Sunday, 8 May 2022

WAZIRI DKT MABULA ATAKA WANASIASA KUWA WAKWELI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

Sehemu ya washiriki wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Mary Masanja akizungumza wakati wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.


Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso akizungumza wakati wa kikao kati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta na viongozi wa wilaya na mkoa wa Mbeya kuhusiana na utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 Mei 6, 2022.

****************************

Na Munir Shemweta, WANMM MBEYA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewataka wanasiasa nchini kuwa wakweli wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuepuka kuleta migongano baina ya Serikali na wananchi.

Dkt Mabula ametoa kauli hiyo Mei 6, 2022 mkoani Mbeya wakati Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta ilipokutana na uongozi wa mkoa na wilaya kwa lengo la kutoa mrejesho wa Maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusiana na utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.

‘’Tusitafute kura kwa kudanganya wananchi halafu mwisho wa siku tunakosa maneno mazuri ya kuwaambia kutokana na kuwaaminisha kuwa ukiwa kiongozi hawataondoka eneo fulani hivyo kupatwa na kigugumizi utaenda kusema nini wakati ushawaaminisha’’ alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Waziri Dkt Mabula, wanasiasa wanatakiwa kuwa wakweli kwenye masuala ambayo ni kwa ajili ya ulinzi, maendeleo na mustakabali wa nchi na kama kuna makosa yalifanyika huko nyuma kwa kusajiliwa vijiji maeneo ya hifsadhi basi wakaeleze ukweli na na kusisitiza serikali haiko tayari kurudia makosa.

Akigeukia uamuzi wa serikali kuhusu vijiji 975, Dkt Mabula alisema serikali ya mkoa wa Mbeya inalo jukumu la kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa kushirikiana na taasisi na mamlaka zote zilizopo ndani ya mkoa.

Mkoa wa Mbeya unahusisha vijiji/Mitaa 58 yenye migogoro ya matumizi ya ardhi ambapo vijiji 31 kati ya hivyo vitabaki kwenye maeneo yake huku vijiji/ mitaa 21 wataalamu wakifanyia tathmini na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua migogoro iliyopo kwa manufaa ya Taifa.

‘’Nitoe angalizo maeneo yote ambayo wataalam wanafanyia kazi serikali imekwisha chukua picha za anga za maeneo husika hivyo hatutegemei kuona shughuli mpya zikifanyika katika maeneo yote ambayo wataalam wanapita’’ alisema Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Share:

Video Mpya : KISIMA 'NYANDA MAJABALA' - MAMA.....INA UJUMBE MZITO MAMA NA VIJANA WASIO NA AJIRA


Hii hapa Ngoma nyingine Msanii Kisima 'Nyanda Majabala' kutoka Bariadi Mkoani Simiyu inaitwa Mama...

AJIRA NGUMU...Wazazi nao wanataka UWAHUDUMIE

Wimbo huu ni maalumu kwa MAMA na vijana wote waliosoma ,wanatafuta maisha Mjini lakini ajira hakuna, wanahangaika tu, wazazi nao wanataka huduma😭😭😰😰

Video hii imetengenezwa Mbasha Studio na Director Migera ..Tazama Hapa chiniTazama hapa chini
Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG UWE UNAPOKEA HABARI KWA URAHISI ZAIDI


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:

Saturday, 7 May 2022

WANAKIJIJI WAUA MAJAMBAZI WALIPORA MILIONI 1.2


Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi
**
Majambazi wawili ambao majina yao hayajafahamika wameuawa na wananchi wilayani Kilwa mkoani Lindi, baada ya kuvamia duka la mfanyabiashara mmoja na kupora fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 1.2.


Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 5, 2022, majira ya saa 2:00 usiku katika Kijiji cha Kisongo Pande wilayani kilwa mkoani humo.

"Watu hawa walikuwa wanne, wawili waliingia ndani na wawili walibaki nje na kupiga risasi juu ili kuwatisha wananchi na yule aliyevamiwa walioingia ndani walipora milioni 1.2, kutokana na Polisi Kata na ulinzi shirikishi wananchi waliweza kujikusanya na kuwadhibiti majambzai hao,"amesema Kamanda Kitinkwi.

CHANZO - EATV
Share:

WANAWAKE WASUSIWA MAZISHI GEITA


Baadhi ya wanawake wakiwa kwenye mazishi Geita
**
Wanawake katika kijiji cha Imaramawazo mtaa wa Ibongo kata ya Ludete wilayani Geita wamesusiwa kuchimba kaburi na kufanya mazishi ya Zawadi Mchele mkazi wa kijiji hicho aliyefariki kwa kuugua ghafla, huku wanawake hao wakihusishwa na tuhuma za mauaji ya wanaume katika kijiji hicho.

EATV imefika kijijini hapo na kuzungumza na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo la wanawake kuchimba kaburi ambapo wamesema kwamba, wanawake hao walisusiwa zoezi hilo baada ya kuhusishwa na imani za kishirikina ambapo wanaume wengi wamekuwa wakifariki bila kuugua ikilinganishwa na wanawake kijijini hapo.

"Leo wanawake ndio wamechimba kaburi, na hii inatokana na kwamba wanaume wamechoshwa na matukio ya wanaume pekee kufaliki ghafla wakati mwingine hata bila kuugua. Kwahiyo hii imefanywa kwama adhabu kwa wanawake kwamba kama wanaua basi waajibike kufanya mazishi"- Eunice Mabula, Mkazi wa Kijiji cha Imaramawazo.

Aidha, mwenyekiti wa mtaa huo Coronel Petro anasema alishangaa kupigiwa simu za jeshi la Polisi juu ya sintofahamu ya wanaume kwenye kijiji hicho kutoshiri mazishi ndipo yeye pamoja na Jeshi la Polisi wakafika kwenye kijiji hicho na kuwaamuru wanaume kijijni hapo kushiriki mazishi.

Hata hivyo, baada ya Jeshi la Polisi kuamuru mazishi yafanywe na wanaume, wakazi wa mtaa huo (wanaume) kwa kushirikiana na wanawake kutoka kijiji cha jirani wakafanikisha mazishi hayo ambayo wanawake wa kijiji husika hawakushiriki kutokana na kuogopa kususiwa tena mazishi.

CHANZO - EATV
Share:

NEMC WAJUMUIKA NA WANANCHI WA MTAA KISUTU KUFANYA USAFI

Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akikabidhi gloves kwa wananchi ambao wamefanya usafi katika mtaa wa Kisutu leo Jijini Dar es Salaam katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama
Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakipata picha ya pamoja mara baada ya kufanya usafi katika mitaa ya Kisutu leo Mei 07,2022 jijini Dar es Salaam.  Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akikabidhi fagio kwa Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri katika mtaa wa Kisutu leo Jijini Dar es Salaam katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya watumishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakiwa pamoja na wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu kama kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kisutu jijini Dar es Salaam wakifanya usafi kwenye maeneo ya mji mara baada ya NEMC kukabidhi vifaa vya Usafi katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kisutu kama kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha Miji na Majiji yanakuwa safi na salama Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi Serikali ya mtaa wa Kisutu katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri akizungumza mara baada ya kupokea vifaa vya usafi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ( NEMC) limekabidhi vifaa vya kufanyia usafi katika serikali ya mtaa wa Kisutu pamoja na kujumuika na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

Akizungumza katika zoezi hilo leo Mei 07,2022, Meneja wa Mawasiliano NEMC, Bi.Irene John amesema jukumu lao ni kuhakikisha mji unakuwa safi na salama, hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha wanashirikiana na wananchi kwa ujumla ili kuona mji unakuwa safi na salama.

"Tukihakikisha mji unakuwa safi na salama hatutaona magonjwa kama kipindupindu na magonjwa mengine ya mripuko, lakini pia miili yetu itakuwa na afya njema na kuongezeka kwa nguvu kazi ambazo ndo tegemezi katika kukuza uchumi". Amesema Bi.Irene.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya mtaa Kisutu Bi.Mariam Bawaziri amewapongeza NEMC kwa kuhakikisha Jiji linakuwa safi na salama ambapo wamepokea vifaa vya kufanyia usafi ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza juhudi kuhakikisha mji unakuwa safi.

Nae Mtaribu wa zoezi la Usafi kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa Bw.Moses Mwakiborwa amesema kutokana na Rais wa nchi kuhakikisha anatuletea wageni wa kutosha kuna umuhimu wa mji kuwa safi na salama kwasababu ndo kitovu cha biashara na utambulisho wa nchi yetu.

Amesema zoezi hilo la kufanya usafi kwao litakuwa ni endelevu mpaka watakapohakikisha jiji linakuwa safi na salama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama walivyofanya leo NEMC.

Pamoja na hayo NEMC imetoa wito kwa taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kuhakikisha wanafanya kila namna ili kuhakikisha jiji linakuwa safi na salama maana hii ni njia ya kuunga juhudi za Serikali la kuhakikisha majiji na miji inakuwa safi na salama.

Share:

MAPACHA 9 WASHEREHEKEA SIKU YAO YA KUZALIWA....



Ni seti mbili ya mapacha kama hawa ambao wamewahi kurekodiwa katika historia, lakini hakuna walioishi zaidi ya siku chache.
 ***

Mapacha tisa wa kipekee waliozaliwa wakati mmoja (wasichana watano na wavulana wanne) wako "katika afya kamilifu" wanaposherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza, baba yao ameambia BBC.


"Sasa wanatambaa. Wengine wanaketi na hata kutembea wakijishikilia mahali," alisema Abdelkader Arby, afisa wa jeshi la Mali.


Bado wako katika uangalizi wa kliniki nchini Morocco walikozaliwa.


Alisema mama yao Halima Cissé, 26, pia anaendelea vyema.


"Sio rahisi lakini twamshukuru Mungu. Hata kama inachosha wakati mwingine,unapowaona watoto wote wakiwa na afya njema, [kwenye laini]kutoka kulia kwenda kushoto tunafarijika.Tunasahau kila kitu," aliambia BBC Afrique.


Ndio amerejea nyumbani kutoka Morocco kwa mara ya kwanza ndani ya miezi sita, akiwa na mtoto wake wa kwanza, Souda, mwenye umri wa miaka mitatu.


"Nafurahi sana kujumuika na familia yangu - mke wangu, watoto."


Watakuwa na sherehe ndogo tu ya kuzaliwa wakiwa na wauguzi na watu wachache kutoka kwa jengo lao la ghorofa, Bw Arby alisema.


"Hakuna kilicho bora kuliko mwaka wa kwanza. Tutakumbuka wakati huu mzuri tunaoenda kuupata."


Watoto hao walivunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa watoto wengi zaidi kuzaliwa kwa wakati moja na kuishi.


Kabla ya kujifungua mnamo Mei 4, 2021, Bi Cissé alisafirishwa hadi Morocco na serikali ya Mali kwa uangalizi maalum.


Kuzaa watoto wengi ni hatari na akina mama walio na zaidi ya vijusi wanne kwa wakati mmoja wanashauriwa kuavya mimba hiyo hasa katika nchi ambazo utoaji mimba ni halali.


Pia kuna hatari ya watoto kupata matatizo ya kiafya kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, kama vile sepsi s(kuvimba tishu na viungo) na kupooza kwa ubongo.


Bi Cissé na watoto hao kwa sasa wanaishi katika kile ambacho baba yao alikitaja kama "gorofa yenye tiba" ambayo ni ya wamiliki wa kliniki ya Ain Borja huko Casablanca ambako watoto hao walizaliwa.


"Kuna wauguzi ambao wako hapa, pamoja na mke wangu, ambao husaidia kutunza watoto," Bw Arby alisema.


"Kliniki imewapa menyu ambayo inasema nini cha kuwapa kula wakati wote - usiku na mchana," aliendelea.


Abdelkader Arby, Halima Cissé binti ya Soudawalifurahi san akuwa na familia kubwa hivyo

Watoto hao  wasichana watano na wavulana wanne  alizaliwa wakiwa na wiki 30 kulingana Waziri wa Afya wa Mali, Fanta Siby. Walikuw ana uzani wa kati ya gramu 500 na kilo moja (1.1lb na 2.2lb), Profesa Youssef Alaoui, mkurugenzi wa matibabu wa kliniki ya Ain Borja clinic aliambia shirika la habari la AFP wakati wa kuzaliwa kwao.


Walizaliwa kupitia njia ya upasuaji.


Wavulana wanaitwa Mohammed VI, Oumar, Elhadji, Bah, nao wasichana wakapewa majina ya Kadidia, Fatouma, Hawa, Adama na Oumou.


Kila mmoja wao ana kitu cha kipekee, baba yao alisema.


"Wate wana tabia tofauti. Wengine ni wapole, huku wengine wakipiga kelele na kulia sana. Wengine wanataka kuokota kila wakati. Wote ni tofauti sana, jambo ambalo ni la kawaida kabisa."


Bw. Arby pia lishukuru serikali ya Mali kwa usaidizi wake.


"Serikali ya Mali ilitayarisha kila kitu kwa ajili ya matunzo na matibabu ya watoto hao tisa na mama yao. Sio rahisi hata kidogo, lakini ni nzuri na ni jambo la kufariji," alisema.


Hawajafika Mali lakini tayari ni maarufu sana nchini humo, baba yao alisema.


"Kila mtu ana shauku kubwa ya kuwaona watoto kwa macho yao - familia zao, marafiki, kijiji chetu, nchi nzima."


Pia ana ujumbe kwa wanandoa wanaojaribu kupata watoto: "Natumai Mungu atabariki kila mtu ambaye bado hajapata watoto - kwamba wanaweza kupata kile tulicho nacho sasa. Ni kitu kizuri, hazina halisi."

Chanzo - BBC Swahili

Share:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU AMUUA 'EX' WAKE DARASANI ALIVYOBAINI KAPATA MWANAUME MWINGINE


Shule ambayo mauaji yalifanyika

Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu aitwaye Tony Kiptoo (19) kwa kosa la kumuua kwa kumchoma na kisu wakiwa darasani aliyewahi kuwa mpenzi wake na wakaachana Irene Chelagat (22), baada ya kugundua amepata mwanaume mwingine na amemnunulia simu janja (Smartphone).


Vijana hao wawili wote walikuwa wakisoma katika shule ya sekondari Keben ya nchini humo na baada ya kuachana wote walikubaliana na kutakiana heri na ndipo Irene alipoanzisha mahusiano mengine.

Tukio la mauaji hayo limetokea Mei 4, 2022, baada ya kumchoma kisu hicho Irene kifuani na kupoteza maisha hapo hapo, tukio ambalo lilitokea kabla ya vipindi vya masomo vya asubuhi.
Share:

DKT MABULA AADHIMISHA MIAKA SITINI YA KUZALIWA KUCHANGISHA MILIONI 41.6 ZA MASOMO


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) akiwa ameshika bilauri ya Mvinyo wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022. Kushoto ni Askofu wa Jimbo la Mtwara Titus Mdoe na Kulia ni aliyekuwa katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi.

Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe akizungumza wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (Kulia), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama (kushoto) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Queen Mlozi wakiwa kwenye Misa Takatifu Parokia ya Kiwanja cha Ndege Dodoma wakati wa kuadhimisha kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa Dkt Mabula tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022. Kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe.

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Isimani mkoani Iringa Mhe. William Lukuvi akizungumza wakati kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Mhe.Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Allan Kijazi (Kulia) wakifurahia jambo wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Dkt Angeline Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Ridhiwani Kikwete akitetea jambo na Waziri wake Dkt Angeline Mabula wakati wa kuadhimisha miaka sitini na kuzaliwa Dkt Mabula jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) akiongoza zoezi la kula keki wakati wa kuadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt Angeline Mabula (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wakinyanyua bilauri yenye mvinyo wakati wa kuadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake jijini Dodoma tarehe 6 Mei 2022.

*************************

Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameadhimisha miaka sitini ya kuzaliwa kwake kwa kuchangisha fedha shilingi milioni 41,616,500/- za kugharamia masomo kwa wanafunzi wenye uhitaji.

Aidha, ameitaka jamii kuangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za kifedha.

Maadhimisho hayo yamefanyika 6 Mei 2022 mkoani Dodoma kwa Waziri Dkt Mabula kushiriki Misa Takatifu kwenye Kanisa la Parokia ya Kiwanja cha Ndege na kufuatiwa na chakula cha hisani kilichofanyika Hoteli ya ST Gasper.

‘’Tukiwa na utaratibu wa kuasaidia basi tutakuwa tumewasaidia wanafunzi wengi wenye uwezo wa kimasomo lakini wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto za kifedha’’ alisema Dkt Mabula.

Alisema, lengo la kuitumia siku yake ya kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa kwake kuchangisha fedha ni kutaka kuwanufaisha wanafunzi kwenye taaluma mbalimbali na kutaka kila mtu kutoa michango kulingana na alivyoguswa.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki Mtwara Titus Mdoe alimsifu Dkt Mabula kwa uamuzi wake wa kutoa shukurani kwa Mungu kwa zawadi ya uhai aliyoipata kufikisha miaka 60 sambamba na uamuzi wa kuchangisha fedha za kusaidia masomo jambo alilolieleza kuwa ni uamuzi wa busara.

‘’Mama ana jambo lake naye ni mpenzi wa masikini wa roho na mali ndiyo maana umechagua kuwasaidia masikini, vijana wanaokosa pesa za ada lakini umeamua kushiriki kutafuta pesa za kuwasaidia’’ alisema Askofu Mdoe.

Askofu Mdoe alibainisha kuwa, wapo vijana wengi waliopo vijijini lakini wanashindwa kuendelea na masomo kutokana na hali ya wazazi wao jambo lililomsukuma Waziri Dkt Mabula kuja na wazo la kuchangisha fedha wakati wa misa ya kusheherekea kutimiza miaka sitini ya kuzaliwa.

Baadhi ya wanafunzi walionufaika na mfuko huo wa kichungaji walieleza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa fursa za kimasomo kwa wale wanafunzi wanaotoka familia za kimasikini.

Thomas Kichenje anayesoma Stashada ya Utawala wa Biashara Chuo cha STeMMUCo Mtwara alisema, bila ya ufadhili wa mfuko wa kichungaji asingekuwa chuoni hapo kwani baada ya kuomba vyuo kadhaa alikosa ufadhili.

Mwanafunzi mwingine Frank Kiwanga anayesomea masomo ya sheria chuo cha SAUT Mtwara alieleza kuwa, alikosa mkopo wa elimu ya juu mara nne lakini kupitia msaada wa mfuko wa kichungaji ameweza kusoma shahada hiyo.

Maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa Dkt Mabula kwa kuchangisha fedha yamefanyika pia katika mikoa ya Mbeya, Mwanza na Mtwara. Uchangiaji wa mfuko huo unafanyika kwa wananchi kununua kadi za kuchangia, udhamini wa wanafunzi, mchango wa hisani kupitia chakula ambapo fedha zinazochangwa hutumika kulipia gharama za Bweni, Ada , Bima pamoja na Mafunzo ya Vitendo.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 7,2022


Magazetini leo Jumamosi Mei 7,2022



Share:

Friday, 6 May 2022

RAIS SAMIA AMTEUA HASSAN OMAR KITENGE KUWA KATIBU WA SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA



*******************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amemteua Bwana Hassan Omani Kitenge kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Kabla ya uteuzi huo Kitenge alikuwa Mkurugenzi wa Mikataba ya Utendaji Kazi Serikalini, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Mei, 2022.


Zuhura Yunus

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Share:

MADIWANI WANUSA UFISADI MAKUSANYO YA FEDHA ZA SERIKALI

 


Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya chato wakiwa kwenye kikao cha Baraza.


Na Daniel Limbe, Chato


BARAZA la madiwani wa halmashauri ya Chato mkoani Geita, limedai kushtushwa na wizi wa fedha za serikali kwenye soko kuu la Buseresere kutokana na baadhi ya watendaji wa serikali kudaiwa kujinufaisha kwa maslahi binafsi.


Hatua hiyo imekuja baada ya Baraza hilo kutaka kujua kiwango cha makusanyo ya fedha toka kwenye chanzo hicho cha mapato ya ndani, ambapo mwenyekiti wa kamati ya Uchumi,mipango na fedha, ambaye ni diwani viti maalumu Muganza,Retisia Isaya, alidai hana majibu ya swali hilo.


Awali Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Christian Manunga, alidai malengo ya ukusanyaji mapato ya ndani umefikia aslimia 71 kwa robo ya tatu ya mwaka hali inayotishia kutofikiwa malengo iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa.


Akichangia hoja hiyo, Diwani wa kata ya Buseresere, Godfrey Miti, ameonekana kushangazwa na ripoti ya halmashauri hiyo kuonyesha kuwa soko la Buseresere halijukusanya hata senti moja kwa robo ya tatu ya mwaka,wakati shughuli za kibiashara zikiendelea kufanyika eneo hilo.


Amependekeza kamati ya Uchumi fedha na mipango kufanya uchunguzi sababu za kukosekana mapato ya serikali kwenye soko hilo ili watakaothibitika kutafuna fedha hizo wachukuliwe hatua za kisheria.


Hata hivyo, Diwani kata ya Kachwamba, Stella Kiwanuka,amekemea tabia ya kupotea kwa mapato ya halmashauri hiyo kutokana na baadhi ya watumishi wa Umma kutaka kujinufaisha pasipo kutazama maslahi mapana ya halmashauri hiyo.


"Mwenyekiti huu mchezo tunapaswa kuutafutia mwarobaini wa kudumu...haiwezekani soko la buseresere lisikusanye mapato hata senti wakati ndiyo chanzo kikubwa cha fedha kwa halmashauri yetu ikiwa ni pamoja na soko la Muganza na Chato"alisema


Ofisa habari halmashauri hiyo, Richard Bagolele, kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, amedai taarifa hiyo imeandaliwa kutokana na kile kilichoonekana kwenye mfumo wa kupokea fedha za halmashauri hiyo.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger