Saturday, 12 February 2022

WAZIRI BASHUNGWA APENDEZWA NA CWT KINAVYOCHOCHEA UBORA WA ELIMU NCHINI, ASIFU MPANGO WA ELIMU BURE

Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog-DODOMA

SERIKALI kupitia Wizara ya Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)imesema imepeleka jumla ya shilingi trilioni 1.43, kwa ajili ya kugharamia Mpango wa elimu msingi bila Malipo ulioanza kutekelezwa 2015 na kuleta fursa ya upatikanaji wa elimu kwa kuongeza uandikishaji wa wanafunzi, kutokana na kuondolewa kwa vikwazo. 

Hayo yameelezwa na Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa Februari 11,2022 jijini hapa katika hafla ya  utoaji tuzo  za ubora wa taaluma kwa walimu,wanafunzi , Shule, Halmashauri na mikoa yote  iliyofanya vizuri kwenye matokeo  ya mitihani ya Mwaka 2021 ya kumaliza elimu ya msingi, kidato cha nne na kidato cha sita.

Amesema katika mwaka 2016, jumla ya wanafunzi 2,670,125 waliandikishwa, kati ya hao wanafunzi 917,137 wa elimu ya awali, 1,386,592 wa darasa la kwanza na wanafunzi 366,396 wa kidato cha kwanza.

Waziri Bashungwa ameeleza mwaka 2022, jumla ya wanafunzi 3,046,919 wameandikishwa, kati ya hao wanafunzi 1,123,800 ni wa Elimu ya Awali sawa na asilimia 82, wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,352, wanafunzi 1,454,544 ni wa darasa la kwanza sawa asilimia 91, huku wanafunzi 664,698 wakiwemo wenye mahitaji maalum ni 2,747.

"Wanafunzi 664,698 wa kidato cha kwanza wameripoti shuleni, sawa na asilimia 73.2 ya wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza Mwaka 2022, wakiwemo wanafunzi 679 wenye mahitaji maalum,"amesema.

Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na walimu nchini katika kuboresha taaluma, hivyo ni dhamira ya Serikali kuendelea na ujenzi wa nyumba za walimu kulingana na bajeti.

"Serikali ya awamu ya Sita imeendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Shule za Msingi na Sekondari Nchini,kwa Mwaka 2021 ufaulu katika mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi umefikia asilimia 81.97, mtihani wa kumaliza kidato cha nne umefikia asilimia 87.30 na kidato cha sita asilimia 99.62.

“Ninawapongeza walimu kupitia CWT kwa kuongeza na kuimarisha ufaulu,hata hivyo nina wahimiza kuongeza usimamizi wa shughuli za Elimu na kuondoa changamoto zinazosababisha baadhi ya shule kutofanya vizuri”amesisitiza Waziri huyo.

Katika kuimarisha utendaji kazi, Bashungwa ameeleza kuwa mipango madhubuti imewekwa ili kuhakikisha walimu, wakuu wa shule, Maafisa Elimu wa Kata, Wilaya na Mikoa wanaendelea kupata mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo katika ufundishaji na usimamizi wa Sekta ya Elimu.

Amefafanua kuwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya walimu 1,817 wanaofundisha wanafunzi wenye mahitaji maalum ya ujifunzaji, wamejengewa uwezo wa kutumia mbinu za kufundishia na kujifunzia. 

Vilevile walimu Wakuu 8,096 walipata mafunzo juu ya matumizi ya Kiunzi cha Uthibiti Ubora wa Shule ili kuhakikisha Uthibiti wa Ubora wa Shule unakuwa na matokeo mazuri, kuanzia katika ngazi ya Shule na kwamba mafunzo kama hayo yataendelea kutolewa kila mwaka ili kutimiza lengo la kumarisha utendaji kazi.

Pamoja na hayo amezielekeza Taasisi za elimu nchini kuhakikisha wanafuata sheria, miongozo na taratibu katika usimamizi wa sekta ya Elimu ili kufikia malengo ya Serikali ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri miradi yote, inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kuwa na miradi yenye viwango vinavyoendana  na thamani ya fedha.

Vile vile amesema Serikali itaendelea kutoa Elimumsingi bila malipo, kuboresha miundombinu, na kusambaza vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Chama Cha Walimu  Tanzanaia (CWT )Mwalimu  Deus Seif amesema Chama hicho kinatambua  jitihada  kubwa zinazofanywa na walimu nchini katika kuhakikisha wanafunzi wanapata ufaulu mzuri.

Kutokana na hayo Katibu huyo kupitia CWT ameahidi kushirikiana na Serikali kuendelea kutatua kero zinazowakabili walimu ili kuwapa ari ya kufanya kazi katika mazingira mazuri.

“Tunatambua Serikali inaendelea kutujali kupitia upandishwaji wa madaraja na  urekebishwaji wa mishahara kwa walimu, pamoja na malimbikizo ya madeni  yasiyo ya mishahara,hivyo na sisi Kwa nafasi yetu tutaendelea kushirikiana Katika kutatua kero nyingine ”amesema Mwl Seif.

Amezitaja changamoto za walimu nchini  kuwa ni uhaba  wa nyumba za walimu, madai mbalimbali  ya walimu  bado yapo katika halmashauri  pamoja na ajira  kwa walimu huku akiwatoa hofu kuwa madai yote hayo Serikali kwa kushirikiana na CWT yatapatiwa ufumbuzi.

Naye  Kaimu rais wa CWT, Dina Mathamani amesema wao kama walimu wanaipongeza Serikali kwa kuona  umuhimu wa kutoa tuzo na pongezi kwa walimu waliofanya vizuri na kuwafanikisha wanafunzi kufaulu vizuri.

“Ni jambo jema ambalo kila mtu angependa lifanyike,kupitia motisha hii ufaulu unaendelea kupanda siku hadi siku taaluma inapanda na mazingira ya walimu yataendelea kuboreshwa zaidi na kusaidia kila mtu kusimama kwenye nafasi yake,

Kwa niaba ya Chama hiki,naahidi  tutafanya kazi usiku na mchana ,kwa weledi mkubwa  ili kuhakikisha ufaulu wa watoto wetu wapendwa unaongezeka,kupitia hili tutapata wataalamu wabobezi na wajuzi na hatimaye kuwa juu kiuchumi,"amesema.



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 12, 2022


Magazetini leo Jumamosi February 12 2022







Share:

Friday, 11 February 2022

SABABU KIFO CHA MWELE MALECELA


BAADA ya kusambaa kwa taarifa za kusikitisha kuhusu aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele, Dk. Mwele Ntuli Malecela kufariki dunia, jana Alhamisi, Februari 10, 2022, Geneva mchini Uswisi, familia ya marehemu imetaja chanzo cha kifo hicho.

Kaka wa Marehemu William Malecela maarufu kama Lemutuz amesema kifo cha dada yake kimesababishwa na kansa.

“Ni kweli amefariki leo Hospitalini Geneva, Switzerland alikua anasumbuliwa na Kansa, msiba utakuwa Dodoma,” amesema Lemutuz.

Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.



Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.



Mwele Ntuli Malecela alizaliwa tarehe 26 Machi 1963, alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI). Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela alikua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambapo alikua Mkurugenzi wa Udhibiti w a Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele.
Share:

NABII Dkt. JOSHUA AITISHA MAOMBI YA SIKU 121 KUMUOMBEA RAIS SAMIA, KUTOKOMEZA MAUAJI


Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Dkt.Joshua Aram Mwantyala

NA GODFREY NNKO

KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Dkt.Joshua Aram Mwantyala ameitisha maombi ya siku 121 kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na kutokomeza roho ya mauaji ambayo imekuwa ikishamiri kwa kasi nchini.

Nabii Dkt.Joshua ameyasema hayo leo Februari 11, 2022 makao makuu ya Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania yaliyopo Yespa, Kihonda mjini Morogoro wakati akitoa taarifa rasmi ya ujumbe ambao amepewa na Mungu katika Taifa letu kuhusu mauaji ambayo yanaendelea kwenye Taifa letu tangu Januari hadi Februari, 2022.


"Huu ni ujumbe ambao Mungu amenipa kwa ajili ya kuliponya Taifa letu na kuliokoa dhidi ya mauaji ambayo yametikisa nchini, na yamekuja kwa tabia ambayo haijazoeleka katika jamii na nchi yetu, Mungu amenionesha kwamba, katika ulimwengu wa roho, ibilisi tayari ameweka ajenda yake ndani ya nchi yetu.

"Na anapelekea kusambaza roho ya mauaji ambayo baadaye itakuja kuingia katika ajenda za kisiasa. Lakini asili yake itaanzia kwenye makundi fulani ya kijamii. Kuna kabila kubwa katika nchi yetu, ambalo mimi ninasema ni kundi fulani katika la kijamii, litapandikiziwa roho ya chuki binafsi dhidi ya Rais wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na wanasiasa watakapogundua hicho kitu watatumia hiyo nafasi kujenga chuki dhidi ya Serikali kwa ajili ya Uchaguzi wa mwaka 2025.

"Kwa hiyo, hiyo roho itasambaa, watu wataanza kulipa visasi na kuleta vurugu itakayosababisha mauaji makubwa sana 2025 ili kutia dosari katika uongozi wa Mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan. Hii inawezekana, kwa sababu Biblia inasema kisha shetani akamuingia Yuda, halafu Yuda akapata tamaa ya kumsaliti Yesu ili auawe,"amesema.

Nabii Dkt. Joshua amesema kuwa,Yuda hakuwa hivyo asili yake, lakini shetani alimuingia,halafu alivyomuingia Mafarisayo waliokuwa wanamchukia Bwana Yesu,wakamtumia Yuda kumsaliti, akasaliti ili wampate kwa sababu wasingempata bila msaliti wake.

"Kwa hiyo katika ulimwengu wa roho hii nguvu itaendelea na watatokea watu ambao wanaaminiwa zaidi na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, watamsaliti.

"Kwa hiyo mifumo ya kiusalama na siasa za nchi zitavurugika kwa wakati huo na watu wabaya watatumiwa sana na ibilisi, kwa sababu ibilisi sasa hivi anatafuta watu wa kuwaingia ambao wana ushawishi katika nchi. Ikishaingia hiyo roho, itajenga sasa mpasuko ambao utatengeneza chuki, vikundi vya uhalifu vitaungwa mkono kufanya mauaji makubwa kwa ajili ya kuua ndoto za Mheshimiwa Rais Samia,"amesema.

Kwa mujibu wa Biliblia takatifu kitabu cha Mathayo 26:14-27:38, Nabii Dkt.Joshua alinukuu maandiko akionesha namna amabvyo Yuda alikubali kumsaliti Yesu.

"Kisha mmojawapo wa wale wanafunzi kumi na wawili aitwaye Yuda Iskariote, alikwenda kwa kuhani mkuu akamwambia. Mtanilipa kiasi gani nikimtoa kwenu? Wakamlipa vipande thelathini vya fedha. Tangu wakati huo Yuda akawa anatafuta nafasi ya kumsaliti Yesu.

"Siku ya kwanza ya sikukuu ya Mikate isiotiwa chachu wale wanafunzi walikuja kwa Yesu wakamwuliza? Ungependa tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?. Akajibu, nendeni kwa mtu fulani huko mjini mkamwambie, Bwana anasema hivi, saa yangu imekaribia, napenda kula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu nyumbani kwako.’

"Wanafunzi wakafanya kama Yesu alivyowaambia, wakaandaa Pasaka. Ilipofika jioni, Yesu aliketi mezani pamoja na wanafunzi wake. Walipokuwa wakila akawaambia. Nawaambieni kweli, mmoja wenu atanisaliti.Wakasikitika sana, wakaanza kumuuliza mmoja mmoja. Ni mimi, Bwana? Yesu akawaambia, yule aliyechovya mkono wake katika bakuli pamoja nami, ndiye atakayenisaliti.

"Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama ilivyoandikwa katika maandiko, lakini ole wake mtu yule atakayenisaliti. Ingalikuwa nafuu kwake kama hakuzaliwa. Kisha Yuda, yule ambaye alimsaliti akasema, “Ni mimi, Bwana? Yesu akamjibu,umetamka mwenyewe. Bwana? Yesu akamjibu, umetamka mwenyewe.

"Walipokuwa wanakula, Yesu akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake akisema, chukueni mle, huu ni mwili wangu.Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa akisema. Kunyweni nyote katika kikombe hiki. Hii ni damu yangu ya agano ambayo inamwagika kwa ajili ya wengi ili wasamehewe dhambi.

"Ninawahakikishia kuwa sitakunywa tena maji ya mzabibu mpaka siku nitakapoyanywa pamoja nanyi katika Ufalme wa Baba yangu. Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa Mizeituni. Kisha Yesu akawaambia, Usiku wa leo kila mmoja wenu atanikimbia kwa maana maandiko yanasema, nitampiga mchungaji, na kondoo wote wa kundi lake watatawanyika.Lakini baada ya kufufuka, nitawatangulia kwenda Galilaya.

"Petro akasema, hata kama wote watakuacha, mimi sitaku acha. Yesu akamjibu,ninakuambia kweli, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu. Lakini Petro akasema,hata kama itabidi nife pamoja na wewe, sitakukana. Na wana funzi wote wakasema hivyo hivyo.

"Kisha Yesu akaenda nao mpaka kwenye bustani iitwayo Gethsemane. Akawaambia, kaeni hapa, mimi ninakwenda mbele zaidi kuomba.Akamchukua Petro, pamoja na wale wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika na kuhuzunika.Kisha Yesu akawaambia,moyo wangu umejaa majonzi karibu ya kufa. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami,"amefafanua Nabii Dkt. Joshua kwa kunukuu maandiko matakatifu.


Pongezi

Aidha,Nabii Dkt.Joshua amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mhadisi Hamad Masauni kwa kazi nzuri ambayo anafanya, ingawa amesema juhudi zake zinatatizwa kwa kukosa watu sahihi.

"Ni kweli vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kubwa sana. Hasa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mhandisi Hamad Masauni) tumemuona anawajibika sana,na kwa kweli Mungu ambariki na Mungu ambariki Mama kwa kuona kuwa anaweza kumsaidia.

"Lakini amekosa watu sahihi, wa kumtia moyo na kumuunga mkono katika kazi anayoifanya. Jukumu letu sasa, mimi kama Nabii, Mungu ameniambia kuwa, nichukue hatua ya kulitahadharisha Taifa, kwanza viongozi wenye dhamana waanze kumtafuta Mungu kila mtu binafsi kwenye dhamiri yake, kwa sababu mamlaka hizi zinawekwa na Mungu,"ameongeza Nabii Dkt.Joshua.

Amefafanua kuwa, "Daudi alipoona hali mbaya ya Kitaifa alimlilia Mungu na Mungu alilipona nchi yake, kwa hiyo rai yangu ya kwanza ni viongozi wenye mamlaka kumlilia Mungu kwa sababu ni na hakika ni wazalendo. Na kazi kubwa ambayo mama yetu anafanya ni tishio kubwa kwa watu wengi ambao wana uchu wa madaraka.

"Kwa hiyo, sisi watumishi wa Mungu tutasimama, mimi binafsi na kanisa langu tumeitisha maombi ya siku 121 kwa ajili ya kutokomeza hii roho ili isistawi kwenye Taifa kiasi cha kuwafikia watu wabaya na kuwaletea maslahi maovu kwenye Taifa letu.

"Tunayo maombi ya siku 121 kwa ajili ya kumuinua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ili Mungu ampiganie na kuweza kumpa nguvu na kuweza kutimiza majukumu yake, halafu pili Mungu aweze kumuondolea watu ambao si sahihi wanaomzunguka ambao wanasubiri siku moja wamsaliti. Na maombi yetu nina hakika kuwa yatafanikiwa.

"Lakini ni muhimu wajibu huu uwafikie viongozi wenye dhamana ya Taifa letu, kumtafuta Mungu kwa sababu nchi yetu imejengwa katika msingi wa bila dini, lakini katika hofu ya Mungu,"amesema Nabii Dkt. Joshua.
Share:

NYUKI NUSURA WAWAUWE MATAPELI WALIONIPORA SHAMBA LANGU

Nilinunua shamba kwa matapeli Kenya kule Kitemgela. Nililipa kiasi kikubwa mno cha hela nikijua nitaanza kujenga hivi nyumba yangu hivi karibuni kumbe walikuwa wamenipangia. 


Mimi natoka Tanzania lakini mke wangu ni wa Mkenya kutoka Ukambani na alipenda tuishi kule Kenya alikozoea. Nilikubali nikamfuata kisha tukaanza kutafuta kipande cha ardhi tulichopata pale Kitengela.

 Nilikuwa na pesa nyingi za mkopo wa benki kama milioni sita unusu. Nililipa milioni mbili nikamaliza nikaanza kuweka ua kando ya ardhi hiyo. Nilipomaliza kuzingira shamba lile, fujo ikaanza na nikafurushwa bila kurejeshewa chochote. 

Maisha yangu yakagonga mwaba karibu nijitie kitanzi. Bibi Yangu alinitia moyo akaniambia nisijali. Sikumsikiza hata nikafikiria yeye ni mmoja wao walinipangia. Asubuhi Ijumaa iliyofuata, bibi yangu alinisihi tuende tutemebee mahali. Sikufahamu ni wapi alitaka kunipeleka lakini vile alivyokuwa akiiongea alitaka mno nisiikose.

 Nilifunga safari naye hadi kwa Daktari mmoja wa miti shamba anayeitwa Kiwanga. Alimsimulia yote yaliyojiri kwa maisha yetu kule Kitemgela. Daktari alicheka na akatuonyesha kioo na pisha ya majangili wale wote.


 Tulimuambia ni hao kabisa! Ilikuwa mshangao. Kachakea na kutuambi kwa muda wa takribani saa mbili hivi shamba letu la Kitengela litakuwa limerudi. Tulitoka kuruidi makwetu huku nikifikia hiyo ni utapeli tu bibi yangu ameamua kunimaliza kabisa sababu mimi ni Mtanzania. Sikutaka kumuuliza maswali sababu yalikwua yashaa fanyika. 

Ningefanya jambo mbaya hivyo nikazuia kabisa sababu ya sheria. Tulipofika nyumbani, jioni hiyo, simu ikapigwa. Aliyekuwa amepiga simu hiyo alikuwa analia kuwa nyuki zimemvamia zinamuua.

 Alinisihi niende haraka anipatie pesa zangu hataki kifo cha mapema. Nikamuuliza pesa zipi akaniambia za shamba la Kitengela. Nikamtumia account number azipeleke benki.

 Kwa kweli aliweka pesa zote takribani milioni mbili walizokuwa wamenitapeli. Kiwanga Doctors ni matata kweli. Nina furaha sana. Pia Kiwanga wanashughulikia shida kama uwezo wa kurudishisha mpenzi aliyekuwacha, Nyota ya biashara, kupata cheo kazini na kupata kazi kwa haraka. 

Wasiliana na Kiwanga Doctors kwa nambari +254 769404965 kwa WhatsApp ipo pia au tembelea Website yao: www.kiwangadoctors.com Unaweza kuandika barua pepe yaani Email kwa: kiwangadoctors @gmail.com.

Share:

Video Mpyaaa!!! NTEMI OMABALA - MAJUNGU


Hii hapa ngoma mpya ya Msanii Ntemi Omabala inaitwa Majungu..




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARI 11,2022

Magazeti ya leo Ijumaa February 11,2022










Share:

Thursday, 10 February 2022

WAENDESHA BODABODA, BAJAJI NA WAJASIRIAMALI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MFUKO WA HIFADHI YA JAMII 'NSSF'


Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umewashauri Waendesha bodaboda,bajaji na Wajasiriamali wajiunge na kujiwekea akiba kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadae, kutimiza malengo yao na kuweza kupata Pensheni ya uzeeni.

Rai hiyo imetolewa Februari 9,2022 na Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance wakati akitoa elimu kwa waendesha bodaboda, bajaji na wafanyabiashara wa Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuwaeleza namna ya kufanya biashara kwenye mfumo rasmi pamoja na fursa zinazotolewa na taasisi mbalimbali ikiwemo NSSF.


Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance alisema NSSF imefungua milango kwa ajili ya Wajasiriamali, wakulima,wavuvi na watu wote waliojiajiri wenyewe hivyo kuwaomba wajiunge na NSSF ili kupata huduma mbalimbali ikiwemo mikopo na kujiwekea akiba ya baadae.

"Mjasiriamali, mkulima,mvuvi na wote waliojiajiri wenyewe NSSF imewafikia, njoo ujiunge na ujiwekee akiba kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii wa NSSF kwa ajili ya kujiwekea akiba ya baadae, kutimiza malengo yako na pia kuweza kupata pension ya uzeeni",alisema Janeth.

"Pia kwa wajasiriamali wenye viwanda vidogo na vya kati kuna fursa ya mikopo ambayo mikopo hii inalenga kuchochea kukua na kuongezeka kwa viwanda vya ndani. Mikopo hii itawasaidia kukuza mtaji ,kununua malighafi na kununua mashine na vitu vitakavyotumika katika uzalishaji kwenye viwanda husika",alieleza.


Alifafanua kuwa Mikopo hii inatolewa kwa ushirikiano kati ya NSSF,SIDO,VETA, NEEC na AZANIA Bank.,Mwanachama anaweza kunufaika na mkopo huo kuanzia shilingi 8,000,000/= mpaka shilingi 500,000,000/= kulingana na uhitaji nawa uwezo wake wa kurudisha mkopo, Marejesho ya mkopo huu ni kuanzia mwaka 1 mpaka 7 kulingana na kiwango huku riba yake ikiwa 13%.


"Ikumbukwe kuwa kujiunga na NSSF ni bure ambapo Kima cha chini cha kujichangia kwa mwezi ni shilingi 20,000/= au zaidi kulingana na kipato. Mwanachama anaweza kuweka mara moja kwa mkupuo au kuweka kidogokidogo kila siku au kila wiki ili kufikia au kuzidi kiwango hicho kulingana na malengo au kipato cha mwanachama",alieleza Janeth.


"Kutolewa kwa mikopo yote hii hakuta angalia kiasi mwanachama alicho jihifadhia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF. Mwanachama anaweza kujichangia pindi atakapopata control namba yake(kumbukumbu namba) kwa watoa huduma wote wa fedha kama Mpesa, Tigo pesa, Airtel Money, Halo pesa pia kwa Mawakala wote wa huduma za Benk",aliongeza.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga Jumatano Februari 9,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde  1 blog
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa wajasiriamali katika Soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.
Waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga wakifuatilia elimu iliyokuwa inatolewa
Afisa Matekelezo NSSF Shinyanga Janeth Evance (katikati) akielezea huduma zinazotolewa na NSSF kwa waendesha bodaboda na bajaji Mjini Shinyanga.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

Breaking News : SERIKALI YAYAFUNGULIA MAGAZETI YA MWANAHALISI, MAWIO, MSETO NA TANZANIA DAIMA




"Agizo la Rais ni Sheria,  Leo hii natoa Leseni kwa Magazeti manne ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima.
Mama kasema Kazi Iendelee tuanze ukurasa mpya" - Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari leo Alhamisi Februari 10,2022

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger