona watoto kwa macho yao - familia zao, marafiki, kijiji chetu, nchi nzima."


Pia ana ujumbe kwa wanandoa wanaojaribu kupata watoto: "Natumai Mungu atabariki kila mtu ambaye bado hajapata watoto - kwamba wanaweza kupata kile tulicho nacho sasa. Ni kitu kizuri, hazina halisi."

Chanzo - BBC Swahili

Share:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU AMUUA 'EX' WAKE DARASANI ALIVYOBAINI KAPATA MWANAUME MWINGINE


Shule ambayo mauaji yalifanyika

Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu aitwaye Tony Kiptoo (19) kwa kosa la kumuua kwa kumchoma na kisu wakiwa darasani aliyewahi kuwa mpenzi wake na wakaachana Irene Chelagat (22), baada ya kugundua amepata mwanaume mwingine na amemnunulia simu janja (Smartphone).


Vijana hao wawili wote walikuwa wakisoma katika shule ya sekondari Keben ya nchini humo na baada ya kuachana wote walikubaliana na kutakiana heri na ndipo Irene alipoanzisha mahusiano mengine.

Tukio la mauaji hayo limetokea Mei 4, 2022, baada ya kumchoma kisu hicho Irene kifuani na kupoteza maisha hapo hapo, tukio ambalo lilitokea kabla ya vipindi vya masomo vya asubuhi.
Share:

DKT MABULA AADHIMISHA MIAKA SITINI YA KUZALIWA KUCHANGISHA MILIONI 41.6 ZA MASOMO


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa ameshika bilauri ya Mvinyo wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022. Kushoto ni Askofu wa Jimbo la Mtwara Titus Mdoe na Kulia ni aliyekuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi.

Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe akizungumza wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (Kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama (kushoto) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi wakiwa kwenye Misa Takatifu Parokia ya Kiwanja cha Ndege Dodoma wakati wa kuadhimisha kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa Dkt Mabula tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022. Kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe.

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa Mhe. William Lukuvi akizungumza wakati kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Mhe.Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Allan Kijazi (Kulia) wakifurahia jambo wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete akitetea jambo na Waziri wake Dkt Angeline Mabula wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Dkt Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) akiongoza zoezi la kula keki wakati wa kuadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wakinyanyua bilauri yenye mvinyo wakati wa kuadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

*************************

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake kwa kuchangisha fedha shilingi milioni 41,616,500/- za kugharamia masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Aidha, ameitaka jamii kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha.

Maadhimisho hayo yamefanyika 6 Mei 2022 mkoani Dodoma kwa Waziri Dkt Mabula kushiriki Misa Takatifu kwenye Kanisa la Parokia ya Kiwanja cha Ndege na kufuatiwa na chakula cha hisani kilichofanyika Hoteli ya ST Gasper.

‘’Tukiwa na utaratibu wa kuasaidia basi tutakuwa tumewasaidia wanafunzi wengi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto za kifedha’’ alisema Dkt Mabula.

Alisema, lengo la kuitumia siku yake ya kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa kwake kuchangisha fedha ni kutaka kuwanufaisha wanafunzi kwenye taaluma mbalimbali na kutaka kila mtu kutoa michango kulingana na alivyoguswa.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe alimsifu Dkt Mabula kwa uamuzi wake wa kutoa shukurani kwa Mungu kwa zawadi ya uhai aliyoipata kufikisha miaka 60 sambamba na uamuzi wa kuchangisha fedha za kusaidia masomo jambo alilolieleza kuwa ni uamuzi wa busara.

‘’Mama ana jambo lake naye ni mpenzi wa masikini wa roho na mali ndiyo maana umechagua kuwasaidia masikini, vijana wanaokosa pesa za ada lakini umeamua kushiriki kutafuta pesa za kuwasaidia’’ alisema Askofu Mdoe.

Askofu Mdoe alibainisha kuwa, wapo vijana wengi waliopo vijijini lakini wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ya wazazi wao jambo lililomsukuma Waziri Dkt Mabula kuja na wazo la kuchangisha fedha wakati wa misa ya kusheherekea kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa.

Baadhi ya wanafunzi walionufaika na mfuko huo wa kichungaji walieleza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa fursa za kimasomo kwa wale wanafunzi wanaotoka familia za kimasikini.

Thomas Kichenje anayesoma Stashada ya Utawala wa Biashara Chuo cha STeMMUCo Mtwara alisema, bila ya ufadhili wa mfuko wa kichungaji asingekuwa chuoni hapo kwani baada ya kuomba vyuo kadhaa alikosa ufadhili.

Mwanafunzi mwingine Frank Kiwanga anayesomea masomo ya sheria chuo cha SAUT Mtwara alieleza kuwa, alikosa mkopo wa elimu ya juu mara nne lakini kupitia msaada wa mfuko wa kichungaji ameweza kusoma shahada hiyo.

Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa Dkt Mabula kwa kuchangisha fedha yamefanyika pia katika mikoa ya Mbeya, Mwanza na Mtwara. Uchangiaji wa mfuko huo unafanyika kwa wananchi kununua kadi za kuchangia, udhamini wa wanafunzi, mchango wa hisani kupitia chakula ambapo fedha zinazochangwa hutumika kulipia gharama za Bweni, Ada , Bima pamoja na Mafunzo ya Vitendo.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger