Sunday, 13 February 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI FEBRUARI 13,2022





 
Share:

CHELSEA FC YACHUKUA KOMBE LA DUNIA NGAZI YA VILABU



Na Emmanuel Mbatilo 

KLABU ya Chelsea imeibuka Mabingwa wa Kombe la Dunia ngazi ya klabu mara baada ya kuichapa Palmeiras ya nchini Brazili kwa mabao 2-1 katika dakika 30 za nyongeza.

Chelsea ilianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Romelu Lukaku akipokea krosi kutoka kwa Hudson Odoi dakika ya 54 ya mchezo.

Dakika ya 64 ya mchezo Thiago Silva beki wa Chelsea aliunawa mpira ndani ya kumi nane akijaribu kuokoa mashambulizi kutoka kwa Palmeiras na kuamuliwa penati ambayo ilikwenda kupigwa na Raphael Veiga na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka dakika 90.

Dakika 30 zilivyoongezwa Chelsea ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji na dakika ya 116 mchezaji wa Palmeiras Luan Garcia nae akanawa mpira na kuamuliwa penati ambayo ilikwenda kupigwa na Kai Harvert na kuiwezesha timu yake kuibuka na ushindi.
Share:

Saturday, 12 February 2022

WAZIRI MCHENGERWA-RAIS SAMIA AWEKA BILIONI 1 KWENYE MFUKO WA MAENDELEO YA SANAA NA UTAMADUNI

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wadau wa Filamu nchini na kufafanua mafanikio ya Serikali kwenye tasnia hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbas akizungumza na wadau wa Filamu nchini na kufafanua mafanikio ya Serikali kwenye tasnia hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam Wadau mbalimbali wa sanaa wakifuatilia mkutano na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa pamoja na viongozi mbalimbali wa tasnia hiyo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam *************************** NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ameweka wazi kuwa Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu ana dhamira ya kuboresha na kunyanyua kazi za Sanaa nchini na ameongeza Fedha Kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni. Akizungumza na wadau wa kazi za Sanaa nchini Waziri Mchengerwa amesema Serikali ya Tanzania inatambua Mchango wa kazi za Sanaa nchini na awamu ya 6 imedhamiria kuboresha Miundombinu ya kazi za Sanaa na kwa kuanza Rais ameweka billion 1 kwa Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni. "Dhamira yangu ni kuona Sekta ninazo simamia kuona zinapiga hatua kubwa tunahitaji kufanya Mapinduzi nakuona Maendeleo ya Sanaa ya Filamu nchini hivyo Serikali Ina dhamira pia ya kuhakikisha kazi za Sanaa zinafika mbali na zinakuwa zenye viwango na Mama Samia ameongeza takribani bilioni 1 na kufikia bilioni 2.5 katika Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa hivyo Wasanii wajitokeze kukopa Fedha hizo ." Hata hivyo Mchengerwa ameeleza kuwa Wasanii Wizara itahakikisha wanachapa kazi na hakuna kazi ya Sanaa itakayosimama Kwa kisingizio cha Fedha kwani Milango ipo wazi Kwa wadau wa Filamu kukopesheka Kwa Fedha hizo Ili kuona Kwa namna gani watayarishaji wanatengeneza kazi zenye viwango na Bora zenye kutambulisha Utamaduni wa Taifa la Tanzania. "Ule mkamwo wa kusitasita kutengeneza Filamu zenye uhalisia Sasa basi tayari Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa una shilingi Bilioni 2.5 ni Fedha Kwa ajili ya kazi za Sanaa ambapo Mtayarishaji atakopeshwa Fedha hizo bila malipo ya riba hivyo tunategemea kazi za Sanaa nzuri zitazalishwa Kwa wingi na zenye ubora Ili kufikia Masoko ya nje." Aidha, Mchengerwa ameeleza dhamira nyingine ya wizara yake kuweka Mkakati wa wizara kuwa na televisheni na radio Ili kuweza kuonyesha kazi za Sanaa Kwa masaa 24 na kuwapa fursa Wasanii wanaochipukia kuonekana Pamoja Mkakati wa wizara kuwa na Vyombo vya kisasa vya kuandaa Filamu ambavyo vitakuwa vikikodishwa . Pamoja na hayo Waziri Mchengerwa amewaomba Wasanii kuonyesha ushirikiano na wizara husika na kuahidi kushikamana na wasanii bega Kwa bega na Wasanii kuhakikisha kazi zinajitangaza na kuwaleta watu wenye Mchango katika Sekta ya Filamu kidunia Ili kusaidia kiwanda cha Filamu nchini kinakua na wigo mpana . Mchengerwa ameongeza kuwa Wizara Ina Mkakati wa kujenga nyumba Kwa Wasanii zenye hadhi kwani Serikali inatambua Mchango wa Sanaa nchini katika kutangaza Utamaduni. Kwa upande wake Katibu Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo amebainisha changamoto na Mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia vikao vilivo fanyika Kwa kushirikisha viongozi,Wasanii na wadau wa Filamu na vyama vya Wasanii. "Katika Mafanikio yaliyopatikana kupitia Serikali ya Jamhuri wa Tanzania Kwa kushirikiana na bodi ya Filamu nchini tuliweza kushirikisha vyama vya Wasanii , Wasanii na wadau na tukagundua vitu mbalimbali ikiwemo swala la kupatiwa Tuzo kama kielelezo Cha kutambua Mchango wa kazi za Sanaa na 2021 tuliweza kufanikiwa kuwepo Kwa Tuzo za Sanaa". Aidha Dkt.Kilonzo ameongeza kuwa mbali na kuwepo Kwa Tuzo kulihitajika Mitaji Kwa ajili ya kuongeza ubora wa kazi zao pamoja na changamoto ya Kodi na tozo Kwa Filamu. Pia amebainisha baadhi ya Mafanikio yaliyopatikana ikiwemo Filamu mbili "Vuta nikuvute" na Filamu ya "Binti" kushinda Tuzo pamoja na Kuonyeshwa katika Mtandao wa Kimataifa wa kuonyesha Filamu Netflix.
Share:

MATUKIO KATIKA PICHA - KAMPENI YA ELIMU KWA MLIPAKODI MLANGO KWA MLANGO SIRARI - MARA


Kaimu Meneja Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara Bw. Robert Busumabu akichangia hoja wakati wa semina kuhusu taratibu za forodha zinazotumika kuwahudumia wafanyabiashara wa kati na wadogo wanaotumia Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani Sirari. Semina hiyo imefanyika kufuatia kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea mkoani Mara.

Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Edwin Iwato akitoa elimu ya taratibu za forodha zinazotumika kuwahudumia wafanyabiashara wa kati na wadogo wanaotumia Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani Sirari. Elimu hiyo imetolewa kufuatia kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea mkoani Mara.

Afisa Msimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Lameck Ndinda akitoa mafunzo ya huduma bora kwa wateja kwa watumishi wanaofanya kazi katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani Sirari. Mafunzo hayo yametolewa kufuatia kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea mkoani Mara.

Afisa Uhusiano kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi Salome Mwandalanga akimsikiliza kwa makini mfanyabiashara wa Sirari Bw. Joseph Mokare wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Abdallah Seif akitoa elimu ya kodi kwa mfanyabiashara wa Sirari Bw. Jumanne Omari wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi mlango kwa mlango inayoendelea katika Wilaya ya Tarime mkoani Mara. (PICHA ZOTE NA TRA).
Share:

KIKWETE KUZINDUA KITABU CHA MAISHA YAKE



Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kuzindua kitabu cha maisha yake alichokiita kwa kimombo “From a barefoot student to President” tafsiri yake kwa Lugha ni Kiswahili ni “Kutoka Mwanafunzi Aliyetembea Peku Hadi Kuwa Rais.”

Kitabu hicho kinachosubiriwa kwa hamu ni muendelezo wa utamaduni mzuri wa marais wastaafu wa Tanzania kuandika vitabu vya kumbukumbu ya maisha yao ya kawaida na uongozi.
Share:

ZAIDI YA WANAFUNZI 2,000 WAFIKIWA NA KAMPENI YA "MKINGE MWANAFUNZI NA AJALI ZA BARABARANI"

Meneja Miradi wa PESACO Bw.Abel Swai akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Elimu hiyo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani. Mwenyekiti wa PESACO Bw.Mfaume Hassani akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Elimu hiyo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani. Katibu wa PASACO Bw.Fransisco Peter akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Elimu hiyo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani. Wanafunzi wa shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakiwasikiliza wataalamu kutoka Taasisi ya PESACO wakitoa elimu ya Usalama barabarani ambapo ni mwendelezo wa Kampeni ya Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani.

*****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Shirika lisilo la Kiserikali linalojihusisha na utoaji elimu ya Usalama barabarani (PESACO) limeendelea na kampeni yake ya "Mkinge Mwanafunzi Dhidi ya Ajali za Barabarani" kwa kutoa elimu ya usalama barabarani katika shule za Msingi na Sekondari nchini.

Akizungumza katika zoezi hilo lililofanyika katika shule ya Sekondari Al-haramain iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa PESACO Bw.Mfaume Hassani amesema ajali za barabarani zimezidi kua miongoni mwa vyanzo vikubwa vinavyo chukua uhai wa watu wengi na kusababisha majeraha na ulemavu kwa maelfu ya watu.

Amesema Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakadiria kuwa watu zaidi ya milioni 1.3 hupoteza maisha kila mwaka, idaidi hii ikiwa ni mara mbili ya vifo vinavyosababishwa na Malaria na UKIMWI. Vifo vingi na majeraha hutokea zaidi katika nchi za uchumi wa kati na zinazoendelea kama Tanzania.

"Ili kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani PESACO imejizatiti kuunga mkono jitihada za serikali na vyombo vyake katika kuhakikisha tunafikia Tanzania isio na ajali. Tukitumia nyenzo ya elimu PESACO inayafikia makundi yote sita ya watumia barabara, kuwapa elimu stahiki itakayowasaidia kudumisha uwiano wa matumizi salama ya barabara ili kuepukana na ajali". Amesema Bw.Hassani.

Pamoja na hayo Bw.Hassani amesema zoezi hilo ni endelevu kwani mpaka sasa wameshawafikia wanafunzi zaidi ya elfu mbili (2,000) ambapo kwa hakika elimu walioitoa itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali za barabarani.

Share:

WAZIRI BASHUNGWA APENDEZWA NA CWT KINAVYOCHOCHEA UBORA WA ELIMU NCHINI, ASIFU MPANGO WA ELIMU BURE

Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)imesema imepeleka jumla ya shilingi trilioni 1.43, kwa ajili ya kugharamia Mpango wa elimu msingi bila Malipo ulioanza kutekelezwa 2015 na kuleta fursa ya upatikanaji wa elimu kwa kuongeza uandikishaji wa wanafunzi, kutokana na kuondolewa kwa vikwazo. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa Februari 11,2022 jijini hapa katika hafla ya  utoaji tuzo  za ubora wa taaluma kwa walimu,wanafunzi , Shule, Halmashauri na mikoa yote  iliyofanya vizuri kwenye matokeo  ya mitihani ya Mwaka 2021 ya kumaliza elimu ya msingi, kidato cha nne na kidato cha sita.

Amesema katika mwaka 2016, jumla ya wanafunzi 2,670,125 waliandikishwa, kati ya hao wanafunzi 917,137 wa elimu ya awali, 1,386,592 wa darasa la kwanza na wanafunzi 366,396 wa kidato cha kwanza.

Waziri Bashungwa ameeleza mwaka 2022, jumla ya wanafunzi 3,046,919 wameandikishwa, kati ya hao wanafunzi 1,123,800 ni wa Elimu ya Awali sawa na asilimia 82, wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,352, wanafunzi 1,454,544 ni wa darasa la kwanza sawa asilimia 91, huku wanafunzi 664,698 wakiwemo wenye mahitaji maalum ni 2,747.

"Wanafunzi 664,698 wa kidato cha kwanza wameripoti shuleni, sawa na asilimia 73.2 ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka 2022, wakiwemo wanafunzi 679 wenye mahitaji maalum,"amesema.

Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na walimu nchini katika kuboresha taaluma, hivyo ni dhamira ya Serikali kuendelea na ujenzi wa nyumba za walimu kulingana na bajeti.

"Serikali ya awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Shule za Msingi na Sekondari Nchini,kwa Mwaka 2021 ufaulu katika mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi umefikia asilimia 81.97, mtihani wa kumaliza kidato cha nne umefikia asilimia 87.30 na kidato cha sita asilimia 99.62.

“Ninawapongeza walimu kupitia CWT kwa kuongeza na kuimarisha ufaulu,hata hivyo nina wahimiza kuongeza usimamizi wa shughuli za Elimu na kuondoa changamoto zinazosababisha baadhi ya shule kutofanya vizuri”amesisitiza Waziri huyo.

Katika kuimarisha utendaji kazi, Bashungwa ameeleza kuwa mipango madhubuti imewekwa ili kuhakikisha walimu, wakuu wa shule, Maafisa Elimu wa Kata, Wilaya na Mikoa wanaendelea kupata mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo katika ufundishaji na usimamizi wa Sekta ya Elimu.

Amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya walimu 1,817 wanaofundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum ya ujifunzaji, wamejengewa uwezo wa kutumia mbinu za kufundishia na kujifunzia. 

Vilevile walimu Wakuu 8,096 walipata mafunzo juu ya matumizi ya Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule ili kuhakikisha Uthibiti wa Ubora wa Shule unakuwa na matokeo mazuri, kuanzia katika ngazi ya Shule na kwamba mafunzo kama hayo yataendelea kutolewa kila mwaka ili kutimiza lengo la kumarisha utendaji kazi.

Pamoja na hayo amezielekeza Taasisi za elimu nchini kuhakikisha wanafuata sheria, miongozo na taratibu katika usimamizi wa sekta ya Elimu ili kufikia malengo ya Serikali ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri miradi yote, inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kuwa na miradi yenye viwango vinavyoendana  na thamani ya fedha.

Vile vile amesema Serikali itaendelea kutoa Elimumsingi bila malipo, kuboresha miundombinu, na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama Cha Walimu  Tanzanaia (CWT )Mwalimu  Deus Seif amesema Chama hicho kinatambua  jitihada  kubwa zinazofanywa na walimu nchini katika kuhakikisha wanafunzi wanapata ufaulu mzuri.

Kutokana na hayo Katibu huyo kupitia CWT ameahidi kushirikiana na Serikali kuendelea kutatua kero zinazowakabili walimu ili kuwapa ari ya kufanya kazi katika mazingira mazuri.

“Tunatambua Serikali inaendelea kutujali kupitia upandishwaji wa madaraja na  urekebishwaji wa mishahara kwa walimu, pamoja na malimbikizo ya madeni  yasiyo ya mishahara,hivyo na sisi Kwa nafasi yetu tutaendelea kushirikiana Katika kutatua kero nyingine ”amesema Mwl Seif.

Amezitaja changamoto za walimu nchini  kuwa ni uhaba  wa nyumba za walimu, madai mbalimbali  ya walimu  bado yapo katika halmashauri  pamoja na ajira  kwa walimu huku akiwatoa hofu kuwa madai yote hayo Serikali kwa kushirikiana na CWT yatapatiwa ufumbuzi.

Naye  Kaimu rais wa CWT, Dina Mathamani amesema wao kama walimu wanaipongeza Serikali kwa kuona  umuhimu wa kutoa tuzo na pongezi kwa walimu waliofanya vizuri na kuwafanikisha wanafunzi kufaulu vizuri.

“Ni jambo jema ambalo kila mtu angependa lifanyike,kupitia motisha hii ufaulu unaendelea kupanda siku hadi siku taaluma inapanda na mazingira ya walimu yataendelea kuboreshwa zaidi na kusaidia kila mtu kusimama kwenye nafasi yake,

Kwa niaba ya Chama hiki,naahidi  tutafanya kazi usiku na mchana ,kwa weledi mkubwa  ili kuhakikisha ufaulu wa watoto wetu wapendwa unaongezeka,kupitia hili tutapata wataalamu wabobezi na wajuzi na hatimaye kuwa juu kiuchumi,"amesema.



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 12, 2022


Magazetini leo Jumamosi February 12 2022







Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger