Thursday, 10 February 2022

WAZIRI GWAJIMA AZINDUA KITUO CHA WATOTO KATIKA SOKO LA MIRONGO MWANZA


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (wa tano kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto kilichopo katika soko la wafanyabiashara wadogo Mirongo jijini Mwanza.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amezindua rasmi Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo kilichopo katika soko la wajasiriamali Mirongo jijini Mwanza na kutoa rai kwa uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kukisimamia vyema Kituo hicho.

Uzinduzi huo ulifanyika Februari 09, 2021 ambapo ujenzi wa Kituo hicho ulienda sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya Soko la Mirongo ambayo ni pamoja na vyoo, mitaro na mabanda mawili ya kufanyia biashara na ujenzi wa visimba ambao unaendelea hivyo kuondoa adha kwa wajasiriamali katika soko hilo ambalo ni maarufu kwa bidhaa za mbogamboga na matunda.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Waziri Gwajima alisema Serikali inaandaa mfumo utakaosaidia malezi na makuzi kwa ajili ya watoto hatua itakayosaidia kuwakinga na vitendo vya ukatili wa kijinsia na hivyo kupingeza hatua ya ujenzi wa kituo hicho katika soko la Mirongo kwani kitasaidia jitihada za malezi bora kwa watoto.

Naye Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kituo hicho, Serikali itasaidia upatikanaji wa waalimu walezi watakaokuwa na jukumu la uangalizi wa watoto watakaokuwa kituoni hapo pindi wazazi wao watakapikuwa kwenye shughuli za biashara.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo ulibaini kuwa asilimia zaidi ya 60 ya wafanyabiashara wadogo masokoni ni wanawake na wanakumbana na changamoto za malezi ya watoto wanapokuwa kwenye biashara na hivyo kuja na wazo la ujenzi wa Kituo hicho ili kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

Maboresho hayo yaligharimu shilingi milioni 88 ambapo shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo I4IF, UKAid, IrishAid limetoa shilingi milioni 60 huku Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikitoa shilingi Milioni 20.

Miundombinu bora katika soko la Mirongo itasaidia wajasiriamali kufanya biashara zao katika mazingira salama na kukuza biashara zao huku Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto kikisaidia kuimarisha usalama wa watoto pindi wazazi wao wanapokuwa kwenye biashara huku pia akina mama wanaonyonyesha wakiwa na eneo maalum la kunyonyeshea.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo jijini Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (katika) akimpongeza Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) kwa kusaidia ujenzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo ambapo shirika lake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo limetoa shilingi milioni 68 na Halmashauri ya Jiji la Mwanza Milioni 20 na kusaidia uboreshaji wa miundombinu katika soko la wajasiriamali Mirongo pamoja na ujenzi wa Kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (katikati) akizungumza kwenye uzinduzi wa Kituo hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (hayuko pichani).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto KIVULINI, Yassin Ally akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo hicho ambapo alisema kitasaidia pia wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo kupata eneo maalum kwa ajili ya kunyonyeshea.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (wa kwanza kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali jijini Mwanza akizindua rasmi Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo jijini Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akimsaidia kubembea mmoja kati ya watoto walio katika Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo kilichojengwa katika soko la wajasiriamali Mirongo jijini Mwanza. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI Yassin Ally.
Baadhi ya akina mama wajasiriamali katika soko la Mirongo jijini Mwanza wakiwa na watoto wao katika Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo hicho.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (katikati) akiwasili katika viunga vya soko la Mirongo kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Nyamagana Amina Makilagi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI Yassin Ally.
Wanawake wajasiriamali katika soko la Mirongo wakimkaribisha Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (hayuko pichani).
Wanachi waliojitokeza kwa ajili ya uzinduzi wa Kituo hicho.
Wakazi wa jiji la Mwanza wakishuhudia uzinduzi wa Kituo cha Malezi na Makuzi kwa Watoto Mirongo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima pia alikutana na Kamati za MTAKUWWA ngazi za Mitaa katika jiji la Mwanza na kuwahimiza wajumbe Kamati hizo kuwajibika ipasavyo ili kuzuia vitendo vya Ukatili wa Kijinsia kutokea katika Mitaa yao.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na wajumbe wa Kamati za MTAKUWWA ngazi za Mitaa katika jiji la Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (hayuko pichani) pia alikutana na wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa Mwanza (pichani) kwa ajili ya kupeana mikakati mbalimbali ya kupambana na Ukatili wa Kijinsia ambapo aliipongeza Kamati hiyo kwa kufanya jitihada kubwa kupamabana na Ukatili wa Kijinsia.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima alikutana pia na viongozi wa Machinga Mkoa Mwanza na kuagiza viongozi wa Serikali mkoani Mwanza kukutana na makundi yote mawili (Shirikisho la Machinga Tanzania na Muungano wa Machinga Mkoa Mwanza) kuja na mikakati ya kupata shirikisho moja la linakalowaunganisha machinga wote.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Ngusa Samike akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima (hayuko pichani) na wajumbe wa Kati ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa Mwanza.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima pia alitembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi (CDTTI) na kuwahimiza wanafunzi wa Chuo hicho kuwa wabunifu na kutumia vyema taaluma wanayoipata kujiajiri na kuajiriwa ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na uongozi na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi (CDTTI).
Tazama Video hapa chini
Share:

Wednesday, 9 February 2022

RAIS SAMIA AELEZA ANAVYOISIKIA SAUTI YA MAGUFULI




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto, wakiondoa kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma itakayotoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3 Hafla hiyo imefanyika kwenye Sherehe zilizofanyika leo tarehe 09 Februari, 2022 katika eneo la Veyula Jijini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi katika Sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma itakayotoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3 katika Sherehe zilizofanyika katika eneo la Veyula Jijini Dodoma.


Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 Blog-DODOMA.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma yenye urefu wa Kilomita 112.3 huku akieleza namna anavyoisikia sauti ya mtangulizi wake hayati Dkt.John Magufuli akimtaka kuendeleza miradi mingine yote aliyoiacha .


Rais Samia amesema atahakikisha anaiendeleza miradi yote iliyoachwa na Dk. John Pombe Magufuli na kuwataka wananchi kuitunza.


Kauli hiyo ameitoa leo Februari 9,2022 wakati akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa arabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma( km 112.3).


Rais Samia amesema siku ya leo toka asubuhi anasikia sauti ya mtangulizi wake ikimueleza kuhusu miradi aiyoiacha ikiwemo ya kuhamia Dodoma na mingine ikiwemo huu wa barabara ya mzunguko wa nje Dodoma.


"Ndugu zangu siku kama ya leo mimi mwenzenu toka asubuhi nasikia sauti ya mtangulizi wangu Dkt John Pombe Magufuli ananiambia kuhusu miradi hii ,,kuhusu Dodoma kuwa makao makuu, kuhusu mambo mengi.


Na leo hii tupo hapa kuweka jiwe la msingi la mradi huu lakini kàzi hii waswahili wanasema ukiona vinaelea vimeundwa na kwa bahati nzuri muundaji wa suala hili aliyetekeleza maono ya taifa kuhamia Dodoma akataka kuipanga Dodoma ,kwa bahati mbaya hatunaye,Mungu amemchukua,


Lakini ameniachia urithi mzito nami niahidi mawazo yote aliyoyaanzisha nita kwenda kuyatekeleza kikamilifu,leo hii ni moja kati ya mawazo aliyoyaanzisha niahidi pamoja na kuungwa mkono na African Bank tunaenda kukamilisha mradi huu kama alivyotaka Magufuli,"alisisitiza Rais Samia.


Katika hatua nyingine Rais huyo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara ambapo gharama ya ujenzi wa kilomita 1 ni shilingi bilioni 1.2 hadi 1.5 hivyo amewaomba watanzania kuzitunza.


Amesema ujenzi wa barabara hiyo unaenda kufungua masoko hivyo ametaka ujenzi huo ukamilike kwa wakati kwani utatoa fursa mbalimbali hivyo watanzania kujiongezea kipato.


"Ndugu zangu Benki kudhamini miradi 11 hii inadhihirisha kweli hii ni Benki kwa ajili ya Waafrika,"amesema.


Amesema kilomita moja ni shilingi bilioni 1.2 hadi 5 hivyo amesema Serikali inatumia fedha nyingi hivyo kutumia nafasi hiyo kuwaomba watanzania Kutunza Miundombinu na kuacha mambo ya hovyo yanayofanywa katika uharibifu huo.


Kadhalika Rais Samia amesema Serikali inajenga barabara 23 kwa fedha za ndani huku 13 kazi ikiwa inaendelea.



"Tunashukuru sana Serikali ya awamu ya tano kuleta vuguvugu hili pamoja na kuungwa mkono na Benk ya Maendeleo na hawapo katika barabara wapo pia katika maji na umeme tumewaomba kutusaidia katika uwekezaji wa watu,"amesema


Akiwasilisha taarifa ya Mradi huo,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Rogatus Mativila amesema lengo la kujenga barabara hiyo ni kupunguza msongamano katika Jiji la Dodoma.


Amesema jumla ya gharama ya Mradi huo ni shilingi bilioni 249 ambazo ni Kwa ajili ya fidia na ujenzi ambapo amedai kuna miradi midogo midogo kama ujenzi wa vituo vya afya,ununuzi wa ambulance wakati wa utekelezaji wa mradi huo.


Mtendaji huyo wa TANROADS ameeleza kuwa lengo ni kupunguza msongomana mkubwa wa magari katika Mkoa wa Dodoma ambao ungesababishwa na muingiliano wa magari yanayosafiri kupitia mjini.


Ameeleza kuwa barabara hiyo ina umbali wa Kil 20 kutoka katikati ya Jiji la dodoma ikiwa imegawanywa kwa wakandarasi wawili ambao ni M/sAVIC INTL Project na China Civil Engineering Construction Cooperation zote kutoka Jamhuri ya watu wa China.


Alifafanua kuwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa Kilomita 52.3 kupitia Nala,Veyula,Mtumba na Ihumwa wakati awamu ya pili itahusisha Kilomita 60 kupitia Ihumwa, Matumbulu na Nala.


Kwa upande wake,Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AFDB) Dk.Akinwumi Adesina amesema wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo amedai wanaamini Tanzania ni sehemu sahihi ya uwekezaji.


Amesema Benki hiyo imewekeza kwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali yenye thamani ya Dola za kimarekani bilioni 2.5.


"Miaka kadhaa iliyopita nilikaa na kuzungumza na rafiki yangu,mtu wa watu hayati Dk.Magufuli kuhusu kutekeleza mradi huu ,Kwa bahati mbaya hayupo tena lakini Kutokana na ushirikiano wake kwetu tunaahidi kuendelea kishirikina na watanzania kwa miradi mingi zaidi,"amesema.



Naye,Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali iliona kuna umuhimu wa Kujenga barabara hiyo kutokana na ongezeko la watu pamoja na Dodoma kuwa Makao Makuu hivyo magari yanayoingia na kutoka kuwa mengi.


"Tunatoa shukrani kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kutekeleza mradi huu,imetoa fedha nyingi katika miradi ikiwa ni pamoja na kulipa madeni ya wakandarasi,


Bila kuwa na Mahusiano mazuri hili lisingetokea niipongeze Wizara kwa mradi huu mkubwa ni ubunifu mkubwa na utafungua fursa nyingi hivyo ,"amefafanua.

Share:

WAZIRI MCHENGERWA-JIUPUSHENI NA RUSHWA, UVIVU NA UPENDELEO KWENYE SANAA TUWEZE KUFIKA MBALI

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikabidhiwa zawadi ya picha na Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) Dkt.Herbert Makoye mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) leo tarehe 09/02/2022 Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TasuBa) akiongozana na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Mhe.Said Yakub na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah. Mkuu wa Taasisi ya TaSuBa Dkt.Herbert Makoye akimkaribisha Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa mara baada ya kuwasili Chuoni hapo leo tarehe 09/02/2022 wilayani Bagamoyo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) leo tarehe 09/02/2022 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah akizungumza mara baada ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) leo tarehe 09/02/2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akikitazam kinanda kilichopo studio za TaSuBa mara baada ya kutembelea Chuo cha Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa)leo tarehe 09/02/2022 Wilayani Bagamoyo.Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akiwa pamoja na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Said Yakub na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah, wakiongozwa na Mkuu wa Taasisi ya TaSuBa Dkt.Herbert Makoye kwenye wakiangalia vifaa vilivyopo studio ya TaSuBa mara baada ya kutembelea Chuo hicho leo tarehe 09/02/2022 Wilayani bagamoyo. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Tamaduni naa Sanaa Baagamoyo (TaSuBa) kuhusu uwepo wa Studio na ufanyaji kazi katika Chuo hicho mara baada ya kutembeleao Chuo hicho leo Wilayani Bagamoyo.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*************************

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa, amezitakaa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo hasa Taasisi ya Utamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) kujiepusha na masula ya Rushwa, Uvivu, ubadhirifu na upendeleo kwenye tasnia ya sanaa ili kuweza kukuza sanaa nchini na itambulike kimataifa.

Ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea Chuo cha Tamaduni na Sanaa Bagamoyo (TaSuBa) kuona mikakati inayoendelea kufanyika katika Chuo hicho na kukitaja kuwa cha kimkakati kwa Taifa.

Aidha Waziri Mchengerwa ameahidi mageuzi makubwa ya chuo hicho na kukipa jukumu la kushirikiana na wadau kufanya utafiti wa falsafa ya muziki wa Tanzania (Tanzanian sound/beat).

Mchengerwa amesema kulingana na kauli ya Rais Mheshimiwa Samia Suluhu kuhusu kutafuta vijana wenye vipaji katika sanaa mtaa kwa mtaa, anategemea TaSuBa kusaidia kuwabaini vijana wenye vipaji na kuwasaidia.

Amesema Wizara inajipanga kuhakikisha Chuo hicho kinakuwa na Televisheni yake ambayo kukiwa na matamasha ya Utamaduni na Sanaa au matangazo mbalimbali yanayohusu sanaa yawe yanarushwa moja kwa moja kwenye televisheni hiyo.

Hata hivyo amesema suala la Rushwa, uzembe na upendelea ataendelea kupiga vita kwa maana yanashusha thamani na kuturudisha nyuma kama taifa, kila jambo linawezekana tunaweza tukashiriki mashindano makubwa ya kimataifa kama tutahamua.

Pamoja na hayo Mchengerwa amesema wapo katika mkakati wa kunazisha shule za michezo nchini ambazo zitakuwa daraja la kuinua vipaji vya michezo kwa vijana wa kitanzania mbao wapo mtaani.

"Tumekubaliana na watendaji kwamba tunakwenda kuanzisha shule 56 za michezo nchini ambapo shule moja itakuwa hapa Bagamoyo kwasababu ya mazingira lakini tutajipanga namna ya kufanya kuweza kuboresha baadhi yya viwanja vyetu ikiwemo kiwanja cha Mwanakalengwe kilichopo wilayani Bagamoyo". Amesema

Katika ziara hiyo Waziri Mchengerwa aliyeambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Mhe.Said Yakub Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Zainab Abdallah.

Share:

WAZIRI GWAJIMA ATAKA MADAWATI YA KIJINSIA KATIKA VYUO VYA MANDELEO YA JAMII.



...................................................................

Na WMJJWM- Mara

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa siku thelathini kwa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini kuunda Madawati ya Kijinsia katika vyuo vyao.

Dkt. Gwajima, ameyasema hayo wakati wa ziara yake kwenye Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Buhare kilichopo Mkoani Mara, ambacho ni miongoni mwa Vyuo ambavyo havijaanzisha madawati hayo.

"Ndani ya siku hizi thelathini Madawati haya yawe yameanzishwa katika Taasisi na Vyuo vya Maendeleo ya Jamii, haikubaliki kuona ninyi mnaosimamia Maendeleo ya Jamii mshindwe kuwa na Dawati husika" alisema Dkt. Gwajima.

Akiongea kwa niaba ya Wajumbe wa Bodi Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara Bi Neema Ibamba, amesema wamezingatia maagizo ya Wizara na atayafikisha kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Chuo watayafanyia kazi kwa kushirikiana na Chuo kutekeleza maelekezo hayo.

Kwa Upande wake rais wa Serikali ya Wanafunzi Feleki Alek, ameiomba Serikali kuona haja ya kuanzishwa kwa kozi za Shahada katika Chuo hicho itakayokipa hadhi Chuo katika kutengeneza wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini.

"Katika Mkoa wetu wa Mara hatuna Chuo chenye kutoa Shahada, hivyo kama Mwakilishi wa Serikali ya Wanafunzi na kutokana na ukongwe wa Chuo hiki, kwanza tunaomba Majengo yaongezwe lakini pili, tunaomba Chuo kipewe hadhi ya kutoa Degree" alisema Felik.

Awali akitoa Salaam za Chuo, Mkuu wa Chuo hicho Paschal Mainyila, alisema Chuo hicho kilianzishwa mwaka 1966 na kwa sasa kinatoa kozi za ngazi ya Stashada na Astashahada na kinaendelea na jitihada za kuhakikisha kinazalisha wataal wa Maendeleo ya Jamii watakaosaidia kubadili fikra katika jamii katika kutataua changamoto mbalimbali katika jamii.

Wakati huo huo Waziri Dkt. Gwajima amekutana na Viongozi wa wamachinga Mkoa wa Mara na kuzungumza nao kuhusu changamoto zinazowakabili katika shughuli zao.

Dkt. Gwajima amesema, masuala ya changamoto za Machinga ikiwepo kuhamahama, watazungumza na Mamlaka za Mikoa ili kuona namna Bora ya kutatua tatizo hilo, na hii itakuwa ni kwa nchi nzima.

"Machinga wasingekuwepo hivi mahitaji ya haraka haraka tungekuwa tunapata wapi? Hivyo kama Serikali tunathamini sana uwepo wenu" alisema Dkt. Gwajima

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Mara, Charles Waitara, ameiomba Serikali kuendelea kuliratibu kundi hilo ili liweze kufanya shughuli katika mazingira wezeshi.

"Mhe. Waziri sisi tunakuwa waanzilishi wa eneo, lakini likishachangamka tunaondolewa, hii kwakweli inanyong'onyeza jitihada zetu, tunaimani chini ya Uongozi wako hili halitajitokeza" alisema Waitara.
Share:

WATENDAJI WA MTAKUWWA WATAKIWA KUBADILIKA


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akizungumza katika kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.Kulia ni Mkurugenzi wa idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bw.Sayi Magessa


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akielezea jambo kwa washiriki wakati wa kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akimsikiliza Mkurugenzi wa idara ya Sera na Mipango Wizara ya Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bw.Sayi Magessa wakati akielezea lengo la kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.


Mratibu wa Mradi wa majaribio wa kukabiliana ba udhalilishaji na unyanyasaji wa watoto,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.


Naibu Mkurugenzi wa shirika la wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika Bi.Cecilia Assey,akielezea mikakati ya shirika hilo wakati wa kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati tendaji ya taarifa ya utekelezaji wa mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2021 kilichofanyika jijini Dodoma.

..........................................................

Na.Alex Sonna,DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amewataka watendaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto (MTAKUWWA) kubadilika na kufanya kazi kwa matokeo.

Dkt. Chaula ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha Kamati tendaji inayojumuisha Idara na Wizara zinazotekeleza Mpango huo.

Dkt. Chaula amesema kila mmoja anayehusika na kutekeleza Mpango huo atekeleze majukumu aliyopewa na matokeo yawe ya takwimu ili kiwe na uhalisia.

Amesema lazima kuwe na vigezo vya kuondoa changamoto za ukatili zilizopo ili matokeo yaonekane kuanzia ngazi ya vijiji na Mitaa.

"Utendaji wetu wa kazi uwe na matokeo, mpango huu wa miaka mitano kila mmoja atekeleze wajibu wake na kazi yoyote uliyopewa lazima iwe na matokeo kwa takwimu" alisema Dkt. Chaula

Ameongeza kuwa kama Kamati ikitekeleza majukumu yake, vitendo vya ukatili vitapungua na havitatokea katika jamii zetu.

Kwa upande wake Geoffrey Chambua mratibu wa mradi wa majaribio kutokomeza ukatili wa kingono amebainisha kuwa katika mradi huo uliofanyika kwa miezi mitatu Wilaya ya Kinondoni ilionekana kuna umuhimu wa kuwa na vituo vya mkono kwa mkono vinavyowasaidia waathirika wa ukatili wa kingono kupata huduma muhimu kwa pamoja na kwa wakati.

Naye Naibu Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo WILDAF Cesilia Assey, ameipongeza Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo kwa karibu na kutoa wito kwa wadau wote kushirikiana kutokomeza tatizo la ukatili.

Aidha amesema lengo ni kufikia hatua ya huduma kwa waathirika wa ukatili zinapatikana kwa urahisi na wananchi wanafikiwa kupata elimu kuhusu madhara ya ukatili katika Jamii.
Share:

Video : BHUTA WA NTEMI - TOKOCHAGA TWABHIPA


Msanii Bhuta wa Ntemi anakualika kutazama video yake mpya inaitwa Tokochaga Twabipa

Share:

INSTALL APP YA MALUNDE 1 BLOG TUWE TUNAKUTUMIA HABARI NA MATUKIO MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:

Tuesday, 8 February 2022

MCHENGERWA -TANZANIA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA


******************

Na John Mapepele

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mohamed Mchengerwa amesema Tanzania inatarajia kushiriki kwenye mashindano ya kombe la dunia baada ya kumalizika mashindano ya mwaka huu 2022 yanayofanyika Qatar kutokana na mikakati kabambe ya maandalizi inayoendelea hivi sasa.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo Februari 8, 2022 jijini Dar es Salaam kwenye halfa iliyoandaliwa na ubalozi wa Qatar, kuadhimisha siku ya michezo ya nchi hiyo inayofanyika kila jumanne ya mwezi Februari kila mwaka, ambapo Mhe.Balozi Hussain bin Ahmad Al Homaid na Mhe. Waziri Mchengerwa waliongoza mazoezi ya kutembea uwanjani kama ishara ya ushiriki wa maadhimisho ya siku hiyo.

Katika halfa hiyo aliambatana ya Katibu Mkuu wake, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Saidi Yakubu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Neema Msitha.Amesema Tanzania inakusudia kushiriki katika mashindano hayo kutokana na mikakati kabambe iliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya michezo nchi nzima.

“Sisi kama taifa ni muhimu tukubali ili kufanikisha zoezi hili la kushiriki mashindano makubwa kama haya lazima kujiandaa na kuboresha miundo mbinu ya michezo ambapo kwa sasa tumeshatenga shule 56 nchi nzima kwa ajili ya michezo”. Amefafanua Mhe, Mchengerwa.

Aidha, amesema Serikali inakusudia kujenga viwanja vikubwa vya ndani ambavyo vinajumuisha michezo mbalimbali viwili kwenye mji wa Dar es Salaam na Dodoma pia tunatarajia kujenga maeneo makubwa ya burudani tatu.

Amemwomba Balozi wa Qatar Mhe. Hussain Bin Ahmad Al Homaid kuiomba Serikali ya nchi yake kuisaidia Tanzania kwenye eneo la miundombinu ili kuendelea kuimarisha uhusiano uliojengeka baina ya nchi hizo mbili.

Amemhakikishia Balozi kuwa Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ipo tayari kuendelea kushikiana wakati wowote kwenye sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni kwa faida ya wananchi wa nchi zote mbili.

Kwa upande wake Mhe. Balozi Al Homaid ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuwa na uhusiano mzuri na nchi yake na kuahidi kuendelea kufanya hivyo.Pia amesema nchi yake imeitenga siku hii ya michezo ili kuendeleza michezo na kuwafanya wananchi wake kuepukana na kupatwa na magojwa yanayoweza kuzuilika kwa kufanya mazoezi.

Amesema kuwa nchi yake inakwenda kuwa nchi ya kwanza miongoni mwa nchi za kiarabu kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia.

Katika Hafla hiyo Mhe. Mchengerwa na Balozi Al Homaid walipiga mpira wa miguu golini kuashiria ufunguzi rasmi wa siku hiyo huku timu ya ubalozi huo na ile ya watumishi wa shirika la ndege la nchi hiyo walicheza mechi ya kirafiki na timu ya ubalozi kufungwa mabao 8-2 dhidi ya timu ya Shirika la ndege la Qatar.
Share:

CHOO CHA SHULE CHAPOROMOKA ... CHAUA NA KUJERUHI WANAFUNZI



MWANAFUNZI mmoja alifariki na wengine watatu walilazwa hospitalini baada ya choo cha shule ya upili ya Nyabondo kuporomoka. Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi alasiri katika eneo la Nyakach, kaunti ya Kisumu nchini Kenya.

Wanafunzi watatu waliookolewa walikimbizwa katika hospitali ya misheni ya Nyabondo ambapo wanaendelea kupokea matibabu. Aliyekuwa CEC wa kaunti ya Kisumu Vincent Kodiera alisema kuwa choo hicho kiliporomoka kikiwa na wanafunzi wanne na kwa bahati mbaya mmoja wao akapoteza maisha.

Polisi walifika kwenye eneo la tukio na marehemu akatolewa kutoka alikokuwa amenaswa. Kodiera ambaye aliwapa pole shule na familia ya mwanafunzi aliyefariki alitoa wito wa amani katika taasisi hiyo na maombi.

Alisema kuwa sasa sio wakati wa kunyoosheana vidole vya lawama na kuongeza kuwa lazima mwili wa mwanafunzi huyo ungetolewa. “Tumeona maafisa wa polisi hapa na tunajua uchunguzi utafanywa kuhusiana na tukio hilo,” alisema.



Gavana wa Kisumu Anyang’ Nyong’o alituma risala zake za rambirambi kwa familia, walimu na wanafunzi wenza wa marehemu katika shule ya Upili ya Nyabondo. Nyong’o vilevile aliwatakia afueni ya haraka wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo.


Gavana huyo alisema serikali ya kaunti ilituma vikosi vya waokoaji katika eneo la tukio ambao walijaribu kila wawezalo kumuokoa mvulana huyo anayesemekana kuwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza.
Share:

SERIKALI YAELEKEZA WAFANYABIASHARA KUSHUSHA BEI YA VIFAA VYA UJENZI


Serikali imesema tathmini iliyofanyika imebaini ongezeko holela la bei ya vifaa vya ujenzi hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Ashatu Kijaji amesema wamebaini ongezeko limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho.

Ameelekeza Wazalishaji na Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela. Mamlaka za Udhibiti zimeagizwa kuchukua hatua dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni.



Share:

WAZIRI GWAJIMA AWAPONGEZA NGARIBA WALIOACHA KUKEKETA,AWAAHIDI USHIRIKIANO WA SERIKALI


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifunga Kongamano la Kupinga Ukeketaji lililofanyika mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,akicheza ngoma wakati wa Kongamano la Kupinga Ukeketaji lililofanyika mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime.


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Kongamano la Kupinga Ukeketaji lililofanyika mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime.

...............................................................

Na WMJJWM

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amewapongeza Ngariba waliokuwa wanajihusisha na vitendo vya ukeketaji baada ya kuacha kufanya vitendo hivyo na kisha kugeuka kuwa wanaharakati wa kukemea vitendo vinavyo dhalilisha utu wa mtoto wa kike na kumuachia maumivu makali.

Akifunga Kongamano Maalum kwajili ya mapambano ya kutokomeza Ukeketaji lilichofanyika mkoani Mara katika Wilaya ya Tarime, Dkt. Gwajima alisema, kitendo cha Ngariba hao kuacha suala la Ukeketaji na kujiunga na Serikali katika mapambano hayo ni ujasiri wa hali ya juu na nicha kupongezwa.

“Mmewasikia wenyewe wakijieleza hapa, kwamba wapo baadhi yao walikata shauri na kuacha kuendelea kukeketa, lazima tuwapongeze sana kwa hatua hii. Lakini baadhi yao wanatishiwa hata kutengwa na jamii zao baada ya kuacha vitendo hivyo vya kikatili, tuseme kama Serikali na wadau tutakuwa nao bega kwa bega kuwatetea kwa nguvu zote bila kuchoka” alisema Waziri Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima alisema dhana ya kwamba, mtoto kumvusha rika kutoka usichana kwenda kuwa mama au mtu mzima sio lazima akeketwe zipo njia mbadala za kumvusha binti rika ikiwepo kuwapatia mafunzo yakujitambua bila kumuathiri mwili wake.

Ameongeza kuwa, zipo athari wanazo kumbana nazo Mabinti wanaokeketwa ikiwepo athari za kisaikolojia na msongo wa mawazo, kwani, vitendo hivyo hufanywa bila ridhaa ya wahusika, kupata maumivu makali, kutokwa damu nyingi, kuuguza kidonda, changamoto za kujifungua na uwezekano wa kupoteza maisha.

“Madhila mengine kusababisha maambukizi ya magonjwa ya ngono, Virusi vya UKIMWI pamoja na magonjwa ya njia ya mkojo (UTI), lakini pia uwepo wa kovu la ukeketaji linalo kusababisha mimba kinzani na unaweza kusababisha fistula”. alisisitiza Dkt. Gwajima, na kuongeza kuwa,

“Mtoto anaweza kupata changamoto wakati wa kujifungua ambapo zinaweza kumsababishia mtindio wa ubongo, na kupata mateso katika maisha yake yote. aliongeza Waziri Dkt. Gwajima.

Awali kabla ya kufunga mafunzo hayo, wakichangia mada zilizowasilishwa katika Kongamano husika, Mangariba hao waliiomba Serikali iwalinde, ili wasikutwe na madhila kutoka ndani ya Jamii zao.

“Tunapo acha shughuli za Ukeketaji ni kama tumetangaza vita na wazee wa Mila, lakini pia Jamii zetu, hivyo Mhe. Waziri, tunaomba sana, tunapo salimisha zana za Ukeketaji, basi Serikali itungalie namna inavyoweza kutuwezesha ili tuwe na mitaji na kufanya shughuli mbadala, lakini zaidi sana, tunaomba tulindwe dhidi ya wanaotutishia, alisisitiza mmoja ya Ngariiba.

Nao viongozi wa Dini ambao walikuwa Sehemu ya Kongamano hilo, wameitaka Serikali kubadili mtazamo wa elimu na kutaka elimu husika izidishwe kwa watoto wa kiume kwani pamoja na kuwachukuwa Wasichana na kuwapeleka katika makaazi salama kwa wale wanaokimbia vitendo hivyo, kazi bado ipo kwa wavulana ambao hawana Elimu ya madhila ya ukeketaji kwa mwanamke

“Ndugu Viongozi na Washiriki wa Kongamano hili, kwa sasa tumewekeza angalau kwa watoto wa kike, lakini kuna kundi kubwa la wavulana, hawa tumewaweka nyuma, niiombe Serikali na Wadau, tulitazame kundi hili, alisema” Sheikh Khalfan Shaban Mtongori.

Kila mwaka, mwezi Februari, Tanzania huungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukeketaji kwa Wanawake na Watoto.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger