Friday, 29 April 2022
BENKI YA CRDB YASHINDA TUZO MBILI ZA MASUALA YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI KITAIFA DODOMA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wanyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Fedha katika maadhimisho ya Usalama na afya Mahala pa Kazi iliyokwenda kwa Benki Benki ya CRDB ambayo ilipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki hiyo, Misana Mutani. Tuzo hiyo pamoja na ile ya Mshindi wa Jumla wa Huduma za Jamii ya OSHA zilitolewa wakati wa ufungaji wa maonesho ya OSHA kitaofa jijini Dodoma tarehe 28 Aprili,2022. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Patrobas Katambi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wanyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili Sekta za Fedha katika maadhimisho ya Usalama na afya Mahala pa Kazi iliyokwenda kwa Benki Benki ya CRDB ambayo ilipokelewa na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki hiyo, Misana Mutani. Tuzo hiyo pamoja na ile ya Mshindi wa Jumla wa Huduma za Jamii ya OSHA zilitolewa wakati wa ufungaji wa maonesho ya OSHA kitaofa jijini Dodoma tarehe 28 Aprili,2022. Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Patrobas Katambi.
Wananchi mbalimbali waliotembelea Banda la Benki ya CRDB katika maonesho ya OSHA wakipata huduma katika banda hilo.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (wapili kulia) akiongozana na Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani (kulia) wakipata maelezo ya huduma mbalimbali za usalama na afya mahala pa kazi katika banda la Benki ya CRDB.
Meneja Uangalizi Majengo wa Benki ya CRDB, Elia Mnonjela (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete.
Afisa wa Usalama na Afya mahala pa kazi wa Benki ya CRDB, Narsisa Kasinde (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete.
Meneja Uangalizi Majengo wa Benki ya CRDB, Elia Mnonjela (kushoto) akizungumza na wateja waliotembelea Banda la benki hiyo lililopo katika Maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Dodoma katika viwanja vya Jakaya Kikwete.
Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika picha ya pmoja na Maofisa wa Benki ya CRDB.
**********Benki ya CRDB imeibuka mshindi wa tuzo mbili za masuala ya usalama na afya mahala pa kazi wakati wa kilele cha madhimisho ya Usalama na Afya mahala pa kazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma leo tarehe 28 April, 2022.
Tuzo hizo za sekta bora ya fedha inayozingatia usalama na afya mahala pa kazi na ile ya utoaji huduma za kijamii (CSR) zilizotolewa na OSHA na kukabidhiwa kwa CRDB na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenyeulemavu, Prof. Joyce Ndalichako wakati akifunga maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo yalifanyika sambamba na Maonesho ya huduma mbalimbali za usalama na afya mahala pa kazi ya siku tatu Yenye kaulimbiu “Kwa pamoja tushirikiane kujenga utamaduni bora wa usalama na afya mahali pa kazi” yalifunguliwa rasmi tarehe 26 April ikiwa ni utekelezaji wa sera na jitihada ya Serikali katika kuhakikisha uhamasishwaji wa Usalama na afya mahali pa kazi unatekelezwa ili kulinda afya na usalama wa wafanyakazi.
Aidha Serikali imekuwa ikishirikiana kwa pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) katika masuala yote yanayohusu kazi na ajira. Kwa kutambua hilo Benki ya CRDB imekuwa mdau kwa kuipa kipaumbele sera ya afya na usalama mahali pa kazi kwakushirikiana na OSHA ambao ndio wasimamizi wa mpango huo.
Akizungumza katika maonesho hayo baada ya kukabidhiwa tuzo hizo, Mkuu wa kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara wa Benki ya CRDB, Misana Mutani alisema, kuongezeka kwa vifaa vya digitali na matumizi ya teknolojia kumebadilisha kabisa mazingira ya kazi hususani kuongezeka kwa vihatarishi mahali pa kazi. Uchafuzi wa mazingira kutokana na baadhi ya shughuli za uzalishaji Viwandani, Migodini na baadhi ya shughuli nyingine za binadamu umesababisha mabadiliko ya tabia nchi.
“Mahitaji ya dunia yanayotokana na utandawazi yamepelekea kuwepo na idadi kubwa ya wafanyakazi wanaofanya kazi kwa saa nyingi kuliko kawaida na matumizi ya vifaa vya kieletroniki, hivyo kwa kulitambua hilo, Benki ya CRDB imekuwa ikilipa kipaumbela swala la afya na usalama kazini,” alisema Mutani.
Mutani amesema Benki imekuwa ikiendesha program mbalimbali kwa wafanyakzi Tanzania nzima ikiwa ni pamoja na upimaji wa afya kwa wafanyakzazi wote kila mwaka, uwepo wa siku ya Afya ya Benki ya CRDB “CRDB Bank Wellness Day” inayofanyika kwa matawi yetu yote, lakini pia kuwa na Chumba maalumu cha huduma ya kwanza, Chumba cha akina mama na watoto (Lactation Room) pamoja na uanzishwaji wa mfuko wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
“Mustakabali wa kazi hasa wakati nchi yetu inaendelea kujenga uchumi wa viwanda na kuelekea uchumi wa kati na ukuaji wa haraka wa teknolojia inayotumika katika viwanda na maeneo mengine ya kazi kunagusa moja kwa moja afya na usalama wa wafanyakazi,” alisema Mutani.
Katika juhudi za kupambana na hali hiyo kwa sasa duniani kote msisitizo umekuwa ni kuhamasisha kazi kijani (green jobs) na viwanda vinahimizwa kupunguza hewa ukaa hali ambayo itasaidia kupunguza vihatarishi sehemu za kazi na hatimaye kupunguza madhara ya kiafya kwa wafanyakazi.
“Muhimu sana kwa sasa kuliko wakati wowote kuanza kutambua vihatarishi vipya katika maeneo ya kazi. Kutambua vihatarishi hivyo ni hatua muhimu ya kwanza kabisa itakayopelekea kuweka mikakati ya kuzuia vihatarishi hivyo ili wafanyakazi wasipate ajali na magojwa yatokanayo na kazi,” alisema Mutani.
Ajali na magonjwa yatokanayo na kazi ni mambo ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuwa vyanzo vyake vinaweza kutambulika na kuonekana tangu mapema kama tutakuwa makini. Ili kutambua vyanzo hivyo Benki yetu ya CRDB imeona uwepo wa umuhimu wa kujenga utamaduni wa masuala ya afya na usalama mahali pa kazi miongoni mwa jamii.
Katika kujenga utamaduni wa kuzuia vihatarishi sehemu za kazi ni wakati muafaka sasa kwa nchi yetu kuingiza masuala ya afya na usalama kazini”. Alisema Misana.
Benki ya CRDB imeshiriki maonesho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Jakaya Kiwete Convation Centre, Jijini Dodoma. Maonesho yalisimamiwa na kitengo cha Ulinzi, Usalama na Mwendelezo wa Biashara cha Benki ya CRDB kilichopo Makao Makuu - Dar es salaam na kushirikiana na wawakilishi wa Osha wa Benki ya CRDB Kanda ya Dodoma. Shughuli mbalimbali zinazohusu usalama na Afya kazini zinazosimamiwa na Benki zilionyeshwa katika Banda la Benki ya CRDB katika viwanja hivyo.
BARRICK YAIBUKA MSHINDI BORA TUZO ZA WIKI YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI (OSHA)
Wafanyakazi wa Kampuni ya Barrick Tanzania wakifurahia tuzo walizojishindia katika maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
**
Kampuni ya Barrick Tanzania, imeshinda tuzo nane katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ya mwaka 2022 iliyofanyika jijini Dodoma huku Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu, ukinyakua Tuzo ya mshindi wa jumla ya kufuata kanuni za Usalama ipasavyo (the Top OSHA Compliance Award).
Mbali na ushindi huo mkubwa, Bulyanhulu, pia iliibuka kidedea kwa kushinda Tuzo za kuelezea kwa ufasaha shughuli za kampuni, na ushindi wa jumla wa mshiriki wa maonesho na katika kipengele cha Ubunifu katika uchimbaji wa Madini katika maonesho ya OSHA ya mwaka huu.
Kwa upande wa Mgodi wa Barrick North Mara, ulishinda Tuzo za juu katika Mpango Bora wa uhamasishaji kanuni za Afya na Usalama na wadau wake na imeshinda kipengele cha Huduma za Usalama. Pia ilikuwa Mshindi wa pili katika kipengele cha uhamasishaji kuzingatia Usalama kwa Wajasiriamali Wadogo (SMEs) na Tuzo la OSHA katika Sekta ya Madini.
Maonesho ya mwaka huu ya OSHA yalifanyika katika Viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako, alikuwa mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za mwaka huu.
Ushindi wa Barrick Tanzania wa mwaka 2022 unatokana na mafanikio ya kampuni ya 2021 ambapo ilipata ushindi wa jumla wa Tuzo za Utekelezaji wa Majukumu ya kusaidia Jamii (CSR),Mshiriki Bora katika maonyesho na Tuzo ya Ubunifu katika Usalama na Afya (OHS Innovation).
Akiongea baada ya hafla ya utoaji wa Tuzo hizo, Meneja wa Barrick Tanzania, Georgia Mutagahywa alisema, "Huu ni wakati mzuri kwa Barrick kwa ushindi wa Tuzo hizi ambao unadhihirisha kazi kubwa inayofanywa na Wafanyakazi wetu na Washirika wetu kibiashara ili kuifanya Kampuni kuwa mahali salama na pazuri pa kufanya kazi.
"Usalama ni suala kuu tunalolipa kipaumbele cha kwanza, hivyo tumejitolea kufanya kila kuweka mifumo itakatayofanikisha kusiwepo na matukio ya kujeruhiwa katika maeneo yetu ya Kazi", alisema Mutagahywa”.
Tuzo hizi ni ushuhuda wa dhamira ya Kampuni ya kuhakikisha kanuni za usalama zinatekelezwa na kuzingatiwa wakati wote na Wafanyakazi , Washirika na Wadau wake.
Afisa Afya wa mgodi wa Bulyanhulu,Dk. Said Kudra, akipokea Tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mheshimiwa Profesa Joyce Lazaro Ndalichako (kushoto) katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Patrobas Katambi.
Wafanyakazi wa Mgodi wa North Mara wakifurahia Tuzo walizojishindia katika maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu wakifurahia tuzo walizojishindia katika maonesho ya OSHA jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Barrrick walioshiriki maonesho ya OSHA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Kampuni kushinda Tuzo
DKT.MPANGO AWASILI NCHINI KENYA KUMUWAKILISHA RAIS KATIKA MAZISHI YA HAYATI MWAI KIBAKI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Aprili 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta uliopo Nairobi nchini Kenya alipoenda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki. Makamu wa Rais ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM-Bara) Komredi Abdulrahman Kinana
IMAM KHOMEINI NA FIKRA ZA KUIKOMBOA QUDS TUKUFU
*************************
Iwapo tutalitambua suala la kuasisi serikali ya Kiislamu nchini Iran kuwa lilipewa kipaumbele cha kwanza katika fikra za kisiasa za Imam Ruhullah Khomeini, basi hapana shaka kwamba suala la kukomboa Quds tukufu na ardhi za Palestina kwa ujumla kutoka kwenye mikono ya Wazayuni Maghasibu wa Israel lilipewa umuhimu mkubwa katika fikra na kazi za kisiasa za shakhsia huyo adhimu nje ya Iran.
Moja kati ya hitilafu za kimsingi za Imam Khomeini na utawala wa Kipahlavi wa Shah ilikuwa ni ushawishi wa Wazayuni ndani ya Iran na kuwepo Waisraeli katika nafasi za serikali ya wakati huo ya Shah. Kwa maneno mengine ni kuwa, tunaweza kusema kuwa suala la kukomboa taifa la Iran na taifa la Palestina lilikuwa jambo la dharura na lenye kipaumbele cha kwanza katika fikra za kimapinduzi za Imam Khomeini, jambo ambalo linadhihiri wazi zaidi katika maandiko, hotuba na mapambano yake ya kisiasa.
Katika ujumbe wake mashuhuri wa sikukuu ya Nouruzi ya mwaka 1341 Hijria Shamsia, unaosadifiana na mwaka 1962, Imam Khomeini alizungumzia mauaji yaliyofanywa na serikali ya Shah dhidi ya Waislamu na wanazuoni wa dini kwa ajili ya kulinda maslahi ya utawala haramu wa Israel nchini Iran. Tangu wakati huo, Imam alikuwa akizungumzia kadhia hiyo kwa nguvu zake zote katika minasaba mbalimbali ndani na nje ya Iran. Kwa mfano katika ujumbe wake kuhusu muswada wa jumuiya za kimkoa.
Moja ya misimamo mikali mno na imara ya kisiasa ya Imam Khomeini dhidi ya utawala ghasibu wa Israel ni hotuba yake mashuhuri katika msikiti wa Aadham mjini Qum, Iran baada ya kuachiwa huru kutoka jela. Imam Ruhullah Khomeini alisema katika hotuba hiyo kwamba: Enyi wananchi! Dini yetu inatuamuru kuwapinga maadui wa Uislamu. Qur'ani inatutaka kutoungana na maadui wa Usilamu mkabala wa safu za Waislamu. Hakika taifa letu linapingana na Shah (mfalme wa Iran) katika kushikamana kwake na dola la Israel.
Upinzani wa Imam Khomeini dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ulipamba moto zaidi baada ya mauaji yaliyofanywa na utawala wa Shah katika chuo cha kidini cha Faidhiya mjini Qum. Imam alitoa hutuba kali na ya kihistoria kwa mnasaba huo akisisitiza juu ya kuendelezwa mapambano na kupinga ushawishi wa Wazayuni katika masuala ya Iran.
Tarehe 18 Agosti 1969 Wazayuni wa Israel waliuchoma moto msikiti wa al Aqsa. Imam Khomeini alilaani vikali kitendo hicho na akawataka Waislamu wasiujenge upya msikiti huo ili ubakie kama ushahidi wa jinai za Wazayuni mbele ya macho ya Waislamu hadi pale Palestina itakapokombolewa kikamilifu kutoka katika makucha ya Maghasibu.
Katika kipindi chote cha kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Imam Khomeini aliendelea kutoa taarifa mbalimbali, kujibu maswali ya maulamaa na kutoa fatuwa zinazowawajibisha Waislamu wote kupigana vita vya jihadi kwa ajili ya kuikomboa Palestina na kuyasaidia makundi ya mapambano ya Kipalestina. Imam Khomeini alihuisha tena maana ya jihadi na kupigania ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
Kilele cha harakati za Imam za kupinga Uzayuni na kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa Palestina kilikuwa ni kuainisha Ijumaa ya mwisho ya kila mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Kuikomboa Quds tukufu na kupambana na Wazayuni. Imam Ruhullah Khomeini alisema katika ujumbe wake kwa mnasaba huo kwamba: Siku ya Quds ni siku ya kimataifa. Si siku ya Quds pekee bali ni siku ya mapambano ya waliodhulumiwa dhidi ya mabeberu. Mataifa yote yanapawa kusimama kidete na kutupa kiini cha ufisadi katika kapu la taka. Siku ya Quds ni siku ya kufanya juhudi za kuikomboa Quds. Ni siku ya Uislamu na kuhuisha dini hiyo tukufu, na siku ya kutekeleza sheria za Kiislamu katika nchi za Waislamu. Siku ya Quds ni siku ya kutengana haki na batili".
Imam Khomeini aliamini kwamba Uzayuni ni mwana wa ukoloni na ubeberu ambao daima unapewa himaya na misaada ya Marekani. Akiashiria uhusiano mkubwa wa Wazayuni na ubepari na mabepari wa nchi za Magharibi hususan Marekani, Imam Khomeini anaeleza chanzo na sababu ya kujitokeza Israel akisema: Israel iliundwa kutokana na njama na ushirikiano wa serikali za kikoloni za nchi za Magharibi na Mashariki kwa shabaha ya kuyakandamiza na kuyakoloni mataifa ya Kiislamu na hii leo inaungwa mkono na kusaidiwa na wakoloni wote. Uingereza na Marekani zimeuimarisha kijeshi na kisiasa utawala ghasibu wa Israel na kuuhamasisha dhidi ya Waarabu na Waislamu kwa kuupa silaha hatari za mauaji".
Miongozi mwa sifa makhsusi za Uzayuni ambazo zinaonekana sana katika hotuba za Imam Khomeini (Mwenyezi Mungu amrehemu) ni aidiolojia yake ya "Kuanzia Nile Hadi Furati". Imam alikuwa akiamini kamba uvamizi wa Israel dhidi ya nchi za Kiislamu hautaishia Palestina, Lebanon na katika miinuko ya Golan huko Syria, bali Wazayuni wanakusudia kuunda dola wanaloliita Israel Kuu na hatari yao inazilenga nchi zote za Kiislamu za Mashariki ya Kati. Imam alikuwa akizitahadharisha nchi za Kiarabu na kuziusia zijizatiti kwa silaha kwa ajili ya kutokomeza utawala huo bandia na ghasibu katika jiografia ya kisiasa na eneo la Mashariki ya Kati.
Imam Ruhullah Khomeini alikuwa akiamini kwamba serikali na makundi ya Kipalestina hayapaswi kupoteza wakati katika mijadala ya kidiplomasia kwa ajili ya kupata haki zilizoghusubiwa za wananchi wa Palestina.
Aliamini kuwa njia pekee ya kumuangamiza adui ghasibu na Mzayuni ni mapambano ya silaha na vita vya jihadi. Imam Khomeini alikuwa akiamini kwamba utawala ghasibu wa Israel ni kama donda la saratani ambalo njia pekee ya kulitibu ni upasuaji, kulikata na kuling'oa kabisa. Imam alikuwa akiwalaumu watu wanaotumia mbinu za kisiasa kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa kadhia ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu na alikuwa akisema: Ninawausia viongozi wa Kipalestina waache kwenda huku na kule kukutana na Wazayuni na wapigane hadi tone la mwisho la damu zao. Wapalestina wanapaswa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kwani kukutana na Wazayuni kunayavunja moyo mataifa ya wanapambano.
Imam Khomeini aliutambua mfarakano na hitilafu kuwa ndio tatizo kuu la Waislamu na nchi za Kiislamu pia na kwamba jambo hilo linawadhoofisha mno mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Imam Khomeini alikuwa akisema, “Lau Waislamu wataungana na kila mmoja wao akamwaga ndoo moja tu ya maji, basi utawala ghasibu wa Israel utaangamia”.
Imam Khomeini ametaja siri ya ushindi kuwa ni kupigana na kuwa tayari kuuawa shahidi na kulitaja suala hilo kuwa ni siri ya Qur'ani ambayo inamfikisha mwanadamu katika mafanikio zaidi na kutimiza matarajio ya mataifa bila ya kuzingatia maisha ya kimaada na kidunia.
Imam Ruhullah Khomeini ametaja mapambano ya Intifadha ya Palestina na harakati ya Kiislamu na ya wananchi kuwa ni mti uliobarikiwa na nyota inayong'ara na kusisitiza kuwa mbinu hiyo ya mapambano ndiyo stratijia kamili zaidi kwa ajili ya kuuangamiza kikamilifu utawala ghasibu wa Israel.
Thursday, 28 April 2022
RAIS SAMIA ATANGAZA SIKU MBILI ZA MAOMBOLEZO YA KITAIFA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza siku mbili za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Hayati Rais Mstaafu wa Kenya, Mhe. Emilio Mwai Kibaki, kilichotokea tarehe 21 Aprili, 2022 jijini Nairobi.
Maombolezo hayo yataanza tarehe 29 Aprili, 2022 hadi tarehe 30 Aprili, 2022.
Katika kipindi chote cha maombolezo, bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini Tanzania zikiwemo kwenye balozi zetu pia.
Rais Samia amewaomba Watanzania wote kuungana na wenzetu wa nchi jirani ya Kenya katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na aliyekuwa kiongozi wao nchini humo.